Monday, November 30, 2020

ELIMU NI MASTER KEY 4

Kila mmoja amezaliwa na uwezo wa asili (Natural ability) lakini wakati mwingine ni ngumu kujijua na kujua thamani ya kile ambacho tumkibeba ndani yetu...

Kipaji ni ni kifurushi kamili (complete package) ambacho tunapaswa kukitengenezea mazingira mazur ya ustawi wake. 

Katika nchi za magharibi kupitia elimu wamewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye uwezo halisi wa mtu ndiyo maana kiwango cha ubora katika mambo mengi wanayofanya iwe katika mambo ambayo tunayaona ni kama kazi zinazoshusha hadhi kwa upande wa nchi za dunia ya tatu.

Wenzetu wanajal sana passion ya mtu kuliko matamanio yetu, ndiyo maana tunaweza kuona hata malezï na makuzi ya watoto hufuatiliwa kwa karibu sana lengo ikiwa ni kugundua ubora na uwezo wa mtoto kupitia michezo ambayo anaifanya kila siku.

Pamoja na kwamba dunia tuliyo nayo imekuwa ni dunia bize sana kwa maana ya wazazi na walezi kutingwa na kazi, lakini pia hata kwa muda mchache wamekuwa wakitoa muda wao kwa ajili ya kuwa karibu na watoto wao, lengo kubwa ni kufanya ugunduzi wa mtoto/watoto wao ni kina nani.

Utambuzi wa vipaji na passïon imesaidia kwa kiwango cha juu kuwapeleka watoto wao kwenye nafasi wanazo fiti kwa kiwango cha juu sana.

Ndiyo maana sasa unaweza kuona kuna watoto wanakwenda shule kupata elimu ya kawaida ambayo kila mtu ni haki yake, lakini bado wana muda wakufanyia mazoezi na kujifunza kwenye eneo la passion zao.

Mfano mzuri ni kwa mcheza mpira wa chini ya miaka 17 Kelvin John ambae alipata nafasi ya kwenda Ubelgiji kwa ajili ya kuendeleza kipaji cha mpira, lakini bado walimpeleka nchini England kwa ajili ya kuendelea na elimu ya kawaida lakini vilevile kupata muda mzuri wa kujifunza kwa ubora namna ya kuboresha na kukipa thamani kipaji chake.

Mtoto akiwekezwa kwenye eneo la uwezo wake na passion yake humfanya kutimiza majukumu yake kwa upendo, na kwa moyo wote kwa sababu anachokifanya sio kazi tu bali ni eneo linalompa furaha pia, hivyo hata kama kazi itakuwa ngumu kiasi gani bado ataendelea kufanya kwa sababu kwanza anapenda, anafanya kwa passion kwa hiyo kiwango cha ubora katika kazi hiyo kitakuwa cha kiwango cha juu sana.

Baadhi ya wazazi wanapenda na wanataka watoto wao kuwa madaktari, wahandisi, nk, lakini mtoto unakuta anataka kuwa mchoraji, mwalimu, au kuwa yeye kwa kile anakita tusiwanyime au kuwazuia kufanya wanachokipenda bali kama unaona mwelekeo au uchaguzi wa mtoto sio sahihi kwa maoni yako mshauri kwa upendo na kumweleza matokeo ya kile anachopenda kuwa haiwezi kumpa future nzuri.




No comments:

Post a Comment