MAMBO MACHACHE AMBAYO NI MUHIMU KUJIFUNZA KUTOKA KWA KIJANA MWENZETU DIAMOND ALIYOYASEMA KWENYE SIKU YA KUZALIWA KWAKE
Tahere 2/10/2018 ilikuwa ni siku maalumu sana ya Nasibu Abdul alimaarufu diamond ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake
Kuna mambo mengi sana alizungumza Diamond kuhusu maisha yake ya muziki hata maisha kabla ya mziki yani alikotoka hadi hapa alipo.
Yako mambo mazuri sana ya kujifunza kutoka kwa Diamond kwa kijana anayetaka kutoka kimaisha sio tu kwa njia ya muziki lakini katika kila jambo unalofanya.
Nimefurahia sana kusikia yeye mwenyewe akizungumza na kuelezea alikopita na mambo aliyofanya hapo kabla hajawa DIAMOND mpaka alipokuja kuwa DIAMOND offcourse amezungumzia mambo mengi mazuri kama ifuatavyo
Hakuchagua kazi diamond alifanya kila kazi iliyokuwa mbele yake ambayo haikuvunja sheria au kwa lugha nyepesi kazi haramu.......Diamonda
1.aliuza mchanga
2.Alifanya kazi petrol station
3.Aliuza nguo
4.Alipiga picha mfumo wa zamani
Then diamond alisema ili uweze kufanikiwa Pamoja na kufanya kazi kwa bidii mambo yafuatayo lazima yachukue nafasi kwenye harakati zako
a. Ubunifu katika kila kazi unafanya
B. Bidii na maarifa ujuzi pia ni lazima
C. Uaminifu katika kazi yako na kazi za watu hii itakusaidia kujenga brand yako ya kuaminika kwa watu na siku nyingine watu watatamani kufanya kazi na wewe.
d. Kutokukata tamaa...kuna wakati unahitaji mtu fulani awe daraja lako kufikia ndoto zako lakini ni ngumu kumpata lakini unachopaswa kufanya pambana hakikisha adhima yako inatimia
e. Mwombe Mungu sana kwa kila jambo
f. Weka nia ya dhati toka moyoni dhamiria kufikia matamanio yako.
Alisema tena kumbuka kutengeneza mazingira ya watu kukupa kazi ajira na mambo mingine
Hapa akasema kuwa smart kuanzia nje hadi namna ya kufikiri jiupushe na mihadarati haisaidii kabisa.
Katika safari ya mafaniko mambo ya kukatisha tamaa ni mengi lakini usikubali yakushinde bali pambana kuyashinda. Wapo watu wengi sana amabao wanakatisha vijana tamaa kuwa wewe huwezi jambo fulani labda jambo fulani ndo unaweza hapana hilo unaloamini unaliweza na linamanufaaa kwako fanya pambana mpaka mwisho utafanikiwa.
Tumia kila nafasi unayopata ukijua nafasi nyeti huja mara moja tu kwenye maisha.
MWISHO
Kile Mungu anakupa baada ya kupambana kumbuka haya
Rudisha kwa jamii hata kama ni kidogo watu watakuombea na Mungu atakuinua zaidi ya mahali utakapokuwa
Aliyofanya diamond leo Tarehe 5/10/2018
Kawapa vijana wenzake wa tandale pikipiki 20
Watu 1000 kuwapa bima
Wakina mama 100 amewapa mtaji
Kuna mama mlemavu amempatia bajaji
Katoa Gari kwa mpiga picha wake
Mengi amefanya hakika sadaka humwinua zaidi mtu
Prepared by Moses Mgema
Source Diamond plutnum
Contacts: 0755632375/0678355394
Facebook Moses zephania
Instagram & Twitter moses mgema
No comments:
Post a Comment