Monday, May 18, 2020

KUSUDI NA NAFASI UBABA KWENYE MALEZI YA WATOTO NA FAMILIA

Sehemu ya 1
Kuwa Baba ni kazi inayotimiza kusudi,  majukumu ambayo mwanaume amepewa na Mungu na kuyatimiza. kama wazazi Wakristo, tuna nafasi ya kipekee ya kufanya uwekezaji wa kudumu wa maadili mema na maisha ya mfano katika maisha ya watoto wetu.

Yesu Kristo alimwita Mungu  "baba" jambo ambalo linakamilisha majukumu ya wazi ya ubaba kwa Mungu kwa mlengo wa maisha yetu ya kila siku.
Mungu kwa nafasi ya  baba kwa mtoto wa pekee Yesu, hutoa upendo usio na mwisho , uongozi, na Mwongozo wa namna ya kuenenda. Yeye hutulinda na kuturuhusu tujifunze kupitia neno lake "Biblia"

Katika miongo michache iliyopita jamii imejitenga mbali na utimizaji wa majukumu  umuhimu ya Ubaba kwa watoto  kutokana na majukumu mengine ambayo yanabana nafasi ya wazazi wa kiume kutimiza wajibu wao kama wazazi na viongozi wa familia.

Muda mwingi baba hayupo hata watoto wanapomuhitaji kwa namna moja au nyingine hawapati nafasi kwa sababu Baba hayupo, watoto wanakosa nafasi ya kudeka, kuelezea hisia zao, changamoto zao lakini pia joto la wazazi wa kiume .

Familia za watu wasio mjua Mungu wakihangaika kutafuta namna bora ya kuwafanya watoto wao kuenenda katika maadili mema na wakitamani kujifunza zaidi kupitia kwa wazazi wanaomjua Mungu lakini mwisho wa siku matamanio yao pia yamekosa ufumbuzi kutoka kwa watu ambao waliwafanya kama mifano inayoishi.


Kwa kutokutimiza majukumu kama Baba kwenye eneo la malezi watoto wengi wameyumba kitabia hii ni changamoto kubwa ambayo inapelekea hata kanisa kukosa wakristo halisi wanaofuta misingi na kanuni za Kimungu kwa sababu Misingi bora huanzia nyumbani na kila mzazi mama & na Baba wananafasi kwenye uwekezaji kwenye maisha ya watoto wao.

Kushindwa kutimizaji Majukumu kwa nafasi ambayo Mungu amempa Baba kama kiongozi wa familia inapelekea  kupoteza baraka za Mungu na kukosa kuweka alama kwenye maisha ya watoto.

Ndiyo maana vijana wengi ukiwauliza Leo unavutiwa na nani yaani (Role model) wako ni nani atamtaja mtu mwingine wa mbali kabisa, hata ukimpa nafasi tano au kumi bado Baba anaweza kukosekana kwenye nafasi ya kijana aliye mzaa anakuwa inspired na kina nani.

Kuwa Baba haichukui muda wako Bali kuwa baba ni muundo na mfumo wa Kimungu. Kuna matendo yasio ya hiyari mfano kuhema kusinzia, kusikia njaa hivyo hata mwanaume kutimiza wajibu wa Kiuoungozi na malezi ni matendo yasiyo ya hiyari Bali ni lazima ufanye kwa usitawi wa familia, kanisa na familia kwa ujumla.

Hivi umewahi kujiuliza swali kuwa endapo Mungu angelifanya jukumu letu la kuishi kama majukumu mengine na siku moja akawa bize na kuacha kukupa pumzi ingekuwaje ?

Kusimama kama baba ni wajibu na mfumo wa Kimungu usiohitaji excuse hata Mara moja, Fanya yote lakini kutimiza wajibu wa nafasi ya ubaba na uongozi ni jambo la lazima na halina mbadala.

Lazima tuwe tayari kuwekeza katika nafasi yetu bila kujali ni kwa kiasi gani majukumu mengine yanatubana kwa asilimia kubwa, kulea ni wajibu kama ambavyo unawajibika kwenye kazi zingine zozote ambazo lazima uzitekeleze.

Baba anapaswa kuwasilisha sifa za msingi za uongozi, majukumu, na uwajibikaji na uwezo wa kulinda nidhamu na baba mwenye upendo ni kazi ya wakati wote.

Kama wanaume lazima tufunze, kukuza/kulea na kujifunza namna  Mungu alivyokusudia kwa familia zetu.
Dk Myles Munroe Mwandishi wa vitabu, aliandika  kitabu cha (FATHERHOOD PRINCIPLES) Ni kitabu  safi cha wakati ambacho kimebeba kanuni zilizopimwa na wengi wamekifurahia kwa wanaume kupima ufanisi wao kama baba katika jamii zetu za kisasa.

Dr Munroe anafundisha jinsi jukumu, maono, uhusiano, usimamizi na ujuzi wa mawasiliano wa baba ndani ya muundo wa familia.

Muundo huo pia  unavyotumika kwa jamii kila mahali na kwa viwango vyote. vidokezo vyake vya U-baba hivyo nakutia changamoto kushiriki nami kwenye kujifunza kanuni hizi ambazo hadi tutakapomaliza basi utakuwa umeongeza maarifa mapya na ya msingi kwenye eneo la kutimiza wajibu kama Baba. Na mwisho wa maada hii tutapata nafasi ya kutafakari na kuuliza maswali.
Tunahitaji baba wazuri zaidi kama wakristo ili tuwe mfano kwa jamii

Imeandikwa na
Moses Zephaniah Mgema akinukuu baadhi ya vipengele kutoka kwenye kitabu cha mchungaji na mwandishi wa vitabu zaidi ya 40 Marehemu Dr. Myles Mathias Munroe
Mawasiliano
0715366003

No comments:

Post a Comment