Friday, July 15, 2022

MY TEN COMMANDMENTS OF LIFE

Nataka kuishi maisha ambayo nitakuwa na ujasiri wa kuyasimulia kwa watoto wangu. Maisha ambayo hata kama wakitaka waishi kama Mimi sitakuwa na haja ya kutoa maelezo.

Ndiyo naweza kukosea wakati mwingine lakini  yawe ni makosa ambayo yana mlengo wa kuleta matokeo chanya ya juhudi zangu katika kutafuta ufanisi na ubora katika kuzifikia ndoto zangu kuliko kufanya ufuska usio kuwa na tija wala faida kwangu na vizazi vijavyo..

Lengo langu pia nikutamani waone namna ninavyo fanya bidii katika kusahihisha makosa ya nyuma ili wasije kudhani makosa kama yangu ndio njia sahihi ya kufikia kusudi na Mpango wa Mungu kwenye maisha yangu na yao pia.

KWA HIYO: NIKIWA NIKO HAI NA MWENYE AKILI ZANGU TIMAMU, NIMEAMUA KWAMBA HIZI NDIYO KANUNI ZANGU ZA MAISHA MPAKA KIFO....(room of amendment for the future)

Nimeamua kwamba;
1. Nitakuwa mwadilifu
2. Nitakuwa mkweli
3. Nitakuwa mchapa kazi.
4. Nitamcha Mungu.
5. Nitawaheshimu watu wengine na kuwasema vizuri.
6. Nitajihidi kwa gharama yoyote kuwa mnyenyekevu.
7. Nitahusiana kimapenzi na mwanamke mmoja nitakae mwoa kwa ndoa ya madhabahuni.
8. Nitakuwa mwaminifu kwa Mungu, mke wangu, wazazi wangu, familia yangu, kanisa na watu wengine.
9. Nitajitoa kwa ajili ya wengine na kwa taifa langu.
10. Nitaamka asubuhi na mapema kuianza siku yangu kwa kuzingatia muda kwa kila jambo langu.

This is my commitment and I will read them every morning...

NB:  Haya mambo ni binafsi yalipaswa kuwa kwenye notebook yangu ya ndani. Nimeshare na wewe ili yanikumbushe wajibu wangu lengo ikiwa na pace katika kufikia malengo na ndoto zangu. Kwa sababu nimeona itanisaidia kuhakikisha nayaishi.

God is Good all the time 
Mgemamoses@gmail.com 

No comments:

Post a Comment