Monday, November 30, 2020

ELIMU NI MASTER KEY 3

Elimu ni ufunguo ambao unatakiwa kutumiwa kwa ajili ya kufungua kila mageti na milango ya fursa kuanzia mtu binafsi mpaka kwenye mazingira ya nje...

Elimu ya kumfanya mtu kujielewa/kujitambua na kuelewa mazingira yake. Mungu ameumba kila mtu na kumpa uwezo na nguvu ya kujitawala, kujimiliki na kuyamudu mazingira yake.

Hivyo kitu ambacho tunapaswa kufanya kwenye mfumo wa elimu yetu, hata kama mitaala ya elimu rasmi bado haujabadilika ni vyema kutumia mifumo mingine ya elimu ambayo inatuwezesha kuwa na uelewa mpana zaidi wakujifahamu.

Elimu isiyo rasmi ipo kila mahali, kuanzia kwenye mazingira tunayoishi, kupitia mitandao ya kijamïï, websites, vitabu na vyanzo vingine vya maarifa ambavyo upatikanaji wake umekuwa rahisi sana.

Hivyo ni vyema kutumia uwepo wa teknolojia kubwa tuliyo nayo kwa sasa hapa duniani ambayo imetusogeża karibu zaidi na wenzetu waliotutangulia katika maendeleo na elimu ya kujitegemea.

Kuendelea kulaumu serikali ni kujichelewesha kufikia malengo hivyo kubaki kwenye maumivu, na lawama ambazo haziwezi kutatulika bila kuchukua hatua.

ufahamu ni jambo la msingi sana katika kufikia hatima na malengo ya kila mtu.
Tuna vipaji, vipawa na karama kubwa ndani yetu ambavyo ni uwekezaji wa Mungu kwetu.. 

Next epsode tutaangalia kwa mfano namna ambavyo tukiongeza maarifa kupitia namna nzuri ya kujifunza tunaweza kuona ni kwa kiwango gani vipawa vyetu vinaweza kutufanya kuishi kwenye ndoto, malengo na kusudi la uwepo wa vipaji hivyo ndani yetu... 
Tukutane next epsode....

No comments:

Post a Comment