Spendi kutangaza umasikini, umasikini sio sifa, umasikini sio fashion, maana ukimwona masikini unaweza kutoka machozi, masikini hawezi kudumu gharama za maisha hata yale ya kula na kuvaa, kujimudu kwenye matibabu ya magonjwa nyemelezi na changamoto ndogo ndogo za afya, masikini hawezi kuwahudumia watoto wake hata kwenye mambo muhimu kama elimu, masikini ni mtu fukara mwenye huzuni, aliyekosa tumaini la maisha mwenye kujiona mwenye laana na asiye na bahati duniani....
Mimi sio masikini, mimi sio fukara, mimi sio ombaomba, mimi nina kila kitu, mimi nimezungukwa na fursa, mimi nina nguvu na maarifa yenye kuona fursa, jambo kubwa zaidi nina utajiri wa afya imara na uwezo wa kufanya kazi yoyote ile yenye kunipa matokeo bora ya kazi zangu zote.
Maisha ya mwafrika tako mikononi mwake mwenyewe, kusinyaa, kulaumu, na kumtegemea mtu akutoe mahali ni ngumu sana bali maamzi ya kuchoka na kuamka tako katika mikono na uwezo wetu wa kufanya jambo ili kubadili hatima na mwelekeo wa maisha yetu...
Usiku wa leo, umekuwa ni usiku mkubwa sana kwangu, maana Mungu amezungumza nami kwa namna ya pekee sana juu ya maisha yangu pamoja na maisha ya kijana wa kitanzania. Amenichukua katika ndoto, akanionyesha Tanzania, akanionyesha Afrika na ulimwengu mzima ile fahari na utajiri mwingi katika bara hili tukufu la Afrika....
Kwa miak mingi moyo wangu alikuwa na simanzi, akili yangu ilipoteza nuru, moyo wangu ulisinyaa na kuna wakati ulikata tamaa ya maisha, sikuona kuishi tena, niliamini mwanadamu ndiyo anaweza kuyafanya maisha yangu kuwa bora tena, niliyatamaza matatizo kama sehemu ya mgandamizo mkubwa uliyoifanya akili yangu kusinyaa na kuamini kuwa maisha yangu yalikuwa yamepoteza mwelekeo....
Ilikuwa ni muda mchache sana baada ya Baba yangu mzazi kufariki dunia, nikaiona nuru na tabasamu using mwangu likififia siku kwa siku, ghadhabu ya moyo, na hasira nyingi moyoni mwangu ilikuwa ni suluhisho sahihi kwangu katika kufanya maamzi, nilimuwaza sana Baba yangu, nilifikiri sana mama yangu, niliona giza zito mbele yangu, akili yangu ilifungwa na uwezo wa kufikiri ulikwisha in short I lost everything.......
My education was not something could help to solve my problems, afya yangu haikuwa mtaji wa kunitoa mahali nilipokuwa, maombi yangu mbele za Mungu haikuwa kitu chochote, imani yangu kwa Mungu iliyumba sana, pamoja na kwamba nilikwenda magotini kila wakati lakini imani yangu ilikuwa chini sana na wala maombi hayakuwa suluhisho ya hali yangu kwa wakati huo.....
Usiku wa leo nimeiona Tanzania, usiku wa leo nimeiona Afrika na usiku wa leo nimeiona dunia yote katika ndoto zangu, kuna jambo Mungu alikuwa ananisemesha, kuna jambo Mungu alikuwa ananikumbusha ndani yangu, kuna jambo Mungu alikuwa ananikumbusha kwa msisitizo mkubwa na kunilazimisha kufanya halafu niseme na kijana mwingine ambae kwake haoni mlango tena......
Mungu amenipa kalama na kipaji kikubwa cha kuandika, sihitaji kufanya nukuu au kusoma mahali ili kutengeneza mada ya kuzungumza, ninachohitaji, ni mikono na utayari wangu kufanya andiko lolote lile kwa lugha yangu ya kiswahili au kwa lugha ya kiingereza, hiyo ni talanta aliyonipa Mungu kufanya....
Mungu akanikumbusha jambo la msingi Sana kupitia stori ya Yesu kristo pamoja na Yusuph, hawa ni watu ambao Mungu alinisemesha kwa upana na kunitaka nawe nikushirikishe kwa mapana na marefu sana. Naandika haya kwa sababu Mungu amenipa ufunguo wa hazina yangu, God has already gave me the key 🔑 to unlock the treasure ahead of me.
Akaniambia kuwa Yusuph alikuwa na ndoto na hiyo ndoto aliiona akiwa katika hali ya umasikini, hali ambayo hakuna mtu angeweza kumwelewa wakati anawasimulia ndugu zake, ndiyo maana baada ya kusimulia habari ya ndoto zake, waliona kitu ambacho kiliwachukiza wao, na ikawq sababu ya Yusuph kwenda shimoni na hatimaye kufika Misri nchi ya Ugenini....
In short alipitia changamoto nyingi za kukatisha tamaa sana, mambo magumu, mambo ambayo hakupaswa kuyapitia katika umri wake, lakini Yusuph aliyapitia kwa maumivu makali kwa jasho na damu. Pamoja na nyakati hizo ngumu, Mungu alikuwa kimya sana, sio wakati akiwapa simulizi wale ndugu zake pamoja na wazazi wake, wala kipindi cha kutupwa shimoni, kuuzwa kwa wafanyabiashara, kwenda kuwa sehemu ya watumwa katika nyumba ya potifa hatimaye kuwa mmoja wa wafungwa Gerezani huko Misri, katika kipindi chote hicho Mungu alikuwa kimya sana tena kimya kisicho na mshindo wowote. Tupumzike hapo.
Mungu akanipitisha kwenye stori ya Yesu Kristo na baada ya kupitia maandiko matakatifu ya Biblia nikagundua kuwa, Mungu hakuwa na Yesu kwa zaidi ya miaka Thelathini, alikuwa kimya, Yesu alikuwa akifanya kazi zake bila mawasiliano yoyote yale ya ana kwa ana mpaka kipindi cha mateso yalipoanza, ndipo Yesu akahitaji msaada wa Mungu lakimi pamoja na Yote, Mungu alimkataa na kukaa pembeni. Ilikuwa ni wakati Mungu, majira ya damu na jasho jingi kwenye mwili wa Yesu lakini Baba yake alikuwa kimya kama haoni....
Habari hizi mbili zimekuwa sehemu ya usiku wangu wa leo, Mungu akinipitisha na kunifundisha jambo kubwa sana kwenye maisha yangu na maisha yako pia. Mungu anapokaa kimya sio kwamba haoni wala sio kwamba hayupo pamoja na wewe, anakuwepo, anakuona na yupo karibu na wewe kuliko unavyofikiri wewe.
Mungu akaruhusu mateso kwa Ayubu si kwamba alikuwa haoni, ndiyo maana shetani alipokuwa anajaribu kumshawishi Mungu amruhusu akaiguse Roho ya Ayubu, Mungu alimkatalia kwa sababu kama shetani angegusa roho ya Ayubu kulikuwa na kifo moja kwa moja lakini Mungu hakuwepo lakini alikuwa pamoja na Ayubu...
Mungu hakuwepo kwa Yusuph na Yesu lakini alikuwa pamoja nao katika yote waliyokuwa wakiyapitia kwa ugumu, jasho na damu. Ni matukio mazito ya UKIMYA WA MUNGU, ni Nyakati ambazo Mungu huwa hayupo kabisa lakini yuko pamoja na wewe katika kila hatua ya mapito yako au mapito yangu......
Baada ya kunipitisha kwa watu hawa wawili Yesu na Yusuph halafu kwa Uchache sana kwa Ayubu, kisha akanikumbusha kwa mapana na marefu jitihada zangu, nguvu zangu, shauku yangu, na nia yangu ya kufanikiwa kwa haraka sana, lakini Mungu akanipitisha kwenye baadhi ya historia ya maisha yangu.
Nikiwa darasa la tatu katika shule ya Nyahanga Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga, I was very young, siku moja katika kanisa la Assemblies, nikiwa na mdogo wangu Japhet siku ile nililia sana, and I tried to wipe the tears 😢 buy wasn't wiped, and my heart was full of sorrow and sudnes, wishing to stay with our beloved father ambae kwa kipindi hicho alikuwa Nzega Tabora, machozi hayo yalihitishwa kwa neno moja kuwa Mungu fanya njia ili tuhamie kwa Baba Nzega, is where the tears ended baada ya wiki moja Baba alipiga simu akasema tunahamia Nzega familia Nzega and that one was time of more than four years since he left us in kahama.
Akanipitisha kwenye nyakati ngumu ambazo niliwahi kupitia baada yakumaliza Elimu ya sekondari, kipindi hicho sikuwa na tumaini la kuendelea na shule, lakini tukiwa katika maombi na kaka na rafiki yangu Cornelio, Mungu alifanya mpenyo ambao mpaka leo sina namna ya kuelezea matendo makuu ya Mungu katika mpenyo huo wa wajabu sana....
Akanikumbusha tena muujiza na mpenyo nilipokuwa nimekaribia kwenda chuo kikuu, kuna jambo kubwa pia alifanya na Eliya John Tikilu aweza kuwa shahidi wa maneno yangu niliyomwambia wakati na msindikiza baada ya kupitia nyumbani pale mwenge mwaka 2013 mwezi wa saba, neno langu lilikuwa nitakwenda kusoma St. Augustine Mwanza I had no any option badala ya SAUT, it was hard but God opened the door after fasting prayer...
Cha mwisho alichonikumbusha Mungu usiku wa leo ni jambo nyeti na muhimu sana kwenye maisha yangu, kwa sababu bado sio officially to the public sitosema hili kwa sababu ya kimaadili ya kipentekoste na kwa sababu pia sijawiwa kuliweka wazi, ila ni jambo kubwa na la muhimu ambalo Mungu alisema na mimi katika kipindi ambacho sikuwa na shauku wala wazo tena la kuwa kama ilivyo sasa kwa sababu jambo lenyewe lilikuwa ni miaka zaidi ya tisa ilikuwa imepita tangu nilipopata shauku na nia yakulifanya jambo hilo, na nilijaribu mara kadhaa lakini was difficult lakini miaka miwili kasoro miaka mitatu iliyopita nikiwa Dar es salaam Mungu akasema na Mimi nikiwa kwenye namna ya sintofahamu na hata niliporudi nilipotaka kupita kushoto bado Mungu alinifanya kuwa kwenye njia sahihi aliyoikusudia.....
Baada ya kunipitisha katika historia ya maisha ya Yesu, Yusuph na kunikumbusha mambo makubwa ambayo amewahi kunifanyia mimi binafsi miaka ya nyuma. Ndipo akasema kwenye ukimya wangu sio kwamba sioni, bali nakuandaa kuwa yule ninaye mtaka mimi, sio unaejitaka wewe.
Naruhusu baadhi ya nyakati ngumu maishani ili kukufanya kuwa bora mara dufu, ili unitukuze mimi, kuna jambo la ziada ambalo nalitaka mimi wewe hulioni. Nyakati ngumu huwa na maana kubwa sana kwangu, kama ilivyotokea kwa Yusuph pamoja na Yesu...
Mnung'uniko, kukataa tamaa, kulaumu, na mutumia akili zetu wenyewe ndiyo sababu ya Mungu kukaa kimya wakati mwingine
No comments:
Post a Comment