Sunday, July 10, 2022

THE VALUE OF DREAM/THAMANI YA NDOTO YAKO

Safari ya maisha, ni safari ya kipekee sana katika ya Safari nyingi ambazo mwanadamu anazifanya akiwa kwenye sayari ya tatu. Safari hii ni Safari pekee ambayo mhusika huianza kwa kilio na wanaompokea duniani hufurahia na kutabasamu kumpokea mgeni duniani, mama hufurahi, Baba hufurahi, Bibi na Babu hufurahi na hata ndugu, jamaa, marafiki hufurahia ujio wa mwanadamu mpya duniani.

Mtoto anapozaliwa huwa amefanya mawasiliano na muumba wake kwa kina, hivyo inapofika miezi tisa tumboni hupaswa kutoka ili kuja kuanza kuyaishi maelekezo na mapenzi ya Mungu hapa duniani. Mapenzi ya Mungu ni ule uwekezaji ambao Mungu ameuwekeza kwa mwanadamu, yale maono, kusudi na ile ndoto kubwa inayokunyima usingizi hiyo ndiyo mipango ambayo Mungu huiweka kwenye maisha ya kila mtu hapa duniani.

Ndoto ya mtu ni fumbo kubwa, maisha ya mtu ni Safari yenye kubeba tumaini na shauku ya kufanikiwa kufikia ile hatima ya Mungu kupitia mwanadamu. Ndiyo maana Safari hii huwa na vikwazo vingi, mabonde mengi, giza katikati ya mapori mengi yenye wadudu, wanyama wakali na hata jua lenye kuchoma utosi na kukatisha tamaa....
Hakuna Safari rahisi ya kuishi kile ambacho Mungu amekiweka ndani ya mtu, ila hakuna ugumu ulio ndani ya kusudi la Mungu ambao hauna mpenyo, wala njia ya kufikia ile hatima kubwa ya uwekezaji wa Mungu kwa Mwanadamu......

Haijalishi milima itakuwa na miinuko mikali kiasi gani, haijalishi jua litachoma kwa kiwango gani, haijalishi vizuizi vitakuwa vingi kwa kiasi gani as long as ni Purpose ya Mungu ndiyo inafanya kazi ndani yako, mlango wa kutokea na kufikia hatima lazima utaonekana tu hata kama bado giza ni nene na lenye kutisha sana...........

Hatima yenye matokeo makubwa haiwezi kupita kwenye kiwango kidogo cha vipimo, ndoto kubwa haiwezi kuwa na formula rahisi ya kufikia jawabu tarajiwa, hatima kubwa haiwezi kubebwa na akili yenye uwezo mdogo wa kuhimili mikimiki ya upanuzi wa barabara ya kupitishia matokeo makubwa ya kesho....

Mtu rahisi huwa haaminiki, mtu rahisi ni hubebwa na upepo wa kila namna, mtu rahisi hana misuli ya kusimama na kuitetea ile hatima anayoiona kesho, bali mwenye misuli, mwenye upeo , mwenye kuona kesho zaidi kuliko leo huyo ndiyo hubeba hatima kubwa maishani na huyo ndiyo huaminiwa na Mungu kwa makubwa 

Yesu kristo alikuwa na misuli, Musa na Joshua walikuwa na Misuli ndiyo maana walikabidhiwa majukumu makubwa kwa ajili ya kuwa njia kwa wengine, Yusuph ni miongoni mwao pia, Esther ni miongoni mwao na wengine wengi ambao walikuwa sababu ya hatima zao na hatima za wengine  kuwa kweli....Mungu amekuamini pia na wewe.

Asilimia kubwa ya sisi vijana leo, hatuamini kile ambacho Mungu ameweka ndani yetu, ugumu wa maisha umetuhamisha kutoka kwenye kufikiri na kuwekeza nguvu nyingi kwenye kuwaza. Kikawaida mtu anapokuwa ana waza hupunguza uwezo wa kufikiri sawasawa na matokeo yake huchukua maamzi yasiyofaa 

Miaka michache nyuma nilipitia changamoto kubwa sana ya ugumu wa maisha, sikuona njia ya kutoka mahali nilipokuwa, niliona giza na tope jingi mbele yangu, nilihitaji kutatua changamoto ngumu mbele yangu, lakini kila mlango ulionekana kufungwa, kila njia ilionekana kuwa na miba, hata nilipojaza baiskeli yangu upepo, mbigiri zilitoboa tairi yangu na upepo kuisha...

Niliwaza sana ni namna gani Baba yangu atatibiwa niliwaza ni namna gani familia yetu itakula, niliwaza sana hatima ya mdogo wangu Miriam na niliwaza sana kwa ajili ya ndoto zangu je kuna siku zitakuwa kweli, kila nilichokipata kilikuwa kinatosha kutatua changamoto tu na changamoto zenyewe nisingeweza kuzimaliza kwa sababu kipato changu kilikuwa chini sana......

Nilitamani walau nipate hela ya kubet, lakini pamoja na kubeti wala sikuweza kupata hela, kila nilichokifanya hakuna majawabu sahihi ambayo yatengenezwa kunitoa kwenye ile hali ya uhitaji. Changamoto hiyo ilinikondesha sana iliufanya mwili wangu kudhoofika sana na kupata hali ya weusi, akili yangu ilisinyaa badala ya kustawi, mwili wangu ulipungua kilo kutoka kilo sabini hadi kilo sitini, ilikuwa ni changamoto kubwa sana...

Siku moja nilikutana na mtu mmoja akaniambia Musa mdogo wangu utakufa, Musa mdogo wangu utafanikiwa ila kwa taabu sana, Musa mdogo utafanikiwa ila unaweza usinufaike na utajiri au mafanikio yako, kwa sababu kwa wakati utakapokuwa umeyapata either unaweza kuwa na maradhi ambayo yatakufanya kuishi kwa madawa au kupunguziwa vyakula vya kula kutokana na changamoto ya afya....

Mdogo wangu, ugumu wa maisha ni kipimo cha akili, ugumu wa maisha ni fursa ya mwenye akili, ila mwenye akili huwa pia haanzishi fursa kwa lengo la kutatua Changamoto iliyoko mbele yake, bali huivumilia hiyo changamoto akitafuta suluhisho la kudumu. Akaniambia ipe akili nafasi ipumue ili kesho uweze kufikiri vyema na sio kuwaza... ...

Akaniambia watu wengi wanawaza kuliko kufikiri, kama unataka kujua kama kweli huwa unawaza ni jawabu gani hata dogo ambalo limekupa hatua hata moja ya kupumua au kukupa way forward ya unachokiwaza kila siku na kupata majibu, ukweli hapana.

Hali hii inawapata vijana wengi sana, wamewekeza nguvu kubwa katika kuwaza tatizo kuliko kuwekeza nguvu ya kufikiri namna ya kuondoka kwenye eneo hilo zito. Akili ya mtu ni zaidi ya kompyuta, akili ya mtu ni kiwanda, karakakana ambayo mtu akiitumia vyema itampa matokeo super ya kazi.....

Nimewekeza kwenye maarifa kwa miaka mitatu, na nilijitahidi sana kukataa kuishi maisha ya watu, maoni na mitamo ya watu, duniani kila mtu ana wazo zuri lakini ukweli ni kwamba sio kila wazo ni jema kwa matumizi yako bali mengi unapaswa kuyaandika na kuyaweka kama kumbukumbu kwa matumizi ya kesho.....

Leo naandika andiko hili kwa sababu, baada ya utulivu wa miaka almost mitano leo nainuka na kukung'uta mavumbi na safari yangu ya maisha inaanza rasmi kwa mwendo usio na kipimo cha kawaida. Nafanya hivi kwa sababu kila mtu alinidefine kwa namna alivyotaka, alinisema alivyotaka lakini, Mungu alinipa kuwa tahira ili kupisha kila aina ya upepo mzuri na mbaya.....

Rafiki yangu maisha ni fursa tosha, maisha ni upendeleo wa Mungu, fahamu kuwa watu wote brave kwa kutazamwa ndiyo waliofeli kwa asilimia kubwa bali watazamwao kwa jicho la kutokupewa thamani hao ndiyo wametengeneza thamani ya maisha yao. Nyakati ngumu kweli hazidumu bali watu imara hudumu....

Chagua kufikiri kuliko kuwaza kwa sababu penye kufikiri kuna jawabu sahihi zaidi bali kwenye kuwaza kuna kiwango kikubwa cha kupunguza uwezo wa kufikiri na kuja na majawabu sahihi.

Mungu amekuamini, Mungu ameniamini ndiyo maana amekupa fursa njema ambayo ni dhahabu, ni wewe tu kuona unafanya nini kwa kutumia utashi na akili yako aliyokupa Mungu, 

Opportunities are equally given but it depends on how you see them and utilise effectively for the purpose of gain what are supposed to be gained....
Enjoy your week...
Mgema Moses Zephania 
0719110760

No comments:

Post a Comment