Jumapili inakuwa ni siku bora sana kwa ajili ya ibada, kumshukuru Mungu kwa kumvusha salama katika wiki inayoisha, kurudisha utukufu Mungu, na kutimiza wajibu wa ibada kama ambavyo ni utaratibu wa Mungu ulivyo, fanya kazi siku sita halafu siku ya saba, itakase maana ni sabato ya Bwana, ni siku muhimu sana.
Wengine siku hizi mbili huzitumia kwa kufanya mambo sio mazuri, kulewa na mambo ambayo yanageuka kuwa kero kwa familia na jamii kwa ujumla. Badala ya kutimiza angalau asilimia kadhaa zakukaa na watoto nyumbani au basi kutoka nao out, mtu anachagua kwenda kula maisha bar na kuwanyima watoto fursa yakuwa pamoja angalau kwa siku moja, ambayo ukiitazama vyema inaweza kuwa inajenga afya ya familia na furaha kwa watoto.
Tuko na mambo mengi kutokana na ulimwengu ulipofikia sasa, mambo mengi na yanamtaka kila mmoja kupambana, lakini bado tunawajibu kama wazazi kuwapa muda angalau wa wasaa kadhaa watoto wetu na familia kufurahia pamoja nasi.
Na hii huleta tabasamu na furaha kwa watoto kwa kuwa pamoja na baba pamoja na mama. Furaha ya watoto ni maombi tosha ya kufanikiwa kwako nakuwa na wiki yenye amani, furaha na shauku ya kutimïza kila jambo lilïlopo kwenye ratiba yako. Maombi ya watoto huwa na maana na nguvu sana kwa wazazi wao, hawawezi kuomba kama kuomba ila tabasamu na kicheko chao ndiyo maombi yao kwa wazazi wao.
Pata muda na familia yako ndiyo msingi wa furaha na mafanikio yako, mambo ni mengi lakini kumbuka kuwa familia ni muhimu sana pia kama ilivyo kazi na mambo mengine ya msingi. Ifanye jumatatu yako kuwa ya furaha kwa kuimalïza wiki na familia pamoja na ibada kwa Mungu wako.
Uwe na jtatu ya Baraka za Mungu.
Mgema Moses
0755632375/0715366003
No comments:
Post a Comment