I
DUNIA YA MAHUSIANO KIFO CHA MENDE
SEHEMU 1.
Kwa miaka ya sasa yaani kizazi cha dot.com kama ambavyo kinaitwa suala la kuanza mahusiano rasmi na yasio rasmi sana limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa Afrika ukilinganisha na miaka ya nyuma kidogo.
Ilikuwa ni nadra sana kwa vijana ambao nia ya dhati ya kuoa au kuolewa kuwakuta kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini sasa limekuwa jambo la kawaida sana.
Miaka ya nyuma kidogo kukuta jamii ikizungumza mambo haya ilikuwa nadra sana lakini sasa ni kawaida sana na wakati mwingine ndiyo zimekuwa stori kubwa za siku kwa rika zote imani zote na kada zote kwa ujumla.
Stori bila kuwepo stori inazungumzia mapenzi hizo siyo stori tena.
Usasa na kuporomoka kwa maadili kwenda na kasi ya mabadiliko ya sayansi na Teknolojia lakini pia uhuru nje ya mipaka na kila japo kuwa chini ya sheria tetezi kwa vijana wa jinsia zote ni chanzo cha yote haya, imefikia mahali binti au kijana wa kiume kutokuwa kwenye mahusiano ni ushamba yawezekana ni kweli kabisa kwa sababu ushamba ni kutokuwa na taarifa kamili juu ya jambo fulani.
Kuwa kwenye mahusiano sio kesi sana kama nia ya dhati au mapatano ya wawili hawa yana nia moja kabisa na mwelekeo wao wanaufahamu vema.
Shida inakuja hapa wengi tunaingia kwenye mahusiano kama fasheni ili mimi nami nionekane nina boy au Girl friend bila hata kujua kwa nini uko kwenye hiyo chaini ya mahusiano inauma sana.
Wengi tumeingia hapa bila kuwa na elimu na kujua Thamani yake matokeo yake watu wameumiza mioyo ya watu wengi sana siyo wasichana wala vijana wa kiume
Watu wanaugulia maumivu makali kama mkuki wenye sumu kupenya kwenye moyo hakika ni majeraha na vidonda visivyopona.
Kwa kutokujua maana na malengo ya kuingia kwenye mahusiano wengi wamejikuta wakicheza mchezo na kujizawadia mimba ambazo hawakuzipanga mwisho ni kuchomoa na kuua.
Laana ya vizazi na vizazi inazitafuna familia nyingi Roho za watoto walionyofolewa damu zao zinalilia kwenye nyoyo na fahamu za waliotenda mambo hayo.
Laana juu ya laana tukijipa matumaini kuwa Mungu anasamehe siwezi bisha ila tunapishana na mafanikio mengi yenye baraka ndani yake.
Kwa nini umwache mwenzako bila sababu mabinti na vijana wakati mwingine watu wanakula viapo na machozi mengi lakini mwisho wa siku bila sababu ya msingi binti anasema kuanzia leo nasitisha mahusiano wewe...........kumbuka ukiumiza moyo mtu alieyekuwa amemanisha ni madhara makubwa sana mbele yako.........kumbuka kila ufanyalo kwa wema ipo siku utapokea ijara njema lakini wewe mrubuni wa mapenzi utakufa kwa namna yoyote either kunyimwa watoto au kuachwa pia au kupewa jitu jeuri sana
Acha niishie hapa tutaendelea kesho kutwa
REMEMBER WHAT GOES AROUNDCOMES AROUND
2018 THE YEAR OF ACHIEVEMENTS
No comments:
Post a Comment