Friday, January 8, 2021

JENGA MAHUSIANO BORA NA WATU.

Duniani tunaishi kwa kutegemeana kwa 100% either moja kwa moja au kupitia mlango wa nyuma ila kwa kifupi tunategemeana ili kuweza kuishi na kuziishi ndoto na malengo yetu. 
Kila jambo ambalo mtu anabuni, anafanya liwe ni la burudani, kazi serikalini au sekta binafsi, biashara na shughuli nyingine mbalimbali mlengwa huwa ni mtu.
Hivyo basi jaribu kujenga mahusiano mazuri na bora na watu kwa sababu hujui kesho mtu huyo atakufaa kwa jambo gani. Kuna baadhi ya watu wanasema yeye anafuata mambo yake, yeye jambo la kuhusiana vyema na watu kwake anaona sio jambo la muhimu, ni kweli yawezekana kuna mtu unamwona hana faida wala umuhimu sana kwa sasa ila hujui kesho atakufaa kwa jambo gani.
Watu ndiyo wateja wetu katika biashara zetu, watu ndiyo watazamaji wa burudani na michezo tunayofanya kupitia vipawa na vipaji vyetu, tunaajïliwa maofsïni tageti kubwa ni watu, pasipo watu hakuna raisi, hakuna waziri, hakuna mwanachezo, muigizaji,wala mwanamuziki, kwa ufupi hakuna chochote pasipo watu.
Matajiri kwa masikini tunaamka mapema kwenda kwenye mahangaiko ya kila siku anaetafutwa ni mtu ahudumiwe kwa namna yoyote ile.
Hivyo ni vyema kujenga mahusiano bora na kila mtu, usipende kutengeneza uadui usiokuwa na lazima kwa kupitia lugha chafu za matusi, kupigana, fitina na mambo mengine yasio faa, tafuta amani na kama haiwezekani ni bora ukaondoka ili kulinda utu na hadhi yako kwa sababu hujui huyo mtu unaetengeneza nae uadui atakufaa kesho kwa jambo gani. Najua sio rahisi kuishi na watu wote vyema ila jaribu kuepuka kile ambacho kinaweza kuepukika kwa manufaa ya kesho, usitengeneze ugomvi na mteja wako wa kesho, daktari wako, mwalimu wako, mbunge wako, Raisi wako, mpiga kura wako mfanyabiashara wako nk. kwa sababu bado unaishi hujui nani atakufaa kesho.
Mahusiano bora na watu ndiyo msingi wa mafanikio yako kwa sababu bidii, ujuzi, maarifa bila watumiaji wa hayo yote ni kazi bure. 
Mgema  Moses
mgemamoses@gmail.com
0715366003/0755632375

No comments:

Post a Comment