Kuna changamoto vijana au watu wengi tumekuwa tukiitengeneza mwisho wa siku imepunguza sana thamani ya watu wengi.
Mtu anaenda ametuma maombi ya kazi mahali, ana elimu na sifa zote zinazotakiwa na waajili, lakini cha ajabu mtu akiitwa kwenye usahili badala yakuwasilisha ubora wake kila anapoulizwa swali basi unakuta anapoteza hali ya kujiamini, anatetemeka, anajibu maswali kwa kuonyesha sura yakutaka kuhurumiwa, akiulizwa unataka tukupe mshahara wa kiwango gani basi anataja kiwango cha chini kabisa ili aonekani hapendi hela, weee watu hawakuchukui kwa sababu umetaja dau dogo, wanachukua ubora wako, ukitaja mshahara mkubwa na unasifa kwanza lazima huyu mtu hana njaa, anajielewa, na anajua thamani yake hivyo lazima wakuchukue mshahara mtajadiliana tu baadae.
Namna utakavyojirahisha ndivyo thamani yako itakavyokuwa chini, hata kama utapata kazi bado wanauwezo wa kukufanya chochote wanataka, sio kwa sababu huna uwezo au bora hapana, una uwezo na ubora ndiyo maana wamekuchukua changamoto namna ambavyö ulijiwasilisha kwa ile mara ya kwanza ndiyo maana wanakufanya wanavyotaka.
Ni kweli wakati wakutafuta maisha hasa kama umetokea maisha duni, umepigika kweli kweli unalazimika kusema ndiyo hata kwenye uonevu lengo nikuitumikia ile kauli isemayo mtumikie kafiri ili mradi mkono unaenda kinywani, hapana jaribu kuheshimu taratibu na kanuni za ofisi ila usijishushe thamani yako.
Kuna watu wana mawazo mazuri, na watu wengi wameyakubali baada yakuyapitia ni mawazo ya miradi mikubwa, bishara kubwa nk., lakini namna ya uwasilishaji wa mawazo hayo basi unajikuta uliopelekea idea hiyo wakuone wewe njaa na kupitia njaa yako basi unatoa mwanya kwao kuishusha thamani ya wazo lako, sababu ulitengeneza unyonge hata kabla.
Ndiyo maana wahenga walisema, umaridadi huficha umasikini na matatizo yako, jaribu kwa kila hali kuiona thamani yako mbele ya watu unao amini wanaweza kuwa daraja la kwako kusogea mbele zaidi kuelekea ndoto zako.
Joel Nanauka mwandishi wa kitabu cha timiza malengo aliwahi kusema: kuna siku alitakiwa kwenda ofïsi moja kubwa jijini Dar es salaam, katika ile ofisi sio mkurugenzi wala wafanya kazi wengine ambao walimfahamu bwana Joel, siku ya mafunzo ilifika na viongozi wa kampuni walijipanga kumpokea cha ajabu walikutana na mtu ambae hawakumtegemea kabisa kutokana na mwonekano wake, umbo dogo, yuko simple sana, na waĺitegemea kuona V-8, mtu mkubwa sana katika mwili. Kwa kweli mwonekano wake ilikuwa dissapointment kubwa sana, mkurugezi alikataa kuwa sie mkufunzi na ilibidi yatengenezwe mazingira kule ndani ili kuwaanda kisaikolojia washiriki wa washa ile na hii ilikuja baada ya mazungumzo marefu kabla hawajakubali hata kwa shingo upande.
Bwana Joel alijeng Utulivu, kuitambua thamani yake, madini yake na maandalizi yalimpa ujasiri mkubwa na aliamini kitu pekee kinachoweza kumbeba ni uwezo wakuwasilisha mada na mafunzo kwa kiwango cha juu, misukosuko na dhoruba ya kugomewa kuwa si yeye mkufunzi haikumwondoa kwenye lengo la uwepo wake katika ile washa...
Muda ulipofika alipanda kwenye podium kwa ujasiri na nguvu na shauku yakufanya vizuri. Baada ya mafunzo kilichobaki ni historia na kila mtu anamfahamu joel Nanauka. Joel hakuwa yule waliyemwona katika umbo dogo, bali alikuwa ni Nanauka mwenye umbo kubwa sana ndani yake.
Una nafasi yakuwa prove wrong wale wanaokuona wewe ni mnyonge, sio kwa kuwalazimisha bali kwa thamani yako. Be you, create confidence, create your trust to the majority by making it to the maximum
Híi anaapply kwenye maisha yote mfano heshima ya mke ni namna ambavyo ulijiposition wakati umefuatwa na mwanaume,....Thamani yako ilipanda au ilishuka baada yakukutana na mtu kwa mara ya kwanza. Jenga heshima yako hata kama unahitaji jambo present yourself in a high value ili kesho mtu asiseme kuwa huyu mtu yuko hapa kwa kuwa alihurumiwa.
Tujifunze kwa mawe ya thamani, dhahabu, Almasi, Tanzanite, na madini mengine hayapatikani kirahisi wachimbaji hutoka jasho na damu ili kuyapata sio kirahisi. Ni mawe lakini thamani yake imekuwa juu kutokana na namna ya upatikanaji.
Fedha ina thamani kubwa kwa sababu sio kila mtu anaweza kuitengeneza, na ili uweze kuipata lazima upambane sana ndiyo uipate.
Hivyo ijenge thamani yako kutokana na kile unachomiliki, kama unakipaji basi kifanye kuwa na thamani.
Mgema Moses
No comments:
Post a Comment