Wednesday, January 20, 2021

MAARIFA NI DIRA YA MWELEKEO SAHIHI.

Maarifa ni ufunguo, maarifa ni daraja laini(soft bridge), Ni ufunguo kwa sababu kupitia maarifa tunafahamu mambo mengi ambayo yamefungiwa kwenye hazina mbalimbali katika dunia yetu na kwetu pia kama watu...
Maarifa ni daraja kwa sababu kabla ya kuwa na ufahamu wa jambo fulani mara nyingi tumeishi kwenye giza, lakini baada ya kupata maarifa kuna vitu vingi vimerahisishwa sana tofauti na hapo kabla yakupata maarifa yakutuvusha kwenda ng'ambo ya upande ambao tulikuwa hatuna namna yakuwaza kama inawezekana lakini baada ya maarifa imekuwa rahisi kufika huko.
 Kabla ya ukoloni wazee wangu pale mwadui walichukua almasi nakuchezea kama kete za bao, mzungu alikuja na golori nakuwarubuni wazee wangu hao, akawaaminisha kuwa golori ni bora zaidi ya almasi, wakavutiwa na mng'ao wa golori wakaona Almasi haifai, Mzungu akachukua mali wazee wakabaki na na golori kwa furaha najua moyoni walisemezana hawa wajinga tumewala, kumbe wao ndiyo waliliwa, hakika wajinga ndio waliwao. Ujinga sio tusi bali ni kukosa ufahamu juu ya jambo fulani, hata mimi ni mjinga wa mambo ambayo sina ufahamu nayo.
Huwezi kuwalaumu wale wazee kwa kuibiwa namna ile ilitokea hivyo kwa sababu hawakuwa na ufahamu juu ya hivyo vitu viwili kwa wakati huo, wakakutana na wajanja wenye uelewa, ufahamu ambao ulitokana na maarifa vichwani mwao, waliojua thamani ya almasi zaidi ya wazee wangu.
Biblia iko wazi inasema kuwa watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa, ni kweli bila maarifa ni ngumu kujigundua binafsi, kugundua fursa zinazotunguka, ni ngumu kupiga hatua, itakuwa ni kawaida kutumia nguvu nyingi kwenye jambo linalohitaji akili na uelewa mdogo tu...
Pasipo maarifa wazee wetu wamelala kwenye yadi za mashamba yetu wakiwa masikini, wameacha utajiri wa mifugo kwenye mazizi mengi, huku wengi wao walikuwa marafiki wa nyumba duni za majani, kulala kwenye ngozi nakula vyakula duni wakati utajiri umelala kwenye himaya zao.
Vipaji vingi vimekufa bila kutumika kwa sababu tulikosa maarifa yakuviendeleza nakuvigeuza kuwa mitaji ambayo ingetuletea utajiri na ajira zakutosha, .. Maarifa, Maarifa ni ufunguo
Bila maarifa tusingekuwa na ndege leo, meli, lami, madaktari bingwa, wahandisi wa majengo yanayopendeza kule Dar es salaam, bila maarifa tungewezaji kupita juu ya maji kama Petro, tungewezaje kupaa angani kama mwewe, bila maarifa tungewezaje kutunza kumbukumbu ya picha, video ya matukio tunayoyafanya katika kizazi hiki, tungejuaje historia ya kule tumetoka, kamera zemetusaidia kupata hifadhi ya matukio ya nyuma kwa manufaa ya kesho.
Matokeo ya haya yote ni zao la maarifa. Maarifa haya yanapatikana wapi ?
Mtu mmoja nilimsikia akisema elimu haina faida tena kwa sababu watu wanamaliza vyuo hata kazi hawapati wanarudi kuuza nyanya kwenye masoko na magenge ya mitaani huko mbagala, keko, kuuza supu ya mapupu huko vingunguti kati ya soko maarufu la mbuzi kutoka Dodoma huko Dar es salaam, nilitamani kushawishika kuwa ni kweli, lakini nikakumbuka tena kuwa Biblia inanikumbusha kwa habari ya Kumkamata sana Elimu nisimwache aende zake...nikashtuka kidogo, mshtuko wangu ukanikumbusha kuwa watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa, kwa stori za yule ndgu yangu, kama nisingekuwa nimepitia ule mstari wa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hakika ningeangamia maana ningemwamini bila kupinga ila kwa sababu nïĺïkuwa na maarifa nïliepuka muangamio mkubwa wa mawazo finyu na mgando toka kwa yule ndugu.
HAYA MAARIFA YANATOKA AU KUPATIKANA WAPI....
Elimu ni chanzo cha maarifa na ndio kiboreshaji cha juzi mbalimbali ambazo Mungu alituzawadia mfano vipaji mbalimbali katika michezo, kuimba, burudani, kwenye ufundi wa vitu mbalimbali ambavyo ni hard na soft skills.
Elimu itupayo maarifa na kuboresha ujuzi wa mtu haishii darasani tu kwenye elimu rasmi hapatana,...elimu ipo kwenye maeneo mengi, nyumbani, shuleni, kwenye jamii, kwenye majarida, vitabu, video, maandiko tofauti kwa maana ya makala, nyimbo, maïgizo nk.
Watu wengi tumekosa mambo mengi kwa sababu ni wavivu wakusoma, kuna msemo unasema ukitaka kumficha jambo Mtanzania jambo hilo weka kwenye maandishi ni hatari sana...
Maarifa hubadilisha fikra mgando, huibua talanta na kufungua hazina ya fursa zilizojificha. Hivyo tupende kuwa na kawaida yakujifunza kupitia kusoma vitabu nk, kwa lengo la kujiongezea maarifa ambayo yatatusaidia kwa matumizi ya sasa na baadae.
Mgema Moses
mgemamoses@gmail.com
0715366003,0755632375

No comments:

Post a Comment