Asilimia kubwa ya watu huwa hawaamini katika michoro ya awali ndiyo maana sio rahisi sana watu kukupongeza unapoianza Safari ya kuhakikisha unazifikia ndoto zako, wengi ukiwashirikisha watakukatisha tamaa, au kukupa wazo mbadala wakijaribu kukuonyesha udhaifu wa hoja yako mbele yao.
Hawa wanaweza kuwa ni watu wako wa karibu zaidi ya unavyozani, anaweza kuwa mzazi, rafiki, mke na hata kiongozi wako wa Imani, kati ya hao watakuambia unawaza vitu visivyowezekanika,unawaza vitu ambavyo ukiwa na njaa ndiyo vinakupelekea huko, ni vyema upatiwe chakula ule ushibe ili kuondoa stress yanayosababishwa na njaa, hivyo ukila na kushiba utakuwa sawa na kuwaza vyema.
Cha ajabu zaidi yule yule anaekukatisha tamaa unaweza kumkuta akimpongeza mtu mwingine ambae walau picha ya wazo lake imeanza kutengeneza mwonekano unaopaswa kuwa, na atamwona shujaa kisa ameona uhalisia na ndiyo maana imekuwa ni rahisi sana mtoto wa kitanzania ndoto yake kufa kuliko mtoto wa kizungu au watoto wa Afrika Magharibi na nchi za Amerika ya kusini.....
Ni rahisi zaidi kumkuta mtu akimwelezea vyema sana Dangote kutoka nchini Nigeria na kumpongeza tajiri huyu kwamba alianzia katika kazi ndogo za kuuza vitu vidogo mtaani kwake huku akimwona shujaa, mtu huyu akimsimulia vyema sana Mzee Bakhresa kwamba alianza kuuza bidhaa ndogo ndogo pale kariakoo jijini Dar es salaam mpaka alipofikia leo na moyo wake ukapata furaha na utulivu sana...
Kwa sababu wanakujua kwa sababu umekuwa wakikuona kwa sababu wanamjua Baba yako na familia yako wanaamini kwenu halijawahi kutoka wazo bora, ndiyo maana hawaoni kwamba unaweza kuifanya ndoto kubwa iliyoko mbele yako.
Asilimia kubwa ya watu wanao kukatisha tamaa wana lengo la kuendelea kukutumia, wamepima hiyo picha na kuona matokeo makubwa kama utaifikia hivyo ni rahisi sana kukuambia jambo hilo ni gumu, linahitaji fedha nyingi, muda mwingi hivyo watakupa wazo mbadala, wazo rahisi (cheap idea) kwa sababu wanajua kwenye wazo dogo hakuna thamani ile ambayo unataka kutengeneza hapo kesho...
Wanafanya hivyo kwa sababu pia wanajua uwezo wako, na wanatamani kuendelea kukutumia na kukupa either ujira mdogo huku wakitumia taaluma yako kwa manufaa yao binafsi, au wao ni furaha yao kukuona unaendelea kuwalamba miguu na Kuwaita boss hiyo ndiyo furaha yao, hawataki ufukie levo zao, wanatamani kukuona mnyonge...
Wengine ufahamu wao ni mdogo, unachokiona sicho wanachokiona wao, wakati wewe unaona mpenyo wao wanaona lile jiwe kubwa ambalo haliwezi kuvunjwa vunjwa na kutoa mpenyo wa kufika ng'ambo ya pili ya mlima. Always ndoto kubwa huwa hazina njia rahisi kuzifikia (has no cheap strategies to be reached).
Angalia sana watu unaofanya nao kazi, watu unaowashirikisha idea zako, aina ya watu wanaokuzunguka, nikuambie kitu kimoja hivi, kuna wengine ni very good friends for you kwa sababu bado wanakutawala na hujawashirikisha wazo lenye afya na misuli ya kukutoa hapo ulipo, wanakupenda na kukushauri,ukipata hela fanya hivi, au watakuuliza una wazo gani au njoo na wazo zuri tutakupiga tafu ili na wewe ujitegemee kiuchumi, au kwa nini usifanye biashara hii, huo ni muda ambao wewe bado huoni kama inawezekana, ukiamua kufanya watakaa nyuma na kukuonyesha ni kwa kiwango gani wazo hilo ni gumu, au kutokukupa ahadi ambayo waliitoa kabla hujalielewa wazo lako au wakati unajitafuta....
Rafiki yangu kipenzi akanishirikisha kusoma kitabu kimoja cha kijana Mzimbabwe ambae alikuwa akifanya kazi sehemu Fulani, na kila jioni alikutana na marafiki zake kwenye eneo Fulani la starehe wakinywa soda na vinywaji vikali huku wakifurahia maisha. Baada ya muda aliona mikusanyiko hiyo haikuwa na faida sana kwenye ustawi wa maisha yao, hivyo aliona fursa kwenye mkusanyiko huo na ungeweza kuwafanya kuishi maisha mengine tofauti kabisa kuliko kuwa na mkusanyiko wa kila siku kwa ajili ya kutumia hata kile kidogo walichokuwa wanapata na kukinywea vinywaji huku wakifurahia urafiki wao...
Alikuja na wazo jema kwa ajili ya manufaa yao wote, lakini kati ya kundi la watu wanaoweza kufika sita hadi nane ni mmoja tu ndiyo alioona ile idea kuwa ni njema na kumsapoti vyema mpaka mwisho ingawa hata yeye hakuwa amelivaa wazo hilo kama ambavyo mwenye wazo alikuwa akiliona na mkusanyiko wao ulifika mwisho kwa sababu namna ya kufikiri kulitofautiana...
Ndivyo ilivyo hata leo kuwa wapo watu watakupa offers, watakupa muda wao wa ziada kwa ajili ya starehe lakini ukitaka kujikwamua kwa kushare nao wazo zuri ambalo litakufanya na wewe kuwa na nguvu ya kifedha vizuizi vitakuwa vingi sana mbele yako kwa sababu either hawako pamoja na wewe katika uhalisia au wanafurahia wanavyokuona na utafikiri wanakuwazia mema kumbe wanakusema hata unapokuwa haupo mbele ya macho yao.....
My take: Ile picha unayoiona kwanza wewe ndiyo hali halisi ya kitu ambacho kiweza kutokea kama utafanya kwa vitendo na kuzuia kelele za watu wenye nia isiyo njema wanaokuja mbele yako na chambo mbele ya ndoano, usiwape nafasi wazo lako ni bora kuliko Lao, bora wakakaa kimya kuliko kukutengenezea wazo jipya ambalo kiuhalisia sio wazo lako kama hawawezi kuliboresha ni vyema wakanyamaza, kama hawawezi kusiaidia ni vyema wakakaa kimya....
Muda uliotumia kuwaza, muda uliotumia kuomba, muda uliotumia kufanya utafiti ni vyema ukauheshimu na kuutendea haki vyema, rafiki wa kweli ni yule ambae unaweza kuona kile unachokiona, hata kama hawezi kuona vyema ila anaweza kusimama na wewe hata kwa kuafuata njia unayopita, hata kwa kukuombea tu....
Yesu alikuwa na watu wengi nyuma yake marafiki zake na wengine hata tembea yake waliiga nankufanana nao, wengine sema yao ikawa kama yake lakini, msalaba na kifo kilikuwa chake, Jesus was chasing his purpose ndiyo maana hata kwenye ugumu na kuachwa na watu, wafuasi wake lakini alikwenda hakubadili msimamo wake bali aliamua kutimiza Safari yake....
Duniani hakuna wazo gumu, duniani hakuna project ngumu, ugumu wa kwanza utaanzia kwako mwenyewe, msimamo wako, watu wanaokuzunguka, watu unaoshare wazo lako, ndiyo inaweza kukupa kile unataka au kutokufikia kabisa
My take two: Simaanishi ukatae ushauri, simaanishi usiwe challenged kwenye idea zako, wengine wapo kukamilisha kwa maana ya kukuboresha wewe, kwa hiyo wanapokupa wazo mbadala wanataka kufahamu hoja yako umeichukua kwa uelewa na upana kwa kiwango gani, je una maanisha, wengine hawatasema is wanakuunga mkono.
Usiache kwenda kwenye nyama choma kwa sababu unawazo lako, usiache kushirikisha watu idea zako kisa unaogopa kuwa opposed no, bali chagua watu sahihi kuwashirikisha, chagua muda sahihi kuwashirikisha pia, what I came to realise is that sio kila mtu anaesema ndiyo kwako ndiyo mtu sahihi au anasapoti idea yako, hivyo chagua
1. Watu sahihi tena wachache kuwashirikisha mambo yako, wengine cheka nao lakini usiruhusu wakujue sana....
2. Sio kila kampani ni sahihi nyingine ni kuptezeana muda tu...
Mwisho kabisa kamapani bora ni wewe mwenyewe na Mungu wako, maana ndiyo anajua kusudi lako, pili ni wewe mwenyewe, tatu mkeo ndiyo maana tunashauriwa kuwa na right partners kwenye maisha ambae atakielewa kile unachokiona kwenye ile picha kabla ya kuja kwenye uhalisia ⏰
Tambua muda sahihi wa kuwashirikisha watu wako muhimu hata kama ni watu sahihi kwako.
Tambua sio kila rafiki utamshirikisha wazo lako, warmup marafiki zako, wapo kwa ajili ya mambo ya kiroho, wengine kwa ajili ya mitoko na nyama choma, wengine kwa ajili ya mambo yako ya msingi zaidi nje ya mambo ya kiroho.
Hivyo kila mtu atakufaa kwa nafasi yake na atafanya vyema sana.
Let us enjoy and share this message
Niachie kommenti na ushauri wako mzuri..
Mgema Moses Zephania
mgemamoses@gmail.com
0755632375
No comments:
Post a Comment