Saturday, January 30, 2021

TAFUTA KUWA BORA NA SIO BINGWA

Unapotafuta kufika kwenye hatima ya ndoto au malengo yako kwenye kichwa chako huwa unawaza swali gani kati ya haya mawili.......
1. Kuwa bingwa ?
2.Kuwa bora.. ?
Kati ya haya maswali mawili kila mtu ana majibu yake katika ufahamu wake. Katika ulimwengu tunaoishi leo, watu wengi wamelazimisha kuwa mabingwa ili kupokea tuzo na sifa kedekede kwa sababu tu ya ile taji ya ubingwa juu ya jambo fulani ambalo alikuwa ana ndoto au shauku nalo.

Watu wengi wamekuwa wahanga wakutafuta tuzo, vyeti na heshima fulani ïlï kuongeza hadhi kwenye jamii zao. Jambo hïli limekuwa likiathili sana mifumo ya elimu kwa wanafunzi wa ngazi zote katika shule na taasisi zingine za elimu ya kati na juu, wafunzi na wanavyuo wengi wanakuwa na bidii ya kuhakikisha wanakuwa na matokeo bora ya mwisho wa kozi zao, mtoto hasomi wakati akiwa form one akifika form two atakazana sana ili asifeli kipimo cha kidato cha pïli atatafuta past papers, atakwenda kila chimbo kutafuta sio uelewa bali material yatakayomfanya kufaulu na kuingia ngazi inayofuata.

Mchakato huo upo kidato cha nne, cha sita hata ngazi ya vyuo vya kati na vikuu, watu wanahudhuria darasani ili kufanya Quiz, assigments na mitihani yakukamilisha kozi zao, akishakamilisha mchakato wa kozi tukutane UE hapo ndiyo zima moto inaanza, kichwani hakuna maarifa wala ujuzi wowote ila watu wanatazama joho la siku ya mwisho, watu wengi wanataka ubingwa hata kama ni wakununua kwa fedha bila jasho, wapo tayari kutoa fedha sio jasho kwa maana yakutafuta kuwa bora.
Watu wanataka kuwa matajiri kwa kubeti, watu wanakutana kimwili kabla ya ndoa na ndoa bora wanazitaka hapo kesho wakati hawataki kufuata misingi sahihi itakayowafanya kuwa na ndoa bora na zenye maadili ya Kimungu, changamoto sana.

Leo tuna watu wenye degree, masters, PhD na hata maprofesa ambao tuzo zao haziendani na uwezo, maarifa na ujuzi ambao uko kwenye fahamu zao, lakini vyeti vina 1st, 2nd na 3rd classes za GPA toka vyuo vikubwa nchini.
Sikushangaa sana marehemu Ruge Mtahaba, Majizo na makampuni mengine yalipoamua kujiongeza nakuondoka kwenye usaili wa kawaida, kuajili vyeti vilivyobebwa na watu wenye uwezo mdogo hata wakutetea vyeti vyao...swali hili limefanya wasomi wengi kuangushwa na watu wa darasa la sababu na wenye elïmu ya kati hasa kwenye vyombo vya habari, wasomi hawezi basi hata kuwa na wazo jipya, basi kuboresha an existing Ideas.....swali kama hïli ni mwiba kwa wasomi wengi, unafikiri una nini cha ziada ukiacha ukubwa wa eĺimu na GPA yako, utatufanyia nini ambacho hata tukikulipa mshahara hatutaumia maana utakuwa umezalisha na sehemu ya ulichozalisha tukafanya malipo yako ya mwezi ?.... Huwezi laumu
Hadhi zakuwa mabingwa, kusifiwa mtaani umeondoka na div 1, div 2 na div 3 hata four umeïtafsiri vipi kwenye uhalisia wa maisha ya kawaida, ni kweli mifumo ya elimu ina changamoto yake lakini ndiyo iliyonipa hata huu uwezo wa kuandika maana yake bado ni bora na inaweza kututoa hapa tulipo.

Watanzania wengi tumekuwa ni watu wa zima moto, final touches hatutaki michakato yenye tija ambayo inaweza kutufanya kuwa mabingwa wenye ubora ndani yake, kifupi vyeti na tuzo zetu zisadifiwe na uwezo wa utendaji wa kazi kwa vitendo ili watu waipe thamani na umuhimu wa elimu nakuondoa kejeli za wasio na elimu.
Tujikite kwenye kutafuta ubora zaidi kuliko nishani za heshima ambazo hazina maana yeyote kama hazitafisiri uhalisia katika vitendo vyetu.

Niliwahi kusoma vitabu vya watu wawili walio wahi kufanya kazi na staa wa mpira duniani Cristiano Ronaldo mmoja wao ni Sir Alex Ferguson alïkuwa kocha wa Staa huyo, Carlos Tevez mchezaji mwenzake na Ronaldo pale Man utd, wanasema Ronaldo hakuwahi kutafuta kuwa bingwa bali alitafuta ubora ambao uliongeza ufanisi wake katika kucheza mpira, walisema pamoja na mafanikio na kiwango bora hata sasa lakini amekuwa akiamka mapema sana kukimbia na kufanya mazoezi, Tevez alijitahidi kuwahi mapema zaidi lakini alimkuta Ronaldo yuko uwanja wa mazoezi na baada ya mazoezi ya timu alibaki kucheza faulo lengo alikuwa akitafuta ubora.
Ronaldo amekuwa kwenye utawala wa mtoto mwenye kipaji sana Leo Messi na aliyekuwa akibebwa kwa kiasi kikubwa na sababu za kibiashara za makampuni ya Adidas na Nike, utawala wa Fifa kipindi hicho na kamati yake kuonyesha upendeleo wa wazi kwa Messi hata aliposhuka kiwango na kuzidiwa na Ronaldo.
Lakini Ronaldo alijikita kwenye kutafuta ubora ambao ndiyo umekuwa ukimpa ufanisi wa kazi yake ambayo mwisho wa siku walishindwa kuzuia ubingwa wa Ronaldo na Ronaldo ni  bingwa sio kwa mbeleko bali kwa kazi na ubora wake.
Historia ya Mbwana Samatta kati ya vijana wakitanzania ambao wameamua kuishi nje ya mfumo wa maisha ya vijana wengi wa kitanzania, kabla yakuwa bingwa aliamua kutafuta ubora ambo ulikuwa ni sababu ya yeye kuhitajika na vilabu vingine, alicheza Simba sehemu ambayo tayari alishafikia kiwango chakujivika ubingwa na heshima ila alikubali kwenda Tp Mazembe kuendelea kujitafuta zaidi ya vile alikuwa akiwa simba, muda ulipofika ubora ulimtambulisha, leo ukifika Lubumbashi jina la Samagoal sio geni kwa mashabiki wa mpira pale DRC nenda Genk pale ubelgiji Samatta anaimbwa na wazungu 
Chanzo cha yote Mbwana alikataa kuwa bingwa kwa kupewa sifa au kutafuta sifa toka nyumbani bali aĺijitahidi kutafuta ubora kwa matumizi ya kesho. 
Nimetumia mifano mingi ya wasomi na wacheza mpira lengo ikiwa nikueleweka vyema zaidi nakuipata poïnt na lengo la kuandika andiko hili.
Tuache Kukimbilha nishani, tuzo na vyeti bali tutafute ubora, bora uwe na wastani wa kati katika vyeti lakini katika utendaji uwe na GPA ya kwanza ndiyo maana halisi ya kuwa bingwa.
We are not supposed to be bĺinded with medals and rewards let us strive for Quality & better
Mgema Moses
0715366003

No comments:

Post a Comment