Good Morning Tanzania
Kila asubui ijapo ina maanisha kuwa tumefungua ukurasa mpya kuendelea na stori yetu tunayoisoma.
Na kila mtu amepewa kitabu na stori tofauti na mwingine, maudhui na wingi au achache wa pages.
Hii imefanyika hivyo kwa sababu kila mtu amepewa talanta, karama, vipaji na vipawa tofauti ili kutimiliza kusudi la Mungu hapa duniani.
Na hii ina maana kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku
kwa nini? ........
Kwa sababu kadri pages unapozifungua ndivyo zinavyoongezeka kule unatoka na kule uendako zinapungua.
Hapa ni kwamba miaka yako ya kuishi inazidi kupungua na kukaribia kurudi ulikotoka.
Lakini kwa maana ya maisha yetu ya kawaida yanayotufanya wakati mwingine tusahau kama kuna kifo basi kadiri unaposogea badala ya pages kupungua hapa pages zinaongezeka tena kwa kasi sana
Nini maana yake..............
Umri unaposogea mahitaji na majukumu yanaongezeka zaidi na jamii kuanzia ngazi ya wewe familia mpaka jamii kwa ujumla inakutazama. Haikutazami tu kwa sababu umekuwa, la hashaaa bali inategemea jambo kutoka kwako.
Ulisoma, wewe ujitegemee uitumie ile elimu yako kuboresha mwonekano style ya maisha mtazamo na kila kitu ili kuiweka hadhi ya taaluma yako salama
Baba mama na familia inakutegemea lakini jamii na Taifa na dunia unailetea nini....ndo maana nikasema inapokuja siku mpya kurasa za kuishi zinapungua lakini kwenye suala la Maisha kurasa huongezeka.
Kila siku dunia inakulazimisha kufikiria mbinu mbalimbali za kuendesha maisha yako huku ikikunong'oneza kuwa angalia kule yule rika lako ulisoma nae lakini anahiki na kile....hapa ndipo unachanganyikiwa ufanyaje ili kufanikiwa.
Ni changamoto moto katikati ya dunia inayohitaji ubunifu, ujuzi na maarifa mengi ili kuweza kuifanya dunia ikukabili wewe badala ya wewe kuikabili.
Ushauri........
Mungu ameniumba mimi vivyo hivyo wewe amekuumba na lengo na kusudi maalumu ambalo hakuna mwingine aweza kulitimiza isipokuwa mimi mwenyewe au wewe mwenyewe.
Mungu alifanya kila jema akakupa kipaji akili focus nguvu maarifa ujuzi na anakuumba kwa namna ulivyo lengo utimize kusudi lake ili Muda ukifika urudi mtupu na salama.
Itumie talanta/Karama na kipaji chako na nafasi uliyonayo sasa ya uhai kazi, biashara,elimu na kila jambo unalofanya, Fanya kwa bidii kwa uaminifu kwa kujitolea na kwa kumaanisha sana.....hapo utafanikiwa utafurahia na kuiona dunia mujarabu sana......
Uvivu masengenyo zogo marafiki wabaya kulala,kulalamika,kulaumu, Kukosa uthubutu, kuchagua kazi nk. kuishi kwenye historia haikusaidii kabisa bali stay focused pekee...lazima utafanikiwa. Kumbuka Mungu huibariki kazi ya mtu mwenye bidii na kuilaani mikono milegevu.
Zaidi mkumbuke muumba wako kila sekunde ya pumzi yako ukisali kwa kushukuru na kutenda mema ili kuhesabiwa haki ya kuishi tena.
Matendo mema ni fahari ya Mungu kwetu sisi....Mungu wetu hutuwazia mema daima.
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako kabla siku mbaya hazijaja kwako
Hii ikawe asubui na siku ya baraka na mafanikio.
Kila unalofanya likapate kibali mbele za Mungu na wanadamu
Moses z. Mgema
0755632375/0678355394
Moses Mgema Twitter and Instagram
2018/2019 Is THE YEAR OF ACHIEVEMENTS
No comments:
Post a Comment