Thursday, November 26, 2020

ELIMU NI MASTER KEY 2

Ugunduzi wa elimu duniani ulikuwa na maana kubwa sana kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu. Elimu ni zaidi ya fedha, ni zaidi ya siasa ni zaidi ya dini, elimu ni jumla ya maisha yetu ya kila siku
( Elimu ni jumla ya yote niliyoyataja hapo juu, ukitaka kujua kuwa elimu ni msingi wa mambo yote, mtu anaweza kupambana pekee yake kutafuta katika hatua za awali akifikia hatua ya kumiliki fedha nyingi na utajiri mwingi atahitaji watu wenye elimu ya fedha ili kuweza kuifanya fedha yake iendelee kuishi na kuongezeka zaidi, atahitaji wataaluma kwenye idara mbalimbali ili kumchorea na kumfungulia ramani na milango ya fursa ili kuifanya fedha iishi na kuzalisha zaidi.

Katika kitabu kitakatifu cha Biblia, Methali anasema mkamate sana elimu usimwache aende zake maana ni uzima wako, wahenga na watunzi wa Methali na misemo mingine wakasema Elimu ni mlango na ufunguo wa mafanikio ya mtu katika levels zote za maish yetu.

Tena wakasema wahenga mali bila daftari hutoweka bila habari, maana yake ni kuwa mali bila kuweka kumbukumbu hupotea bila kujua (elimu ya kutunza kumbukumbu hufundishwa kuanzia nyumbani, hapo ndipo unajua umuhimu wa elimu).
Watu wengi tumeishi nje ya ndoto na kusudi la Mungu kwa sababu ya kukosa ufahamu juu ya hazina kubwa ambayo Mungu amewekeza ndani yetu.

Elimu tumeiweka kwenye mfumo wa maisha ambayo jamii imeamua kuishi kwa kukariri, jamii inaamini kuwa elimu ipo kwa ajili ya kutumilikisha nafasi za juu katika ajira nasio kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa ajiri ya wengine kupitia ugunduzi wa mambo au kuongeza ubora katika vile ambavyo vilishakuwepo tayari.

Wazazi wengi wameua ndoto za vijana wengi kwa sababu ya kukubali kuishi mfumo wa kukariri katika jamii zetu,
Kwa kukosa maarifa, na elimu yenye kuimarisha ufahamu tumeamua kuchagua maisha ya aina moja, sio ajabu mzazi kuua ndoto ya mtoto wake kwa sababu anataka matakwa yake yatimizwe na mtoto wake, utasikia mzazi/mlezi anamwambia mtoto, umemaliza kidato cha sita uende ukasomee Ualimu ili upate ajira uwasaidie ndugu zako, mtoto alitaka kuwa daktari, mwanasheria na taaluma hizo zinakuwa hazina nafasi kwa upande wa mzazi kwa sababu zinachukua muda mrefu nk.

Mtoto anataka kutumia kipaji chake badala yakusaidiwa mzazi anakuwa mkali kama pilipili, usïponisikia ntakulaani, kama sijakuzaa mimi tutaona sasa mimi na wewe nani alitangulia kuliona jua, au nani amemzaa mwenzake si umekuwa, kijana wa watu anaanza safari nje ya ndoto zake bali  kutimiza matakwa ya mzazh

Kama wazazi, walezi tunamalaka juu ya watoto wetu, lakini sïo kuua kilicho uwezo na kusudi la maisha yao, tuna nafasi ya kushauri na kuwajeng ila sio kutaka kutimiziwa matakwa yetu, tuwasaidie tusiwazime, akiwa anauchaguzi sio sawa tafuta namna nzuri ya kusema nae akuelewe kuliko kutumia nafasi yako kama mzazi kuua

Jamii imeua vipaji na karama za asili nyingi kwa vivuli vya kwamba nataka usome ikiambatana na mifano mingi ya walïoshindwa, wazazi na walezi tumeua asili ya uwezo na uwekezaji wa vipaji wa Mungu kwenye maisha yetu  njia ya kivuli na kisingizio cha elimu...

Mwana wa Mungu Yesu anasema hakuja kutengua torati bali kuiendeleza, kuiboresha, kuifanya iondoe mamlaka ya kuchukua maamzi ya kuumiza wengi
Ndivyo ilivyo hata katika ugunduzi wa elimu, lengo la elimu ni kutupa uwezo na kujenga ufahamu wa kila mmoja kwanza kujijua zaidi, kuziona fursa, kuongeza ufanisi na ubora katika vile tulivyo navyo
Elimu nzuri ni ile ambayo imesemwa kwenye Methali kuwa ni uzima.

Elimu sio kiua ndoto, sio mficha na muua vipaji na vipawa vya asili ( dream killer, Is not a Talent hider and killer ).

Elimu ni ufunguo hazina kubwa iliyo kwa watu wengi, lakini namna gani tunaweza kuitumia elimu ili kutufanya kuishi kwenye kusudi la maisha ya ndoto zetu..
kwa kisingizio cha elimu tumelazimisha vipaji vya waimbaji, wacheza michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, pete, wavu, kikapu, wachekeshaji, wafanyabiashara nk kwa sababu ya kukosa ufahamu wa elimu tunayoihitaji...

Mfugaji wa mifugo mingi alikufa akilalia ngozi, kula nyamafu, kulala kwenye tembe huku utajiri ukienda mbugani kuchunga na kurudi jioni zizini na aliona fahari, Je yule mama aliyefurahia kuona vikombe, masufuria, flask nzuri, masahani ya udongo nk. kwenye kabati lake zuri la vyombo akisubiri wageni asiojua watakuja lini ndô wavitumie, Je ile familia ya mama mfuga kuku ambae aliwafanya watoto na familia ishi kwenye kauri ya wageni njoo ili nasi tupone. Kwa kukosa elimu masikini mama, baba na familia zile walikwa katika hali ambayo hawakuistahili kabisa, sababu ya yote hapa ukosefu wa elimu ya ufahamu.

Ndivyo tunavyoishi tulio wengi leo, tuna hazina zimetuzunguka kwenye familia zetu, jamii kwa ujumla, tunalia kwa uchungu kwa kukosa vyanzo vya ajira wakati ajira tunaishi nazo makwetu....

Mwandishi nguli wa vitabu na journals toka Marekani hayati Dr. Myles Munroe aliwahi kuandika kweye kitabu chake cha Maximize your potential, alisema '' yadi chache kutoka kwenye milango yetu kuna nyimbo zimerudi nyumbani bila kuimbwa, vitabu vimerudi bila kusomwa, na vipawa vingi viko kweye makaburi ndani ya mashamba yetu

Dr. Myles alisema utajiri wa dunia hii hauko kwenye vitaru vya mafuta kule Qatar, Kuwait, vitaru vya mïgodi ya dhahabu kule kusini mwa bara la Afrika, Congo hata Katika migodi ya Tanzanite kule mererani, Almasi na dhahabu kwenye ardhi ya nyumbani kahama na shinyanga na maeneo mengi ya nchi yetu, bali utajiri either tumekubali watu kufa na talanta zao, au tumeamua kuvifungia kwenye kifungo kinaitwa elimu isiyo na matendo....
Tunahitaji kujua maana halisi ya elimu, elimu, kwa sababu Elimu ni master key wa mambo yote, ufunguo elimu hutumika kufungua mageti ya hazina zetu......
Next.......
Tukutane kesho...

2 comments:

  1. Bwana Mgema, ngoja nisome hii risala yako nione kama yaliyomo yako,kisha ntarejea na chochote.

    ReplyDelete