Watoto walichomwa jua, miba na kunyeshewa mvua wakiwa kwenye nguo chafu zilizochakaa (madaso) wakichunga mifugo ya baba yao, shule kwao haikuwa fahari, nyumba nzuri kwao ilikuwa habari ngeni, macho yaliwaonyesha hazina ya Baba ilivyotengeneza fahari na majivuno kijijini, familia iliheshimika kijijini na watu ambao waliishi kwenye nyumba angalau za bati na kulala kwenye vitanda vya kamba.
Lakini pamoja na ufahari wa macho ya wale mifugo, lakini leo wanaishi ya kujiinamia na majuto mengi mioyoni mwao, baba akiwa amelala milele, shubiri ijuu yao kutwa mkono shavuni, ile fahari haipo tena...ndipo ambapo tunasema bora kufa huku fikra zako zinaishi kuliko kuishi mwili wakati fikra zimekufa.....
Mzee huyu tajiri wa ng'ombe namfananisha na mama mmoja aliyemiliki kabati zuri la vyombo na kununua vyombo vya Thamani nakuviacha kwenye kabati zuri vikipigwa vumbi akisubiri wageni asiojua watakuja linĂ¯ ili wavitumie ajabu....
Hawa wawili nawaunganisha na msemo wa kale usemao kwamba MGENI NJOO MWENYEJI APONE, eti kama hakuna mgeni basi kuku wataendelea kuzaliana na kuliwa na mwewe huku familia wakila mlenda na mchicha pori...
Hawa wote wamekufa wakiwa na utajiri kweye hazina zao, walidhani kumiliki mifugo, kuhifadhi vyombo kabatini, kusubiri wageni ndo wachinje kuku ndo fahari na ndiyo maisha...
Baba huyu amekufa akiwa amezoea kula mboga za majani, amelala kwenye tembe, amewanyima watoto haki ya elimu, sasa amekufa, mama leo watu wanatumia vyombo vyako ukiwa umelala kwenye sanduku....
Yako mambo mengi ambayo yanaweza kutupa mifano hai ya maisha ya wazee wetu ambao waliishi maisha ambayo hawakuyastahili. ...
Mungu amewekeza kwa kila mtu hazina (Treasure)kubwa sana ambayo ni full package ambayo kila mtu inaweza kumfanya kuishi kwenye lengo na kusudi la Mungu...
Upo uwezo wa ajabu kwenye uumbaji wa kila mtu, asili ya mwanadamu ni uwezo, kutawala na kutumia ile hazina iliyo ndani yeke, tumechagua maisha ya mfugaji, mama mwenye kabati zuri na vyombo vya gharama ndani yake au yule mama mfuga kuku aliyechagua kusubiri wageni waje ili na yeye apone...
Elimu ni master key ambayo inaweza kutufungua macho ya ndani na kufungua hazini iliyosheheni utajiri wa aina mbalimbali....
Tukutane kesho kwenye makala hii ambayo naamini itakupa kuijua hazina yako na ya watoto wako na itakusaidi kuepuka maisha ya mfugaji, mama mmiliki wa kabati zuri lenye vyombo vizuri au mama mfuga kuku anaesubiri mgeni aje ili nae apone....
0715366003/0755632375
No comments:
Post a Comment