Wakati nasoma article hii, ilikuwa kama stori hivi kwangu, sikuchukulia kiundani sana kwa sababu niliona kama ni stori za kawaida za watu ambao tayari wamekwisha piga hatua kwenye maisha yao, niliona ni stori za kawaida kwa mtu ambae amefanikiwa, maana hata akisema uongo anaamini watu watakubali tu kwa sababu yeye ametimiza malengo na ndoto zake.
Nimekuwa nikifanya kazi nyingi na mara nyingi kazi ikiwa imekwisha kuanza hasa ikiwa imeanza kuonyesha matokeo, watu hunipongeza na kunitia moyo, lakini karibuni nimetaka kuanzisha kitu pamoja na rafiki yangu, kwa sababu ya usomi na akili Fulani ya kuamini katika kuanza, tulifanya utafiti kidogo kwa watu wa eneo hilo, pamoja na watu wanaofanya biashara kama hiyo
Asilimia kubwa ya washindani katika ile biashara walisema hapana, hii biashara kwa sasa ni ngumu, biashara hii inahitaji uzoefu maana changamoto zake zinahitaji mtu mzoefu sana na biashara. Nikajikumbusha baadhi ya michakato ya kuomba kazi kwenye mashirika binafsi (Private sectors) kwamba ukitaka kuomba kazi au tangazo la kazi likitoka lazima uwe na uzoefu Fulani....
Swali langu likaja kusema, hivi huyu asie na uzoefu afanye nini sasa maana kila sehemu uzoefu unahitajika, kazini uzoefuzi, biashara ni changamoto inahitaji mtu mzoefu, sasa tufanye nini.....
Ili kutoka hapa ni vyema kuwa na watu sahihi au ambao wanaweza kukwambia fanya hili linawezekana, usipofanya umasikini itakuwa halali yako, katu hautaweza kuijua potential yako, katu hutoweza kupiga hatua hata moja.
Watu wengi wanakatisha tamaa sana, watu wengi wanacheka na wewe ila katika mioyo yao hawakutakiii mema hata kidogo, wengine wanaogopa kukwambia ukweli wa biashara wanayofanya kwa sababu wanajua unaenda kuongeza options kwa wateja wa bidhaa yako.
Wakatu mwingine wamekutazama wamegundua kuwa unayo potential kubwa katika kazi, Ubuntu, pengine wanaogopa Elimu yako, pengine wanaogopa IQ yako, maana unauwezo wa kwenda kufanya zaidi ya wao.
Wapo dream killers Waepuke, usiwape Wazo lolote, usiwape nafasi katika maisha yako, usiwape chansi kwenye maisha yako, wanakupotezea muda, wanashikilia hatua zako, put them aside move forward, have right people kwenye njia yako.
Hakuna asie weza, pamoja na changamoto zote hizi lakini, hakuna mtu aliye wahi kujaribu kwa moyo akashindwa kufanya jambo, akiwa na bidii, maarifa kidogo lazima aone hatua kwenye jambo lolote hata kama shetani atasimama mbele yako
Nimejifunza mambo mengi sana unaposhare jambo lako na watu hata wale wa karibu yako wanaweza kuwa mwiba kwako, achana na watu wasio na msaada kwako, share nao kwa mambo unahisi ndio yaliwakutanisha.
Chagua watu wa msingi ambao watakupa mawazo mazuri, watakupush, watakushauri kwa lengo la kujenga, watakuencourage kufanya hatua katika kila jambo lako
Play fair, Be positive
2022 ni mwaka wa kupiga hatua
No comments:
Post a Comment