Saturday, October 27, 2018

UPANDE WA PILI NA MTAZAMO WA WAJASIRIAMALI WENGI

-Kuna mwamko mkubwa sana wa watu kujiingiza kwenye ulimwengu wa biashara, ujasiriamali na utumiaji wa kila fursa ambayo inapatikana kwenye mazingira yanayowazunguka lakini pia watu kusafiri mahali mahali kuzifuata fursa zinakopatikana.
Lakini pia watu wameenda mbali zaidi kwa kuwa wabunifu, wenye kutumia maarifa, ujuzi na taarifa zinazopatikana lengo likiwa ni kutimiza malengo na ndoto zao.
Ugumu wa maisha na kuongezeka kwa mifumo ya Teknolojia mpya ambayo inawafanya watu wengi kujifunza kutoka kwa mataifa tofauti tofauti ambayo mfumo wa biashara na ujasiriamali umeendelea zaidi.
 Ukosefu wa ajira kwa watu waliobahatika kwenda shule hata ambao elimu kwao ilipita pembeni ni sababu nyingine ya vijana na watu wa rika zote kuingia kwenye biashara na kazi zingine binafsi.
Wengine wamejaribu kuthubutu na wanachukia tu  kufanya kazi za watu huku wakiona wanauwezo wakutumie kidogo walicho nacho kujiajiri na kuendesha maisha yao bila bughuza na kero za waajiri.
Ukwel ni kwamba ni nadra sana kwa waajiliwa kutajirika kwa sababu ya ratiba za waajiri kuwashepu kwenye mazingira fulani magumu ambayo hayawapi nafasi hata kidogo ya wao kuwa na miradi mingine mikubwa nje ya ajira.
Lakini pia wapo waliojaribu kuendesha Maisha ya ajira na miradi mingine nje lakini wameshindwa kwa sababu usimamizi kuwa hafifu mwisho wa siku biashara kuanguka na kufungwa.
Kutokana na hayo yote kuifanya dunia kuwa katika mfumo tulionao. Je wajasiriamali wamewahi kujiuliza kwamba si kila ujasiriamali ni uwekezaji( Investment) kuna biashara ambazo ni special kwa ajira ya kuyafanya maisha yaende tu na biashara kama hizi humwitaji mtu wenyewe kuwepo au kusimamia.
Biashara yoyote ile ambayo inakuhitaji wewe kuwepo hakika biashara hiyo ni sawa na mfanyakazi katika makapuni binafsi  (Private sector) kwa mtu anapougua muda mrefu kuna hatari ya kuachishwa kazi.
Akifariki dunia no body can run the business inamwitaji yeye tu ili iweze kwenda ni hatari sana.
Biashara yoyote unayofanya leo ambayo inakuhitaji uwe mzima na Lazima uwepo eneo la business basi jiangalie sana kwa sababu upo kwenye hatari utakapopata changamoto yoyote inayokulazimisha kutokuwepo kwenye eneo la kazi
Lazima ukumbuke kuwa Maisha yetu hayana garantii wakati wowote tuko kwenye janga la kupata ajali ambayo itakufanya kukaa ndani kwa muda mrefu.
Biashara inakuhitaji wewe ukifa je kuna mtu ataweza kusismama na kufanya kama ulivyokuwa unafanya wewe ni ngumu sana.
Kwa sababu kwenye business kuna mbinu, umafia na kujua tabia ya biashara fulani na ndo maana ni ngumu sana mtu anaefanya biashara ya nguo akawa bora kwenye biashara ya mazao, sio kwamba hawezi no anaweza ila inamwitaji muda kidogo kuzoea na kujua namana soko la mazao  linavyokwenda.
Sasa jiulize kama hiyo biashara inakuhitaji wewe kuwa mzima utafanyaje unapopata changamoto
Fikiri juu ya biashara yako leo hakikisha kama una mtoto basi anajua njia za mfumo wa biashara zako ili hata unapopata changamoto awepo mtu wa karibu kuisimamia biashara yako kwa ufanisi mkubwa.
Wenzetu wazungu sio wajinga hata wachaga kuwahusisha watoto wao kwenye kazi zao biashara na kila jambo wanalofanya ni kwa sababu tu wanajua na wamegundua kuwa duniani mwanadam hana garantii na Maisha at any time unakuwa marehemu kilema nk. hivyo anahitajika mtu wa kusimamia kazi zako mwenye kuona uchungu wa mali zako na kumbuka kuwa si kila mtu anafaa kubeba mikoba yako. Stori ya Yesu na Yuda inaweza kutukumbusha
Lakini pia unapofanya biashara yoyote ile hata kama ni ya millions of money kama si strong investment hiyo sio investment bali ni chanzo cha kipato tu ili kukusaidia kuendesha maisha.
Invest vitu visivyohamishika viwanja nyumba hata siku ukifa basi kama ulikuwa na familia isiteseke kabisa
Mwisho kumbuka Maisha yetu hayana siku at any moment mwenye uhai wake aweza kukuchukua je umejipanga vipi watoto na mke au watoto na mume unawaachaje kama ulikuwa ukifanya mambo yako pekee yako
Husisha watoto, mke ili wajue njia za biashara unayofanya ili hata ukipata shida wawepo makamanda kuisimamia
Jenga nyumba za biashara kama una uwezo usiridhike tu kuwa unaishi kwenye nyumba yako, kumbuka hiyo nyumba ni sawa na kaburi utaripaka rangi utapalilia lakini katu kamwe maiti aliyeko ndani hatofufuka.
Jenga na business houses ili Maisha yaende hata ukiwa kwenye changamoto Maisha yaendelee kuwa kwenye ubora ule ule
Kwa hapa Dar nimeona na nimekutana na wazee wengi sana wanapiga stori vijiweni wanakunywa kahawa kuanzia asubui wapo kariakoo unajiuliza hawa wanakula nini wanaendeshaje maisha yao mbona kila wakati wako na bao tu. Nikaja gundua kuwa kumbe walijenga nyumba za kupangisha siku nyingi leo hawana nguvu ya kufanya kazi lakini wanakula kuku kwa mirija waliyoiandaa miaka ya nyuma na wala hawana muda ya kusumbua watoto wao
Kumbuka wewe kijana uwekezaji ni sasa wekeza kila single amount unayopata ili ikusaidie leo hata kesho.
Ngamia hubeba maji mengi kwenye nundu yake yanayoweza kumfanya akasavaivu kwa wiki kadhaa bila shida
Kama ngamia na chungu wana akili ya kuiandaa vema siku ya uhitaji wao wewe je?.     ......Hilo ni swali nakuachia.
Moses zephania Mgema
0755632375
Instagram moses mgema
Fb moses zephania

No comments:

Post a Comment