Wednesday, January 6, 2021

CONNECTION...

Katika dunia ya leo kumekuwa na lawama nyingi kwa baadhi ya watu kwamba kuna sehemu walïstahili kuwepo kwa sababu ya sifa na uwezo ambao wanaamini wanao, wanataaluma, uwezo, maarifa na ujuzi katika mambo mbalimbali ambayo bila shaka yanawastahilisha kuwa sehemu fulani.
Changamoto ambayo wengi wanaamini ndiyo imekuwa sababu ya wao kutokuwepo wanapostahili ni ukosefu wa CONNECTION hawana mtu wa kuwavusha na kuwafikisha kwenye nafasi fulani. Changamoto hii imeanza tangu zamani utamsikia mzee anasema mimi nilikuwa na akili sana lakini kutokana na kukosekana kwa shule, kutokana na umasikini wa familia yangu sikwenda shule yawezekana ningekuwa waziri au mtu fulani mkubwa serikalini.
Hali hii imekuwa mwendelezo wa maisha yetu, wengi ambao hatujapata nafasi tunaamini kuwa hatupo kwenye position fulani, hatuna maisha fulani kwa sababu hatuna watu wakutupa connection/hatuna watu wakutushika mkono.
Ni kweli maisha yetu yanahitaji connection, maisha yetu yanahitaji watu ili kufikia hatua fulani. Pamoja na hayo yote huwezi kubweteka tu nakukaa unalalamika nakulaumu watu eti unakosa nafasi kwa sababu yakukosa nafasi.
Tunapaswa kuelewa kuwa hata hao ambao wanaconnection leo hawakuanza na connection za watu bali uwezo, uthubutu, kujionyesha nakuitangazia dunia kuwa mimi nina hiki kitu cha tofauti nastahili kuwa mahali fulani, hawatasema leo lakini kwenye mioyo yao watakuwa wamekubali, yawezekana wasikutafute leo, ila kesho watakutafuta tu.
Connection ya maana ni uwezo wako, sifa zako katika taaluma na unavyoweza kuifanya taaluma yako kuwa tofauti na wengine. Lawama, malalamiko sio suluhisho la kukufanya upate unachotaka.
Kumbuka kama huna mtu wakukutia birikani wewe unawajibu wakujitia birikani hata kama ni kwa kujivuta, dunia ya leo inahitaji utofauti wako ili wakupe connection, kama huna mtu pale mbele, ufanye uwezo wako, kipaji chako, taaluma yako kuwa connector, jionyeshe, iambie dunia kuwa mimi nina hiki chatofauti, sio kwa maneno bali kwa matendo na matokeo ya kazi yako hata kama ni ndogo, wenye akili wataona tu, hata kama hawatakuambia ila kumbukumbu zitabaki kichwani.
Jitambulishe hata kwa lazima, walazimishe watu wakujue wewe una uwezo gani, halafu kila kitu cha uwezo wako kifanye kwa uwezo wa kiwango ch juu sana, kama wewe ni mwimbaji, mtangazaji, mwandishi, photographer, videographer etc hata kama ni bure fanya kwa kiwango kama kuna dau nono mbele yako, ukienda kufanya Interview fanya, usionyeshe huruma ili watu wakuhurumie, umasikini wako sio sababu ya watu kukupa kazi au nafasi kweye jambo fulani, watu wanahitaji uwezo wako tu. Huruma peleka nyumbani kwa wazazi watakuhurumia, wala watu hawakuhitaji wewe wanauhitaji ujuzi, maarifa na uwezo wako period
Mgema Moses.
mgemamoses@gmail.com
0715366003/0755632375

No comments:

Post a Comment