Tuesday, January 25, 2022

KUFIKIA NDOTO NI MCHAKATO...


Ukimwona mtu amekaa juu ya kilele cha mlima au yuko juu kabisa ya paa la nyumba, juu ya mti mkubwa basi jambo la kwanza kabla hujatamani kuwa hapo alipo, cha kwanza kabisa tambua gharama na hatua alizopitia ili kuwa hapo juu ya kilele cha kitu chochote kile...

Mfano mtu anapomwona amesimama katika kilele cha mlima wowote ule, jambo la kwanza fahamu hakuwa hapo kwa bahati mbaya bali kulikuwa na mchakato Fulani alioufanya hatimae akifika katika kilele hicho cha mlima, hali kadhalika katika paa la nyumba, au juu ya mti mrefu...

Ukiona mtu unazaa matunda yenye afya ambayo yakakufanya ukayatamani katika macho yako basi fahamu kuwa kabla ya hayo matunda kulikuwa na mchakato mrefu sana mpaka ustawi wa matunda katika mti yakaonekana mazuri na yakuvutia sana

Ukimwona mbunge, mchungaji, tajiri, mfanyabiashara, Daktari, mwalimu, mhandisi nk, fahamu kuna mchakato ulitumika ili kufika katika kigezo hicho, haikuwa ghafla kama uyoga uotavyo katika vichaka na vichuguu porini.

Ukiona ndoa bora jua msingi wake haukuwa wakawaida, hapana kuna michakato na hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuwa na ndoa imara ambayo leo ikaonekana hata katika macho yako.

Kwa nini nimeandika jambo hili....

Nimeandika kukumbusha kuwa, kila jambo katika dunia yetu ni mchakato, ni hatua ni zero, halafu 1 ndio 2,3,4,5.......hakuna 10 pasipo 0, halafu 1kile unachokitamani hakikuwa chochote kabla yakuwa hapo kilipo....

Vijana wengi tunatamani sana kuwa sehemu Fulani lakini hatuko tayari kupitia michakato Fulani ambayo itatufanya kufika katika kilele cha mlima wa ndoto zetu, vijana wengi tunataka kila kitu kiwe katika hatua ya kumi kabla ya hatua ya kwanza kabisa

Wengi wanataka maisha ya uyoga, leo ameota katika kichaka au kichuguu halafu kesho awe tayari kwa kuliwa. Hakuna mmea wenye changamoto kama uyoga, uyoga ukishachomoza tayari unaelekea mwisho wa maisha yake au unaelekea katika anguko la milele...

Ndivyo tulivyo vijana wengi, kila mtu anataka kufikia kilele cha ndoto yake ndani ya usiku mmoja kama uyoga, tunasahau kuwa hakuna mafanikio ya haraka yanayoweza kudumu....ndio maana leo vijana wengi tumejiunga na masuala ya kubet lakini bahati mbaya asilimia kubwa ya hata ambao wamewahi kushinda fedha hizi, pesa haikuwatoa mahali walipo bali iliingia na kupita.....

Hayo ndio maisha ya uyoga, huwa hayana maandalizi, huwa hayana formula, huwa ni yakujionyesha na mihemko, hivyo huwa hayana maandalizi kwa ajili ya kuishi miaka mingi....

Kabla hujatamani kufika hapo kwenye ile ndoto yako kubwa kabisa ni vyema kupitia michakato sahihi ambayo itakuandaa vyema kwa ajili ya mafanikio yako ya kesho.....

Usimtamani aliye juu bali tamani kujifunza ni namna gani yeye ameweza kupenya, kwenye misitu, miinuko na changamoto nyingi njiani mpaka kufikia kilele cha mafanikio yake....

Kila mmoja ana ndoto kubwa, lakini kama huna ubavu wakufikia ndoto hiyo kwq sababu tu inahitaji either fedha nyingi na mtaji mkubwa basi ni vyema kutafuta njia mbadala na sahihi ambayo itaanza kuchora Romania yakufika kwenye kilele cha ndoto na maono yako.....

Unataka kumiliki petrol ⛽ na gharama yake ni zaidi ya mamilioni, basi uangushe mti wa mbuyu kwa shoka dogo ambalo utalitumia vyema kuukata ule mbuyu kwakuuzunguka taratibu hatimae utaungusha....

Lengo lako litabiki palepale maana unalijua ila changamoto ni.mtaji hivyo kama huna million Mia 600 lakini huwezi kukosa elfu kumi kama mtaji ambao utautumia kama msingi na daraja la kuelekea kileleni. Biashara ndogo inaweza kukupa uzoefu na kuwa daraja la kwako kesho....

Usitamani kuwa kileleni katika usiku mmoja tamani kuwa kileleni kwa kufuata njia sahihi ambazo zitakufikisha hapo kileleni, huku chini ukiwa umejenga msingi imara....

Yaogope maisha ya uyoga, ishi maisha ya Tembo, uzao mmoja, wanyama wote wanatambua kuna mkubwa anazaliwa leo, lakini miezi  yakutosha sana, ukilinganisha na uyoga au mbwa wabwekaji...

Mgemamoses@gmail.com 
Mgema Moses

No comments:

Post a Comment