Tuesday, October 16, 2018

UKWELI NI UHURU 7

13.UKWELI NI UHURU.
UCHAMBUZI WA KITABU.

Kanuni na Nguvu ya Maono.

Mwandishi :
       Dr. Myles Munroe.

Kanuni ya 7.

...................   ...................
Tengeneza vipao mbele vya maono yako /Set the priorities of your Vision.
.................     ...................

Maisha yako ni mjumuisho wa maamuzi unayofanya kila siku,/ your life is the some total of the decision you make every day.

Kanuni hii inasema kama unataka kufanikiwa lazima utengeneze vipaombele kulingana na maono yako.

Kama kila siku tunafanya maamuzi basi, maamuzi sahihi ni zao la vipao mbele sahihi, utofauti wa kufanikiwa na kufeli unachangiwa na vipao mbele ulivyo navyo, kama huna vipaombele jua huwezi kufanya maamuzi sahihi katika maisha ya kila siku na hata kutimiza ndoto zako utashindwa.

Nguvu ya vipaombele katika kusema *YES* au *No*
   Kama unasema Yes kila linalokuja mbele yako ujue unatatizo la vipaombele. Myles anasema ukiwa na vipaombele utajua kipi useme Yes kulingana na vipaombele vya maono yako na nini useme No kama ni nje ya maono yako.

Ndio na hapana ni maneno ya muhimu sana katika safari ya mafanikio, huwezi kuwekeza kila mahali hata ushawishiwe kiasi gani, huwezi kufanya kila biashara au kudaga kila fursa, isipo kuwa ipo kwenye vipaombele vyako vya siku, wiki, mwezi na mwaka, hakika utafanikiwa sana.

1corintho 6:12.

*Vitu vyote ni halali kwangu lakini si vyote vifaavyo,......*

Ni kwamba Kuna vitu vingi ni halali lakini kwa kulingana na maono yako, si vyote vifaavyo lasivyo unauwa ndoto yako, hii ni kweli kitu kile kile mwingine akifanya anafanikiwa ila wewe ukijaribu una umia kwa nini,?  Hakipo kwenye maono yako rafiki, jifunze Kusema No.

Kwa kigezo kipi useme hapana?

Toka mwanzo tumejifunza kuwa mwanzilishi wa maono ndani yako ni Mungu mwenyewe, hivyo kama kuna jambo utakiwa ulifanye ila Mungu hawezi kulikubali, yani ukilifanya unakuwa unavunja uhusaino wako na Mungu acha, sema haoana, yani hapana rushwa, hapana kuwanyima watu haki na kuondoa furaha yao kwajili ya faida yako mwenyewe.

Vipaombele vinakupa nafasi ya kuzingatia jambo moja mpaka kuhakikisha limetimia kabisa, pia linakufanya uwe na uhakika kuwa baada ya miaka kadhaa ijayo utakuwa upo mahali gani kwani yapo mambo mengi ambayo utayakwepa kuyafanya na utashughulika na yale muhimu tu.

Kama vipaombele vyako vinatokana na maono yako, basi jua kabisa nidhamu itakuwa kitu rahisi kwako, kwani wengi wanakosa nidhamu sababu kubwa ni kukosa vipaombele.

Jiulize maswali haya kujua kama unaishi maisha yenye nidhamu kufuatana na ndoto zako?

.Nguvu zako nyingi unatumia kufanya nini? Wapi moyo wako upo?  Je, ni mambo yenye uhusiano na ndoto zako.

.Wapi unawekeza pesa zako? Je, unanunua vitu vya gharama kuliko hata uwezo wa Maisha yako binafsi? Unajikuta unamadeni mengi kiasi kwamba kila pesa unayopata haiendi kufanya mambo yanayohusu maono yako?

.Ni Movies gani unaangalia, unafuatilia nini kwenye mitandao ya kijamii, habari gani unafuatilia katika maisha yako kila siku, utajua maono yako?

.Vitabu gani unasoma, je, ni vitabu vya mapenzi na hadithi za umbea? Aina ya vitabu unavyotakiwa kusoma vitokane na maono yako.

.Ni mtazamo gani unao juu ya maisha?  Vitu gani hatari unafanya?(ngono, pombe, au madawa).

Amua kuchukua hatua ya kufanya mambo makubwa katika maisha yako, kama kuna jambo la kubadilisha maisha yako anza mara moja.

Mwisho.

Mambo ya kuchukua hatua.

1.Andika vipaombele vyako kila eneo la maisha yako,  (kiroho, kiuchumi, kiafya, kiakili na kimahusiano).

2.Vitu gani unataka kuviondoa kwenye maisha yako ili uweze kuishi maisha yako (Orodhesha na anza mara moja hatua za kuachana navyo)

3.Jibu maswali ya hapo juu vizuri kabisa Kwa kujichunguza Mwenyewe .

         

No comments:

Post a Comment