Sunday, December 13, 2020

JANA SIO MWAMZI WA KESHO YAKO.

Usiichukie jana kwa sababu ya mapito uliyopitia, machungu,maumivu makali, kukataliwa kunyanyaswa na kuonekana hufai, umeonyesha juhudi nyingi ukitafuta kuwa wewe halisi, lakini pamoja na juhudi unazofanya lakini hazijakupa matokeo na matarajio sawa na nguvu ambazo umekuwa ukitumia muda wote....

Umefika mahali umeyachukia maisha, umesikia maneno ya walimwengu kuwa riziki ni mafungu saba, umeyabeba nakuyakiri kwenye moyo wako na akili imepokea na kujenga picha kwamba wewe uko upande wa fungu la kukosa.

Umefika mahali juhudi za jana ambazo hazikukupa matokeo uliyotarajia zimekufanya uichukie jana na kuamini kuwa haiwezekani tena, Umekaa chini umesońoneka, huzuni imejaa moyoni, huoni tumaini tena wala mwanga na mwelekeo mpya wa kesho yako, umejiinamia kwa uchungu na uchovu mwisho umelia umechoka

Ushauri wangu kwako.............
Kesho yako usikubali iamuliwe na jana, jana imepita, ifanye kuwa darasa, ujifunze kuwa pamoja na juhudi yawezekana kuna mahalï nimekosea, au nilipatia ila kuna eneo nilïkuwa sifanyi kwa usahihi, fanya Tathimini yako binafsi, jikague kwa uaminifu baada ya evaluation yako ya uhakika, majibu utakayopata usiyapindishe, yakubali halafu yafanyie kazi.

Penye udhaifu wako kubali halafu aanza kupafanyia kazi, penye uimara wako jitahidi kuongeza jitihada mara dufu, jiboreshe zaidi.......

Baada ya hapo simama chukua hatua ya imani, anza upya kwa nguvu kubwa, ikanyage jana kawa jiwe la kuvukia mto, tembea mbele, tazama kesho kwa kujenga msingi imara leo.

Bora kesho msingi wake ni leo, jana imepita, haiwezi kufutwa ila inaweza kufanyiwa masahihisho leo, nakuleta matokeo tarajiwa kesho....

Wote tunapitia changamoto lakini tunakabiliana nazo kwa kuamini kiĺa jambo hutokea maisha for a reason not otherwise.
Moses zephania Mgema

Tuesday, December 1, 2020

BE POSITIVE

Changomoto huimalisha uwezo wa akili na namna ya kuwaza na kufikiri hasa ukichukulia kila jambo kwa namna ya mtazamo chanya. Bila kujali ugumu, hali ya jambo lilivyokuja iwe umetendewa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, au unapitia hali fulani ambayo hujawahi kuitegemea hapo kabla, bado inakupa nafasi ya kuzichulia changamoto hizo katika mlengo chanya.

Chanya huonyesha wepese, huleta kupumua, kulilax, kujipa muda na kuonyesha hatua, njia na mlango wakutatulia au kukabiliana na changamoto iliyoko mbele.

Chanya huleta courage na nguvu ya ziada ndani yako, huleta imani kuanzia ndani ya uwezekano, hujenga ujasiri na hali ya kujiamini bila kujali ukubwa au mlima ulioko mbele..

Hivyo ni vyema kuchukulia kila jambo katika mwelekeo chanya, yakutukwaza na kutuumiza ni mengi, yetu binafsi ya ndugu, rafiki, na mifumo ambayo huendesha maisha yetu,
Hivyo ni vyema kuchukua kila hatua kwa mlengo chanya ili kuweza kuishi maisha ya furaha na afya ya akili, nafsi mwili na roho.
Relax
Be positive, 
Focus

Monday, November 30, 2020

ELIMU NI MASTER KEY 4

Kila mmoja amezaliwa na uwezo wa asili (Natural ability) lakini wakati mwingine ni ngumu kujijua na kujua thamani ya kile ambacho tumkibeba ndani yetu...

Kipaji ni ni kifurushi kamili (complete package) ambacho tunapaswa kukitengenezea mazingira mazur ya ustawi wake. 

Katika nchi za magharibi kupitia elimu wamewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye uwezo halisi wa mtu ndiyo maana kiwango cha ubora katika mambo mengi wanayofanya iwe katika mambo ambayo tunayaona ni kama kazi zinazoshusha hadhi kwa upande wa nchi za dunia ya tatu.

Wenzetu wanajal sana passion ya mtu kuliko matamanio yetu, ndiyo maana tunaweza kuona hata malezï na makuzi ya watoto hufuatiliwa kwa karibu sana lengo ikiwa ni kugundua ubora na uwezo wa mtoto kupitia michezo ambayo anaifanya kila siku.

Pamoja na kwamba dunia tuliyo nayo imekuwa ni dunia bize sana kwa maana ya wazazi na walezi kutingwa na kazi, lakini pia hata kwa muda mchache wamekuwa wakitoa muda wao kwa ajili ya kuwa karibu na watoto wao, lengo kubwa ni kufanya ugunduzi wa mtoto/watoto wao ni kina nani.

Utambuzi wa vipaji na passïon imesaidia kwa kiwango cha juu kuwapeleka watoto wao kwenye nafasi wanazo fiti kwa kiwango cha juu sana.

Ndiyo maana sasa unaweza kuona kuna watoto wanakwenda shule kupata elimu ya kawaida ambayo kila mtu ni haki yake, lakini bado wana muda wakufanyia mazoezi na kujifunza kwenye eneo la passion zao.

Mfano mzuri ni kwa mcheza mpira wa chini ya miaka 17 Kelvin John ambae alipata nafasi ya kwenda Ubelgiji kwa ajili ya kuendeleza kipaji cha mpira, lakini bado walimpeleka nchini England kwa ajili ya kuendelea na elimu ya kawaida lakini vilevile kupata muda mzuri wa kujifunza kwa ubora namna ya kuboresha na kukipa thamani kipaji chake.

Mtoto akiwekezwa kwenye eneo la uwezo wake na passion yake humfanya kutimiza majukumu yake kwa upendo, na kwa moyo wote kwa sababu anachokifanya sio kazi tu bali ni eneo linalompa furaha pia, hivyo hata kama kazi itakuwa ngumu kiasi gani bado ataendelea kufanya kwa sababu kwanza anapenda, anafanya kwa passion kwa hiyo kiwango cha ubora katika kazi hiyo kitakuwa cha kiwango cha juu sana.

Baadhi ya wazazi wanapenda na wanataka watoto wao kuwa madaktari, wahandisi, nk, lakini mtoto unakuta anataka kuwa mchoraji, mwalimu, au kuwa yeye kwa kile anakita tusiwanyime au kuwazuia kufanya wanachokipenda bali kama unaona mwelekeo au uchaguzi wa mtoto sio sahihi kwa maoni yako mshauri kwa upendo na kumweleza matokeo ya kile anachopenda kuwa haiwezi kumpa future nzuri.




ELIMU NI MASTER KEY 3

Elimu ni ufunguo ambao unatakiwa kutumiwa kwa ajili ya kufungua kila mageti na milango ya fursa kuanzia mtu binafsi mpaka kwenye mazingira ya nje...

Elimu ya kumfanya mtu kujielewa/kujitambua na kuelewa mazingira yake. Mungu ameumba kila mtu na kumpa uwezo na nguvu ya kujitawala, kujimiliki na kuyamudu mazingira yake.

Hivyo kitu ambacho tunapaswa kufanya kwenye mfumo wa elimu yetu, hata kama mitaala ya elimu rasmi bado haujabadilika ni vyema kutumia mifumo mingine ya elimu ambayo inatuwezesha kuwa na uelewa mpana zaidi wakujifahamu.

Elimu isiyo rasmi ipo kila mahali, kuanzia kwenye mazingira tunayoishi, kupitia mitandao ya kijamïï, websites, vitabu na vyanzo vingine vya maarifa ambavyo upatikanaji wake umekuwa rahisi sana.

Hivyo ni vyema kutumia uwepo wa teknolojia kubwa tuliyo nayo kwa sasa hapa duniani ambayo imetusogeża karibu zaidi na wenzetu waliotutangulia katika maendeleo na elimu ya kujitegemea.

Kuendelea kulaumu serikali ni kujichelewesha kufikia malengo hivyo kubaki kwenye maumivu, na lawama ambazo haziwezi kutatulika bila kuchukua hatua.

ufahamu ni jambo la msingi sana katika kufikia hatima na malengo ya kila mtu.
Tuna vipaji, vipawa na karama kubwa ndani yetu ambavyo ni uwekezaji wa Mungu kwetu.. 

Next epsode tutaangalia kwa mfano namna ambavyo tukiongeza maarifa kupitia namna nzuri ya kujifunza tunaweza kuona ni kwa kiwango gani vipawa vyetu vinaweza kutufanya kuishi kwenye ndoto, malengo na kusudi la uwepo wa vipaji hivyo ndani yetu... 
Tukutane next epsode....

Thursday, November 26, 2020

ELIMU NI MASTER KEY 2

Ugunduzi wa elimu duniani ulikuwa na maana kubwa sana kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu. Elimu ni zaidi ya fedha, ni zaidi ya siasa ni zaidi ya dini, elimu ni jumla ya maisha yetu ya kila siku
( Elimu ni jumla ya yote niliyoyataja hapo juu, ukitaka kujua kuwa elimu ni msingi wa mambo yote, mtu anaweza kupambana pekee yake kutafuta katika hatua za awali akifikia hatua ya kumiliki fedha nyingi na utajiri mwingi atahitaji watu wenye elimu ya fedha ili kuweza kuifanya fedha yake iendelee kuishi na kuongezeka zaidi, atahitaji wataaluma kwenye idara mbalimbali ili kumchorea na kumfungulia ramani na milango ya fursa ili kuifanya fedha iishi na kuzalisha zaidi.

Katika kitabu kitakatifu cha Biblia, Methali anasema mkamate sana elimu usimwache aende zake maana ni uzima wako, wahenga na watunzi wa Methali na misemo mingine wakasema Elimu ni mlango na ufunguo wa mafanikio ya mtu katika levels zote za maish yetu.

Tena wakasema wahenga mali bila daftari hutoweka bila habari, maana yake ni kuwa mali bila kuweka kumbukumbu hupotea bila kujua (elimu ya kutunza kumbukumbu hufundishwa kuanzia nyumbani, hapo ndipo unajua umuhimu wa elimu).
Watu wengi tumeishi nje ya ndoto na kusudi la Mungu kwa sababu ya kukosa ufahamu juu ya hazina kubwa ambayo Mungu amewekeza ndani yetu.

Elimu tumeiweka kwenye mfumo wa maisha ambayo jamii imeamua kuishi kwa kukariri, jamii inaamini kuwa elimu ipo kwa ajili ya kutumilikisha nafasi za juu katika ajira nasio kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa ajiri ya wengine kupitia ugunduzi wa mambo au kuongeza ubora katika vile ambavyo vilishakuwepo tayari.

Wazazi wengi wameua ndoto za vijana wengi kwa sababu ya kukubali kuishi mfumo wa kukariri katika jamii zetu,
Kwa kukosa maarifa, na elimu yenye kuimarisha ufahamu tumeamua kuchagua maisha ya aina moja, sio ajabu mzazi kuua ndoto ya mtoto wake kwa sababu anataka matakwa yake yatimizwe na mtoto wake, utasikia mzazi/mlezi anamwambia mtoto, umemaliza kidato cha sita uende ukasomee Ualimu ili upate ajira uwasaidie ndugu zako, mtoto alitaka kuwa daktari, mwanasheria na taaluma hizo zinakuwa hazina nafasi kwa upande wa mzazi kwa sababu zinachukua muda mrefu nk.

Mtoto anataka kutumia kipaji chake badala yakusaidiwa mzazi anakuwa mkali kama pilipili, usïponisikia ntakulaani, kama sijakuzaa mimi tutaona sasa mimi na wewe nani alitangulia kuliona jua, au nani amemzaa mwenzake si umekuwa, kijana wa watu anaanza safari nje ya ndoto zake bali  kutimiza matakwa ya mzazh

Kama wazazi, walezi tunamalaka juu ya watoto wetu, lakini sïo kuua kilicho uwezo na kusudi la maisha yao, tuna nafasi ya kushauri na kuwajeng ila sio kutaka kutimiziwa matakwa yetu, tuwasaidie tusiwazime, akiwa anauchaguzi sio sawa tafuta namna nzuri ya kusema nae akuelewe kuliko kutumia nafasi yako kama mzazi kuua

Jamii imeua vipaji na karama za asili nyingi kwa vivuli vya kwamba nataka usome ikiambatana na mifano mingi ya walïoshindwa, wazazi na walezi tumeua asili ya uwezo na uwekezaji wa vipaji wa Mungu kwenye maisha yetu  njia ya kivuli na kisingizio cha elimu...

Mwana wa Mungu Yesu anasema hakuja kutengua torati bali kuiendeleza, kuiboresha, kuifanya iondoe mamlaka ya kuchukua maamzi ya kuumiza wengi
Ndivyo ilivyo hata katika ugunduzi wa elimu, lengo la elimu ni kutupa uwezo na kujenga ufahamu wa kila mmoja kwanza kujijua zaidi, kuziona fursa, kuongeza ufanisi na ubora katika vile tulivyo navyo
Elimu nzuri ni ile ambayo imesemwa kwenye Methali kuwa ni uzima.

Elimu sio kiua ndoto, sio mficha na muua vipaji na vipawa vya asili ( dream killer, Is not a Talent hider and killer ).

Elimu ni ufunguo hazina kubwa iliyo kwa watu wengi, lakini namna gani tunaweza kuitumia elimu ili kutufanya kuishi kwenye kusudi la maisha ya ndoto zetu..
kwa kisingizio cha elimu tumelazimisha vipaji vya waimbaji, wacheza michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, pete, wavu, kikapu, wachekeshaji, wafanyabiashara nk kwa sababu ya kukosa ufahamu wa elimu tunayoihitaji...

Mfugaji wa mifugo mingi alikufa akilalia ngozi, kula nyamafu, kulala kwenye tembe huku utajiri ukienda mbugani kuchunga na kurudi jioni zizini na aliona fahari, Je yule mama aliyefurahia kuona vikombe, masufuria, flask nzuri, masahani ya udongo nk. kwenye kabati lake zuri la vyombo akisubiri wageni asiojua watakuja lini ndô wavitumie, Je ile familia ya mama mfuga kuku ambae aliwafanya watoto na familia ishi kwenye kauri ya wageni njoo ili nasi tupone. Kwa kukosa elimu masikini mama, baba na familia zile walikwa katika hali ambayo hawakuistahili kabisa, sababu ya yote hapa ukosefu wa elimu ya ufahamu.

Ndivyo tunavyoishi tulio wengi leo, tuna hazina zimetuzunguka kwenye familia zetu, jamii kwa ujumla, tunalia kwa uchungu kwa kukosa vyanzo vya ajira wakati ajira tunaishi nazo makwetu....

Mwandishi nguli wa vitabu na journals toka Marekani hayati Dr. Myles Munroe aliwahi kuandika kweye kitabu chake cha Maximize your potential, alisema '' yadi chache kutoka kwenye milango yetu kuna nyimbo zimerudi nyumbani bila kuimbwa, vitabu vimerudi bila kusomwa, na vipawa vingi viko kweye makaburi ndani ya mashamba yetu

Dr. Myles alisema utajiri wa dunia hii hauko kwenye vitaru vya mafuta kule Qatar, Kuwait, vitaru vya mïgodi ya dhahabu kule kusini mwa bara la Afrika, Congo hata Katika migodi ya Tanzanite kule mererani, Almasi na dhahabu kwenye ardhi ya nyumbani kahama na shinyanga na maeneo mengi ya nchi yetu, bali utajiri either tumekubali watu kufa na talanta zao, au tumeamua kuvifungia kwenye kifungo kinaitwa elimu isiyo na matendo....
Tunahitaji kujua maana halisi ya elimu, elimu, kwa sababu Elimu ni master key wa mambo yote, ufunguo elimu hutumika kufungua mageti ya hazina zetu......
Next.......
Tukutane kesho...

Tuesday, November 24, 2020

ELIMU NI MASTER KEY YA HAZINA YAKO

Hazina ya Baba ambae hakujua kuwa duniani anaishi mara moja alifuga maelfu ya mifugo ya aina mbalimbali kondoo, ng'ombe, mbuzi nk, aliishi maisha ya shida akilala kwenye nyumba ya tembe, akilala kwenye ngozi ya mnyama, alikula michembe, makande, ugali na migagani(michicha pori) na aina nyingine ya mbogamboga kutoka kwenye ardhi...
Watoto walichomwa jua, miba na kunyeshewa mvua wakiwa kwenye nguo chafu zilizochakaa (madaso) wakichunga mifugo ya baba yao, shule kwao haikuwa fahari, nyumba nzuri kwao ilikuwa habari ngeni, macho yaliwaonyesha hazina ya Baba ilivyotengeneza fahari na majivuno kijijini, familia iliheshimika kijijini na watu ambao waliishi kwenye nyumba angalau za bati na kulala kwenye vitanda vya kamba.
Lakini pamoja na ufahari wa macho ya wale mifugo, lakini leo wanaishi ya kujiinamia na majuto mengi mioyoni mwao, baba akiwa amelala milele, shubiri ijuu yao kutwa mkono shavuni, ile fahari haipo tena...ndipo ambapo tunasema bora kufa huku fikra zako zinaishi kuliko kuishi mwili wakati fikra zimekufa.....

Mzee huyu tajiri wa ng'ombe namfananisha na mama mmoja aliyemiliki kabati zuri la vyombo na kununua vyombo vya Thamani nakuviacha kwenye kabati zuri vikipigwa vumbi akisubiri wageni asiojua watakuja linï ili wavitumie ajabu....

Hawa wawili nawaunganisha na msemo wa kale usemao kwamba MGENI NJOO MWENYEJI APONE, eti kama hakuna mgeni basi kuku wataendelea kuzaliana na kuliwa na mwewe huku familia wakila mlenda na mchicha pori...
Hawa wote wamekufa wakiwa na utajiri kweye hazina zao, walidhani kumiliki mifugo, kuhifadhi vyombo kabatini, kusubiri wageni ndo wachinje kuku ndo fahari na ndiyo maisha...
Baba huyu amekufa akiwa amezoea kula mboga za majani, amelala kwenye tembe, amewanyima watoto haki ya elimu, sasa amekufa, mama leo watu wanatumia vyombo vyako ukiwa umelala kwenye sanduku....
Yako mambo mengi ambayo yanaweza kutupa mifano hai ya maisha ya wazee wetu ambao waliishi maisha ambayo hawakuyastahili.   ...
Mungu amewekeza kwa kila mtu hazina (Treasure)kubwa sana ambayo ni full package ambayo kila mtu inaweza kumfanya kuishi kwenye lengo na kusudi la Mungu...
Upo uwezo wa ajabu kwenye uumbaji wa kila mtu, asili ya mwanadamu ni uwezo, kutawala na kutumia ile hazina iliyo ndani yeke, tumechagua maisha ya mfugaji, mama mwenye kabati zuri na vyombo vya gharama ndani yake au yule mama mfuga kuku aliyechagua kusubiri wageni waje ili na yeye apone...
Elimu ni master key ambayo inaweza kutufungua macho ya ndani na kufungua hazini iliyosheheni utajiri wa aina mbalimbali....
Tukutane kesho kwenye makala hii ambayo naamini itakupa kuijua hazina yako na ya watoto wako na itakusaidi kuepuka maisha ya mfugaji, mama mmiliki wa kabati zuri lenye vyombo vizuri au mama mfuga kuku anaesubiri mgeni aje ili nae apone....
0715366003/0755632375

Thursday, October 22, 2020

Dr. Paul book

Aliweza kununua kiwanja maeneo ya mtaa wa kindai Mkoani Singida na kuanza kazi ya kufyatua tofauli na kuanza ujenzi kwa mikono yake mwenyewe  kwa sababu alijigunza ujuzi wa kujenga nyumba, hivyo kwa kushirikiana na Mke pamoja na watoto wake waliweza kujenga nyumba ambayo ipo katika mtaa wa kindai mkoani Singida.
Maamzi ya Dr. Paul ya kuamua kujenga nyumba yake na kuondoka kwenye nyumba ya kanisa pamoja na kwamba haikupokelewa vyema na baadhi ya wachungaji na waumini wa kanisa kutokana na utamaduni ambao ulikuwa umezoeleka tangu awali kwamba makazi ya mchungaji yalipaswa kuwa kanisani, lakini Dr. Paul alisimamia malengo na sababu za kutoka kwenye nyumba ya kanisa sababu ili kuwa ni (.............)
Miaka michache baadae watumishi wa Mungu walimwelewa kwa nini alichukua uamzi huo, na kupitia maono yake ya kuhakikisha mchungaji anajitenga na kanisa kwa maana ya sehemu ya kuishi umeleta manufaa kwa watumishi wa Mungu na kujenga heshima kuanzia kwa mchungaji na familia kwa ujumla.
Pamoja na kwamba yeye alijenga nyumba yake, lakini pia amekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wachungaji wote kuwa na nyumba zao ili kujenga heshima ya utumishi wao kwa kanisa lakini pia kwa familia zao, baadhi ya juhudi zake kwa wachungaji kuwa na nyumba zao ni pamoja na hamasa aliyoitoa kwa Mchungaji Boniface Ntandu kujenga nyumba yake pamoja na Mchungaji Philipo Sospeter ambae aliweza kujenga nyumba yake pia katika mtaa wa jineri na wachungaji mbalimbali wamekuwa wakifanya hivyo na kuondokana na mtazamo wakuishi kwenye nyumba za kanisa.
 

Saturday, July 18, 2020

NGUVU YA MUNGU NDANI YA MKRISTO.

SOMO: NGUVU YA MUNGU NDANI YA KANISA.
 2 Wakorintho 2 :4…., Wakorintho 4:20
NGUVU ni uweza au mamlaka ya kufanya jambo Fulani,
 sisi kama wakristo tunahitaji nguvu ya kutuwezesha kutenda mapenzi ya Mungu na kazi za Mungu duniani, na Biblia inasema hatuwezi kutenda , kwa usahihi duniani kama hatutakuwa na nguvu za Mungu.

unapoongelea ukristo mahali jua unaongelea nguvu kwa maana ukristo ni nguvu.

Injili ya Yesu kristo imejengwa katika nguvu za MUNGU.
Kama tulivyoona ukristo sio maneno matupu tu au tunavyokili bali ukristo umejengwa kwenye nguvu ya Mungu.. nguvu ya kuponya, kufufua, kufungua na kuokoa..
na ndio maana mtume Paulo anasema Wathethalonike 1:8
1 Timotheo 1:7.. ´´Mungu hakutupa roho ya hofu bali roho ya nguvu ´´
na ndio maana biblia inasema kuwa ´´nanyi mtapokea nguvu akishawajilia juu yenu Roho Mtakatifu
Waefeso 3:20.. ´´ kulingana na NGUVU itendayo kazi ndani yetu´´ ndani ya kila mtu aliyeokoka kuna nguvu ya Mungu..
Waefeso 6:10 ´´katika uweza..¨ uweza unamaanisha nguvu.
1 Wakorintho 1:18 ¨ujumbe wa msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi lakini kwetu sisi tunaoamini ni nguvu ya Mungu¨ kumbe kwenye msalaba wa Yesu Kristo kuna uweza uletao wokovu. Msalaba wa Kristo una nguvu.

UKIWA NA NGUVU YA MUNGU NDANI YAKO UNAWEZA KUFANYA HAYA.
i.)Msamaha.
 Luka 23: 34 - alisamehe.. watu wa dunia wanaweza kukwambia nimekusamehe lakini sitasahau lakini Yesu akiwa msalabani na katikati ya maumivu makuu ya msalaba akasema ´´ baba wasamehe maana hawajui walitendalo
ii.)Nguvu ya Mungu ndani yetu inatupa nafasi ya kukumbukwa na Yesu.
 Luka 23:42-43 - ¨
na kwa andiko hili tunajifunza kuwa nguvu ya Mungu inatupa nafasi ya kukumbukwa kwenye Ufalme wa Yesu.Mungu anakumbuka maombi yako, kazi yako nk.
iii.)Hutakufa
Luka 23:46, Kwa mtu yeyote aliyeokoka ,amekabidhiwa kwenye mikono ya Yesu kristo.. na hutakufa mpaka siku ya Bwana , kwasababu roho yako imekabidhiwa kwenye mikono ya Yesu Kristo.. huu ni ulinzi ambao kila mtu aliyeokoka anakuwa nao.. tupo mikononi mwa Mungu na hakuna mtu awezaye kututoa kutoka katika mikono ya Yesu Kristo..
iv.) Ukiwa na nguvu ya Mungu unajenga mahusiano na Mungu.
Yohana 19:29 Yesu akiwa msalabani , alikuwa anajali mahusiano.. hii inaonyesha kuwa msalaba wa Yesu unatupa usalama ndani ya mahusiano na wazazi na watu wengine.. Msalaba wa Yesu unatupa mahusiano bora . ukimwomba Mungu akupe nguvu ya mahusiano.. Kumbe msalaba ulileta Nguvu ya upatanisho.. Nguvu ya Mungu inaleta watu pamoja , pamoja, familia pamoja.

v) Nguvu ya Mungu inatupa kiu ya kumtafuta Mungu. Yohana 19:28
vi) Ukiwa na Nguvu ya Mungu unakuwa na mamlaka Luka 10:19
vii) Unapata uwezo wa kuombea na watu kupokea uponyaji
Luka 5:17..... Luka 4:18

Friday, July 3, 2020

Faida za kumtumikia Mungu

The benefits of serving God - Part 1
The apostle Paul made an intriguing statement in his letter to Timothy,
'This know also, that in the last days perilous times shall come. For men shall be lovers of their own selves...' (2 Timothy 3:1, 2) Pay attention to these words, 'Perilous time shall come because men shall be lovers of their own selves.' Our minds automatically go to the world when we hear and read these words especially when we see what is going on in the secular but the same can be applied to the church. Today a lot of believers in the church are happy to only show up for Sunday services and most are self serving and wallowing in self indulgence without ever giving a thought to serving the Lord who redeemed them from sin and eternal damnation.  That is not a criticism of the modern church but a matter of fact statement.
The Christians of yesteryear had a different concept of serving God. They would lay their lives down for the Gospel. It would not be unusual for a young soul to be converted years ago and be aflame to reach the world for Jesus. This was in spite of a lack of technological and communication advancement as well as the travel facilities that we enjoy today. Yet the Gospel reverberated around the world as wild fire. Millions upon millions of souls were added to the kingdom of God. Today we have everything at our disposal and we are not taking advantage of it because many in the church are simply not passionate about serving the Lord.
God has done much for us in the saving of our lives by sending his own Son as our redeemer and sin-bearer. To serve God is not a grievous or hard task because God is a great boss and a great rewarder. In fact the Bible reveals to us that there are great benefits in serving God.
And ye shall serve the Lord your God , and he shall bless thy bread, and thy water; and I will take sickness away from the midst of thee . There shall nothing cast their young, nor be barren, in thy land: the number of thy days I will fulfil . I will send my fear before thee, and will destroy all the people to whom thou shalt come, and I will make all thine enemies turn their backs unto thee. And I will send hornets before thee, which shall drive out the Hivite, the Canaanite, and the Hittite, from before thee.
Exodus 23:25-28
These verses could not be any more clearer to us that serving God is for our betterment and profit. Here are a few benefits of serving God. When you serve God,
He will bless your bread and water
He will take away sickness from your midst
There will be no miscarriage
There will be no barrenness
There will be no premature death
You will have long life and fulfill destiny
Your enemies will turn away from you
THERE IS NO MAN OR WOMAN WHO SERVES GOD THAT WILL WALK AWAY EMPTY HANDED. GOD WILL NEVER OWE YOU ANYTHING
Here is another great undeniable verse that shows the profitability of serving God,
 If they obey and serve him, they shall spend their days in prosperity, and their years in pleasures.
Job 36:11
I want to encourage YOU to get involved in serving God. You may ask,
'So how do I serve God?' Allow me to give you seven ways,
1. Serve God with your life
2. Serve God in your church
3. Serve God with your talents
4. Serve God with your time
5. Serve God with prayers and fastings
6. Serve God with your money - tithes and offerings
7. Serve God by serving others
You will never be at a loss when you serve God. He has done much for us and he will do much more for you. I want to challenge you with the words of President John Kennedy. In 1961 during his Inaugural Address, President Kennedy uttered these powerful words, 'My fellow Americans, ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country.'
Today, I am asking you, 'My fellow believers, ask not what your God can do for you, ask what can you do for your God.'
A few words about Glenn

Friday, June 26, 2020

KUMTUMIKIA MUNGU NI NINI ?

KUMTUMIKIA MUNGU NI NINI?
Martin Luther King alisema"Fundi viatu mkristo hataweka misalaba midogo midogo kwenye kiatu anachotengeneza ili kuonyesha ukristo wake, bali atatengeneza viatu vizuri na imara".
Wengi tunajua kumtumikia Mungu ni nini...lkn leo nataka tuongeze ufahamu kidogo tu. Tujue zaidi.
Kumtumikia Mungu ni kufuata yale ambayo anatuagiza tuyafanye kwa kiwango kitakacho mfanya yeye Mungu kuwa Mkuu sana. Ni kujikabidhi kwake na kufanya yale yampendezayo kwa namna ambayo utukufu wake utaonekana.
Joshua 24:15
Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
Kumtumikia Mungu ni neno pana sana. Ni zaidi ya kushinda kanisani. Ni zaidi ya kusafisha kanisa. Ni zaidi ya kujenga kanisa kuuubwa. Ni zaidi ya kuimba praise team na kwaya. Ni zaidi ya kutoa sadaka nene. Ni zaidi ya kuwa mzee wa kanisa na mhubiri. Kumtumikia Mungu ni kule kuishi kwa unyoofu ambao tunakuwa kielelezo kwa wengine na hivyo utukufu kurudi kwa Mungu.
Matendo ya Mitume 17:24-25
Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na nchi; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu. 25 Wala hatumikiwi kwa mikono ya watu kana kwamba anahitaji chochote kile, kwa maana yeye mwenyewe ndiye anayewapa watu uhai, anawawezesha kupumua na anawapa kila kitu.
Kumtumikia Mungu ni tofauti na kutumikia wanadamu. Wanadamu hupokea kitu kutoka kwako pale unapowatumikia la sivyo kuna madhara yatatokea. Mungu hata kama anasema anataka sifa, asipopokea hapati madhara yoyote. Ataendelea kuwa Mungu na ukuu wake unabaki palepale. Anachotaka kwetu ni uchaji tu. Tena ni kwa ajili yetu zaidi.
Mzee Petro anaandika maneno magumu kidogo kuhusu utumishi. Msikie..
1 Petro 4:11
Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumika anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.
Huo ndio utumishi. Kuna mahali Yesu anasema "msiposifu ninyi mawe yatasifu". Ana maanisha, kama wasipofanya wale waamini,basi hata wasio waamini watafanya. Mungu atamtumia hata asiyemjua yeye Mungu kutimiza kusudi lake. Kumbuka,kusudi la Bwana husimama hata iweje. Iwe mvua au jua. Mawio au machweo.
Ukimcha Mungu, vitu vitakutumikia. Usiseme sina chochote, wewe si mahiti. Tumika kwa kidogo ulichonacho maana Mungu wetu yeye huangalia moyo.
Kuna mtu alimuomba Yesu ruhusa ya kwenda kuzika mzazi wake, lakini pamoja na heshima ya mahiti, Yesu akamwambia waacheni wafu wazike wafu wao. Yesu hapa alikuwa akionyesha uthamani wa kumtumikia Mungu haulinganishwi na kitu chochote.
Muinjilisti Marko ananukuu Maneno ya Yesu juu ya utumishi
Marko10:45 "Maana hata mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe, bali nilikuja ili niwe mtumishi na kutoa maisha yangu yawe fidia kwa ajili ya watu wengi.”
Kujitoa kwa ajili ya wengine ndio utumishi. Wale ambao hawapo kwa ajili ya kutumikiwa bali kutumika ndio watumishi. Na sio other way around. Lkn watumishi wa leo wengi wetu hatupendi kutumika tu. Tunapenda kutumikiwa na kama sio kutumikiwa basi tupate kitu kutoka kwa hao tunaowatumikia in return!
Warumi 12:1-2
Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho. 2 Msiige tabia na mienendo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.
Paulo anatuambia kuwa kwakuwa tumepata wokovu kwa damu ya Yesu,sasa ni jukumu letu kujitoa sisi wenyewe kama sadaka hai mbele za Mungu (kama shukrani zetu kwa Mungu au sadaka kwa Mungu) huku tukichukua tabia mpya za nje ya dunia hii (mbinguni). Kwa kufanya hivyo tutaweza kuyajua mapenzi ya Mungu kwetu ili tuishi kwa ukamilifu na kumpendeza yeye ambako ndiko kumtumikia Mungu.
Petro anasema( kwenye hiyo 4:11) kuwa,kila mtu atumie kipawa alichopewa kwa uaminifu. Popote pale ulipo kazi yako na yangu ni kuwa balozi wa Mungu kupitia matendo yetu katika mahali tulipo. Kila MTU atumie kipawa chake kwa namna ambayo inamuinua Mungu. Ndio maana ya kuwa kielelezo. Pale watu wengine wanapotutazama kwenye mambo yetu na kila kitu tunachofanya kama wakristo wamuone Mungu. Wauone Upendo wa Mungu. Wauone uwepo wa Mungu.
Martin Luther anasema yule fundi viatu anapoweka misalaba midogo midogo kwenye kiatu FEKI,hapo hajawa mkristo wa kweli kwa kuweka hiyo misalaba. Kwanini? Hajatumia talanta au kipaji chake kwa uaminifu. Kumbe UAMINIFU ndio msingi wa utumishi.
Vipawa tulivyonavyo ni kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu na kuwasaida wengine. Nia ya Mungu kwenye hii dunia ni kufanya kuwa mahali pazuri sana pa kuishi. Na nia hii inatimia kupitia sisi ambao ndio tunakaa kwenye hii dunia. Hakuna mtu asiye na kipaji chochote. Kila mtu ana kipaji labda kama hajui kipaji chake. Sasa vipaji ni vya nini? Kwanini wanadamu tupewe vipaji ndani yetu? Ni kwa ajili ya kuwatumikia wengine na utukufu urudi kwa Mungu.
Leo wengi tunadhani kumtumikia Mungu ni kusimama madhabahuni na kuhubiri. Au kuwa wazee wa kanisa. Au kuimba kwaya flani au kufanya chochote ndani ya kuta za kanisa. Lkn si wote wanaweza kupata nafasi za kufanya hayo. Wengi hujikuta wana maisha nje kabisa na mbali ya kanisa. Kumbe hapo ulipo ndio utumishi wako ulipo.
Twaweza kumtumikia Mungu kwa..
1)Kusambaza Upendo.
Wagalatia 5:14
"Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Inashangaza ambavyo tunaishi pamoja lkn hatujishughulishi kujuana. Tunawekeana mipaka ambayo haina upendo ndani yake. Kwa mfano ,mlinzi wa geti Ia kanisa lako,umeshawahi kumuuliza mara ngapi familia yake inaendeleaje wakati unampa kadi ya kukuruhusu kutoka na gari yako? Shoe shiner(muosha viatu) wa pale ofisini kwenu je? Yule mpika chai wa ofisi? Anayekuoshea gari je? Unadhani wao wanakutazamaje? Lini umeshawahi kuwa" tip"kama unavyowatip kule kwingine? Kupeana moyo,kuongea kwa Upendo ndio kutumika huko. Tunakuwa mfano wa maisha ya ukristo kweli.
2)Kuwasaidia wenye uhitaji
Mathayo 25:40
“Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinifanyia mimi.’
Kuna mambo madogo madogo mengi ambayo hatuyapi umuhimu kwetu lkn kwa Mungu yana maana sana. Unaweza ukainunulia familia flani masikini unga kidogo na kuwapatia kwa ajili ya chakula chao cha mlo mmoja. Machoni kwa Mungu hicho ni kitu kikubwa sana. Mungu kawaumba hao kuleta uwiano baina yetu. Au kumsaidia bibi kuvuka barabara.. Kumpisha mama mjamzito au mzee kwenye seat ya daladala ni vitu vidogo lkn vina maana kubwa. Kadri tunavyowatendea hao ndivyo tunavyomtendea Mungu. Sio lazima uende Orphanage Centers na makamera kedekede ili kuwatangazia watu unayofanya. Haufanyi kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Waebrania 13:2
Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.
3) Kuitafuta hekima
Mithali 16:16
"Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha".
Visu hunolewa. Magari huitaji mafuta na mkristo anahitaji hekima ya Mungu na ufahamu. Ni jukumu la kila mkristo kujibidisha kupata elimu juu ya Mungu. Maarifa juu ya Mungu. Sio vema kuacha kila kitu kwenye mikono ya wachungaji pekee bila sisi wenyewe kujibidisha kutafuta maarifa juu ya Mungu. Namna hii tunakuwa tunayajua mapenzi ya Mungu na hivyo kumtumikia. Kumbuka, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe siku ile ya hukumu.
4)Samehe
Marko 11:24-25
Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. 26 Lakini msipowasamehe wengine, hata Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.
5) Weka nafasi kwaajili ya ibada
(Wagalatia 5:24-25)
Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Unapoamka asubuhi na kujiona mzima au unaumwa,unamshukuru Mungu? Unamtukuza Mungu? Kila ambacho anakifanya kwako na ukajiona upo hai bado ni cha kumshukuru yeye. Mwambie asante kwa kazi yako uliyonayo. Uhai wako. Ndugu zako. Kila kitu mshukuru maana kuna wengi hawana hivyo ulivyonavyo. Shukrani ni utukufu kwa Mungu.
Kumtumikia Mungu ni muhimu kwakuwa tunatimiza yale ambayo Mungu ametuumbia kuwepo hapa duniani na kuyafanya. Kila mtu pale alipo kwenye anachofanya akifanye kwa uaminifu. Akifanye sio kwa sifa binafsi bali kwa ajili ya kuwa kielelezo cha ukristo wake. Yani Kristo ainuliwe kupitia matendo yetu. Kila tunachofanya kifanyike kwa namna Mungu anayopenda tufanye. Ukiwa rubani, muosha magari, fundi muwashi, engineer, mfanyabiashara,mhasibu, nesi au popote pale ulipo kwenye hicho unachofanya, kifanye kwa uaminifu. Kwa kadri kilivyopaswa kufanyika ndio kumtumikia Mungu. Kuacha zile 10% ambazo si za halali. Rushwa. Kuonea wengine. Kuwachukia wengine, kuwasingizia wengine na mengine mabaya tuyajuayo hakumpi Mungu utukufu.
Kumbe unaweza ukamtumikia Mungu ukiwa mwanasheria, muhasibu, mkulima, mfugaji, mwalimu au yeyote pale ulipo,kitu kikubwa ni kufanya hicho ufanyacho kwa namna ambayo inamuinua na kumrudishia Mungu utukufu. Yani kila anayekuja kwenye nafasi yako anaona unyoofu.
Ndio mama Martin Luther King anasema,mkristo wa kweli hataweka misalaba kwenye kiatu anachotengeneza ili kuonyesha ukristo wake,bali atatengeneza kiatu madhubuti kuonyesha ukristo wake.
UELEWA ZAIDI KUHUSU KUMTUMIKIA MUNGU
Luka 13:22 - Mtu mmoja akamuuliza Bwana Yesu Je! Watu wanaookolewa ni wachache? Bwana akamjibu akamwambia jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawambia kuwa wengi watataka kuingia wasiweze.
Mahali pengine maandiko yanasema tangu enzi za Yohana mbatizaji habari njema ya ufalme inahubiriwa, na wenye nguvu wauteka huo ufalme.
KUMTUMIKIA MUNGU
Katika Mathayo 19:27 tunaona maneno ambayo mtume Petro alimuuliza Bwana Yesu kuwa walikuwa wameacha vitu vyote na kumfuata Yesu, Je! Watapata NINI? Mara nyingi napenda kusema kuwa hakuna mtu yeyote duniani mwenye akili timamu anayependa HASARA. Petro alitaka kujua atakachokipata, baada ya kuwa ameamua kuacha vyote na kumfuata Yesu. Kama ingetokea Bwana Yesu amjibu kuwa fanya kazi maana UNAJITOLEA, nadhani hapo ndipo ingekuwa mwisho wa Petro. Lakini kwa kumjibu alimwambia atapata mara mia, katika ulimwengu huu na uzima wa milele baadaye.
Habari hii pia tunaiona katika Marko 10:28-31 huku tofauti ikiwa ni kuongezwa maneno PAMOJA NA DHIKI katika Marko. Ndiyo maana katika Galatia 6:9 mtume Paulo aliandika maneno fulani ili kuwaambia Wakristo waendelee kufanya kazi ya Mungu bila kuchoka, maana malipo yapo baada ya kazi hii katika dunia hii. Maneno hayo ni:
Tena tusichoke katika kutenda mema, kwa maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho.
1Kor 15:58; “Basi,ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mwajua kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana”. Yaani kazi ambayo italipwa ni ile iliyofanywa katika Bwana,( sio kazi yoyote, katika Bwana. Ndiyo maana anasema ni wale tu wafanyao MAPENZI YA BABA YANGU). Kumbe unaweza ukafanya kazi ya Mungu, lakini yakawa siyo mapenzi ya Mungu.
Katika Ebrania 6:10 tunaona kuwa Mungu si dhalimu hata aisahau kazi ya mtu. Hii ina maana kuwa Mungu hawezi kudhulumu mtu yeyote. Ndio maana imeandikwa “kila mtuatavuna kile alichokipanda”.
Faida ya Kumtumikia Mungu.
Faida utakazozipata kama ukiamua kumtumikia Mungu kwa dhati. Faida hizi ni zile utakazopata ukiwapo hapa hapa duniani. Najua tutalipwa pia na mbinguni, lakini leo naongelea faida za hapa hapa duniani.
-Mithali 11:31 – Mwenye haki atalipwa duniani, na mkosaji pia.
-Mithali 11:25 – Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa. Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Maana yake ni chochote unachofanya kwa watu, ujue na watu pia watakufanyia. Ukifanya ubaya, ndivyo utafanyiwa; Ukifanya wema ndivyo utafanyiwa.
-Mith 12:14 – Utavuna chochote utakachokipanda
.
-Mith 20:7 – Chochote utakachokifanya, kizuri au kibaya, utawaachia watoto wako. Wakati mwingine unaweza kudhani uko salama, kumbe utawaachia watoto wako ama BARAKA, au LAANA. Ukiangalia kwa makini katika 1Falme 4:24-25 kuna maandiko maneno yanayosema kuwa Sulemani alistarehe pande zote. Swali ni kwa ninialistarehe? Hii ni kwa sababu baba yake alikuwa amepigana vita vya kutosha, alikuwa amesukumia mbali maadui kiasi cha kuwa mbali sana na Ufalme wake Sulemani.
-Mith 13:22 – Huwaachia WANA WA WANA–
Unaona sasa imekwenda kwa WAJUKUU. Ndiyo maana tunasema Mungu wa IBRAHIM, ISAKA, na YAKOBO. Leo hii watu wengi wanahangaika kwa sababu ya yale ambayo baba, babu zao walifanya; Wao wanahangaika leo, au wanafurahia leo.
-Luka 7:2-5 -Kuna maneno yanayoonyesha jinsi Wazee walivyomwambia Yesu kumtendea jambo jema mtu ambaye aliwajengea sinagogi. Hivyo kwa kuwa alijenga SINAGOGI basi alistahili kutendewa jambo hilo. Kumbukumbu ni muhimu sana. Leo hii kuna watu wameshapita lakini hakuna kumbukumbu lolote. Walikuwa na mali, walikuwa na uwezo, lakini leo hakuna kumbukumbu lolote kuwa walikuwepo duniani.
-Mith 10:27-Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu. Mpendwa Neno linasema wazi wazi kuwa kama utakuwa ni mcha Mungu miaka yako itaongezwa, mahali pengine inasema AKASHIBA SIKU.
Katika Isaya 54:12-17 tunaona faida tupu kama ukimcha Mungu, sitaikopi hapa, tafadhali tafuta muda uisome uone. Waweza soma pia faida tele katika Isaya 43:2 na uone kuwa hakuna hasara yoyote katika kumcha Mungu.
-Ayub 5:19-27. Ayubu alikuwa ni mzee wa siku nyingi hivyo alijua faida tele za kumtumikia Mungu. Ndiyo maana aliandika namna hiyo hapo, ebu soma uone!
Watu waliomtumikia Mungu na kuona faida zake, ambao habari zao tunazipata katika Biblia. Pata muda usome maandiko kuhusu mifano hii:
-Mdo 9:36-Dorkas.
-Isaya 38:1-Hezekiah.
-Esta 3:12-Mordekai.
-Mdo 10:1-Cornelio

Sunday, May 24, 2020

BABA NI MZIZI NA NGUZO YA FAMILIA

BABA NI MZIZI NA NGUZO YA FAMILIA.
Sehemu ya 5
• Kazi za Baba.
• Kiwango ambacho tunapaswa kupima na Kufundisha akina baba kinaweza kupatikana ndani ya hizi Kazi kumi za msingi za baba wa kweli.
1.Baba ni Mzazi, Ni mlezi na mwelekezaji wa mwelekeo wa familia yake kwa maana ya mke & Watoto.

2. Chanzo, kama ambavyo alivyo umbwa alipewa majukumu na Mungu kwa hiyo yeye ni chanzo cha yote katika familia, kuanzia upatikanaji wa mke, watoto, mpaka kwenye maisha yote duniani.

3. Msimamiaji, pamoja na mama na watoto kuweza kufanya mambo mengine lakini msimamiaji mkuu na msemaji wa mwisho huwa ni Baba.

4. Mlinzi wa familia, mali, maadili na hii ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa salama katika familia.

5. Mwalimu, anafundisha, kuelekeza, namna ya mambo kufanyika kwenye familia kwa hali ya mpangilio, na kwa ufasaha mkubwa.

6. Nidhamu, Baba ndiye mlinzi wa nidhamu namba moja, mambo yakiharibika wa kwanza kulaumiwa ni Baba kushindwa kutimiza wajibu na majukumu yake.

7. Kiongozi, Baba ni kiongozi wa familia, jamii na hata kwa ngazi ya kanisa na Taifa.

8. Kichwa, ni master planner, ni kichwa ndiye amebeba hatima na mwelekeo wa familia yake maana yake yeye ni mkuu wa familia.

9. Kujali, sifa nyingine ya mwanaume/Baba ni kujali, kutunza familia na kuhakikisha familia inapata mahitaji yake ya kila siku.

10. Mleta maendeleo, kwa kazi zake mipango yake na namna ya kuyatimiza majukumu yake basi mwisho wa siku huleta faida na maendeleo katika familia, pamoja na mama kufanya kazi, biashara lakin kiini namba moja ni baba, Baba akilala familia inaanguka na kupoteza mwelekeo hasa kama hakujenga misingi imara kwa watoto na mke wake.

Mwanaume, Baba Timiza wajibu, wajengee watoto, mke uwezo wa kuyaishi mazuri na maarifa ambayo yatawasaidia siku ukipumzishwa na Mungu.

Moses Zephania Mgema

Saturday, May 23, 2020

MAMBO 8 MUHIMU YANAYOONYESHA MWANAUME ALIVYO MSINGI WA FAMILIA NA JAMII YOTE.

1. Ufalme wa Mungu unafundisha kwamba, Mwanaume ndiye msingi wa Nyumba- yeye hubeba kila kitu.

2. Mungu alimpa Mwanaume habari/Taarifa yote kuwafundisha wale waliokuja baada yake.

3. Mungu aliwaweka wanaume kama msingi wa familia, na wanahitaji kuwa waangalifu wasiruhusu nyufa zozote katika tabia zao ambazo zinaweza kusababisha maafa kwa familia zao.

4. Msingi hufanya kazi bila kuonekana. Kama msingi wanaume wanapaswa kufanya kile wanachostahili kufanya kwa wale walio karibu nao bila kujikuta zaidi.

5. Wanaume sio msingi tu bali pia nanga ya familia zao na watu wao.Nanga ni nguzo ya kuaminika.

6. Kwa nanga inamaanisha kufunga, kuona, au kupumzika "Nanga huleta  Usalama & Na huleta pumziko.

7. Nguvu ya nanga inaweza kupimwa tu wakati wa shinikizo kali.

8. Udhaifu wetu unafunuliwa Kupitia Mtihani na majaribu tunayopitia kila siku kwenye maisha yetu. Uimara wa mwanaume huiweka familia salama na kuishi kwa tumaini kubwa kwa sababu ngzo yao haiteteleki.

Mwanaume wewe ni nguzo katika familia yako jitahidi kuwa imara na mwenye kujenga na kutia matumaini kwa unaowaongoza.

Na Moses Zefaniya Mgema
Kurejelea kutoka kifungu cha Dk. Myles Munroe.

Wednesday, May 20, 2020

MWANAUME NI MSINGI WA FAMILIA YAKE.

BONYEZA KAMA UTAFITI.
Wanaume waliumbwa kuwa chanzo na mtunzaji. Wao sio msingi tu kwa nyumba zao, bali pia kwa makanisa yao, jamii na Mataifa.
Kuwa chanzo na msimamiaji haimaanishi kuwa wewe ni Bwana juu ya wengine au kwamba mahitaji yako yanaendesha mambo. Inamaanisha kuwajibika kwako kwa kila kitu.
MFUMO WA MALE.
> Ufalme wa Hod hufundishwa kuwa dume ndio msingi wa nyumba-Yeye hubeba kila kitu. Kama mume ndio msingi wa nyumba yako. Kama mchungaji ndio msingi wa kanisa.
> Ubaba ni njia ya Mungu ya kujenga na kudumisha familia ya wanadamu. Mpango wake ni kutimiza maono yake ya Dunia kama nyongeza ya ufalme wake wa mbinguni. Hii hufanyika kama kiume hufanya kazi kama msingi wa kiume wa nyumba, ikiruhusu wale wote ambao yeye ndiye anayewajibika kwa usalama & Uhuru kukua na kufanikiwa kama vile Mungu alivyokusudia kwa utukufu wake na kupanuka kwa njia zake Duniani.
> Katika utangulizi, tulijadili sanduku la matokeo Ujinga wetu na Ukosefu wa kuelewa juu ya maumbile ya baba kwa msingi wa neno la Zaburi 82: 5 ukisoma kwa umakini aya hiyo utaelewa kuwa Giza linamaanisha ujinga.
> Ukosefu wa maarifa na uelewa huendeleza ujinga ambao unahatarisha msingi wa jamii.
> "Msingi" katika zaburi 82: 5 inamaanisha kanuni na sheria za msingi zinazosimamia kazi / kufanya kazi wakati watu wanakosa ufahamu na ufahamu wa sheria za kimsingi za Mungu, maisha yote yanakwenda bila mafanikio. Ubaba wa kweli ni njia ya kurudisha msingi wa jamii zetu.
> Ufunguo wa ujenzi wa jengo lolote ni msingi wa muundo kwa sababu msingi hubeba uzito wa jengo. Kumbuka kuwa ubora wa msingi huamua utulivu na thamani ya kile umeijenga juu yake.
> Mungu aliumba mtu kupata kizazi kijacho kuwa msingi ambao wao hua. Kuwa na sifa za msingi wenye nguvu kwa hivyo ni muhimu kwa kila mtu.
> Mungu alimuumba Adamu kutoka kwa mchanga na ndiye mtu pekee ambaye alitoka kutoka kwa udongo wengine hutoka kwa watu wawili. Kwa hivyo Mungu aliumba Adamu kama chini ya mapumziko.
> Tumeona kuwa wanadamu wote walitoka kwa Adamu, lakini kiume ndio msingi kwa njia nyingine vile vile. Kumbuka kwamba alikuwa Adamu pekee kwamba Mungu alitoa maagizo ya kufanya kazi hapa duniani na kwa kile kisichoweza & hichiweza kufanywa. Ilikuwa tu baada ya hii ambapo Eva aliumbwa. Mwanzo 2: 15-18, 21-23
> Mungu hakutoa maagizo yoyote kwa mwanamke bali kwa wanaume tu. Habari zote zilipewa mtu huyo kufundisha wale waliokuja baada yake. Tafadhali kumbuka kuwa ninarejelea kazi kulingana na uumbaji. Wanaume hufanya kazi kama msingi sio udhuru wa kutoa udhibiti juu ya wengine.
√ • SIFA ZA MFIDUO WAKATI WA KUONA.
• Maziko iko chini huwezi kuiona lakini unaweza kuona ukuta, milango, madirisha, taa na vifaa vya ujenzi. Hii ni sawa kwa wanaume, wanaume hawana budi kufanya kile wanachostahili kufanya kwa wale walio karibu nao bila kujielekeza kwao.
• Huoni msingi kwa nini ni busy sana kubeba kila kitu. Wanaume wa kweli hawatangazi majukumu yao
• Wanaume wa kweli hawamwambii kila mtu pamoja na wake wake kile wanachowafanyia. Wanaume halisi hawatamki kwa jamii kile wanachofanya kwa familia zao. Unaona tu familia inafanya kazi vizuri na ikifanya kazi kwa pamoja tunaweza kusema kuwa mwanadamu alimaanisha kushikilia familia.
Mwanadamu ni gundi ambayo inaweka familia yake pamoja vivyo hivyo, mchungaji mzuri huwaambia washiriki wa kanisa kila kitu anachokuwa akiwafanyia, jamii huona tu / hupata matokeo ya kazi hiyo.
Sehemu muhimu zaidi ya jengo ni sehemu ambayo hauwezi kuona. Kuwa mtu ambaye familia yako, jamii na taifa linaweza kusimama na liko salama, ukijua kuwa hautaanguka chini yao. Bila kujali ni nguvu gani zinazokuja dhidi yako.

MWANAUME NDIYO MSINGI WA YOTE KATIKA FAMILIA NA JAMII YAKE.

Sehemu 3.
Wanaume wameumbwa kuwa chanzo na watunzaji. Wao sio msingi tu wa nyumba zao, bali pia kwa makanisa yao, jamii na Mataifa. Kuwa chanzo na wasimamiaji haimaanishi kuwa wewe ni Bwana juu ya wengine au kwamba mahitaji yako yanaendesha mambo. Inamaanisha kuwajibika kwako kwa kila kitu.

MWANAUME NI MSINGI.
> Ufalme wa Mungu hufundishwa kuwa mwanaume  ndio msingi wa nyumba-Yeye hubeba kila kitu. Kama mume ndio msingi wa nyumba yako, Kama mchungaji ndio msingi wa kanisa.
> Ubaba ni njia ya Mungu ya kujenga na kudumisha familia ya wanadamu. Mpango wake ni kutimiza maono yake Duniani kama kupanua  ya ufalme wake wa mbinguni. Hii hufanyika kama mwanaume  hufanya kazi kama msingi wa nyumba, ikiruhusu wale wote ambao yeye ndiye anayewajibika kwa usalama, Uhuru, kukua na kufanikiwa kama vile Mungu alivyokusudia kwa utukufu wake na kupanuka kwa njia zake Duniani.

> Katika utangulizi, tulijadili matokeo ya Ujinga wetu na Ukosefu wa uelewa juu ya asili  ya baba kwa msingi wa neno la Zaburi 82: 5 ukisoma kwa umakini aya hiyo utaelewa kuwa Giza linamaanisha ujinga.

> Ukosefu wa maarifa na uelewa huendeleza ujinga ambao unahatarisha msingi wa jamii.

> "Msingi" katika zaburi 82: 5 inamaanisha kanuni na sheria za msingi zinazosimamia kazi / kufanya kazi wakati watu wanakosa ufahamu na ufahamu wa sheria za kimsingi za Mungu, maisha yote yanakwenda bila mafanikio. Ubaba wa kweli ni njia ya kurudisha msingi wa jamii zetu.

> Ufunguo wa ujenzi wa jengo lolote ni msingi kwa sababu msingi hubeba uzito wa jengo. Kumbuka kuwa ubora wa msingi huamua utulivu na thamani ya kile umeijenga juu yake.

> Mungu aliumba mtu kupata kizazi kijacho kuwa msingi ambao wao hua. Kuwa na sifa za msingi wenye nguvu kwa hivyo ni muhimu kwa kila mtu.
> Mungu alimuumba Adamu kutoka kwa udongo na ndiye mtu pekee ambaye alitoka udongoni wengine hutoka kwa ushirika wa watu wawili. Kwa hivyo Mungu alimuumba Adamu kwa mfumo tofauti na wanadamu wengine ambao waliumbwa kupitia ushirika wa watu wawili

> Tumeona kuwa wanadamu wote walitoka kwa Adamu, lakini mwanaume  ndio msingi kwa njia nyingine vile vile. Kumbuka kwamba alikuwa Adamu pekee aliyepokea maelekezo kutoka kwa Mungu kwamba kufanya kazi hapa duniani na kazi ya kwanza ilikuwa kuita majina viumbe wengine na kutunza bustani. Halafu baadae ndipo Eva aliumbwa. Mwanzo 2: 15-18, 21-23 > Mungu hakutoa maagizo yoyote kwa mwanamke bali kwa wanaume tu. Habari zote zilipewa mtu huyo kufundisha wale waliokuja baada yake. Tafadhali kumbuka kuwa ninarejelea kazi kulingana na uumbaji. Wanaume hufanya kazi kama msingi sio udhuru wa kutoa udhibiti juu ya wengine.

√ • KAZI ZA MSINGI.

• Msingi uko chini huwezi kuuona lakini unaweza kuona ukuta, milango, madirisha, taa na vifaa vya ujenzi. Hii ni sawa kwa wanaume, wanaume hawana budi kufanya kile wanachostahili kufanya kwa wale walio karibu nao bila kujieleeza kwao.

• Huoni msingi kwa nini kwa Sababu uko bize kutekeleza majukumu yake ya kubeba kila kitu kilicho juu yake.
•Wanaume wa kweli hawatangazi majukumu yao • Wanaume wa kweli hawamwambii kila mtu pamoja na wake zake kile wanachowafanyia. Wanaume halisi hawatamki kwa jamii kile wanachofanya kwa familia zao. Unaona tu familia inafanya kazi vizuri na ikifanya kazi kwa pamoja.
•Mwanaume ni gundi ambayo inaunganisha familia yake pamoja vivyo hivyo, mchungaji mzuri hawaambii washirika wa kanisa kila kitu anachokuwa akiwafanyia Bali wakati mwingine huona matokeo yakazi  yake/ hupata matokeo ya kazi hiyo.
•Sehemu muhimu zaidi ya jengo ni sehemu ambayo hauwezi kuiona (MSINGI). Kuwa mtu ambaye familia yako, jamii na taifa linaweza kusimama na likawa salama juu yako, ukijua Bila kujali ni nguvu na uzito kiasi gani ulioubeba juu yako.
Asante sana

MWABAUME NI MSINGI WA FAMILIA.

Sehemu 3. Wanaume waliumbwa kuwa chanzo na mtunzaji. Wao sio msingi tu kwa nyumba zao, bali pia kwa makanisa yao, jamii na Mataifa. Kuwa chanzo na msimamiaji haimaanishi kuwa wewe ni Bwana juu ya wengine au kwamba mahitaji yako yanaendesha mambo. Inamaanisha kuwajibika kwako kwa kila kitu. MFUMO WA MALE. > Ufalme wa Hod hufundishwa kuwa dume ndio msingi wa nyumba-Yeye hubeba kila kitu. Kama mume ndio msingi wa nyumba yako. Kama mchungaji ndio msingi wa kanisa. > Ubaba ni njia ya Mungu ya kujenga na kudumisha familia ya wanadamu. Mpango wake ni kutimiza maono yake ya Dunia kama nyongeza ya ufalme wake wa mbinguni. Hii hufanyika kama kiume hufanya kazi kama msingi wa kiume wa nyumba, ikiruhusu wale wote ambao yeye ndiye anayewajibika kwa usalama & Uhuru kukua na kufanikiwa kama vile Mungu alivyokusudia kwa utukufu wake na kupanuka kwa njia zake Duniani. > Katika utangulizi, tulijadili sanduku la matokeo Ujinga wetu na Ukosefu wa kuelewa juu ya maumbile ya baba kwa msingi wa neno la Zaburi 82: 5 ukisoma kwa umakini aya hiyo utaelewa kuwa Giza linamaanisha ujinga. > Ukosefu wa maarifa na uelewa huendeleza ujinga ambao unahatarisha msingi wa jamii. > "Msingi" katika zaburi 82: 5 inamaanisha kanuni na sheria za msingi zinazosimamia kazi / kufanya kazi wakati watu wanakosa ufahamu na ufahamu wa sheria za kimsingi za Mungu, maisha yote yanakwenda bila mafanikio. Ubaba wa kweli ni njia ya kurudisha msingi wa jamii zetu. > Ufunguo wa ujenzi wa jengo lolote ni msingi wa muundo kwa sababu msingi hubeba uzito wa jengo. Kumbuka kuwa ubora wa msingi huamua utulivu na thamani ya kile umeijenga juu yake. > Mungu aliumba mtu kupata kizazi kijacho kuwa msingi ambao wao hua. Kuwa na sifa za msingi wenye nguvu kwa hivyo ni muhimu kwa kila mtu. > Mungu alimuumba Adamu kutoka kwa mchanga na ndiye mtu pekee ambaye alitoka kutoka kwa udongo wengine hutoka kwa watu wawili. Kwa hivyo Mungu aliumba Adamu kama chini ya mapumziko. > Tumeona kuwa wanadamu wote walitoka kwa Adamu, lakini kiume ndio msingi kwa njia nyingine vile vile. Kumbuka kwamba alikuwa Adamu pekee kwamba Mungu alitoa maagizo ya kufanya kazi hapa duniani na kwa kile kisichoweza & hichiweza kufanywa. Ilikuwa tu baada ya hii ambapo Eva aliumbwa. Mwanzo 2: 15-18, 21-23 > Mungu hakutoa maagizo yoyote kwa mwanamke bali kwa wanaume tu. Habari zote zilipewa mtu huyo kufundisha wale waliokuja baada yake. Tafadhali kumbuka kuwa ninarejelea kazi kulingana na uumbaji. Wanaume hufanya kazi kama msingi sio udhuru wa kutoa udhibiti juu ya wengine. √ • SIFA ZA MFIDUO WAKATI WA KUONA. • Maziko iko chini huwezi kuiona lakini unaweza kuona ukuta, milango, madirisha, taa na vifaa vya ujenzi. Hii ni sawa kwa wanaume, wanaume hawana budi kufanya kile wanachostahili kufanya kwa wale walio karibu nao bila kujielekeza kwao. • Huoni msingi kwa nini ni busy sana kubeba kila kitu. Wanaume wa kweli hawatangazi majukumu yao • Wanaume wa kweli hawamwambii kila mtu pamoja na wake wake kile wanachowafanyia. Wanaume halisi hawatamki kwa jamii kile wanachofanya kwa familia zao. Unaona tu familia inafanya kazi vizuri na ikifanya kazi kwa pamoja tunaweza kusema kuwa mwanadamu alimaanisha kushikilia familia. Mwanadamu ni gundi ambayo inaweka familia yake pamoja vivyo hivyo, mchungaji mzuri huwaambia washiriki wa kanisa kila kitu anachokuwa akiwafanyia, jamii huona tu / hupata matokeo ya kazi hiyo. Sehemu muhimu zaidi ya jengo ni sehemu ambayo hauwezi kuona. Kuwa mtu ambaye familia yako, jamii na taifa linaweza kusimama na liko salama, ukijua kuwa hautaanguka chini yao. Bila kujali ni nguvu gani zinazokuja dhidi yako.

Tuesday, May 19, 2020

KUSUDI NA NAFASI YA UBABA KWENYE MALEZI 2

SEHEMU YA 2: KANUNI ZA UBABA.
Ubaba ni sheria ya msingi ambayo inasimamia kazi na tabia. lazima tuelewe sheria za msingi za kuwa baba ili tuwe kina baba wenye ufanisi. Baba ndiye chanzo kinachosimamia, kulinda, kulisha na kutoa utambulisho kwa uzao wake.

Wanaume wanajulikana katika Majukumu yao ya Ubaba kwa kanuni zifuatazo.

1. Mwanaume ndio chanzo cha uzao
Yeye ndiye chanzo cha uzima, ambapo kwa kuwa mwanamke ana wajibu wake pia katika mfumo  wa maisha ya kifamilia.

2. Mwanaume ndiye Mlezi wa watoto. Mfano Mbegu ya mti hupandwa na kisha inakuwa mti mwingine ambao huzaa matunda. Kwa hivyo baba kama chanzo ni jukumu la kulisha kulinda, kutunza watoto na familia.

3. Mwanaume ndiye chanzo cha maisha. 1kor 11: 8. Utukufu wa mwanaume ni mwanamke (1 Kor 11: 7) kwa maneno mengine mwanaume ana  wajibu kwa kile kitokanacho na yeye. Kwa kuwa mwanamke alitoka kwa mwanamume, mwanaume ana wajibu wa kutekeleza mahitaji ya Mwanawake kwa kitu ambacho mwanamke anapaswa kufanyiwa kama ilivyo kwa uzao wa mwanaume, kuwa ana wajibu wa kulinda kutunza na kulea.. Ikiwa wewe ni kijana ambaye umechumbia , lazima umchukulie kwa heshima mchumba na mkeo mtarajiwa  kama vile ungetamani mtu amfanyie binti yako mwenyewe. Wakati mwanamke anatoka na mwanaume, anapaswa kuhisi analindwa kimwili, kihisia na kiroho pia.
4. Mwanaume aliumbwa na kupewa mamlaka ya kulinda uzao wake. Mungu alimpa mwanaume nguvu za mwili, Muundo wamifupa yake ni mizito na mikubwa kuliko ya mwanamke, Kwa hiyo haifai kumpiga mwanamke bali kumlinda na kumpa matunzo. Wanaume wengi wanapiga makofi, wanalaani wake zao na wanafikiria ndiyo  uanaume wa kweli. ni wadanganyifu na wapumbavu hawajui kusudi lao waliopewa.

Mahali salama kabisa ya mwanamke inapaswa kuwa mikononi mwa mumewe. Kumbuka kila kinachotokea ndani yako ni sehemu yako. Ikiwa mwanamume anamchukia mkewe basi pia hujichukia mwenyewe Marko 10: 7-8, Efeso 5: 25-33.

5. Mwanaume huamua watoto waenende katika njia zipi kwa kutimiza wajibu wake sawasawa.  Una nguvu ya kushawishi, kuonya na kuelekeza namna unataka familia yako ienende. mti huzaa matunda na mbegu za miti zikipewa matunzo bora huleta matokeo chanya hivyo uboreshaji wa mti husika huleta matokeo yenye  tabia ya mti wa  kwanza. Kwa hiyo Baba ni mti wa kwanza mwenyewe. Wagalatia 6: 7.

6. Kanuni za baba ni kudumisha maadili mema,  kuwajibika kwa usalama wa mke na watoto, na ustawi wake.

7. Mwanaume hufundisha uzao wake. Mwanaume ni baba anayemwogopa Mungu wakati anachukua jukumu kwa watoto wake na kutoa ujuzi na maarifa yake kwa watoto . Huo ni baba mwema na wakiungu ndani yake.

Wanawake wengi wanafanya mafundisho na mafunzo katika familia nyingi kwa sababu wanaume wengi hawatimizi wajibu wao, lakini Mungu anasema kuwa baba anapaswa kufanya mafundisho ya msingi ya kiroho na mafunzo katika nyumba yake. Hivyo inamaanisha wewe kama kiongozi wa familia una jukumu la kufundisha watoto hao na kuwafundisha kutembea katika njia za Bwana. Ni ngumu kuwaongoza watoto kwa njia ya Bwana ikiwa wewe ni baba wa mbali nao.
Je unaweza kupeleka  familia yako mahali ambapo haupendi ?.
Hizi ni kanuni za msingi sana za baba. Jiulize  mwenyewe kutokana na maswali yafuatayo na kisha kuacha maoni yako chini hapo..

1. Je! Uko tayari kuwa baba ambae Mungu alikuumba uwe?
2. Je! Unajua baba afanye nini?
3. Je! Unajua jinsi baba anapaswa kuzungumza na kutenda?
Acha maoni yako hapo chini
Its done by
Moses Zephaniah Mgema referencing from the book of fatherhood principles written by Dr. Myles Mathias Munroe.
Tukutane kesho kwa sehemu ya 3

Monday, May 18, 2020

KUSUDI NA NAFASI UBABA KWENYE MALEZI YA WATOTO NA FAMILIA

Sehemu ya 1
Kuwa Baba ni kazi inayotimiza kusudi,  majukumu ambayo mwanaume amepewa na Mungu na kuyatimiza. kama wazazi Wakristo, tuna nafasi ya kipekee ya kufanya uwekezaji wa kudumu wa maadili mema na maisha ya mfano katika maisha ya watoto wetu.

Yesu Kristo alimwita Mungu  "baba" jambo ambalo linakamilisha majukumu ya wazi ya ubaba kwa Mungu kwa mlengo wa maisha yetu ya kila siku.
Mungu kwa nafasi ya  baba kwa mtoto wa pekee Yesu, hutoa upendo usio na mwisho , uongozi, na Mwongozo wa namna ya kuenenda. Yeye hutulinda na kuturuhusu tujifunze kupitia neno lake "Biblia"

Katika miongo michache iliyopita jamii imejitenga mbali na utimizaji wa majukumu  umuhimu ya Ubaba kwa watoto  kutokana na majukumu mengine ambayo yanabana nafasi ya wazazi wa kiume kutimiza wajibu wao kama wazazi na viongozi wa familia.

Muda mwingi baba hayupo hata watoto wanapomuhitaji kwa namna moja au nyingine hawapati nafasi kwa sababu Baba hayupo, watoto wanakosa nafasi ya kudeka, kuelezea hisia zao, changamoto zao lakini pia joto la wazazi wa kiume .

Familia za watu wasio mjua Mungu wakihangaika kutafuta namna bora ya kuwafanya watoto wao kuenenda katika maadili mema na wakitamani kujifunza zaidi kupitia kwa wazazi wanaomjua Mungu lakini mwisho wa siku matamanio yao pia yamekosa ufumbuzi kutoka kwa watu ambao waliwafanya kama mifano inayoishi.


Kwa kutokutimiza majukumu kama Baba kwenye eneo la malezi watoto wengi wameyumba kitabia hii ni changamoto kubwa ambayo inapelekea hata kanisa kukosa wakristo halisi wanaofuta misingi na kanuni za Kimungu kwa sababu Misingi bora huanzia nyumbani na kila mzazi mama & na Baba wananafasi kwenye uwekezaji kwenye maisha ya watoto wao.

Kushindwa kutimizaji Majukumu kwa nafasi ambayo Mungu amempa Baba kama kiongozi wa familia inapelekea  kupoteza baraka za Mungu na kukosa kuweka alama kwenye maisha ya watoto.

Ndiyo maana vijana wengi ukiwauliza Leo unavutiwa na nani yaani (Role model) wako ni nani atamtaja mtu mwingine wa mbali kabisa, hata ukimpa nafasi tano au kumi bado Baba anaweza kukosekana kwenye nafasi ya kijana aliye mzaa anakuwa inspired na kina nani.

Kuwa Baba haichukui muda wako Bali kuwa baba ni muundo na mfumo wa Kimungu. Kuna matendo yasio ya hiyari mfano kuhema kusinzia, kusikia njaa hivyo hata mwanaume kutimiza wajibu wa Kiuoungozi na malezi ni matendo yasiyo ya hiyari Bali ni lazima ufanye kwa usitawi wa familia, kanisa na familia kwa ujumla.

Hivi umewahi kujiuliza swali kuwa endapo Mungu angelifanya jukumu letu la kuishi kama majukumu mengine na siku moja akawa bize na kuacha kukupa pumzi ingekuwaje ?

Kusimama kama baba ni wajibu na mfumo wa Kimungu usiohitaji excuse hata Mara moja, Fanya yote lakini kutimiza wajibu wa nafasi ya ubaba na uongozi ni jambo la lazima na halina mbadala.

Lazima tuwe tayari kuwekeza katika nafasi yetu bila kujali ni kwa kiasi gani majukumu mengine yanatubana kwa asilimia kubwa, kulea ni wajibu kama ambavyo unawajibika kwenye kazi zingine zozote ambazo lazima uzitekeleze.

Baba anapaswa kuwasilisha sifa za msingi za uongozi, majukumu, na uwajibikaji na uwezo wa kulinda nidhamu na baba mwenye upendo ni kazi ya wakati wote.

Kama wanaume lazima tufunze, kukuza/kulea na kujifunza namna  Mungu alivyokusudia kwa familia zetu.
Dk Myles Munroe Mwandishi wa vitabu, aliandika  kitabu cha (FATHERHOOD PRINCIPLES) Ni kitabu  safi cha wakati ambacho kimebeba kanuni zilizopimwa na wengi wamekifurahia kwa wanaume kupima ufanisi wao kama baba katika jamii zetu za kisasa.

Dr Munroe anafundisha jinsi jukumu, maono, uhusiano, usimamizi na ujuzi wa mawasiliano wa baba ndani ya muundo wa familia.

Muundo huo pia  unavyotumika kwa jamii kila mahali na kwa viwango vyote. vidokezo vyake vya U-baba hivyo nakutia changamoto kushiriki nami kwenye kujifunza kanuni hizi ambazo hadi tutakapomaliza basi utakuwa umeongeza maarifa mapya na ya msingi kwenye eneo la kutimiza wajibu kama Baba. Na mwisho wa maada hii tutapata nafasi ya kutafakari na kuuliza maswali.
Tunahitaji baba wazuri zaidi kama wakristo ili tuwe mfano kwa jamii

Imeandikwa na
Moses Zephaniah Mgema akinukuu baadhi ya vipengele kutoka kwenye kitabu cha mchungaji na mwandishi wa vitabu zaidi ya 40 Marehemu Dr. Myles Mathias Munroe
Mawasiliano
0715366003

Tuesday, May 12, 2020

MZAZI AMEUNGANISHWA NA BARAKA/MAFANIKIO YAKO.

MZAZI AMEUNGANISHWA NA BARAKA AU MAFANIKIO YAKO.
Na Moses Zephania Mgema.
Iko faida kubwa sana kumkumbuka mzazi kwa chochote ambacho Mungu anakuwezesha kupata, bila kujali uwezo wa Mama/Baba kifedha au kiuchumi kwa ujumla.
•Ina maana kubwa sana kwenye mwelekeo wa mafanikio yako.
• Ulipokuwa mdogo mama, angekuombea ili uwe na afya njema, ukuwe, usome na kufaulu vzr.
• Umekuwa mkubwa Mzazi ana kuombea na kukutakia heri katika utafutaji wako.
•Umekuwa mtu mzima lakini huna kazi Baba/mama walikupatia chochote bila kujali wao watabaki na nini lengo likiwa ni wewe kufanikiwa.

>UMEFANIKIWA/UMEPATA KAZI, BIASHARA UMEMSAHAU MZAZI KWA NINI ?
•Baada ya Mungu kukupa kazi, Biashara yako umesahau kama kuna wazazi nyuma ya mafanikio yako.
•Unataka mama au baba apige simu kukuomba umfanyie jambo Fulani, au umpe pesa.
• Umesahau kuwa wazazi wako wamecheza nafasi kubwa ktk wewe kufika hapo ulipo.
•Mpenzi ambae huna uhakika wa kumuoa au kuolewa nae umempa nafasi kubwa kuliko mzazi, umesahau uliko toka.
• Uko busy hata hukumbuki nyumbani hata kupiga simu.

IPO SIRI KATIKA KUFANYA HAYA KWA MZAZI.
•Mbariki mzazi hata kwa kitu kidogo bila kujali ana utajiri kiasi gani.
•Ukimpa mzazi chochote bila kujali wingi wa Mali zake, unampa sababu ya yeye kukuombea wakati wote.
•Usitoe pesa kwa kuombwa,  jiongeze mwenyewe wakati mwingine mzazi ana mahitaji ila hawezi kukuomba anahisi huna.
•Mpe sababu ya kukuombea kwa moyo wa upendo sio kwa sababu wewe ni mtoto wake.
• Kumpa mzazi hata kama unajua anacho ni sawa na kutoa sadaka kanisani huku ukijua kuwa unachompa Mungu yeye anacho zaidi ila anataka kuona ni kwa kiasi gani unajali, kuthamini na kukumbuka.
•Iko connection/mahusiano makubwa sana kwenye mafanikio yako na wazazi wako, wape, wasalimie watumie chochote unafungua milango ya mafanikio zaidi.
• Usisubiri waanze kulalamika na kujutia walichokupa wafanye wafurahie uzao wao.
• Wamekuzaa na walichofanya kwako ilikuwa niwajibu wao, lakini ukitoa ni kuonyesha unajali na una upendo nao.
•Kumbuka kuna watoto kama wewe na walipenda kufikia hapo ulipo katika kazi, elimu na mafanikio mengine.

Lakini hawakuwahi kumwona baba wala mama, wazazi walishindwa kutimiza wajibu kwa sababu zao au ufukara kitu ambacho kimepelekea wenzako wawe nje ya ndoto zao..

Lakini Mungu amekupa neema ya kuwapata wote na wametimiza wajibu wao na wewe Fanya hata kwa asilimia ndogo. Ubarikiwe
RAFIKI HAWEZI KUAMBATANISHWA NA UFUNGUO WA MAFANIKIO YAKO ILA NI MZAZI KWANZA NA MKE NA MUME KAMA UMEFIKIA HATUA HIYO.