Sunday, July 10, 2022

PENYE MITI WAJENZI WAPO

Ni ngumu sana kuamini maneno ya kale, kwamba penye miti hapana wajenzi, ni ngumu sana kumwamini mtu tajiri anapo yakiri maisha yake ya ufukara miaka ya nyuma kabla yakuwa namna alivyo leo.
Ukimsikiliza Barack Obama, Oprah Wilfred, Mzee Yusuph Bakhresa, Eric Shigongo, mwanzo wa Joseph kusaga, kaka Yangu Francis Sizya (Majizo) Mmiliki wa Radio 📻 ya E-Fm na wengine wengi, wanasema maisha magumu wanayajua na waliyaishi kwa vitendo kutoka kwenye familia zao...

Majizo anasema kuwa katika kila hatua aliyopita kwenye maisha yake, katika ukoo wake yeye ndiye amekuwa wa kwanza kwa kila hatua ya mafanikio, alikuwa wa kwanza kununua gari na vitu vingine vya Thamani kutoka kwenye familia masikini isiyojiweza kufanya jambo lolote lile la maendeleo...

Historia ya Shigongo Eric, niliisikia kupitia kinywa chake akisimulia lakini kupitia maandiko ya vitabu vyake ambavyo vimeelezea historia ya maisha yake ya ufukara. Kama haitoshi nilikuwa sehemu ya familia yake ya Global publishers ambayo imebeba baadhi ya watu wakubwa kiumri ambao walishuhudia ukuaji wa Eric pale Jijini Mwanza, wanasema ametokea familia duni sana yenye kunuka umasikini, kikwetu ukiitwa madaso basi fahamu uko kwenye level mbaya sana ya umasikini....

Asilimia kubwa ya sisi vijana wa kitanzania, tunaamini katika watu fulani kutubeba, tunaamini tulivyo ni kwa sababu ya historia mbovu ya familia zetu, tunaamini kuwa ndoto zetu ziko gizani kwa sababu  ya watu fulani, au serikali na wazazi wetu. 

Tunaamini kuwa kufikia utajiri na fahari ya dunia sio rahisi, ila tunaamini kwenye bahati kuwa ndiyo inaweza kuwa njia nzuri ya kufikia malengo na ndoto zetu. 

Kuna wakati wa kukubaliana na hali ya familia uliyotoka, hali uliyo nayo kwa sasa, kwa sababu kwa kufanya hivyo unatengeneza relief na chumba cheque hewa kwenye ufahamu wako. Unapokubaliana na hali hujenga nafasi nzuri ya kufikiri, kujifunza na kutafuta mbinu mpya ya kuhakikisha kwanza haurudii makosa ya wazazi, kuikataa hali uliyo nayo na hii inakupa courage na mwanzo mpya wa safari ya kuzifukuzia ndoto zako...
Tunajifunza kwa wazazi wetu waliofeli lakini baada ya kujifunza kwao tunageuka upande wa pili wa shilingi kwa kusema wazazi wangu walishindwa kwa sababu kadhaa lakini kuna familia ya moja kati ya vijana ambao tayari wameshaona mwanga wa maisha na vijana hawa ni wale wenye kutokea kwenye familia duni, wao walifanya nini mpaka wakaleta ukombozi wa kiuchumi katika familia zao.
Ndiyo maana ni vyema na ni nzuri sana kujifunza kwa aina vijana au watu waliofanikiwa ambao pia walipitia kwenye mikono ya wazazi wenye uchumi duni.
Inaweza isiwe rahisi kupitia njia ambazo wao walipita kufikia hapo walipo lakini kuwa kwenye kiwango cha maisha mazuri inaweza kukutia hamasa ya kuamini kuwa hata wewe unaweza kutoboa tundu la mafanikio kama wao...

Nimekuja gundua kuwa dunia iko na equal opportunity sasa ni mimi na wewe tunavyotazama hizo fursa na namna ya kuzitumia hizo fursa. Kama Mungu wetu yupo basi you can be a person you need to be and is very possible at any cost 

Wewe ni shujaa, make it to the maximum, trust the way you need to pass, and everything are possible under the beautiful world we have..
Glory be to God.
Mgemamoses@gmail.com 
Mgema Moses Zephania 

No comments:

Post a Comment