SEHEMU YA 2: KANUNI ZA UBABA.
Ubaba ni sheria ya msingi ambayo inasimamia kazi na tabia. lazima tuelewe sheria za msingi za kuwa baba ili tuwe kina baba wenye ufanisi. Baba ndiye chanzo kinachosimamia, kulinda, kulisha na kutoa utambulisho kwa uzao wake.
Wanaume wanajulikana katika Majukumu yao ya Ubaba kwa kanuni zifuatazo.
1. Mwanaume ndio chanzo cha uzao
Yeye ndiye chanzo cha uzima, ambapo kwa kuwa mwanamke ana wajibu wake pia katika mfumo wa maisha ya kifamilia.
2. Mwanaume ndiye Mlezi wa watoto. Mfano Mbegu ya mti hupandwa na kisha inakuwa mti mwingine ambao huzaa matunda. Kwa hivyo baba kama chanzo ni jukumu la kulisha kulinda, kutunza watoto na familia.
3. Mwanaume ndiye chanzo cha maisha. 1kor 11: 8. Utukufu wa mwanaume ni mwanamke (1 Kor 11: 7) kwa maneno mengine mwanaume ana wajibu kwa kile kitokanacho na yeye. Kwa kuwa mwanamke alitoka kwa mwanamume, mwanaume ana wajibu wa kutekeleza mahitaji ya Mwanawake kwa kitu ambacho mwanamke anapaswa kufanyiwa kama ilivyo kwa uzao wa mwanaume, kuwa ana wajibu wa kulinda kutunza na kulea.. Ikiwa wewe ni kijana ambaye umechumbia , lazima umchukulie kwa heshima mchumba na mkeo mtarajiwa kama vile ungetamani mtu amfanyie binti yako mwenyewe. Wakati mwanamke anatoka na mwanaume, anapaswa kuhisi analindwa kimwili, kihisia na kiroho pia.
4. Mwanaume aliumbwa na kupewa mamlaka ya kulinda uzao wake. Mungu alimpa mwanaume nguvu za mwili, Muundo wamifupa yake ni mizito na mikubwa kuliko ya mwanamke, Kwa hiyo haifai kumpiga mwanamke bali kumlinda na kumpa matunzo. Wanaume wengi wanapiga makofi, wanalaani wake zao na wanafikiria ndiyo uanaume wa kweli. ni wadanganyifu na wapumbavu hawajui kusudi lao waliopewa.
Mahali salama kabisa ya mwanamke inapaswa kuwa mikononi mwa mumewe. Kumbuka kila kinachotokea ndani yako ni sehemu yako. Ikiwa mwanamume anamchukia mkewe basi pia hujichukia mwenyewe Marko 10: 7-8, Efeso 5: 25-33.
5. Mwanaume huamua watoto waenende katika njia zipi kwa kutimiza wajibu wake sawasawa. Una nguvu ya kushawishi, kuonya na kuelekeza namna unataka familia yako ienende. mti huzaa matunda na mbegu za miti zikipewa matunzo bora huleta matokeo chanya hivyo uboreshaji wa mti husika huleta matokeo yenye tabia ya mti wa kwanza. Kwa hiyo Baba ni mti wa kwanza mwenyewe. Wagalatia 6: 7.
6. Kanuni za baba ni kudumisha maadili mema, kuwajibika kwa usalama wa mke na watoto, na ustawi wake.
7. Mwanaume hufundisha uzao wake. Mwanaume ni baba anayemwogopa Mungu wakati anachukua jukumu kwa watoto wake na kutoa ujuzi na maarifa yake kwa watoto . Huo ni baba mwema na wakiungu ndani yake.
Wanawake wengi wanafanya mafundisho na mafunzo katika familia nyingi kwa sababu wanaume wengi hawatimizi wajibu wao, lakini Mungu anasema kuwa baba anapaswa kufanya mafundisho ya msingi ya kiroho na mafunzo katika nyumba yake. Hivyo inamaanisha wewe kama kiongozi wa familia una jukumu la kufundisha watoto hao na kuwafundisha kutembea katika njia za Bwana. Ni ngumu kuwaongoza watoto kwa njia ya Bwana ikiwa wewe ni baba wa mbali nao.
Je unaweza kupeleka familia yako mahali ambapo haupendi ?.
Hizi ni kanuni za msingi sana za baba. Jiulize mwenyewe kutokana na maswali yafuatayo na kisha kuacha maoni yako chini hapo..
1. Je! Uko tayari kuwa baba ambae Mungu alikuumba uwe?
2. Je! Unajua baba afanye nini?
3. Je! Unajua jinsi baba anapaswa kuzungumza na kutenda?
Acha maoni yako hapo chini
Its done by
Moses Zephaniah Mgema referencing from the book of fatherhood principles written by Dr. Myles Mathias Munroe.
Tukutane kesho kwa sehemu ya 3
No comments:
Post a Comment