Saturday, October 27, 2018

I LIVE MY OWN LIFE....LEAVE MY LIFE ALONE

Nini.....niacheni naishi maisha yangu sitaki mtu anifuatilie kila mtu na maisha yake.
Nini......?
Nimemaliza ukiendelea kufuatilia Maisha yangu ntakuja pasua mtu sina swalia mtume........
Ok.........anyway

Socialization, civilization, Corporation,
Are are among of The fundamental which will take you to the place where you want to be.
Stori nyingi sana za vijiweni vinasikitisha na kukatisha tamaa kwa sababu vijana wengi tunapenda kuona

UPANDE WA PILI NA MTAZAMO WA WAJASIRIAMALI WENGI

-Kuna mwamko mkubwa sana wa watu kujiingiza kwenye ulimwengu wa biashara, ujasiriamali na utumiaji wa kila fursa ambayo inapatikana kwenye mazingira yanayowazunguka lakini pia watu kusafiri mahali mahali kuzifuata fursa zinakopatikana.
Lakini pia watu wameenda mbali zaidi kwa kuwa wabunifu, wenye kutumia maarifa, ujuzi na taarifa zinazopatikana lengo likiwa ni kutimiza malengo na ndoto zao.
Ugumu wa maisha na kuongezeka kwa mifumo ya Teknolojia mpya ambayo inawafanya watu wengi kujifunza kutoka kwa mataifa tofauti tofauti ambayo mfumo wa biashara na ujasiriamali umeendelea zaidi.

Thursday, October 18, 2018

GOODMONING TANZANIA

Good Morning Tanzania

Kila asubui ijapo ina maanisha kuwa tumefungua ukurasa mpya kuendelea na stori yetu tunayoisoma.
Na kila mtu amepewa kitabu na stori tofauti na mwingine, maudhui na wingi au achache wa pages.

Hii imefanyika hivyo kwa sababu kila mtu amepewa talanta, karama, vipaji na vipawa tofauti ili kutimiliza kusudi la Mungu hapa duniani.
Na hii ina maana kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku
kwa nini? ........
Kwa sababu  kadri pages unapozifungua ndivyo zinavyoongezeka kule unatoka na kule uendako zinapungua.
Hapa ni kwamba miaka yako ya kuishi inazidi kupungua na kukaribia kurudi ulikotoka.
Lakini kwa maana ya maisha yetu ya kawaida yanayotufanya wakati mwingine tusahau kama kuna kifo basi kadiri unaposogea badala ya pages kupungua hapa pages zinaongezeka tena kwa kasi sana
Nini maana yake..............
Umri unaposogea mahitaji na majukumu yanaongezeka zaidi na jamii kuanzia ngazi ya wewe familia mpaka jamii kwa ujumla inakutazama. Haikutazami tu kwa sababu umekuwa, la hashaaa bali inategemea jambo kutoka kwako.
Ulisoma, wewe ujitegemee uitumie ile elimu yako kuboresha mwonekano style ya maisha mtazamo na kila kitu ili kuiweka hadhi ya taaluma yako salama
Baba mama na familia inakutegemea lakini jamii na Taifa na dunia unailetea nini....ndo maana nikasema inapokuja siku mpya kurasa za kuishi zinapungua lakini kwenye suala la Maisha kurasa huongezeka.
Kila siku dunia inakulazimisha kufikiria mbinu mbalimbali za kuendesha maisha yako huku ikikunong'oneza kuwa angalia kule yule rika lako ulisoma nae lakini anahiki na kile....hapa ndipo unachanganyikiwa ufanyaje ili kufanikiwa.

Ni changamoto moto katikati ya dunia inayohitaji ubunifu, ujuzi na maarifa mengi ili kuweza kuifanya dunia ikukabili wewe badala ya wewe kuikabili.
Ushauri........
Mungu ameniumba mimi vivyo hivyo wewe amekuumba na lengo na kusudi maalumu ambalo hakuna mwingine aweza kulitimiza isipokuwa mimi mwenyewe au wewe mwenyewe.

Mungu alifanya kila jema akakupa kipaji akili focus nguvu maarifa ujuzi na anakuumba kwa namna ulivyo lengo utimize kusudi lake ili Muda ukifika urudi mtupu na salama.

Itumie talanta/Karama na kipaji chako na nafasi uliyonayo sasa ya uhai kazi, biashara,elimu  na kila jambo unalofanya, Fanya kwa bidii kwa uaminifu kwa kujitolea na kwa kumaanisha sana.....hapo utafanikiwa utafurahia na kuiona dunia mujarabu sana......
Uvivu masengenyo zogo marafiki wabaya kulala,kulalamika,kulaumu, Kukosa uthubutu, kuchagua kazi nk. kuishi kwenye historia haikusaidii kabisa bali stay focused pekee...lazima utafanikiwa. Kumbuka Mungu huibariki kazi ya mtu mwenye bidii na kuilaani mikono milegevu.

Zaidi mkumbuke muumba wako kila sekunde ya pumzi yako ukisali kwa kushukuru na kutenda mema ili kuhesabiwa haki ya kuishi tena.
Matendo mema ni fahari ya Mungu kwetu sisi....Mungu wetu hutuwazia mema daima.

Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako kabla siku mbaya hazijaja kwako
Hii ikawe asubui na siku ya baraka na mafanikio.

Kila unalofanya likapate kibali mbele za Mungu na wanadamu
Moses z. Mgema
0755632375/0678355394
Moses Mgema Twitter and Instagram
2018/2019 Is THE YEAR OF ACHIEVEMENTS

Tuesday, October 16, 2018

NGUVU YA MAONO Na MAYLES

10. UKWELI NI UHURU.

Uchambuzi Wa Kitabu.
Misingi na Nguvu Ya Maono.

Mwandishi(Author).
        Dr. Myles Munroe.
        (1954- 2014)
Kanuni ya nne , ya kukuweza kuishi na kutimiza maono yako ni pamoja na :-
........................................
*Kuwa na shauku ya maono yako /Posses the Passion of Your Vision* .
........................................
Je, unahasira kiasi gani na maono yako? Unajisikiaje pale bado hujaanza kugusa maisha ya watu na uwezo umepewa?

Watu waliyotambua kuwa kuwepo hapa Duniani ni zaidi ya kuishi, ndio wanafanya mabadiliko makubwa katika ulimwengu huu toka mwanzo, watu ambao kwao maisha ni zaidi ya kula, kuvaa, kustarehe, yani watu ambao furaha yao haitokani na uwingi wa pesa wanazotengeza ila alama wanazo achilia ndani ya mioyo ya watu.

Watu wengi hawana shauku ya kufanya mambo makubwa katika maisha yao kwa sababu hawana shauku kutoka ndani ya Mioyo yao, na maono Pekee ndio chanzo cha shauku.

Shauku/Passion ina maanisha kile unacho kiamini ni kikubwa kuliko unacho kiona.

Ni shauku / Passion itakusaidia kushinda vikwazo kwa sababu kilichopo ndani ya moyo wako ndio kinakusukuma katika maisha yako ya kila siku, kuna wakati tunatafuta namna mbalimbali ili tuweze kufikia ndoto zetu lakini, bila kuwa na shauku ndani Mioyo yetu hatuwezi kustahimili vikwazo na changamoto zitakazo tokea njiani, zaidi ya yote ukiwa na shauku hata kama watu watakuangusha mara ngapi, utasimama Mpaka wao wachoke na kukuacha wenyewe.

Shauku ya moyo wako juu ya maono itakusaidia Kuzingatia ndoto yako bila kuishia njiani.

Hongera rafiki kwa mfululizo huu, endelea kupata Kilicho bora zaidi...

Kiu yangu ni kuona watu wanaoishi zaidi ya wanacho kiona leo, wenye uwezo wa kugusa maisha ya ulimwengu huu.

Mwisho.
Kwa mgeni karibu, kwenye kundi hili, tunajifunza na kuchukua hatua ili kufanya maisha yetu na wengine kuwa bora,zaidi.

Pia taarifa ya darasa la leo 14/10/018 juu ya uwekezaji, kwanzia saa 2:00-4:00usiku.

💥Maeneo tunayoenda kujifunza,
  1.maana ya uwekezaji na uhuru wa kifedha pamoja na umuhimu wake.

2.Maeneo matano ya kufanya uwekezaji katika maisha yako.

3.Mbinu za kufanya uwekezaji bora.

UKWELI NI UHURU 7

13.UKWELI NI UHURU.
UCHAMBUZI WA KITABU.

Kanuni na Nguvu ya Maono.

Mwandishi :
       Dr. Myles Munroe.

Kanuni ya 7.

...................   ...................
Tengeneza vipao mbele vya maono yako /Set the priorities of your Vision.
.................     ...................

Maisha yako ni mjumuisho wa maamuzi unayofanya kila siku,/ your life is the some total of the decision you make every day.

Kanuni hii inasema kama unataka kufanikiwa lazima utengeneze vipaombele kulingana na maono yako.

Kama kila siku tunafanya maamuzi basi, maamuzi sahihi ni zao la vipao mbele sahihi, utofauti wa kufanikiwa na kufeli unachangiwa na vipao mbele ulivyo navyo, kama huna vipaombele jua huwezi kufanya maamuzi sahihi katika maisha ya kila siku na hata kutimiza ndoto zako utashindwa.

Nguvu ya vipaombele katika kusema *YES* au *No*
   Kama unasema Yes kila linalokuja mbele yako ujue unatatizo la vipaombele. Myles anasema ukiwa na vipaombele utajua kipi useme Yes kulingana na vipaombele vya maono yako na nini useme No kama ni nje ya maono yako.

Ndio na hapana ni maneno ya muhimu sana katika safari ya mafanikio, huwezi kuwekeza kila mahali hata ushawishiwe kiasi gani, huwezi kufanya kila biashara au kudaga kila fursa, isipo kuwa ipo kwenye vipaombele vyako vya siku, wiki, mwezi na mwaka, hakika utafanikiwa sana.

1corintho 6:12.

*Vitu vyote ni halali kwangu lakini si vyote vifaavyo,......*

Ni kwamba Kuna vitu vingi ni halali lakini kwa kulingana na maono yako, si vyote vifaavyo lasivyo unauwa ndoto yako, hii ni kweli kitu kile kile mwingine akifanya anafanikiwa ila wewe ukijaribu una umia kwa nini,?  Hakipo kwenye maono yako rafiki, jifunze Kusema No.

Kwa kigezo kipi useme hapana?

Toka mwanzo tumejifunza kuwa mwanzilishi wa maono ndani yako ni Mungu mwenyewe, hivyo kama kuna jambo utakiwa ulifanye ila Mungu hawezi kulikubali, yani ukilifanya unakuwa unavunja uhusaino wako na Mungu acha, sema haoana, yani hapana rushwa, hapana kuwanyima watu haki na kuondoa furaha yao kwajili ya faida yako mwenyewe.

Vipaombele vinakupa nafasi ya kuzingatia jambo moja mpaka kuhakikisha limetimia kabisa, pia linakufanya uwe na uhakika kuwa baada ya miaka kadhaa ijayo utakuwa upo mahali gani kwani yapo mambo mengi ambayo utayakwepa kuyafanya na utashughulika na yale muhimu tu.

Kama vipaombele vyako vinatokana na maono yako, basi jua kabisa nidhamu itakuwa kitu rahisi kwako, kwani wengi wanakosa nidhamu sababu kubwa ni kukosa vipaombele.

Jiulize maswali haya kujua kama unaishi maisha yenye nidhamu kufuatana na ndoto zako?

.Nguvu zako nyingi unatumia kufanya nini? Wapi moyo wako upo?  Je, ni mambo yenye uhusiano na ndoto zako.

.Wapi unawekeza pesa zako? Je, unanunua vitu vya gharama kuliko hata uwezo wa Maisha yako binafsi? Unajikuta unamadeni mengi kiasi kwamba kila pesa unayopata haiendi kufanya mambo yanayohusu maono yako?

.Ni Movies gani unaangalia, unafuatilia nini kwenye mitandao ya kijamii, habari gani unafuatilia katika maisha yako kila siku, utajua maono yako?

.Vitabu gani unasoma, je, ni vitabu vya mapenzi na hadithi za umbea? Aina ya vitabu unavyotakiwa kusoma vitokane na maono yako.

.Ni mtazamo gani unao juu ya maisha?  Vitu gani hatari unafanya?(ngono, pombe, au madawa).

Amua kuchukua hatua ya kufanya mambo makubwa katika maisha yako, kama kuna jambo la kubadilisha maisha yako anza mara moja.

Mwisho.

Mambo ya kuchukua hatua.

1.Andika vipaombele vyako kila eneo la maisha yako,  (kiroho, kiuchumi, kiafya, kiakili na kimahusiano).

2.Vitu gani unataka kuviondoa kwenye maisha yako ili uweze kuishi maisha yako (Orodhesha na anza mara moja hatua za kuachana navyo)

3.Jibu maswali ya hapo juu vizuri kabisa Kwa kujichunguza Mwenyewe .

         

HATUA 10 ZA KUSAJILI KAMPUNI

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

HATUA 10 ZA USAJILI

1: Taarifa za msajili
Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
Simu ya kiganjani
Barua pepe yaani email
Hatua

2: Taarifa za kampuni (Company Information)
Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
Jina la kampuni
Kazi zitakazokuwa zikifanywa na hiyo kampuni tarajiwa (Activity description)
Hatua

3: Ofisi za kampuni (Office Location)
Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa.
Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, namba ya kitalu na namba ya nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe (email)
Hatua

4: Shughuli za Kampuni (Company Activities)
Taja shughuli za kampuni kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification
Hatua

5: Taarifa za Wakurugenzi (Directors Information)
Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
TIN
Simu ya kiganjani
Barua pepe yaani email
Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua

6: Taarifa za katibu wa kampuni (Company Secretary)
Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
Simu
Barua pepe - email
Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua

7: Taarifa za wanachama/wenye hisa (Subscribers Information)
Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
Simu
Barua pepe - email
Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua

8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua

9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
Kusajili kampuni
Kuhifadhi nyaraka na
Stamp Duty
Hatua

10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni
Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money na HaloPesa
Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo.

USHAURI WA BURE

Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:
Nashauri kama unataka kufanya usajili wa Haraka na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia.

Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho.

Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.

UKWELI NI UHURU

UKWELI NI UHURU

Misingi na nguvu ya Maono.

Mwandishi.
        Dr. Myles Munroe.

Kanuni ya sita ya kutusaidia kutimiza maono,..
........................................
Uwelewe mchakato wa maono /Understand the Process of Vision.
........................................
Mithali 16:9
Moyo wa mtu hufikiri(hupanga) njia yake, bali Bwana huziongoza hatua zake/In his heart a man plans his course but the Lord determine his steps. (emphasis added).

Maono ni mchakato wa siku nyingi, Mimi na wewe tunatakiwa kuwa na mipango lakini kazi ya Mungu ni Kuongoza hatua zetu.  Nini muhimu kujua ni kuwa utimilifu wa maono unaanza pale unapogundua maono yako na kupanga mipango ya kuishi maono.

Hii ni rahisi sana, unatakiwa kuishi maono yako, kwanzia sasa kwa kuwa umesha fahamu, huku ukijua kila siku kuna kitu Mungu atakuongoza kufanya.

Njia ya kufikia kutimiza ndoto zetu, inatuandaa kwa vitu viwili muhimu.
   Kwa sababu pamoja na kuona picha ya maono yako ambayo inaweza kukupelekea utamani kufika kesho lakini anakuwa amekuandalia njia ya kwake ya kufikia maono hayo. Kumbuka muda wa mfalme Daudi kupakwa mafuta na kuja kuwa mfalme ulikuwa mrefu sana,

Je, vipi kuhusu Joseph akiwa na miaka 17 aliota ndoto ya kuwa mkuu siku za usoni (Mwanzo 37:9-10), lakini mchakato wa wao haukuwa rahisi ilitakiwa wapite kwenye shule ya Mungu, ili Joseph kuja kuwa mtu mkuu sana Misri, kwanza njia alizopita kama Mungu angemwambia au muonyesha asingefika,angeishia njiani kwa sababu ya ugumu wake.

Ni kweli una ndoto kuwa sana za kugusa maisha ya wengine kwa maana hiyo unaenda kuwa mtu mkubwa na mwenye nguvu hata Kifedha lakini swali ni ulifikia hiyo hatua kubwa bado utaendelea kutenda mema kwa watu au utapotea?

Basi ukiwa katikati ya kufikia ukuu wako Mungu anafanya mambo mawili,

*Moja*
Mungu anatengeza sifa zetu /God develops our character.
Mungu anaanza kukupitisha kwenye mazingira mepesi na magumu ili kukuimarisha, na hapa mtu akipita kwenye changamoto nzito, ndio anakuwa mtu bora zaidi, Joseph alikataliwa na ndugu zake, akauzwa utumwani, hata alipofika utumwani akasingiziwa amembaka mke wa bosi, akitiwa jela na badae kutoka waziri Mkuu. Hapo tayari amejifunza uvumilivu, kusubiri, upole, kuchagua mambo mema, upendo na tabia ambazo hata akiwa kiongozi watu hawata juta, tofauti na leo kuna watu wamekuwa viongozi bila kuandaliwa na kupotelea kwenye nafasi na kusahau kilicho wapeleka.

  Unaweza kuwa na biashara kubwa, huduma, kazi n, nzuri, kampuni kubwa swali je, vipi ukipewa nafasi ya kumiliki leo, utaweza kugusa maisha ya watu au unajitazama wewe tu?

*Mbili*
Kuzalisha majukumu sahihi ndani yetu, Mungu anaruhusu changamoto ili tutambue majukumu yetu, hutakiwi kuogopa, kwani wakati tunazaliwa Mungu alitupa kusudi la kuishi duniani ila hatukujua majukumu yetu kutimoza hilo kusudi, hivyo ni muhimu ukae kwenye Darasa la Mungu ili uweze kujifunza namna bora ya kupifikia kule uwendako.

Mungu alihitaji kumtengeneza Joseph aweze kujizuia au kuwa na kiasi, /self control, ndio maana alimpitisha kwenye jaribu la kusingiziwa kumbaka mke wa bosi wake Potifa.

Ugumu wa maisha ni sehemu ya mpango wa  Mungu kukufikisha kule kwenye kusudi lako.

Mafanikio ni mchakato mrefu sana kuliko tunavyo danganywa na wahamsishaji tukichulia rahisi, ila ukweli tunatakiwa kuweka nguvu, bila kukata tamaa na kuwa na imani kubwa juu ya utimilifu wake.

Saturday, October 13, 2018

BADO WATU WANA NDOTO ZA KUWA MABILIONEA

BADO WATU WANANDOTO ZA KUWA MABILIONEA.

Kuna mabilionea 1,645 duniani.Lakini ni 400 hivi ambao wamekuwa hivyo wenyewe(wengine waliobaki wamerithi fedha zao.)

Katika hawa walioutengeneza wenyewe kwa idadi kubwa ni WAWEKEZAJI.

WAWEKEZAJI.

Haijalishi ni aina gani ya biashara unayotaka kuifanya,anza kuwa na mtazamo,siyo wa ujasiriamali au mfanyabiashara,bali wa mwekezaji.

Hata kama unataka kufungua kibanda cha kahawa,ubunifu wa mavazi,nk.-fikiri kama mwekezaji.

Na hii hapa ni misemo ambayo itakujenga zaidi.Minne niya wawekezaji wakubwa kwa sasa duniani na mmoja ni wa mtu mwenye hekima:

1."Kama hutofurahia kuwekeza katika kitu kwa miaka 10,basi acha kuwekeza hata kwa dakika 10."---Warren Buffett

2."Changamoto huja pale ambapo hujui cha kufanya."----Warren Buffett.

3."Bila ya hamasa,huwezi kuwa na nguvu.Bila ya nguvu,huna chochote".---Warren Buffett

4."Hatuhitaji kuwa na akili nyingi kuzidi wote.Tunahitaji kuwa na nidhamu zaidi ya wote."---Warren Buffett.

5."Uwekezaji wa fikra unalipa faida nzuri."---Benjamin Franklin

Katika biashara ishi na uvute pumzi ya kanuni hizo.Zikumbuke,zitakulinda hata usishindwe.

Chagua kitu kimoja,ambacho una hamasa na nguvu ya kukifanya na kifanye kwa muda mrefu.

Nidhamu itakuja yenyewe ukiwa na kitu kimoja ulicho lenga kukifanyia kazi.

Anza kwa kuwekeza muda mwingi kwenye kujifunza-ijenge akili yako.
Soma vitabu,hudhuria makongamano,tafuta mshauri,ukiwa kwenye gari sikiliza hotuba za wahamasishaji badala ya Singeli....

Mgema Jr

KUACHANA NI FASHION MBOVU

DUNIA YA MAHUSIANO KIFO CHA MENDE-SEHEMU YA 2

DUNIA YA MAHUSIANO KIFO CHA MENDE

I
DUNIA YA MAHUSIANO KIFO CHA MENDE
SEHEMU 1.
Kwa miaka ya sasa yaani kizazi cha dot.com kama ambavyo kinaitwa suala la kuanza mahusiano rasmi na yasio rasmi sana limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa Afrika ukilinganisha na miaka ya nyuma kidogo.
Ilikuwa ni nadra sana kwa vijana ambao nia ya dhati ya kuoa au kuolewa kuwakuta kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini sasa limekuwa jambo la kawaida sana.
Miaka ya nyuma kidogo kukuta jamii ikizungumza mambo haya ilikuwa nadra sana lakini sasa ni kawaida sana na wakati mwingine ndiyo zimekuwa stori kubwa za siku kwa rika zote imani zote na kada zote kwa ujumla.
Stori bila kuwepo stori inazungumzia mapenzi hizo siyo stori tena.
Usasa na kuporomoka kwa maadili kwenda na kasi ya mabadiliko ya sayansi na Teknolojia lakini pia uhuru nje ya mipaka na kila japo kuwa chini ya sheria tetezi kwa vijana wa jinsia zote ni chanzo cha yote haya, imefikia mahali binti au kijana wa kiume kutokuwa kwenye mahusiano ni ushamba yawezekana ni kweli kabisa kwa sababu ushamba ni kutokuwa na taarifa kamili juu ya jambo fulani.
Kuwa kwenye mahusiano sio kesi sana kama nia ya dhati au mapatano ya wawili hawa yana nia moja kabisa na mwelekeo wao wanaufahamu vema.
Shida inakuja hapa wengi tunaingia kwenye mahusiano kama fasheni ili mimi nami nionekane nina boy au Girl friend bila hata kujua kwa nini uko kwenye hiyo chaini ya mahusiano inauma sana.
Wengi tumeingia hapa bila kuwa na elimu na kujua Thamani yake matokeo yake watu wameumiza mioyo ya watu wengi sana siyo wasichana wala vijana wa kiume
Watu wanaugulia maumivu makali kama mkuki wenye sumu kupenya kwenye moyo hakika ni majeraha na vidonda visivyopona.

Kwa kutokujua maana na malengo ya kuingia kwenye mahusiano wengi wamejikuta wakicheza mchezo na kujizawadia mimba ambazo hawakuzipanga mwisho ni kuchomoa na kuua.
Laana ya vizazi na vizazi inazitafuna familia nyingi Roho za watoto walionyofolewa damu zao zinalilia kwenye nyoyo na fahamu za waliotenda mambo hayo.
Laana juu ya laana tukijipa matumaini kuwa Mungu anasamehe siwezi bisha ila tunapishana na mafanikio mengi yenye baraka ndani yake.

Kwa nini umwache mwenzako bila sababu mabinti na vijana wakati mwingine watu wanakula viapo na machozi mengi lakini mwisho wa siku bila sababu ya msingi binti anasema kuanzia leo nasitisha mahusiano wewe...........kumbuka ukiumiza  moyo mtu alieyekuwa amemanisha ni madhara makubwa sana mbele yako.........kumbuka kila ufanyalo kwa wema ipo siku utapokea ijara njema lakini wewe mrubuni wa mapenzi utakufa kwa namna yoyote either kunyimwa watoto au kuachwa pia au kupewa jitu jeuri sana
Acha niishie hapa tutaendelea kesho kutwa
REMEMBER WHAT GOES AROUNDCOMES AROUND
2018 THE YEAR OF ACHIEVEMENTS

Monday, October 8, 2018

GUNDUA UWEZO NDANI YAKO

DISCOVER YOUR POTENTIAL IN YOU/ GUNDUA UWEZO NDANI YAKO ----1

Kila mtu ana uwezo wa kipekee.Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuongoza lakini bado hajafahamu uwezo alio nao .Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuzungumza lakini bado hajielewi .Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kuandika lakini hadi anavyosoma makala hii bado hajielewi maana hajawi kuanza kuonesha uwezo wake .Kwa kutambua uwepo wa watu wengi wasiojua uwezo walio nao nimekuandalia makala zitakazoamsha uwezo ulio ndani yako ili ukufikishe kule unakotaka kufika.

Mungu alivyokuumba aliweka ndani yako uwezo mkubwa sana kwa bahati mbaya watu tumeshindwa kutambua uwezo tulionao.Ni lazima kama unataka kufika kule unakotaka kufika kufahamu kabisa nini unaweza kufanya vizuri kwa uwezo uliopewa na Mungu .Acha kuwasikiliza watu wanaokukosoa na watu wanaokurudisha nyuma .Wewe amini katika uwezo wako ambao uko ndani yako .

Kama unaweza kuimba vizuri fahamu huo ndio uwezo Mungu alikupa .Tumia vizuri uwezo huo bila kugeuka nyuma na utafika mbali sana .Acha kuangalia madhaifu uliyonayo lakini angalia uwezo ulio nao .

Watu waliofahamu uwezo wao (maeneo yao ya kujidai ) na wakajua namna ya kuwajibika ,walifika mbali sana .Je ,watu hawa waliofika mbali hawakuwa na madhaifu ?  Jibu ni Hapana walichokiangalia ni uwezo ambao walikuwa nao kuliko madhaifu yao .

Uwezo ulionao hauzuiliwi na jambo lolote.Haijalishi umezaliwa wapi na unaishi wapi uwezo wako ukiamua kuutumia utaonekana tu.Kama unaweza kucheza mpira vizuri  hakikisha unacheza mpira kwa nguvu na akili yako yote maana hapa ndipo mafanikio yako yaliko .Kama unaweza kuchekesha watu fanya hivyo ukielewa kabisa wapo watu ambao wamefanikiwa kupitia uchekeshaji .

Watu hawa walivyoelewa uwezo walionao maisha yao leo yamebadilika.

Nick Vujic
Nick ni mlemavu asiyekuwa na miguu wala mikono ambaye mbali na kuwa alizaliwa mlemavu hivyo alielewa eneo lake ambalo alikuwa na uwezo nalo .Nick baada ya kuona hawezi kazi za kutumia mikono au miguu alianza kufikiri nini ana uwezo nacho na akagundua anaweza kuhamasisha watu na watu wakahamasika .Nick bila kuchelewa alianzisha taasisi yake ambaye yeye aliiita  taasisi ya maisha bila miguu (life without limbs) na akaanza kuzunguka dunia nzima kuhamasisha watu hasa walemavu .Leo Nick Dunia nzima inamfahamu.

Mwalimu Julius Nyerere
Mwalimu Nyerere ni ni mtu  ambaye alifahamu kuwa alikuwa na uwezo wa kuongoza watu na akatumia uwezo wake kwa viwango vikubwa sana leo Mwalimu Nyerere Dunia nzima inamkumbuka kwa kuwa alitumia uwezo wake aliokuwa nao.

Mbwana Sammatta
Mbwana Samatta baada ya kufahamu kuwa Mungu ameweka uwezo wa kucheza mpira vizuri ndani yake alianza mara moja kucheza mpira .Samatta hakuwa anacheza kama wachezaji wengine wanaofikiria kucheza mpira Simba na Yanga maisha yao yaishie hapo lakini yeye alicheza huku akijua siku moja dunia itakuwa ikimsikia na kufuatilia uwezo wake .Mtazamo wake ulikuwa mtazamo mpana wa kuhakisha uwezo wake unamtangaza Duniani .Leo Mbwana Sammatta Dunia inamjua na hakika mafanikio yake si haba.

MC PILIPILI
MC Pilipili alivyogundua kuwa ana uwezo wa kupangilia maneno na kuongea mbele za watu aliamua kuwa mshereheshaji (Master of Ceremony) .Leo Mc Pilipili amefika mbali sana kwa kuwa siku moja aliamua kutumia kile kilichoko ndani yake

Ni lazima ujue wewe ni mzuri na kufanya katika viwango vikubwa sana bila kuangalia mwenzako anafanya nini .Lazima ufike mahali uorodheshe vitu unavyofanya kwa uzuri na hivyo ndivyo vitakutoa katika maisha .Acha kuamini kuwa vyeti vyako ndivyo pekee vitakufanikisha utachelewa sana .Inuka anza kuangalia nini unaweza kufanya ili maisha yako yabadilike .

Unajua nini ? Unaweza kufanya nini ? unaweza kufanya nini kwa uzuri ? .Amsha uwezo wako leo

Itaendelea.

Friday, October 5, 2018

MANENO YA DIAMOND KATIKA SAFARI YA MAISHA YAKE

MAMBO MACHACHE AMBAYO NI MUHIMU KUJIFUNZA KUTOKA KWA KIJANA MWENZETU DIAMOND ALIYOYASEMA KWENYE SIKU YA KUZALIWA KWAKE

Tahere 2/10/2018 ilikuwa ni siku maalumu sana ya Nasibu Abdul alimaarufu diamond ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake

Kuna mambo mengi sana alizungumza Diamond kuhusu maisha yake ya muziki hata maisha kabla ya mziki yani alikotoka hadi hapa alipo.
Yako mambo mazuri sana ya kujifunza kutoka  kwa Diamond  kwa kijana anayetaka kutoka kimaisha sio tu kwa njia ya muziki lakini katika kila jambo unalofanya.

Nimefurahia sana kusikia yeye mwenyewe akizungumza na kuelezea alikopita na mambo aliyofanya hapo kabla hajawa DIAMOND mpaka alipokuja kuwa DIAMOND offcourse amezungumzia mambo mengi mazuri kama ifuatavyo

Hakuchagua kazi diamond alifanya kila kazi iliyokuwa mbele yake ambayo haikuvunja sheria au kwa lugha nyepesi kazi haramu.......Diamonda
1.aliuza mchanga
2.Alifanya kazi petrol station
3.Aliuza nguo
4.Alipiga picha mfumo wa zamani
Then diamond alisema ili uweze kufanikiwa Pamoja na kufanya kazi kwa bidii mambo yafuatayo lazima yachukue nafasi kwenye harakati zako
a. Ubunifu katika kila kazi unafanya
B. Bidii na maarifa ujuzi pia ni lazima
C. Uaminifu katika kazi yako na kazi za watu hii itakusaidia kujenga brand yako ya kuaminika kwa watu na siku nyingine watu watatamani kufanya kazi na wewe.
d. Kutokukata tamaa...kuna wakati unahitaji mtu fulani awe daraja lako kufikia ndoto zako lakini ni ngumu kumpata lakini unachopaswa kufanya pambana hakikisha adhima yako inatimia
e. Mwombe Mungu sana kwa kila jambo
f. Weka nia ya dhati toka moyoni dhamiria kufikia matamanio yako.


Alisema tena kumbuka kutengeneza mazingira ya watu kukupa kazi ajira na mambo mingine
Hapa akasema kuwa smart kuanzia nje hadi namna ya kufikiri jiupushe na mihadarati haisaidii kabisa.


Katika safari ya mafaniko mambo ya kukatisha tamaa ni mengi lakini usikubali yakushinde bali pambana kuyashinda. Wapo watu wengi sana amabao wanakatisha vijana tamaa kuwa wewe huwezi jambo fulani labda jambo fulani ndo unaweza hapana hilo unaloamini unaliweza na linamanufaaa kwako fanya  pambana mpaka mwisho utafanikiwa.

Tumia kila nafasi unayopata ukijua nafasi nyeti huja mara moja tu kwenye maisha.
MWISHO
Kile Mungu anakupa baada ya kupambana kumbuka haya
Rudisha kwa jamii hata kama ni kidogo watu watakuombea na Mungu atakuinua zaidi ya mahali utakapokuwa
Aliyofanya diamond leo Tarehe 5/10/2018
Kawapa vijana wenzake wa tandale pikipiki 20
Watu 1000 kuwapa bima
Wakina mama 100 amewapa mtaji
Kuna mama mlemavu amempatia bajaji
Katoa Gari kwa mpiga picha wake
Mengi amefanya hakika sadaka humwinua zaidi mtu
Prepared by Moses Mgema
Source Diamond plutnum
Contacts: 0755632375/0678355394
Facebook Moses zephania
Instagram & Twitter moses mgema

NA MAONO YA MAYLES MUNROE

MISINGI NA NGUVU: Dr. Myles Munroe alikuwa raia wa Bahama, aliyezaliwa tar 20/04/1954 na kufariki 09/11/2014.(64) kwa ajali ya ndege Binafsi aliyokuwa akitumia akienda kwenye moja ya mikutano yake akiwa na mke wake na wengine nane walipoteza maisha katika ajali hiyo moja.

Shughuli zake
Alikuwa mhubiri wa kimataifa, mwandishi, mwanzilishi wa huduma ya BFMI (Bahamas Faith Ministry International). mwalimu wa masomo ya uongozi, uchumi, kiroho na maisha ya mafanikio.

Pamoja na kuwa Dr. Myles Munroe ni hayati lakini bado mpaka sasa anaishi kufuatana na kazi yake aliyofanya katika kugusa maisha ya vizazi vyake na kwa kauli yake *nitakufa mtupu* nafikiri ilitimia japo ukianza kufuatilia masomo yake mbalimbali unaweza kuona aliwahi kufa.

Kwa nini Nimekuletea hiki kitabu

Maono ni kitu muhimu sana na kama mtu yeyote anataka mafanikio makubwa sana ya kifedha, kiroho, kiafya, kielimu, kimahusiano na kiakili basi cha kwanza kabisa ni kuwa na maono, na hiki ni moja ya vitabu ambavyo vinaeleza vizuri sana kuhusu MAONO, yani kinaeleza kwa lugha rahisi sana, nini maana ya maono, misingi na nguvu yake katika maisha ya kila mtu

Binafsi nilikuwa nafuatilia namna watu wanavyofundisha kuhusu maono, ndoto na kusudi ila waliyo wengi wameshindwa kuelezea kiusahihi eneo hili, kwani kila mtu amekuwa na uwelewa tofauti lakini nilipo pata kitabu hiki niliona suluhisho kwa kila mtu endapo atapata nafasi ya ya kukisoma kitabu hiki cha Maisha bila maono

Maisha mazuri ni yale ambayo yanatokana na mtu kuwa na picha ya baadae yake, kujua unaenda kufanya nini miaka michache ijayo, kuishi maisha ya namna gani, kukaa na watu gani, na kugusa watu wa aina gani.

Mungu aliweka kusudi ndani ya kila mmoja ndani yake na hiyo ndio thamani yako katika Dunia hii, ndani yako kuna dhahabu ila haiwezi kuchimbwa na mtu yoyote ila wewe mwenyewe hivyo lazima uamue mwenyewe kuishi maono yako, kuwa na maana harisi ya maisha yako.

Pasipo maono huwezi kuona Mbali zaidi ya hapo ulipo leo, kuwa na maono ni sawa na kwenda kukaa kilele cha mlima na muono wako unaongezeka.

Hivyo kama umeishi muda mrefu bila maono ,Myles anatuonyesha kitu ambacho wachache wamekuwa wakiishi na kufanikiwa.

Wednesday, October 3, 2018

JIFUNZE USIIGE MAISHA YA MWINGINE

OHabari za muda huu
Napenda kushare nanyi jambo muhimu sana kwa muda huu inaweza kuwa faida kwako leo hata kesho

Duniani kuna watu ambao wamekuwa wakiishi maisha ya ku copy na ku paste.......Yaani mtu anamuiga mtu fulani kwa kila kitu anachofanya wakati mwingine bila hata kujiuliza kwa nini mtu huyu amefanya jambo hili mwisho wa siku wamejikuta wakiangamia na kupotea kabisa lakini pia kupoteza ndoto na uwezo wao kwa sababu tu waliamua kuishi Maisha fulani ya kukopi.
Kuiga sio jambo baya lakini pia kumbuka kuwa kila mtu ameumbwa kwa kusudi na kazi yake hapa duniani hivyo unapoondoka kwenye kusudi au kazi ambayo Mungu alikupa mwisho wa siku maisha yako yatakoma duniani hapa hakuna ulichokifanya maana uliamua kuishi nje ya kusudi la Mungu

Kumbuka kuwa maisha ni mtihani ambao kila mtu amepewa mtihani wenye maswali tofaut na mwingine.
Kumbuka Maisha ni moja ya mtihani mgumu sana na watu wengi wanafeli kwa sababu ya kukopi Maisha ya wengine pasipo kufahamu kwamba kila Mtu ana maswali yake katika katika chumba cha mtihani.

Hivyo Kijana jaribu sana kukaa chini jikague jitathimini ili kuweza kujipambanua kuwa wewe ulizaliwa na lengo gani
Fanya kazi kwa bidii kuwa mbunifu ongeza maarifa katika kila jambo unalofanya.
Note
Sijasema kuwa usiwe na watu unaopenda kuwa kama wao hapana jifunze kwao njia na kanuni walizopitia kufika mahali walipo then baada ya hapo kaa chini chukua jema tupa kule lisilo faa
Halafu anza kufanya kile moyo na akili yako inakuambia kuwa ukifanya hiki utafanya katika ubora kwa kiwango cha juu na kwa ubora mkubwa zaidi.
Life is too short try to utilize every single second effectively through the natural gift or talent that God created with
Be blessed and have a very good moment 
By Moses