Tuesday, July 12, 2022

IT'S YOUR OWN JOURNEY

Unapowaza kuwa mtu mkubwa, unapowaza kuifanya ile ndoto yako kuwa katika uhalisia, unapowaza kuwa lazima niwe na maisha mazuri, kuna maamzi unapaswa kuyafanya, kuna namna unapaswa kufanya ili kuwa yule Moses unayemtaka.
Kumbuka yule unayejitaka kuwa, haiwezi kuwa katika uhalisia kwa kutegemea msaada wa mtu, mtu Fulani kukupa chance, yupo kukutengenezea maisha hapana, utafurahia nao lakini mwisho wa siku kuna wakati wa kubaki wewe pekee yako.

Maisha yako yanakuhitaji wewe kuyafanyia maamzi, yanakuhitaji wewe kuyabadilisha na kuwa unavyotaka, sio Baba  sio mama wala sio hisani ya marafiki zako au marafiki wa Baba yako, ila ni wewe mwenyewe  ndiyo mwenye misuli yakuifanya ndoto yako kuwa katika uhalisia mkubwa na mpana.

Dunia ya leo iko wazi kwa kila mtu, dunia ya leo ni fursa sawa kwa kila mtu, hivyo ni uchaguzi wa kuwa wewe unavyotaka, ni uchaguzi wa kuchagua ni aina gani ya maisha unayataka sio watu wanataka nini kwenye maisha yako...

Ukitegemea kama kuna mtu atakuja kuwa sababu ya wewe kuishi ndoto yako sahau  hata kama huyo mtu atakuja kuwa daraja la maisha unayoyataka basi fahamu kuwa kuna kitu kimemfanya kuja ili kutengeneza WIN WIN situation, hakuna One side win, hivyo ni vyema kutambua nafasi yako wewe kama wewe...

Njia ya mafanikio ni pana sana ila pia ni nyembamba sana, ukiwa na fukra pana mlango wa kuyaendea mafanikio ni mpana sana bali ukiwa na chumba kidogo cha kuwaza na kufukiri basi mlango wa mafanikio ni mdogo kuliko lile tundu la sindano.

Ishi ndoto, ishi unavyotaka kwa kufanya maazi hata kama ni makali na yenye kuuma kiasi gani  just make it for your own benefit what I can say hata kama utakuwa na rafiki mzuri namna gani, ndugu wakati mwingine hata Baba yako, gawezi kukupa njia zote za mafanikil kwa sababu sio rahisi kufanya hivyo...

Kila mtu anapenda kuheshimiwa, kutawala na kuwaongoza wengine ndiyo maana ni ngumu sana kuigeuza nafsi iliyojaaa utajiri ikakupa mbinu bora ya kufanikiwa kwa uwazi na mapana kabisa bali mara nyingi watakupa samaki aliyevuliwa muda mrefu....

Fight your dream alone, let others come and witness the results 
Mgema Moses 
0719110760/0755632375
mgemamoses@gmail.com 
www.mosesmgema.blogspot.com
Instagram moses_mgema
amaris

No comments:

Post a Comment