Friday, January 7, 2022

MAISHA NI MAHUSIANO BORA

Maisha ni fumbo amabalo ni ngumu sana kulifumbua inahitaji hekima, busara na mtazamo wenye ukomavu ndani  yake. Hakuna dunia ya pekee yako, hakuna mtu anae ishi katikati ya watu wengine akaishi kama yuko nyikani au jangwani.

Hii ni kwa sababu  tumeumbwa kwa kutegemeana, kushirikiana, kusaidiana na kuinuana, iwe moja kwa moja au kupitia mlango wa nyuma. Maisha ni picha isiyohitaji maelezo ya ziada, kwa aliye komaa kupitia picha tu anaweza kuelewa kinachomaanishwa na picha yenyewe.

Ni vyema kuishi maisha kwa utulivu, ushirika mwema, upendo, kuthamini wengine na kusameheana pale inapotokea mtofautiano. Kumbuka  katikati  ya watu kutofautiana, kupishana, kukwaruzana ni jambo la kawaida.

Kama kwenye nyumba za ibada watu wanaweza kutofautiana, kama Shetani pamoja na mazuri yote ambayo  alikuwa akipata huko mbinguni lakini bado, alitofautiana na Mungu  sembuse mtu kwa mtu, kutofautiana ni jambo  la kawaida kabisa.

Kutofautiana huletwa na kupishana kwa mitazamo na hoja, kukutetea maslahi ya kila mtu na Jamii yake, mambo  ya kazi, biashara na mambo mengine mengi kwenye  Jamii yetu, maofsini yawezekana ukatofautiana na sera ya mwajiri, mwajiri asiridhishwe na utendaji kazi wa mwajiriwa, hivyo lazima iwepo tofauti.

Lakini kutofautiana kwa hoja au mitazamo sio sababu ya kutengeneza uadui na chuki za kudumu kati yetu sisi kama binadamu, jitahidi  kufanya mambo ambayo yanalenga kuleta upendo kati yenu ili amani itawale, amani ikitawala lazima kuwe na matokeo yenye ufanisi katika kila jambo.

Unapoondoka mahali hata kama umeondoka kwa namna sio nzuri, ni vyema kusamehe na kusahau, kwa sababu  hata baada ya kazi kuna maisha. Ukifukuzwa kazi au mahali Fulani hata kama unahisi au unajua umekosewa ni vyema kuondoka mahali pale na kumshukuru Mungu kwa yote.

Pale unapofikri umeonewa, kunyanyaswa, kutokutendewa haki, udhika kwa muda kama binadamu lakini usishikilie jambo kwa miaka na miaka, huwezi jua kwa nini uliondoka mahali pale, Mungu huwa anajua kabla ya sisi kujua.

Tinachofikiri kwetu ni kibaya au kinatuumiza kumbuka kwa Mungu  inaweza kuwa ni sawa, na kile tunachohisi ni kizuri kwa upande wetu kwa Mungu inaweza kuwa sio sawa.

Mifano miwili halisi, Ayubu baada ya kupata majaribu makali, ilionekana kama Mungu amemwacha mpaka watu wake wa karibu wakaanza kusema amkufuru Mungu afe lakini alijua Mungu kwake ni nani.

Hawa aliona wema wa nyoka katika ile bustani, akaona huyu Mungu hafai kwa nini anatukatalia tenda hili, akaona kilichoko mbele yake ni chema kuliko yake kina faida kuliko maagizo ya awali kutoka kwa Mungu.

Matokeo ya watu hawa wawili yanaonyesha ni kwa kiasi gani maisha yetu ni fumbo na kesho yetu iko mikononi mwa Mungu, na Mungu ndie mwamzi wa kila kesho yetu. Usiishi kwa kufuata hisia na matakwa binafsi, tulia, jifunze, toa nafasi kabla ya kuchukua maamzi ambayo  unafikiri ni maamzi sahihi kwako.

Jenga mahusiano  bora na imara maana kesho yako huijui, ukifukuzwa kazi mahali, usitengeneze uadui pamoja na kufukuzwa kesho wanaweza kukurejesha maana yawezekana wanachukua maamzi kwa sababu ya maneno ya watu ambao wametengeneza fitina  na wanaona wewe ni bora kuliko wao.

Kuna wakati unafukuzwa kazi kwa sababu  watu wanataka kuprove yale mashitaka unayoshitakiwa nayo kama ni kweli, hivyo ukiondolewa jitahidi sana kuzuia hasira, kinywa kunena matusi, ugomvi na ukorofi, jitahidi kutulia na kuondoka.

Kama ulionewa haki yako haiwezi kupotea, pengo lake litaonekana kama walikuondoa kwa hila na fitina, yawezekana waliokuondoa walikuwa wanataka kuyadhibitisha yale mashitka kama ni ya kweli au uongo, 

Ukichoka mahali, usiondoke kama umefukuzwa, fuata utaratibu mzuri wa kuomba kuondoka mahali Fulani, kama walivyokupokea katika familia, kazini, kwenye nyumba za ibada, au mahali popote ni vyema ukiwa umepata mwanga wa kuweza kujitegemea, Mungu  amekuinua umepata kazi mpya, umepandishwa cheo ndani ya ofsi, umechoka kuwa sehemu ya familia, ofsi, biashara  nk, ondoka kwa amani, aga vyema, ili iwe kwa heri ya kuonana.

Kesho yangu siijui, kesho yako huijui ni vyema kulinda mahusiano  yako na watu, hao hata kesho watakutetea mahali, utakuwa na ujasiri wa kurudi mahali, maana uliondoka kwa amani, uliaga na kuondoka kwako, itakuwa kwa heri ya kuonana tena.
Hatuwezi kupendezana katika yote ila tunaweza kupunguza pengo la chuki, uadui na uhasama usiokuwa wa lazima.

Mwaka huu, utumiae kama mwaka wakujenga mahusiano bora kwa kadri  uwezavyo, hakika utakuwa mwaka bora wa kuzaa matunda. Zaidi jifunze kunyamaza, sio kila neno lazima uongee....

Moses_mgema Zephaniah 
0755632375
0719110760

1 comment: