Ndoto ni rahisi sana kuitamka, kuota ni rahisi sana na kusema ni rahisi sana pia lakini ukweli ni kwamba ndoto inahitaji vitu vingi sana ili kuweza kuikamilisha na kuwa kweli. Mtu akikusimulia waweza kuona ni rahisi sana lakini ukweli ni kwamba unahitaji mambo mengi sana binafsi ili kuweza kuifanya ndoto yako kuwa halisi....
Vijana wengi tuna tamani sana kumiliki, tunatamani sana kuwa watu wakubwa lakini, njia za kuelekea kumiliki hatutaki kuzipitia, katu kamwe tutabaki katika msongo wa mawazo na shauku ya kumili pasina kumiliki hizo ndoto...
Vijana wengi, tunapenda kuwa na magari mazuri, tunapenda kuwa nanyumba nzuri, familia nzuri lakini hatutaki kuitii michakato ambayo itatufanya kuwa wakubwa na wenye kumiliki mali na fedha tunazozitaka.....
Kumiliki hakuja kirahisi, kumiliki hakuji kama usiku na mchana, kumiliki kunahitaji sana kujitoa, kufanya kazi kwa jasho na damu, kuwa na nidhamu, kutumia muda na kuweza kusimamia kile unachokiamini, kuondoa aibu, kuondoa vijisababu vidogo vidogo, kuamini katika kile unachokiona na kukifuatilia kwa bidii na maarifa mengi...
Vijana wengi tunapenda kulala, vijana wengi tunapenda starehe, vijana wengi tunapenda fahari mbele za watu kuliko uhalisia wa maisha yenyewe, mwisho wa siku tunajikuta tunatengeneza lawama kwa watu wengine ambao tunahisi ndiyo chanzo cha maisha yetu kuharibika....
Kama una ndoto kubwa ndugu na rafiki yangu ni vyema kuhakikisha kuwa unakuwa askari wa maisha yako mwenyewe, ndoto inafukuziwa na wewe/mimi.
Rafiki yangu muda bado tunao ni vyema kuhakikisha tunakwenda kwenye haki na njia
No comments:
Post a Comment