Sunday, July 10, 2022

Ni ngumu sana kuamini maneno ya kale, kwamba penye miti hapana wajenzi, ni ngumu sana kumwamini mtu tajiri anapo yakiri maisha yake ya ufukara miaka ya nyuma kabla yakuwa namna alivyo leo.
Ukimsikiliza Barack Obama, Oprah Wilfred, Mzee Yusuph Bakhresa, Eric Shigongo, mwanzo wa Joseph kusaga, kaka Yangu Francis Sizya (Majizo) Mmiliki wa Radio 📻 ya E-Fm na wengine wengi, wanasema maisha magumu wanayajua na waliyaishi kwa vitendo kutoka kwenye familia zao...

Majizo anasema kuwa katika kila hatua aliyopita kwenye maisha yake, katika ukoo wake yeye ndiye amekuwa wa kwanza kwa kila hatua ya mafanikio, alikuwa wa kwanza kununua gari na vitu vingine vya Thamani kutoka kwenye familia masikini isiyojiweza kufanya jambo lolote lile la maendeleo...

Historia ya Shigongo Eric, niliisikia kupitia kinywa chake akisimulia lakini kupitia maandiko ya vitabu vyake ambavyo vimeelezea historia ya maisha yake ya ufukara. Kama haitoshi nilikuwa sehemu ya familia yake ya Global publishers ambayo imebeba baadhi ya watu wakubwa kiumri ambao walishuhudia ukuaji wa Eric pale Jijini Mwanza, wanasema ametokea familia duni sana yenye kunuka umasikini, kikwetu ukiitwa madaso basi fahamu uko kwenye level mbaya sana ya umasikini....

Asilimia kubwa ya sisi vijana wa kitanzania, tunaamini katika watu fulani kutubeba, tunaamini tulivyo ni kwa sababu ya historia mbovu ya familia zetu, tunaamini kuwa ndoto zetu ziko gizani kwa sababu  ya watu fulani, au serikali na wazazi wetu. 

Tunaamini kuwa kufikia utajiri na fahari ya dunia sio rahisi, ila tunaamini kwenye bahati kuwa ndiyo inaweza kuwa njia nzuri ya kufikia malengo na ndoto zetu. 

No comments:

Post a Comment