Tuesday, January 19, 2021

MCHAKATO NDIYO MAFANIKIO SIO MATOKEO.

 watu wengi tumekuwa wahanga wa matokeo ya mwisho yanayoonekana kwa macho, tunazungumzia kwa kina na kupongeza kwa sababu tunamwona mtu akiwa na fedha nyingi, akimiliki nyumba, biashara na vitu vingine kama kazi nzuri.
Mara nyingi tumekuwa wagumu wakufuatilia chanzo cha mafanikio ya mtu alikoanzia, sio kila matokeo yanapaswa kupongezwa, jua chanzo kïlichomfanya kuwa hapo juu, ni kweli tunapaswa kupongezana pale mtu anapofanikiwa au kufanya vizuri lakini pongeza panapostahili kupongeza, mtu amepambana mpaka ametusua maisha,amekuwa na bidii yakusoma na mwisho wake amefanya vizuri, hivyo pongeza bidii na mchakato unaoambana na uvumilivu ambao umeleta matokeo yanayoonekana.
Usipende kumpongeza mtu kwa kuona matokeo ambayo hata hujui matokeo yale yametokana na nïni, kuna watu wana maisha mazuri kwa sababu yakuiba, kuna watu wamefaulu mitihani kwa kuigia na ukimwambia mtu yule ufaulu wa kwenye karatasi apeleke kwenye utendaji unakuwa ziro.
Mafanikio bora ni yale yanayopikwa kuanzia chini kwa kufuata misingi na mchakato sahihi ambayo siku ikionekana kwa macho inakuwa ni reflection ya mafanikio ambayo yameleta matokeo yanayoonekana kwa macho ya wengi.
Mafanikio ya ndoa sio kile kicheko kionekanacho kwenye nyuso za wanandoa no, mafanikio yao ni namna ambavyo kila mtu amempokea mwenzake nakuamua kustiliana na kubeba kwenye madhaifu na uimara nakuhesabiana kuwa bora kwa kila mtu
Ukiona timu ya mpira inapata matokeo bora kiwanjani, fahamu hayo ni matokeo ya mafanikio ya uwekezaji, na kupitia mchakato sahihi kwa kutengeneza mseto mzuri kuanzia utawala, team management, coaching stuff, wachezaji na timu nzima kwa ujumla, kionekanacho uwanjani ni matokeo ya mafanikio nyuma ya pazia.
ukiona matokeo bora kwenye biashara, fahamu akili ilifikiri vyema sana na kupeleka kwenye mawazo hayo kwenye karatasi na baadae kwenye utekelezaji.
Usipende kumpongeza mtu kwa matokeo yaonekanayo kwa sababu hujui matokeo hayo yametokana na mchakato sahihi au usio sahihi tujifunze Kupongeza mchakato ulisababisha matokeo yanayoonekana sio matokeo ambayo wakati mwingine huja bila kupitia njia na mchakato sahihi.
UKIONA  KOBE AMEINAMA FAHAMU TU KUWA ANATUNGA SHERIA,....
Mgema Moses

No comments:

Post a Comment