Monday, October 8, 2018

GUNDUA UWEZO NDANI YAKO

DISCOVER YOUR POTENTIAL IN YOU/ GUNDUA UWEZO NDANI YAKO ----1

Kila mtu ana uwezo wa kipekee.Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuongoza lakini bado hajafahamu uwezo alio nao .Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuzungumza lakini bado hajielewi .Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuandika lakini hadi anavyosoma makala hii bado hajielewi maana hajawi kuanza kuonesha uwezo wake .Kwa kutambua uwepo wa watu wengi wasiojua uwezo walio nao nimekuandalia makala zitakazoamsha uwezo ulio ndani yako ili ukufikishe kule unakotaka kufika.

Mungu alivyokuumba aliweka ndani yako uwezo mkubwa sana kwa bahati mbaya watu tumeshindwa kutambua uwezo tulionao.Ni lazima kama unataka kufika kule unakotaka kufika kufahamu kabisa nini unaweza kufanya vizuri kwa uwezo uliopewa na Mungu .Acha kuwasikiliza watu wanaokukosoa na watu wanaokurudisha nyuma .Wewe amini katika uwezo wako ambao uko ndani yako .

Kama unaweza kuimba vizuri fahamu huo ndio uwezo Mungu alikupa .Tumia vizuri uwezo huo bila kugeuka nyuma na utafika mbali sana .Acha kuangalia madhaifu uliyonayo lakini angalia uwezo ulio nao .

Watu waliofahamu uwezo wao (maeneo yao ya kujidai ) na wakajua namna ya kuwajibika ,walifika mbali sana .Je ,watu hawa waliofika mbali hawakuwa na madhaifu ?  Jibu ni Hapana walichokiangalia ni uwezo ambao walikuwa nao kuliko madhaifu yao .

Uwezo ulionao hauzuiliwi na jambo lolote.Haijalishi umezaliwa wapi na unaishi wapi uwezo wako ukiamua kuutumia utaonekana tu.Kama unaweza kucheza mpira vizuri  hakikisha unacheza mpira kwa nguvu na akili yako yote maana hapa ndipo mafanikio yako yaliko .Kama unaweza kuchekesha watu fanya hivyo ukielewa kabisa wapo watu ambao wamefanikiwa kupitia uchekeshaji .

Watu hawa walivyoelewa uwezo walionao maisha yao leo yamebadilika.

Nick Vujic
Nick ni mlemavu asiyekuwa na miguu wala mikono ambaye mbali na kuwa alizaliwa mlemavu hivyo alielewa eneo lake ambalo alikuwa na uwezo nalo .Nick baada ya kuona hawezi kazi za kutumia mikono au miguu alianza kufikiri nini ana uwezo nacho na akagundua anaweza kuhamasisha watu na watu wakahamasika .Nick bila kuchelewa alianzisha taasisi yake ambaye yeye aliiita  taasisi ya maisha bila miguu (life without limbs) na akaanza kuzunguka dunia nzima kuhamasisha watu hasa walemavu .Leo Nick Dunia nzima inamfahamu.

Mwalimu Julius Nyerere
Mwalimu Nyerere ni ni mtu  ambaye alifahamu kuwa alikuwa na uwezo wa kuongoza watu na akatumia uwezo wake kwa viwango vikubwa sana leo Mwalimu Nyerere Dunia nzima inamkumbuka kwa kuwa alitumia uwezo wake aliokuwa nao.

Mbwana Sammatta
Mbwana Samatta baada ya kufahamu kuwa Mungu ameweka uwezo wa kucheza mpira vizuri ndani yake alianza mara moja kucheza mpira .Samatta hakuwa anacheza kama wachezaji wengine wanaofikiria kucheza mpira Simba na Yanga maisha yao yaishie hapo lakini yeye alicheza huku akijua siku moja dunia itakuwa ikimsikia na kufuatilia uwezo wake .Mtazamo wake ulikuwa mtazamo mpana wa kuhakisha uwezo wake unamtangaza Duniani .Leo Mbwana Sammatta Dunia inamjua na hakika mafanikio yake si haba.

MC PILIPILI
MC Pilipili alivyogundua kuwa ana uwezo wa kupangilia maneno na kuongea mbele za watu aliamua kuwa mshereheshaji (Master of Ceremony) .Leo Mc Pilipili amefika mbali sana kwa kuwa siku moja aliamua kutumia kile kilichoko ndani yake

Ni lazima ujue wewe ni mzuri na kufanya katika viwango vikubwa sana bila kuangalia mwenzako anafanya nini .Lazima ufike mahali uorodheshe vitu unavyofanya kwa uzuri na hivyo ndivyo vitakutoa katika maisha .Acha kuamini kuwa vyeti vyako ndivyo pekee vitakufanikisha utachelewa sana .Inuka anza kuangalia nini unaweza kufanya ili maisha yako yabadilike .

Unajua nini ? Unaweza kufanya nini ? unaweza kufanya nini kwa uzuri ? .Amsha uwezo wako leo

Itaendelea.

No comments:

Post a Comment