Tuesday, May 12, 2020

MZAZI AMEUNGANISHWA NA BARAKA/MAFANIKIO YAKO.

MZAZI AMEUNGANISHWA NA BARAKA AU MAFANIKIO YAKO.
Na Moses Zephania Mgema.
Iko faida kubwa sana kumkumbuka mzazi kwa chochote ambacho Mungu anakuwezesha kupata, bila kujali uwezo wa Mama/Baba kifedha au kiuchumi kwa ujumla.
•Ina maana kubwa sana kwenye mwelekeo wa mafanikio yako.
• Ulipokuwa mdogo mama, angekuombea ili uwe na afya njema, ukuwe, usome na kufaulu vzr.
• Umekuwa mkubwa Mzazi ana kuombea na kukutakia heri katika utafutaji wako.
•Umekuwa mtu mzima lakini huna kazi Baba/mama walikupatia chochote bila kujali wao watabaki na nini lengo likiwa ni wewe kufanikiwa.

>UMEFANIKIWA/UMEPATA KAZI, BIASHARA UMEMSAHAU MZAZI KWA NINI ?
•Baada ya Mungu kukupa kazi, Biashara yako umesahau kama kuna wazazi nyuma ya mafanikio yako.
•Unataka mama au baba apige simu kukuomba umfanyie jambo Fulani, au umpe pesa.
• Umesahau kuwa wazazi wako wamecheza nafasi kubwa ktk wewe kufika hapo ulipo.
•Mpenzi ambae huna uhakika wa kumuoa au kuolewa nae umempa nafasi kubwa kuliko mzazi, umesahau uliko toka.
• Uko busy hata hukumbuki nyumbani hata kupiga simu.

IPO SIRI KATIKA KUFANYA HAYA KWA MZAZI.
•Mbariki mzazi hata kwa kitu kidogo bila kujali ana utajiri kiasi gani.
•Ukimpa mzazi chochote bila kujali wingi wa Mali zake, unampa sababu ya yeye kukuombea wakati wote.
•Usitoe pesa kwa kuombwa,  jiongeze mwenyewe wakati mwingine mzazi ana mahitaji ila hawezi kukuomba anahisi huna.
•Mpe sababu ya kukuombea kwa moyo wa upendo sio kwa sababu wewe ni mtoto wake.
• Kumpa mzazi hata kama unajua anacho ni sawa na kutoa sadaka kanisani huku ukijua kuwa unachompa Mungu yeye anacho zaidi ila anataka kuona ni kwa kiasi gani unajali, kuthamini na kukumbuka.
•Iko connection/mahusiano makubwa sana kwenye mafanikio yako na wazazi wako, wape, wasalimie watumie chochote unafungua milango ya mafanikio zaidi.
• Usisubiri waanze kulalamika na kujutia walichokupa wafanye wafurahie uzao wao.
• Wamekuzaa na walichofanya kwako ilikuwa niwajibu wao, lakini ukitoa ni kuonyesha unajali na una upendo nao.
•Kumbuka kuna watoto kama wewe na walipenda kufikia hapo ulipo katika kazi, elimu na mafanikio mengine.

Lakini hawakuwahi kumwona baba wala mama, wazazi walishindwa kutimiza wajibu kwa sababu zao au ufukara kitu ambacho kimepelekea wenzako wawe nje ya ndoto zao..

Lakini Mungu amekupa neema ya kuwapata wote na wametimiza wajibu wao na wewe Fanya hata kwa asilimia ndogo. Ubarikiwe
RAFIKI HAWEZI KUAMBATANISHWA NA UFUNGUO WA MAFANIKIO YAKO ILA NI MZAZI KWANZA NA MKE NA MUME KAMA UMEFIKIA HATUA HIYO.

No comments:

Post a Comment