Sunday, January 3, 2021

WEWE SI UNAISHI LEO, WEWE UTAISHI KESHO.

Kuna mawazo yanakujia kwenye ufahamu wako na wakati mwingine yanakutia unyonge kwa sababu ni kama unaona umeshatumia kila njia ili kufikia malengo yako lakini inaonekana ni ngumu kufikia kusudi la juhudi zako, umefika mahali picha kubwa inakujia kichwani mwako kuwa wewe uko kwenye fungu la kukosa..........
Hapana wewe ni shujaa, wewe ni uwekezaji wa Mungu, kuna kitu cha tofauti umebeba ndani yako, wewe ni ardhi ambayo ndani yake imebeba utajiri mwingi wa madini, nani mgunduzi na mchimbaji, bado hajapatikana, nani atakuja kugundua kuwa katika ardhi wewe umehifadhi madini ambayo bado hayajagundulika...
Baba na mama walishindwa kugundua mapema, bahati mbaya kuanzia mwalimu wako wa chekechea hadi chuo kikuu hajafanikiwa kugundua madini yaliyo katika ardhi wewe, Jirani na mtaa kwa ujumla nao umeshindwa kugundua nakutambua kwenye ardhi wewe kuna madini yanayosubiri kugunduliwa na kuanza kuchimbwa.
>Kuna majiolojia wachache wamefahamu kuwa ardhi wewe umehifadhi madini lakin bahati mbaya wamepatwa na woga kuwekeza mitaji yao kwa kuhofia kula hasara kwa sababu serikali haina swalia mtume, muda wa janja janja umekwisha, TRA na serikal wako macho kudai chao mapema ingawa kwa sasa ni kama hawaoni....
Nani mwekezaji mwenye uthubutu, mwekezaji mwenye kufuata kanuni na taratibu za serikali ïli akipata kibali cha kazi kesho asiletewe taabu, nani yuko tayari kuwekeza fedha muda, kwa manufaa ya kesho, nani ambae haionei serikali wivu kwamba mimi niweke mtaji wangu halafu tuje tuvune wote faida...
Uwezo ulio nao, hujaugusa, wazazi, ndugu, marafiki, walimu na jamii kwa ujumla hawakutambua uwezo huo. Ni wakati wako kukaa chini na kujitathimini ili kujigundua uwezo wako, ukifanikiwa kujigundua basi wewe si wewe unaishi sasa, wewe ni yule ambae alikusudiwa na Mungu ambae aĺiweka uwezo wa kipekee ndani yako. Kwa sababu hujaishi leo umebaki kuzurura, Wewe wa Mungu anakutegemea uishi kesho.
Rudi kwenye kiti, jisome, jitathimini ndiyo njia sahihi yakujifahamu na ukishajifahamu ndiyo utakuwa umefika muda wa kuishi ndoto na maono yako, kubali kurudi kwenye kiti na meza ya tathimini kule mahali pautulivu.
Mgema Moses

1 comment:

  1. Nakuelewa sana.kesho yetu ni kubwa hata kama leo yetu haina matumaini..Mungu yuko pamoja nasi

    ReplyDelete