Friday, January 29, 2021

KIPAJI NI BORA, ELIMU NI MUHIMU JUU YA KIPAJI.

Nimekuwa napenda sana kusoma quotes ya Albert Einstein ambayo inasema ''Everybody is a genius. But if you judge a fish by it's ability to climb a tree, it will live it's whole life believing that it is stupid'' 
Naupenda sana msemo kwa sababu ni elimu na somo tosha kwa jamii ambayo imekuwa ikiishi maisha ya kukariri pasipokujua kuwa maisha ya mtu tangu mwanzo yalijengwa kwenye msingi wa kutembea kwenye channel ya kipaji chake.
Elimu imekuwa ni kificho cha watu wengi, huku pia asilimia kubwa tukiwa hatujui maana na lengo la elimu hasa kwa watoto, vijana na watu wote kwa ujumla. Elimu sio ajira, elimu haikutenganishi na talanta ambayo Mungu aliiweka ndani yako.
Elimu inakipa thamani ambacho tayari kinaishi ndani ya mtu, elimu tunayoipata shuleni, kwenye washa, semina na makongamano ya elimu rasmi na isiyo rasmi ina lengo kutujengea mtazamo mpana zaidi ya ule tunaokuwa nao kabla yakupata elimu hiyo.
Elimu ni mkusanyiko wa maarifa na ujuzi wa mambo mengi ambayo yanatugawanya na kila mtu kujigundua kuwa mimi ni wa sehemu au niko kundi gani. Changamoto kubwa imekuwa kwa wazazi na walezi kuwalazimisha watoto kufanya vitu ambavyo katu hata kama angekesha kusoma usiku kucha hawezi kuwa unavyotaka wewe mzazi au mlezi, mwisho wa siku atafeli nakuichukia shule .
Nimeandika makala hii baada ya ijumaa kumwona mtoto wa miaka nane, Juh Juh Ruge Mtahaba akifanyiwa mahojiano katika kituo cha redio clouds, namna anavyojielezea wakati anawasilisha kipindi cha watoto cha Smart Bees, unaona ambavyo mzazi alivyo karibu na mtoto na kufuatilia nini amebeba ndani yake ndiyo maana anaanza kumsogeza karibu na mahali ambapo anaweza kukifanya kipaji chake kuanza kuonekana vyema, mtoto yule sio kama hasomi ana soma lakini elimu yake imejikita zaidi katika kuboresha na kuinua kipaji chake vyema.
Tumekuwa na changamoto kama jamii ya watanzania na mgawanyiko mkubwa ndani yake, wakati vijana asilimia kubwa wakiamini kipaji pekee ndiyo suluhisho la wao kutoka kimaisha, wazazi wengi wanaamini njia pekee yakumfanya mtoto kutoka kimaisha nikusoma ili aajiriwe, vijana wamewekeza nguvu maana wanaona wasomi wengi hawana na ajira hivyo kudiriki kusema kuwa elimu imeshuka thamani.
Kipaji ni muhimu, ila elimu ni muhimu zaidi kwa sababu inakufanya kujitambua, kujua namna yakukipa thamani kipaji chako, namna yakufanya branding, kujiweka kwenye masoko, hata kama una watu wanakusimamia ni rahisi kujua mchakato wa mikataba maana elimu ipo.
Wazazi tubadilishe mtazamo juu ya elimu tunayopata kuwa sio kila unaempeleka shule lazima apate ajira serikalini bali elimu ifanyike kuwa mtaji wa kwanza kwenye kuelekea ndoto ya kijana au mtoto wako.
Tukiendelea kuwalazimisha watoto kufanya yaliyo matakwa yetu, tutakuwa tukiihalalisha kwa viteńdo kauli ya Albert Einstein ya samaki kushindwa kupanda mtini, nakubaki kuamini kwamba yeye ni mpumbavu, kumbe amevamia eneo ambalo sio eneo aliloumbiwa kuwa bora.
Elimu ni mhimu sana ila, kipaji ni chanzo kikubwa cha ajira na utajirh, vyote tutembee navyo, kipaji isibaki kama mbadala wa watu walioshindwa shule au watu masikini.
Open your mind
Mgema Moses
0715366003

1 comment: