Tuesday, January 11, 2022

JIHUSIANISHE NA WATU WENYE MUONO CHANYA

Kwa sisi wakristo  tukisoma katika Biblia takatifu, kuna maandiko yanasema (ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo) ni ujumbe ambao umesimamia kwenye msimamo wa kiimani zaidi ukiusoma kwa haraka haraka bila kuwa na takafakari ya ndani zaidi ili kujua nini mwandishi alikuwa Ana maanisha wakati anaavuviwa na Roho Mtakatifu.

Kujiona, kujiweka katika nafasi Fulani, iwe kifikra, mtazamo, watu unaojihusianisha nao wana asilimia kubwa sana yakuamua uishi vipi. Kuna wakati ni ngumu sana kumtambua kenge au nyoka katikati  ya samaki wenye umbo kama la nyoka au kenge, vilevile inaweza kuwa ni ngumu sana kumfahamu kamongo akiwa katikati  ya nyoka

Maana yangu ni kwamba aina ya watu unaotembea nao wanaasilimia kubwa ya kuathiri maisha yako katika, mwenendo, mtazamo na fikra zako, mfano ukitembea na watu wanaoishi uswahilini kuna asilimia kubwa sana ya wewe kuadapt yale mazingira  ya uswahilini, tabia na aina ya maisha wanayoishi watu wa uswahilini, hata kama ulitokea kwenye aina Fulani ya maisha.

Asilimia  kubwa ya watu wanaoishi uswahilini  wana aina yao ya maisha, staili  na mfumo wa maisha yao, umbea, kuwekeana miziki ya masimango, vichambo na kusutana, sio jambo la kushitusha mtoto kupata ujauzo na jamii isishangae, kuacha shule ni jambo la kawaida, hii inatokea kwa sababu  ya mazingira kuwashepu katika aina hiyo ya maisha.

Vilevile watu wanaoishi kwenye  mitaa Fulani  hivi ambayo haina uswahili  mwingi wana mtindo wao wa maisha ambao hata kama mtu hana kipato lakini mara nyingi anakuwa na mtazamo Fulani wa tofauti juu ya watoto wake na familia yake, hata utakuta hana elimu, hana kazi nzuri, mbangaizaji tu, na watoto wake wanasoma government  schools  bado atawasisitiza kusoma na kuwapa mtazamo ulio chanya zaidi.

Nilichojifunza association ya watu inaathili sana maisha ya mtu kuanzia, mtazamo wa ndani na mpaka tabia na matendo ya nje. Mtu anaweza kuwa alikuwa bora lakini akajiungamanisha na aina Fulani  ya watu na wale watu wakam-affect either chanya  au hasi

Hapa nataka kusema nini......?

Ni vyema kutambua kuwa hali ya maisha uliyo nayo isiwe sababu  ya kuamua kuishi kwenye kundi lenye aina moja ya maisha na wewe hasa kwa sisi ambao bado tunapambania kufikia level Fulani ya maisha, jenga tabia yakujichanganya na watu ambao tayari wanahatua zinazoonekana au tayari wanamwanga katika maisha yao....

Watu ambao wanahatua za maendeleo katika maisha yao na umeona wakipambana sana hadi kufika leo waliyopo. Ukiishi kwenye aina Fulani ya maisha, ukazungukwa na aina Fulani ya watu wenye mtazamo duni una hatari kubwa yakuishia kwenye matamanio  na kushindwa kuondoka kwenye eneo hilo kwa sababu  hakuna mtu anakupa kutamani kuondoka kwenye hiyo hali.

Watu wote wanafaida na umuhimu wake katika maisha ya kila siku, lakini tunapozungumzia hatua ya kusonga mbele katika maisha Fulani  ni vyema sana kuapply kanuni ya kujipendekeza kwa faida.

Mfano ukiwa na marafiki 20 wenye uwezo wa kati na wewe pekee yako ukawa na uwezo wa Chini zaidi yao, ni rahisi zaidi wewe kuinuka na kuwafikia wao kwa sababu kwanza kuanzia kuvaa, kuzungumza, fikra zako zitakuwa katika level ya hao rafiki zako hata kama bado katika umiliki wa Mali haujawa sawa nao, mfano unaweza ukawa huna uwezo wa kununua nguo za special  dukani lakini ukatumia nguo zako za mtumba kuziweka vizuri na kuwa katika mwonekano sawa na wenzako hata kama sio mlingano wa kila kitu.

Katika zama hizi za kukuwa kwa sayansi  na teknolijia  ni vyema sana, kuishi maisha yenye faida na focus  Fulani kuliko kuishi kishikaji zaidi, usiishi kwenye level ya watu ambao hawawezi kukuongezea chochote  kwenye  maisha yako, ni kweli ni ngumu kupewa pesa na mtu lakini walau wakupe machango wa mawazo na fikra chanya ambazo zitakutoa hatua moja kwenda hatua nyingine.

Maisha ni uamzi wa nini unakitaka katika kuhakikisha unatimiza malengo na ndoto zako, cha msingi ni kutengeneza channel sahihi na watu sahihi wenye mtazamo mpana katika maisha yao, kuliko kuwa na watu ambao mara zote wanafikri kidogo na baadhi yao kuishi kwenye misemo ya kiafrika etc maisha ni haya haya, hakuna ukiamua kuikataa hali yako mambo yanawezekana hakika.

Siku moja rafiki yangu aliniambia tukutane eneo Fulani maarufu sana hapa singida, chakula chake kidogo bei yake inahitaji moyo kutoa malipo ya chakula ambacho kiasi kile kile naweza kukipata tena katika ujazo mkubwa kuliko hicho wakati mwingine hata ubora unaweza kuwa sawa au wa mamantilie uwe bora zaidi, akaniambia mimi ntalipia wewe njoo, nikaenda pale, baada ya kukaa nikamwona mbunge wangu, mara akaja meneja wa kampuni Fulani, mara watu wa benki, mara wafanyabiashara Fulani wakubwa na maarufu sana hapa mkoani kwetu....

Baada ya kutoka akaniambia umejifunza nini, kabla sijajibu akasema, michongo yenye maana hupatikana maeneo kama haya, connection zenye kukuexpose wewe ziko maeneo haya, cheini za watu wenye uwezo wa kukushika mkono na kukupa hatua moja wako hapa, watu wenye kuweza walau kukuonyesha njia asilimia kubwa wanapatikana maeneo haya.

Ni kweli huna fedha, lakini huwezi kukosa elfu mbili ya kunywa soda eneo kama hili ambalo, linakutanisha watu wengi  wenye nafasi serikalini, wamiliki wa makampuni, mameneja wa makampuni na watu wenye mishe za kueleweka m hapa mjini...

Ni kweli  tupaswa kuwa watu wenye  bajeti yakupunguza matumizi yetu kwa asilimia kubwa, lakini katika kidogo unachopata basi kifanye kwa asilimia ndogo kiwe daraja la wewe kufanya hatua mpya kwenye maisha yako

Yawezekana upo mahali kwa sababu ya watu wanaokuzunguka, watu wenye fikra hafifu, watu ambao hawawezi hata kukushika mkono, watu ambao wanapambania kodi na chakula cha kila siku, kama una ndoto kubwa huwezi kuzifikia utaziota kama njozi za usiku tu...

Badilisha mtazamo, kumbuka ukikaa karibu na ua ridi utanukia walau manukato mazuri ya ua hilo. Ukikaa karibu na watu wakubwa katika mkoa au katika nchi ni rahisi zaidi kudodosa hata michongo ambayo kwa elimu yako, uzoefu wako unaweza ukajikuta unasikia hiyo nafasi na ukajipima na kujiona unafiti kwa nafasi hiyo

Ukiishi ndani ya box moja utapotea, jaribu kuwa na mambo mengi ambayo yatakupa uwanja mpana wakufikiri zaidi, ile kuona watu wanachoma nyama, wanateketeza laki kwa mara moja, kama una akili yenye mtazamo wakujifunza utahamasika kupambana na kumiliki fedha nyingi ambazo zitakupa kufanya chochote  unachotaka katika haya maisha......

Unajua wakati mwingine walevi wanafaida sana kwenye  baadhi ya maeneo, unaweza kujenga urafiki na mlevi na wewe sio mlevu lakini kwa sababu  upo karibu nao, akilewa anaweza  kukuambia jambo ambalo asingefanya hata kama ungemwekea bunduki kama hajalewa.

Jifunze  kutanua channel  zako kwa kuwa na watu wenye kada  tofauti na wewe, usiwaache marafiki zako lakini jaribu kutengeneza  watu wangine ambao unaweza kujifunza kwao, watu ambao unaweza kuwauliza jambo ikawa rahisi kukupa mawazo chanya......

Tembelea maeneo Fulani Fulani ambayo yatakupa changamoto mpya katika maisha yako, usiishi kwenye eneo moja la mzunguko wa watu wakawaida wenye mtazamo hasi.....

Prepared by 
Musa Zephaniah Mgema
0719110760
0755632375
mgemamoses@gmail.com 

No comments:

Post a Comment