Sunday, January 31, 2021

Kila hatua ya ukuaji huanza na mbegu kufa na kuoza, ndipo inaanza mchakato wakuchanua tena. Mfano mzuri uko kwenye upandaji wa miti, mbegu hufukiwa ardhini na kufuata hatua zote zinazotakiwa kufuatwa ili mmea tarajiwa ukue kwa kupitia njia sahihi ukiwa umepokea na kupitia mchakato sahihi wa ukuaji na hatimae matunda.
Mti ambao utakuwa na matunda bora yanaweza kuuzika kwenye soko la ndani lakini hata kwenye soko la kimataifa kutokana nakupitia mchakato sahihi ambao huleta ustawi wenye manufaa.
Niliwahi kuhudhuria semina moja ambayo 

Saturday, January 30, 2021

TAFUTA KUWA BORA NA SIO BINGWA

Unapotafuta kufika kwenye hatima ya ndoto au malengo yako kwenye kichwa chako huwa unawaza swali gani kati ya haya mawili.......
1. Kuwa bingwa ?
2.Kuwa bora.. ?
Kati ya haya maswali mawili kila mtu ana majibu yake katika ufahamu wake. Katika ulimwengu tunaoishi leo, watu wengi wamelazimisha kuwa mabingwa ili kupokea tuzo na sifa kedekede kwa sababu tu ya ile taji ya ubingwa juu ya jambo fulani ambalo alikuwa ana ndoto au shauku nalo.

Watu wengi wamekuwa wahanga wakutafuta tuzo, vyeti na heshima fulani ïlï kuongeza hadhi kwenye jamii zao. Jambo hïli limekuwa likiathili sana mifumo ya elimu kwa wanafunzi wa ngazi zote katika shule na taasisi zingine za elimu ya kati na juu, wafunzi na wanavyuo wengi wanakuwa na bidii ya kuhakikisha wanakuwa na matokeo bora ya mwisho wa kozi zao, mtoto hasomi wakati akiwa form one akifika form two atakazana sana ili asifeli kipimo cha kidato cha pïli atatafuta past papers, atakwenda kila chimbo kutafuta sio uelewa bali material yatakayomfanya kufaulu na kuingia ngazi inayofuata.

Mchakato huo upo kidato cha nne, cha sita hata ngazi ya vyuo vya kati na vikuu, watu wanahudhuria darasani ili kufanya Quiz, assigments na mitihani yakukamilisha kozi zao, akishakamilisha mchakato wa kozi tukutane UE hapo ndiyo zima moto inaanza, kichwani hakuna maarifa wala ujuzi wowote ila watu wanatazama joho la siku ya mwisho, watu wengi wanataka ubingwa hata kama ni wakununua kwa fedha bila jasho, wapo tayari kutoa fedha sio jasho kwa maana yakutafuta kuwa bora.
Watu wanataka kuwa matajiri kwa kubeti, watu wanakutana kimwili kabla ya ndoa na ndoa bora wanazitaka hapo kesho wakati hawataki kufuata misingi sahihi itakayowafanya kuwa na ndoa bora na zenye maadili ya Kimungu, changamoto sana.

Leo tuna watu wenye degree, masters, PhD na hata maprofesa ambao tuzo zao haziendani na uwezo, maarifa na ujuzi ambao uko kwenye fahamu zao, lakini vyeti vina 1st, 2nd na 3rd classes za GPA toka vyuo vikubwa nchini.
Sikushangaa sana marehemu Ruge Mtahaba, Majizo na makampuni mengine yalipoamua kujiongeza nakuondoka kwenye usaili wa kawaida, kuajili vyeti vilivyobebwa na watu wenye uwezo mdogo hata wakutetea vyeti vyao...swali hili limefanya wasomi wengi kuangushwa na watu wa darasa la sababu na wenye elïmu ya kati hasa kwenye vyombo vya habari, wasomi hawezi basi hata kuwa na wazo jipya, basi kuboresha an existing Ideas.....swali kama hïli ni mwiba kwa wasomi wengi, unafikiri una nini cha ziada ukiacha ukubwa wa eĺimu na GPA yako, utatufanyia nini ambacho hata tukikulipa mshahara hatutaumia maana utakuwa umezalisha na sehemu ya ulichozalisha tukafanya malipo yako ya mwezi ?.... Huwezi laumu
Hadhi zakuwa mabingwa, kusifiwa mtaani umeondoka na div 1, div 2 na div 3 hata four umeïtafsiri vipi kwenye uhalisia wa maisha ya kawaida, ni kweli mifumo ya elimu ina changamoto yake lakini ndiyo iliyonipa hata huu uwezo wa kuandika maana yake bado ni bora na inaweza kututoa hapa tulipo.

Watanzania wengi tumekuwa ni watu wa zima moto, final touches hatutaki michakato yenye tija ambayo inaweza kutufanya kuwa mabingwa wenye ubora ndani yake, kifupi vyeti na tuzo zetu zisadifiwe na uwezo wa utendaji wa kazi kwa vitendo ili watu waipe thamani na umuhimu wa elimu nakuondoa kejeli za wasio na elimu.
Tujikite kwenye kutafuta ubora zaidi kuliko nishani za heshima ambazo hazina maana yeyote kama hazitafisiri uhalisia katika vitendo vyetu.

Niliwahi kusoma vitabu vya watu wawili walio wahi kufanya kazi na staa wa mpira duniani Cristiano Ronaldo mmoja wao ni Sir Alex Ferguson alïkuwa kocha wa Staa huyo, Carlos Tevez mchezaji mwenzake na Ronaldo pale Man utd, wanasema Ronaldo hakuwahi kutafuta kuwa bingwa bali alitafuta ubora ambao uliongeza ufanisi wake katika kucheza mpira, walisema pamoja na mafanikio na kiwango bora hata sasa lakini amekuwa akiamka mapema sana kukimbia na kufanya mazoezi, Tevez alijitahidi kuwahi mapema zaidi lakini alimkuta Ronaldo yuko uwanja wa mazoezi na baada ya mazoezi ya timu alibaki kucheza faulo lengo alikuwa akitafuta ubora.
Ronaldo amekuwa kwenye utawala wa mtoto mwenye kipaji sana Leo Messi na aliyekuwa akibebwa kwa kiasi kikubwa na sababu za kibiashara za makampuni ya Adidas na Nike, utawala wa Fifa kipindi hicho na kamati yake kuonyesha upendeleo wa wazi kwa Messi hata aliposhuka kiwango na kuzidiwa na Ronaldo.
Lakini Ronaldo alijikita kwenye kutafuta ubora ambao ndiyo umekuwa ukimpa ufanisi wa kazi yake ambayo mwisho wa siku walishindwa kuzuia ubingwa wa Ronaldo na Ronaldo ni  bingwa sio kwa mbeleko bali kwa kazi na ubora wake.
Historia ya Mbwana Samatta kati ya vijana wakitanzania ambao wameamua kuishi nje ya mfumo wa maisha ya vijana wengi wa kitanzania, kabla yakuwa bingwa aliamua kutafuta ubora ambo ulikuwa ni sababu ya yeye kuhitajika na vilabu vingine, alicheza Simba sehemu ambayo tayari alishafikia kiwango chakujivika ubingwa na heshima ila alikubali kwenda Tp Mazembe kuendelea kujitafuta zaidi ya vile alikuwa akiwa simba, muda ulipofika ubora ulimtambulisha, leo ukifika Lubumbashi jina la Samagoal sio geni kwa mashabiki wa mpira pale DRC nenda Genk pale ubelgiji Samatta anaimbwa na wazungu 
Chanzo cha yote Mbwana alikataa kuwa bingwa kwa kupewa sifa au kutafuta sifa toka nyumbani bali aĺijitahidi kutafuta ubora kwa matumizi ya kesho. 
Nimetumia mifano mingi ya wasomi na wacheza mpira lengo ikiwa nikueleweka vyema zaidi nakuipata poïnt na lengo la kuandika andiko hili.
Tuache Kukimbilha nishani, tuzo na vyeti bali tutafute ubora, bora uwe na wastani wa kati katika vyeti lakini katika utendaji uwe na GPA ya kwanza ndiyo maana halisi ya kuwa bingwa.
We are not supposed to be bĺinded with medals and rewards let us strive for Quality & better
Mgema Moses
0715366003

Friday, January 29, 2021

KIPAJI NI BORA, ELIMU NI MUHIMU JUU YA KIPAJI.

Nimekuwa napenda sana kusoma quotes ya Albert Einstein ambayo inasema ''Everybody is a genius. But if you judge a fish by it's ability to climb a tree, it will live it's whole life believing that it is stupid'' 
Naupenda sana msemo kwa sababu ni elimu na somo tosha kwa jamii ambayo imekuwa ikiishi maisha ya kukariri pasipokujua kuwa maisha ya mtu tangu mwanzo yalijengwa kwenye msingi wa kutembea kwenye channel ya kipaji chake.
Elimu imekuwa ni kificho cha watu wengi, huku pia asilimia kubwa tukiwa hatujui maana na lengo la elimu hasa kwa watoto, vijana na watu wote kwa ujumla. Elimu sio ajira, elimu haikutenganishi na talanta ambayo Mungu aliiweka ndani yako.
Elimu inakipa thamani ambacho tayari kinaishi ndani ya mtu, elimu tunayoipata shuleni, kwenye washa, semina na makongamano ya elimu rasmi na isiyo rasmi ina lengo kutujengea mtazamo mpana zaidi ya ule tunaokuwa nao kabla yakupata elimu hiyo.
Elimu ni mkusanyiko wa maarifa na ujuzi wa mambo mengi ambayo yanatugawanya na kila mtu kujigundua kuwa mimi ni wa sehemu au niko kundi gani. Changamoto kubwa imekuwa kwa wazazi na walezi kuwalazimisha watoto kufanya vitu ambavyo katu hata kama angekesha kusoma usiku kucha hawezi kuwa unavyotaka wewe mzazi au mlezi, mwisho wa siku atafeli nakuichukia shule .
Nimeandika makala hii baada ya ijumaa kumwona mtoto wa miaka nane, Juh Juh Ruge Mtahaba akifanyiwa mahojiano katika kituo cha redio clouds, namna anavyojielezea wakati anawasilisha kipindi cha watoto cha Smart Bees, unaona ambavyo mzazi alivyo karibu na mtoto na kufuatilia nini amebeba ndani yake ndiyo maana anaanza kumsogeza karibu na mahali ambapo anaweza kukifanya kipaji chake kuanza kuonekana vyema, mtoto yule sio kama hasomi ana soma lakini elimu yake imejikita zaidi katika kuboresha na kuinua kipaji chake vyema.
Tumekuwa na changamoto kama jamii ya watanzania na mgawanyiko mkubwa ndani yake, wakati vijana asilimia kubwa wakiamini kipaji pekee ndiyo suluhisho la wao kutoka kimaisha, wazazi wengi wanaamini njia pekee yakumfanya mtoto kutoka kimaisha nikusoma ili aajiriwe, vijana wamewekeza nguvu maana wanaona wasomi wengi hawana na ajira hivyo kudiriki kusema kuwa elimu imeshuka thamani.
Kipaji ni muhimu, ila elimu ni muhimu zaidi kwa sababu inakufanya kujitambua, kujua namna yakukipa thamani kipaji chako, namna yakufanya branding, kujiweka kwenye masoko, hata kama una watu wanakusimamia ni rahisi kujua mchakato wa mikataba maana elimu ipo.
Wazazi tubadilishe mtazamo juu ya elimu tunayopata kuwa sio kila unaempeleka shule lazima apate ajira serikalini bali elimu ifanyike kuwa mtaji wa kwanza kwenye kuelekea ndoto ya kijana au mtoto wako.
Tukiendelea kuwalazimisha watoto kufanya yaliyo matakwa yetu, tutakuwa tukiihalalisha kwa viteńdo kauli ya Albert Einstein ya samaki kushindwa kupanda mtini, nakubaki kuamini kwamba yeye ni mpumbavu, kumbe amevamia eneo ambalo sio eneo aliloumbiwa kuwa bora.
Elimu ni mhimu sana ila, kipaji ni chanzo kikubwa cha ajira na utajirh, vyote tutembee navyo, kipaji isibaki kama mbadala wa watu walioshindwa shule au watu masikini.
Open your mind
Mgema Moses
0715366003

Wednesday, January 20, 2021

MAARIFA NI DIRA YA MWELEKEO SAHIHI.

Maarifa ni ufunguo, maarifa ni daraja laini(soft bridge), Ni ufunguo kwa sababu kupitia maarifa tunafahamu mambo mengi ambayo yamefungiwa kwenye hazina mbalimbali katika dunia yetu na kwetu pia kama watu...
Maarifa ni daraja kwa sababu kabla ya kuwa na ufahamu wa jambo fulani mara nyingi tumeishi kwenye giza, lakini baada ya kupata maarifa kuna vitu vingi vimerahisishwa sana tofauti na hapo kabla yakupata maarifa yakutuvusha kwenda ng'ambo ya upande ambao tulikuwa hatuna namna yakuwaza kama inawezekana lakini baada ya maarifa imekuwa rahisi kufika huko.
 Kabla ya ukoloni wazee wangu pale mwadui walichukua almasi nakuchezea kama kete za bao, mzungu alikuja na golori nakuwarubuni wazee wangu hao, akawaaminisha kuwa golori ni bora zaidi ya almasi, wakavutiwa na mng'ao wa golori wakaona Almasi haifai, Mzungu akachukua mali wazee wakabaki na na golori kwa furaha najua moyoni walisemezana hawa wajinga tumewala, kumbe wao ndiyo waliliwa, hakika wajinga ndio waliwao. Ujinga sio tusi bali ni kukosa ufahamu juu ya jambo fulani, hata mimi ni mjinga wa mambo ambayo sina ufahamu nayo.
Huwezi kuwalaumu wale wazee kwa kuibiwa namna ile ilitokea hivyo kwa sababu hawakuwa na ufahamu juu ya hivyo vitu viwili kwa wakati huo, wakakutana na wajanja wenye uelewa, ufahamu ambao ulitokana na maarifa vichwani mwao, waliojua thamani ya almasi zaidi ya wazee wangu.
Biblia iko wazi inasema kuwa watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa, ni kweli bila maarifa ni ngumu kujigundua binafsi, kugundua fursa zinazotunguka, ni ngumu kupiga hatua, itakuwa ni kawaida kutumia nguvu nyingi kwenye jambo linalohitaji akili na uelewa mdogo tu...
Pasipo maarifa wazee wetu wamelala kwenye yadi za mashamba yetu wakiwa masikini, wameacha utajiri wa mifugo kwenye mazizi mengi, huku wengi wao walikuwa marafiki wa nyumba duni za majani, kulala kwenye ngozi nakula vyakula duni wakati utajiri umelala kwenye himaya zao.
Vipaji vingi vimekufa bila kutumika kwa sababu tulikosa maarifa yakuviendeleza nakuvigeuza kuwa mitaji ambayo ingetuletea utajiri na ajira zakutosha, .. Maarifa, Maarifa ni ufunguo
Bila maarifa tusingekuwa na ndege leo, meli, lami, madaktari bingwa, wahandisi wa majengo yanayopendeza kule Dar es salaam, bila maarifa tungewezaji kupita juu ya maji kama Petro, tungewezaje kupaa angani kama mwewe, bila maarifa tungewezaje kutunza kumbukumbu ya picha, video ya matukio tunayoyafanya katika kizazi hiki, tungejuaje historia ya kule tumetoka, kamera zemetusaidia kupata hifadhi ya matukio ya nyuma kwa manufaa ya kesho.
Matokeo ya haya yote ni zao la maarifa. Maarifa haya yanapatikana wapi ?
Mtu mmoja nilimsikia akisema elimu haina faida tena kwa sababu watu wanamaliza vyuo hata kazi hawapati wanarudi kuuza nyanya kwenye masoko na magenge ya mitaani huko mbagala, keko, kuuza supu ya mapupu huko vingunguti kati ya soko maarufu la mbuzi kutoka Dodoma huko Dar es salaam, nilitamani kushawishika kuwa ni kweli, lakini nikakumbuka tena kuwa Biblia inanikumbusha kwa habari ya Kumkamata sana Elimu nisimwache aende zake...nikashtuka kidogo, mshtuko wangu ukanikumbusha kuwa watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa, kwa stori za yule ndgu yangu, kama nisingekuwa nimepitia ule mstari wa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hakika ningeangamia maana ningemwamini bila kupinga ila kwa sababu nïĺïkuwa na maarifa nïliepuka muangamio mkubwa wa mawazo finyu na mgando toka kwa yule ndugu.
HAYA MAARIFA YANATOKA AU KUPATIKANA WAPI....
Elimu ni chanzo cha maarifa na ndio kiboreshaji cha juzi mbalimbali ambazo Mungu alituzawadia mfano vipaji mbalimbali katika michezo, kuimba, burudani, kwenye ufundi wa vitu mbalimbali ambavyo ni hard na soft skills.
Elimu itupayo maarifa na kuboresha ujuzi wa mtu haishii darasani tu kwenye elimu rasmi hapatana,...elimu ipo kwenye maeneo mengi, nyumbani, shuleni, kwenye jamii, kwenye majarida, vitabu, video, maandiko tofauti kwa maana ya makala, nyimbo, maïgizo nk.
Watu wengi tumekosa mambo mengi kwa sababu ni wavivu wakusoma, kuna msemo unasema ukitaka kumficha jambo Mtanzania jambo hilo weka kwenye maandishi ni hatari sana...
Maarifa hubadilisha fikra mgando, huibua talanta na kufungua hazina ya fursa zilizojificha. Hivyo tupende kuwa na kawaida yakujifunza kupitia kusoma vitabu nk, kwa lengo la kujiongezea maarifa ambayo yatatusaidia kwa matumizi ya sasa na baadae.
Mgema Moses
mgemamoses@gmail.com
0715366003,0755632375

Tuesday, January 19, 2021

MCHAKATO NDIYO MAFANIKIO SIO MATOKEO.

 watu wengi tumekuwa wahanga wa matokeo ya mwisho yanayoonekana kwa macho, tunazungumzia kwa kina na kupongeza kwa sababu tunamwona mtu akiwa na fedha nyingi, akimiliki nyumba, biashara na vitu vingine kama kazi nzuri.
Mara nyingi tumekuwa wagumu wakufuatilia chanzo cha mafanikio ya mtu alikoanzia, sio kila matokeo yanapaswa kupongezwa, jua chanzo kïlichomfanya kuwa hapo juu, ni kweli tunapaswa kupongezana pale mtu anapofanikiwa au kufanya vizuri lakini pongeza panapostahili kupongeza, mtu amepambana mpaka ametusua maisha,amekuwa na bidii yakusoma na mwisho wake amefanya vizuri, hivyo pongeza bidii na mchakato unaoambana na uvumilivu ambao umeleta matokeo yanayoonekana.
Usipende kumpongeza mtu kwa kuona matokeo ambayo hata hujui matokeo yale yametokana na nïni, kuna watu wana maisha mazuri kwa sababu yakuiba, kuna watu wamefaulu mitihani kwa kuigia na ukimwambia mtu yule ufaulu wa kwenye karatasi apeleke kwenye utendaji unakuwa ziro.
Mafanikio bora ni yale yanayopikwa kuanzia chini kwa kufuata misingi na mchakato sahihi ambayo siku ikionekana kwa macho inakuwa ni reflection ya mafanikio ambayo yameleta matokeo yanayoonekana kwa macho ya wengi.
Mafanikio ya ndoa sio kile kicheko kionekanacho kwenye nyuso za wanandoa no, mafanikio yao ni namna ambavyo kila mtu amempokea mwenzake nakuamua kustiliana na kubeba kwenye madhaifu na uimara nakuhesabiana kuwa bora kwa kila mtu
Ukiona timu ya mpira inapata matokeo bora kiwanjani, fahamu hayo ni matokeo ya mafanikio ya uwekezaji, na kupitia mchakato sahihi kwa kutengeneza mseto mzuri kuanzia utawala, team management, coaching stuff, wachezaji na timu nzima kwa ujumla, kionekanacho uwanjani ni matokeo ya mafanikio nyuma ya pazia.
ukiona matokeo bora kwenye biashara, fahamu akili ilifikiri vyema sana na kupeleka kwenye mawazo hayo kwenye karatasi na baadae kwenye utekelezaji.
Usipende kumpongeza mtu kwa matokeo yaonekanayo kwa sababu hujui matokeo hayo yametokana na mchakato sahihi au usio sahihi tujifunze Kupongeza mchakato ulisababisha matokeo yanayoonekana sio matokeo ambayo wakati mwingine huja bila kupitia njia na mchakato sahihi.
UKIONA  KOBE AMEINAMA FAHAMU TU KUWA ANATUNGA SHERIA,....
Mgema Moses

Monday, January 18, 2021

MTI WENYE MATUNDA UNAPIGWA MAWE

Watu wengi tumekuwa na kasumba ya kutokupongeza jitihada za wenzetu kwa maana ya vijana wenzetu na watu wazima ambao wamepiga hatua za maendeleo kwa kiasi fulani. Unakuta watu wanapiga stori kwenye vijiwe wakisema mtu yule anajisikia sana, amekuwa na roho mbaya, anatupita bila kutusalimia wakati jamaa wakati bado hajatoboa alikuwa mwana kinyama.
Wengine wanaanza kutengeneza scenario za kuwa hata mafanikio yake sio halali, haiwezekani atoboi kirahisi hivi itakuwa amejiunganisha na mambo ya freemason, atakuwa amewatoa ndugu zake sadaka na nk.
Yote yananenwa kwa sababu ya chuki, roho isiyokubali na kuamini kuwa mapambano ya maisha yanaweza kumpa hatua mtu kufikia malengo na ndoto zake. Bahati mbaya sana akifanikiwa Mtanzania ndio itakuwa habarï kubwa yakusemwa kwa mtazamo hasi, tumewaona wanamuziki wetu hapa nchini wamepambana wameutoa muziki kwenye vumbi lakini unakuta kuna mtu yuko swekeni huko anamponda anamsema vibaya, wakati huo huo anamsifia mwimbaji wa Nigeria, USA na nchi zingine kama vile wanawafahamu sana...
Hii inatokea kwenye maeneo yote kwenye maisha yetu, iwe kwenye biashara nje na muziki, madukani, kwenye soka, kwenye mafanikio ya dini zetu hasa watumishi wa Mungu, kwenye siasa, kwenye kazi za maofisini na maeneo mengine, utakuta watu wanasema huyu asingekuwa baba yake asingekuwa hapo, sasa tujiulize baba yako angekuwa kwenye nafasi ya kukunyanyua asingefanya ivo. Na asipofanya hivyo si ataonekana mpuuzi na asiye na akili.
Ukiona unaandamwa sana na maneno jua wewe una kitu cha ziada, watu wakawaida huwa hawazungumzwi maana hawana kitu chakuwafanya watu kuwazungumzia.
Huwezi kwenda kuchuma matunda kwenye mchongoma, na shida ya mchongoma kama mti una faida moja au mbili ambazo pia utazipata kwenye mchungwa, mwembe, mpera na mpeazi pia, unatoa kivuli labda na mbao ambazo pia sio mbao bora, kumbuka pia mwembe na miti mingine inatoa kivuli na mbao ambazo zinaweza zisiwe bora pia ila inatoa.
Sasa kama una sifa za mchongoma nani atakuzungumzia, maana sifa ulizo nazo kila mtu anazo, sifa za kawaida. lakini mti wa matunda unapigwa mawe kwa sababu una sifa ya ziada, wakati wa jua, wakati wa mvua na wakati wa hali zote watu wataufikia ule mti, watakula matunda, watajikinga mvua au jua nk.
Ndivyo ilivyo kwa watu wenye sifa za ziada, watasemwa vibaya vijiweni, wakipewa tuzo huko mataifani watapokelewa kwa nderemo na vifijo, kila mmoja atajifanya anampenda huyo shujaa.
Hivyo basi ni vyema kuilinda miti yenye matunda maana inatufaa sote, wapo watu wameajiliwa kupitia mafanikio ya mtu ambae ametutangulia, mfano mzuri ni Diamond ni zaidi ya familia hata hamsini wanakula kwa sababu ya matunda ya kazï yake. Hakika mti wenye matunda hupigwa mawe
Mgema Moses
mgemamoses@gmail.com

Thursday, January 14, 2021

VITO VYA THAMANI HAVIPATIKANI KIRAHISI.

Kuna changamoto vijana au watu wengi tumekuwa tukiitengeneza mwisho wa siku imepunguza sana thamani ya watu wengi.
Mtu anaenda ametuma maombi ya kazi mahali, ana elimu na sifa zote zinazotakiwa na waajili, lakini cha ajabu mtu akiitwa kwenye usahili badala yakuwasilisha ubora wake kila anapoulizwa swali basi unakuta anapoteza hali ya kujiamini, anatetemeka, anajibu maswali kwa kuonyesha sura yakutaka kuhurumiwa, akiulizwa unataka tukupe mshahara wa kiwango gani basi anataja kiwango cha chini kabisa ili aonekani hapendi hela, weee watu hawakuchukui kwa sababu umetaja dau dogo, wanachukua ubora wako, ukitaja mshahara mkubwa na unasifa kwanza lazima huyu mtu hana njaa, anajielewa, na anajua thamani yake hivyo lazima wakuchukue mshahara mtajadiliana tu baadae.
Namna utakavyojirahisha ndivyo thamani yako itakavyokuwa chini, hata kama utapata kazi bado wanauwezo wa kukufanya chochote wanataka, sio kwa sababu huna uwezo au bora hapana, una uwezo na ubora ndiyo maana wamekuchukua changamoto namna ambavyö ulijiwasilisha kwa ile mara ya kwanza ndiyo maana wanakufanya wanavyotaka.
Ni kweli wakati wakutafuta maisha hasa kama umetokea maisha duni, umepigika kweli kweli unalazimika kusema ndiyo hata kwenye uonevu lengo nikuitumikia ile kauli isemayo mtumikie kafiri ili mradi mkono unaenda kinywani, hapana jaribu kuheshimu taratibu na kanuni za ofisi ila usijishushe thamani yako.
Kuna watu wana mawazo mazuri, na watu wengi wameyakubali baada yakuyapitia ni mawazo ya miradi mikubwa, bishara kubwa nk., lakini namna ya uwasilishaji wa mawazo hayo basi unajikuta uliopelekea idea hiyo wakuone wewe njaa na kupitia njaa yako basi unatoa mwanya kwao kuishusha thamani ya wazo lako, sababu ulitengeneza unyonge hata kabla. 
Ndiyo maana wahenga walisema, umaridadi huficha umasikini na matatizo yako, jaribu kwa kila hali kuiona thamani yako mbele ya watu unao amini wanaweza kuwa daraja la kwako kusogea mbele zaidi kuelekea ndoto zako.
Joel Nanauka mwandishi wa kitabu cha timiza malengo aliwahi kusema: kuna siku alitakiwa kwenda ofïsi moja kubwa jijini Dar es salaam, katika ile ofisi sio mkurugenzi wala wafanya kazi wengine ambao walimfahamu bwana Joel, siku ya mafunzo ilifika na viongozi wa kampuni walijipanga kumpokea cha ajabu walikutana na mtu ambae hawakumtegemea kabisa kutokana na mwonekano wake, umbo dogo, yuko simple sana, na waĺitegemea kuona V-8, mtu mkubwa sana katika mwili. Kwa kweli mwonekano wake ilikuwa dissapointment kubwa sana, mkurugezi alikataa kuwa sie mkufunzi na ilibidi yatengenezwe mazingira kule ndani ili kuwaanda kisaikolojia washiriki wa washa ile na hii ilikuja baada ya mazungumzo marefu kabla hawajakubali hata kwa shingo upande.
Bwana Joel alijeng Utulivu, kuitambua thamani yake, madini yake na maandalizi yalimpa ujasiri mkubwa na aliamini kitu pekee kinachoweza kumbeba ni uwezo wakuwasilisha mada na mafunzo kwa kiwango cha juu, misukosuko na dhoruba ya kugomewa kuwa si yeye mkufunzi haikumwondoa kwenye lengo la uwepo wake katika ile washa...
Muda ulipofika alipanda kwenye podium kwa ujasiri na nguvu na shauku yakufanya vizuri. Baada ya mafunzo kilichobaki ni historia na kila mtu anamfahamu joel Nanauka. Joel hakuwa yule waliyemwona katika umbo dogo, bali alikuwa ni Nanauka mwenye umbo kubwa sana ndani yake.
Una nafasi yakuwa prove wrong wale wanaokuona wewe ni mnyonge, sio kwa kuwalazimisha bali kwa thamani yako. Be you, create confidence, create your trust to the majority by making it to the maximum
Híi anaapply kwenye maisha yote mfano heshima ya mke ni namna ambavyo ulijiposition wakati umefuatwa na mwanaume,....Thamani yako ilipanda au ilishuka baada yakukutana na mtu kwa mara ya kwanza. Jenga heshima yako hata kama unahitaji jambo present yourself in a high value ili kesho mtu asiseme kuwa huyu mtu yuko hapa kwa kuwa alihurumiwa.
Tujifunze kwa mawe ya thamani, dhahabu, Almasi, Tanzanite, na madini mengine hayapatikani kirahisi wachimbaji hutoka jasho na damu ili kuyapata sio kirahisi. Ni mawe lakini thamani yake imekuwa juu kutokana na namna ya upatikanaji.
Fedha ina thamani kubwa kwa sababu sio kila mtu anaweza kuitengeneza, na ili uweze kuipata lazima upambane sana ndiyo uipate.
Hivyo ijenge thamani yako kutokana na kile unachomiliki, kama unakipaji basi kifanye kuwa na thamani.
Mgema Moses

Sunday, January 10, 2021

IFANYE JTATU YAKO IMARA KWA KUMALIZA WIKI NA FAMILIA YAKO.

Jumatatu ni siku ya kwanza ya wiki, ni siku ambayo huja baada ya mapumziko ya weekend. Siku hii huamliwa na namna ambavyo weekend uliimaliza. Kuna watu huitumia weekend kwa kukaa na familia, kucheza na watoto, ni siku ambayo hata kama atakuwa na kazi za hapa na pale lakini hujitahidi angalau kuwepo nyumbani mapema tofauti na siku za week, atakaa na watoto, atasikiliza kero na changamoto zao, atacheza na watoto, lakini ni muda mzuri wa tabasamu na mke au mume nk.
Jumapili inakuwa ni siku bora sana kwa ajili ya ibada, kumshukuru Mungu kwa kumvusha salama katika wiki inayoisha, kurudisha utukufu Mungu, na kutimiza wajibu wa ibada kama ambavyo ni utaratibu wa Mungu ulivyo, fanya kazi siku sita halafu siku ya saba, itakase maana ni sabato ya Bwana, ni siku muhimu sana.
Wengine siku hizi mbili huzitumia kwa kufanya mambo sio mazuri, kulewa na mambo ambayo yanageuka kuwa kero kwa familia na jamii kwa ujumla. Badala ya kutimiza angalau asilimia kadhaa zakukaa na watoto nyumbani au basi kutoka nao out, mtu anachagua kwenda kula maisha bar na kuwanyima watoto fursa yakuwa pamoja angalau kwa siku moja, ambayo ukiitazama vyema inaweza kuwa inajenga afya ya familia na furaha kwa watoto.
Tuko na mambo mengi kutokana na ulimwengu ulipofikia sasa, mambo mengi na yanamtaka kila mmoja kupambana, lakini bado tunawajibu kama wazazi kuwapa muda angalau wa wasaa kadhaa watoto wetu na familia kufurahia pamoja nasi.
Na hii huleta tabasamu na furaha kwa watoto kwa kuwa pamoja na baba pamoja na mama. Furaha ya watoto ni maombi tosha ya kufanikiwa kwako nakuwa na wiki yenye amani, furaha na shauku ya kutimïza kila jambo lilïlopo kwenye ratiba yako. Maombi ya watoto huwa na maana na nguvu sana kwa wazazi wao, hawawezi kuomba kama kuomba ila tabasamu na kicheko chao ndiyo maombi yao kwa wazazi wao.
Pata muda na familia yako ndiyo msingi wa furaha na mafanikio yako, mambo ni mengi lakini kumbuka kuwa familia ni muhimu sana pia kama ilivyo kazi na mambo mengine ya msingi. Ifanye jumatatu yako kuwa ya furaha kwa kuimalïza wiki na familia pamoja na ibada kwa Mungu wako.
Uwe na jtatu ya Baraka za Mungu.
Mgema  Moses
0755632375/0715366003

Friday, January 8, 2021

JENGA MAHUSIANO BORA NA WATU.

Duniani tunaishi kwa kutegemeana kwa 100% either moja kwa moja au kupitia mlango wa nyuma ila kwa kifupi tunategemeana ili kuweza kuishi na kuziishi ndoto na malengo yetu. 
Kila jambo ambalo mtu anabuni, anafanya liwe ni la burudani, kazi serikalini au sekta binafsi, biashara na shughuli nyingine mbalimbali mlengwa huwa ni mtu.
Hivyo basi jaribu kujenga mahusiano mazuri na bora na watu kwa sababu hujui kesho mtu huyo atakufaa kwa jambo gani. Kuna baadhi ya watu wanasema yeye anafuata mambo yake, yeye jambo la kuhusiana vyema na watu kwake anaona sio jambo la muhimu, ni kweli yawezekana kuna mtu unamwona hana faida wala umuhimu sana kwa sasa ila hujui kesho atakufaa kwa jambo gani.
Watu ndiyo wateja wetu katika biashara zetu, watu ndiyo watazamaji wa burudani na michezo tunayofanya kupitia vipawa na vipaji vyetu, tunaajïliwa maofsïni tageti kubwa ni watu, pasipo watu hakuna raisi, hakuna waziri, hakuna mwanachezo, muigizaji,wala mwanamuziki, kwa ufupi hakuna chochote pasipo watu.
Matajiri kwa masikini tunaamka mapema kwenda kwenye mahangaiko ya kila siku anaetafutwa ni mtu ahudumiwe kwa namna yoyote ile.
Hivyo ni vyema kujenga mahusiano bora na kila mtu, usipende kutengeneza uadui usiokuwa na lazima kwa kupitia lugha chafu za matusi, kupigana, fitina na mambo mengine yasio faa, tafuta amani na kama haiwezekani ni bora ukaondoka ili kulinda utu na hadhi yako kwa sababu hujui huyo mtu unaetengeneza nae uadui atakufaa kesho kwa jambo gani. Najua sio rahisi kuishi na watu wote vyema ila jaribu kuepuka kile ambacho kinaweza kuepukika kwa manufaa ya kesho, usitengeneze ugomvi na mteja wako wa kesho, daktari wako, mwalimu wako, mbunge wako, Raisi wako, mpiga kura wako mfanyabiashara wako nk. kwa sababu bado unaishi hujui nani atakufaa kesho.
Mahusiano bora na watu ndiyo msingi wa mafanikio yako kwa sababu bidii, ujuzi, maarifa bila watumiaji wa hayo yote ni kazi bure. 
Mgema  Moses
mgemamoses@gmail.com
0715366003/0755632375

Wednesday, January 6, 2021

CONNECTION...

Katika dunia ya leo kumekuwa na lawama nyingi kwa baadhi ya watu kwamba kuna sehemu walïstahili kuwepo kwa sababu ya sifa na uwezo ambao wanaamini wanao, wanataaluma, uwezo, maarifa na ujuzi katika mambo mbalimbali ambayo bila shaka yanawastahilisha kuwa sehemu fulani.
Changamoto ambayo wengi wanaamini ndiyo imekuwa sababu ya wao kutokuwepo wanapostahili ni ukosefu wa CONNECTION hawana mtu wa kuwavusha na kuwafikisha kwenye nafasi fulani. Changamoto hii imeanza tangu zamani utamsikia mzee anasema mimi nilikuwa na akili sana lakini kutokana na kukosekana kwa shule, kutokana na umasikini wa familia yangu sikwenda shule yawezekana ningekuwa waziri au mtu fulani mkubwa serikalini.
Hali hii imekuwa mwendelezo wa maisha yetu, wengi ambao hatujapata nafasi tunaamini kuwa hatupo kwenye position fulani, hatuna maisha fulani kwa sababu hatuna watu wakutupa connection/hatuna watu wakutushika mkono.
Ni kweli maisha yetu yanahitaji connection, maisha yetu yanahitaji watu ili kufikia hatua fulani. Pamoja na hayo yote huwezi kubweteka tu nakukaa unalalamika nakulaumu watu eti unakosa nafasi kwa sababu yakukosa nafasi.
Tunapaswa kuelewa kuwa hata hao ambao wanaconnection leo hawakuanza na connection za watu bali uwezo, uthubutu, kujionyesha nakuitangazia dunia kuwa mimi nina hiki kitu cha tofauti nastahili kuwa mahali fulani, hawatasema leo lakini kwenye mioyo yao watakuwa wamekubali, yawezekana wasikutafute leo, ila kesho watakutafuta tu.
Connection ya maana ni uwezo wako, sifa zako katika taaluma na unavyoweza kuifanya taaluma yako kuwa tofauti na wengine. Lawama, malalamiko sio suluhisho la kukufanya upate unachotaka.
Kumbuka kama huna mtu wakukutia birikani wewe unawajibu wakujitia birikani hata kama ni kwa kujivuta, dunia ya leo inahitaji utofauti wako ili wakupe connection, kama huna mtu pale mbele, ufanye uwezo wako, kipaji chako, taaluma yako kuwa connector, jionyeshe, iambie dunia kuwa mimi nina hiki chatofauti, sio kwa maneno bali kwa matendo na matokeo ya kazi yako hata kama ni ndogo, wenye akili wataona tu, hata kama hawatakuambia ila kumbukumbu zitabaki kichwani.
Jitambulishe hata kwa lazima, walazimishe watu wakujue wewe una uwezo gani, halafu kila kitu cha uwezo wako kifanye kwa uwezo wa kiwango ch juu sana, kama wewe ni mwimbaji, mtangazaji, mwandishi, photographer, videographer etc hata kama ni bure fanya kwa kiwango kama kuna dau nono mbele yako, ukienda kufanya Interview fanya, usionyeshe huruma ili watu wakuhurumie, umasikini wako sio sababu ya watu kukupa kazi au nafasi kweye jambo fulani, watu wanahitaji uwezo wako tu. Huruma peleka nyumbani kwa wazazi watakuhurumia, wala watu hawakuhitaji wewe wanauhitaji ujuzi, maarifa na uwezo wako period
Mgema Moses.
mgemamoses@gmail.com
0715366003/0755632375

NYAKATI ZOTE NI BORA KWENYE MAISHA YETU.

wakati mwingine sio rahisi kueleweka na baadhi ya watu kutokana nakuwa na fikra na mitazamo tofauti juu ya mambo mbalimbali ya maisha. Ila ukweli ni kwamba NYAKATI ZOTE KWENYE MAISHA NI BORA bila kujali ni ngumu, chungu au nyepesi na tamu.
Kuna nyakati unapitia kwenye maisha mpaka unafikiri kuwa Mungu amegeukia ukutani au hayupo kabisa, unapitia mambo magumu kana kwamba uliwahi kumkufuru Mungu, au wewe ni mvivu, na hautimizi majukumu sawasawa, kila jambo unalojaribu kufanya halifanikiwi, mengine hayafanikiwi wakati una sifa na vigezo vyakuwa navyo au kuvifanya.
Una Elimu ila kila ukiomba kazi hufanikiwi sio kwa sababu umefanya vibaya kwenye usaili, unafanya kazi kwa bidii, biashara, unaongeza na ubunifu, kauli nzuri kwa wateja nk. lakini ndo kwanza unadidimia nakurudi nyuma, unafanya ibada na umwaminifu mbele za Mungu lakini kwanza ni kama vile uko jangwani.
Wengeni kila wakigusa jambo kwao ni vema na mafanikio, ana każi lakini akiomba kazi nyingine anapata madili yanamfuata, lakini wewe hata ukipata hela, utasikia mke ana umwa, mama anachangamoto fulani ni kama dunia iko kwako yote, kuna mahali umekata tamaa kabisa.
Nikukumbushe kuwa wewe ni bora sana,kuna kitu Mungu anakijenga kwako, kuna jambo Mungu analitaka kwako, Mungu anajua wewe ni zaidi ya vile ulivyo, anakujua vyema, anajua kama atayafanikisha mahitaji yako mapema kwa wakati unaotaka wewe kuna vitu ?hautavifanya kwa ubora na uwezo anaoutaka Mungu, maana utaridhika na kubweteka, labda utawadharau wengine, hautatambua kuwa ulipo ni kwa sababu ya Mungu ni kwa uwezo wako.
Kuna nyakati zakukufanya wewe kuwa ile dhahabu pure ambayo ikiingia sokoni kila mhitaji ataigombania, Mungu anakutaka wewe bora sio wewe unavyojitaka ....waoo kumbe bado hujawa tayari kuwa yule Mungu anamtaka
Turudi kwa Yusuph, habari hii huwa ina ujumbe mkubwa sana kwetu kujifunza kwa mfano, tazama pia mchakato na mapito ya Daudi kabla ya yeye kuwa Mfalme, alifanyiwa kila jambo gumu, lakini kumbe Mungu alikuwa anamwandalia hatima iliyo bora sana, kutukanwa na ndugu zake, kutokubalika, kutupwa shimoni, kuuzwa na kufungwa gerezani vyote hivyo vilikuwa vinamtafuta Yusuph pure/halisi...
Nyakati ngumu ni daraja la kukupeleka kwenye ubora wako, hivyo usijutie nyakati ngumu zifurahie ila usiridhike kuwa hapo, pambana huku ukijua malipo ya juhudi ni faida isiyo na mwisho
Mgema Moses

Monday, January 4, 2021

BADILI MBINU ZA MAPAMBANO ILA SIO MALENGO, MAONO NA NDOTO YAKO.

Asilimia kubwa ya vijana Afrika husimama pekee yao.wazazi wengi wakishasomesha au ukishafikisha umri wa miaka 18 na hukufanya vizur kwenye masomo ndiyo muda wa mzazi kuachana na wewe, bila kujali una mtaji wakuanzia au la, kwa sababu tu umefikia hayo maeneo mawili, moja ulimalïza darasa la saba/kidato cha nne na haukufanikiwa kuendelea ngazi zinazofuata au baada ya chuo kwa waliofika hatua hiyo mzazi anakuwa amemaliza na wakati mwingine kuanza kudai marejesho ya kazi yake.

Hii inachangiwa na mtazamo wa watu wengi kuamini baada yakusomesha lazima asaidiwe na mtoto bila kujal ana nguvu au amezeeka, maisha duni ya familia zetu nk.Baadhi wanamaliza masomo yao wanakuta mazingira yako sawa, kazi ameandaliwa maana mzazi ana connection, ana kampuni yake, au ana mtaji wakumfungulia biashara nzuri mtoto wake. 

Haya ndiyo maisha yetu huwa tunatofautishwa na mazingira ya nyumbani wakati mwingine, wakati wengine ufaulu wa masomo sio kigezo chakupata kazi, wengine wanalazimika kupata alama zajuu ilikuwashawishi waajiri na serikali kuwapatia ajira kama mtaji wa kwanza wakuyaanza maisha.

Tuna ndoto na malengo, lakini wakati mwingine tunaanzia mbinu ya muda mrefu kwenye soka tunasema inabidi kuanzia lamansia, kuwa na mbinu ya Grass root kutengeneza wachezaji wa gharama ndogo ili miaka ijayo watufae katika kuyatimiza malengo na ndoto za team yetu.
Wengine wanamfumo wa Real Madrid, PSG, chelsea, man utd na man cïty, wana uwezo wakuchukua cream safi tayari kwa matumizi.

Unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini huna mtaji, ukienda benki wanadai hati ya kiwanja, serikalini mikopo haitoshelezi au mnahitakika watu wengi ili mpate milioni kumi, tańo au moja ili mgawane. Mazingira hayo yanakulazimisha kufanya kama umeisahau ndoto yako kwenda kumtumikia mwingine ïĺi kujenga misuli ya uchumi ndiyo uanze kuïfukuzia ndoto yako. 
Rafiki yangu kubali tu kuanzia huko ila isiwe sababu yakuyasaliti maońo, ndoto na malengo yako kwa msala upitao.Pambana jenga mtaji ila fahamu ulichepuka ili kwenda kujenga msingi imara wa kuyaweka maońo yako.
Kwa kila hali tupambane ila tusisahau kuwa tuna maono, ndoto na malengo ambayo hatupaswi kuyasaliti. Badili mbinu ila usibadili malengo na maono yako
Mgema Moses
Mwaka 2011 nilifika St. Augustine University Jijini kwa mara ya kwanza kumsalimia kaka yangu George aliyekuwa akisoma hapo chuoni. Baada yakufika chuoni, nilivutiwa sana na mazingira ya chuo, pamoja na namna ambavyo kilikuwa kinapendeza, lakini hata baada yakufuatilia taarifa za ndani kabisa nikavutiwa sana na nilifanya maamzi kwamba baada ya masomo ya Advance ilikuwa lazima katika chuo hicho.
Mwaka 2013 ndiyo ulikuwa mwaka ambao nilipaswa kuanza masomo yangu ya chuo, lengo na mpango wangu haikuwa chuo kingine hapa nchini isipokuwa St. Augustine. Mchakato ulipofanyika nikama niliingiwa na roho yakutokujiunga na chuo, lakini rafiki yangu Jose Mdamanyi alinishauri nijiunge na chuo, lakinï muda wakutuma maombi ulikuwa uko ukingoni, lakini alijitahidi mpaka akafanikiwa kutuma maombi ya chuo. Baada ya wiki mbili baadhi ya majina yalirudi 

Sunday, January 3, 2021

WEWE SI UNAISHI LEO, WEWE UTAISHI KESHO.

Kuna mawazo yanakujia kwenye ufahamu wako na wakati mwingine yanakutia unyonge kwa sababu ni kama unaona umeshatumia kila njia ili kufikia malengo yako lakini inaonekana ni ngumu kufikia kusudi la juhudi zako, umefika mahali picha kubwa inakujia kichwani mwako kuwa wewe uko kwenye fungu la kukosa..........
Hapana wewe ni shujaa, wewe ni uwekezaji wa Mungu, kuna kitu cha tofauti umebeba ndani yako, wewe ni ardhi ambayo ndani yake imebeba utajiri mwingi wa madini, nani mgunduzi na mchimbaji, bado hajapatikana, nani atakuja kugundua kuwa katika ardhi wewe umehifadhi madini ambayo bado hayajagundulika...
Baba na mama walishindwa kugundua mapema, bahati mbaya kuanzia mwalimu wako wa chekechea hadi chuo kikuu hajafanikiwa kugundua madini yaliyo katika ardhi wewe, Jirani na mtaa kwa ujumla nao umeshindwa kugundua nakutambua kwenye ardhi wewe kuna madini yanayosubiri kugunduliwa na kuanza kuchimbwa.
>Kuna majiolojia wachache wamefahamu kuwa ardhi wewe umehifadhi madini lakin bahati mbaya wamepatwa na woga kuwekeza mitaji yao kwa kuhofia kula hasara kwa sababu serikali haina swalia mtume, muda wa janja janja umekwisha, TRA na serikal wako macho kudai chao mapema ingawa kwa sasa ni kama hawaoni....
Nani mwekezaji mwenye uthubutu, mwekezaji mwenye kufuata kanuni na taratibu za serikali ïli akipata kibali cha kazi kesho asiletewe taabu, nani yuko tayari kuwekeza fedha muda, kwa manufaa ya kesho, nani ambae haionei serikali wivu kwamba mimi niweke mtaji wangu halafu tuje tuvune wote faida...
Uwezo ulio nao, hujaugusa, wazazi, ndugu, marafiki, walimu na jamii kwa ujumla hawakutambua uwezo huo. Ni wakati wako kukaa chini na kujitathimini ili kujigundua uwezo wako, ukifanikiwa kujigundua basi wewe si wewe unaishi sasa, wewe ni yule ambae alikusudiwa na Mungu ambae aĺiweka uwezo wa kipekee ndani yako. Kwa sababu hujaishi leo umebaki kuzurura, Wewe wa Mungu anakutegemea uishi kesho.
Rudi kwenye kiti, jisome, jitathimini ndiyo njia sahihi yakujifahamu na ukishajifahamu ndiyo utakuwa umefika muda wa kuishi ndoto na maono yako, kubali kurudi kwenye kiti na meza ya tathimini kule mahali pautulivu.
Mgema Moses

Friday, January 1, 2021

MIPANGO, MALENGO NA MIKAKATI

MWANZO MPYA BAADA YA COVID19, 2020

2020 Umekuwa ni mwaka ambao umeacha alama na historia kubwa kwa ulimwengu, kutokana na kulipuka kwa ugonjwa wa Covid19 ambao umekuwa na madhara na matokeo hasi kwenye maisha ya watu wengi Duniani.Nyanja zote za maisha ziliguswa, kuanzia maisha ya watu, tumepoteza ndugu, rafiki, jamaa zetu wakaribu,  mfumo wa ajira, watu wamepoteza ajira zao kutokana na kuyumba kwa mifumo ya uendeshaji wa makampuni hasa sekta binafsi, biashara nk.
Pamoja na hayo Mungu hata sasa anabaki kuwa Shujaa wetu maana ametupigania natuko salama 
Inawezekana hali hii ilibadili mwelekeo na malengo yako maana ilikuwa hali isiyotegemewa, imetokea hatuwezi kulaumu bali imetuachia funzo na darasa tumejifunza.
Kupitia changamoto hii naamini imekuimarisha na kukupa nguvu mpya tena, Na sasa uko tayari kwa mapambano ya mwaka huu wenye ishara ya mwanzo mpya kwa sababu unaanza na 1, kwa ufupi yakale yamepita na huu ni ukurasa mpya wenye matumaini mapya, Naamini umekaa chini umeweka mipango yako sawa na uko tayari kwa 2021.
Mungu ukupe nguvu mpya, maarifa na shauku yakufanya kazi kwa bidïï ili kufikia malengo yako
Mungu akubariki sana 
2021 Is the year of Greatness.
Mgema Moses.