Sunday, January 30, 2022

Siku nilikuwa namsikiliza Eric Shigongo moja kati ya wafanyabiashara wakubwa katika nchi yetu ambae amwekeza nguvu na akili yake katika kutengeneza mtazamo chanya kwa vijana juu ya ndoto zao.....
Shigongo Eric alisema kuna wakati unapaswa kutembea kwenye njia ambayo wewe mwenyewe unaiona sio ambayo wengine pia wanaiona ilimradi hiyo njia unaiona inakupeleka kwenye njia ya kufikia ndoto na malengo yako basi tembea hiyo njia bila kujali ni wangapi wataiunga mkono.

Kati ya sababu za watu wengi kushindwa kufikia malengo na ndoto katika ulimwengu nikuishi katika mawazo ya wengi, mawazo ambayo watu wengi wanasapoti na kuyakubali, mara nyingi mawazo kama hayo huwa hayana maajabu katika dunia iliyojaa ubunifu na uthubutu kila mahali....

Njia ngumu huwa na upkeep sana, njia ambayo wengi hawaiungi mkono, mara nyingi njia hiyo huwa na mafanikio au matokeo makubwa mbeleni kuliko easy way ambayo kila mtu anaweza kupita.

Yesu ni miongoni mifano hai ambao ulipita kwenye njia ambayo hakuna hata mmoja anae tamani kupita njia hiyo. Yesu mpaka anafikia lengo na kusudi la kuwepo duniani alipitia kukataliwa, kuwindwa kufa tangu akiwa katika umri mdogo, njia yake ilisongwa na changamoto nyingi kwa lengo la kumkatisha tamaa, lakini alifanikiwa kuishi kwenye kusudi lake kwa sababu tu kabla wengine hawajajua yeye alikuwa anajua nini anachofanya.....

Yusuph pia ni.miongoni mwa watu wa mfano katika ulimwengu, ni mtu aliyekoswa kuuwawa na ndugu zake, aliuzwa utumwani, pamoja na kuwa katika utumwani lakini hakuacha kufuatilia ndoto yake maana aliijua na alijua kusudi la Mungu ndani yake

Tuesday, January 25, 2022

KUFIKIA NDOTO NI MCHAKATO...


Ukimwona mtu amekaa juu ya kilele cha mlima au yuko juu kabisa ya paa la nyumba, juu ya mti mkubwa basi jambo la kwanza kabla hujatamani kuwa hapo alipo, cha kwanza kabisa tambua gharama na hatua alizopitia ili kuwa hapo juu ya kilele cha kitu chochote kile...

Mfano mtu anapomwona amesimama katika kilele cha mlima wowote ule, jambo la kwanza fahamu hakuwa hapo kwa bahati mbaya bali kulikuwa na mchakato Fulani alioufanya hatimae akifika katika kilele hicho cha mlima, hali kadhalika katika paa la nyumba, au juu ya mti mrefu...

Ukiona mtu unazaa matunda yenye afya ambayo yakakufanya ukayatamani katika macho yako basi fahamu kuwa kabla ya hayo matunda kulikuwa na mchakato mrefu sana mpaka ustawi wa matunda katika mti yakaonekana mazuri na yakuvutia sana

Ukimwona mbunge, mchungaji, tajiri, mfanyabiashara, Daktari, mwalimu, mhandisi nk, fahamu kuna mchakato ulitumika ili kufika katika kigezo hicho, haikuwa ghafla kama uyoga uotavyo katika vichaka na vichuguu porini.

Ukiona ndoa bora jua msingi wake haukuwa wakawaida, hapana kuna michakato na hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuwa na ndoa imara ambayo leo ikaonekana hata katika macho yako.

Kwa nini nimeandika jambo hili....

Nimeandika kukumbusha kuwa, kila jambo katika dunia yetu ni mchakato, ni hatua ni zero, halafu 1 ndio 2,3,4,5.......hakuna 10 pasipo 0, halafu 1kile unachokitamani hakikuwa chochote kabla yakuwa hapo kilipo....

Vijana wengi tunatamani sana kuwa sehemu Fulani lakini hatuko tayari kupitia michakato Fulani ambayo itatufanya kufika katika kilele cha mlima wa ndoto zetu, vijana wengi tunataka kila kitu kiwe katika hatua ya kumi kabla ya hatua ya kwanza kabisa

Wengi wanataka maisha ya uyoga, leo ameota katika kichaka au kichuguu halafu kesho awe tayari kwa kuliwa. Hakuna mmea wenye changamoto kama uyoga, uyoga ukishachomoza tayari unaelekea mwisho wa maisha yake au unaelekea katika anguko la milele...

Ndivyo tulivyo vijana wengi, kila mtu anataka kufikia kilele cha ndoto yake ndani ya usiku mmoja kama uyoga, tunasahau kuwa hakuna mafanikio ya haraka yanayoweza kudumu....ndio maana leo vijana wengi tumejiunga na masuala ya kubet lakini bahati mbaya asilimia kubwa ya hata ambao wamewahi kushinda fedha hizi, pesa haikuwatoa mahali walipo bali iliingia na kupita.....

Hayo ndio maisha ya uyoga, huwa hayana maandalizi, huwa hayana formula, huwa ni yakujionyesha na mihemko, hivyo huwa hayana maandalizi kwa ajili ya kuishi miaka mingi....

Kabla hujatamani kufika hapo kwenye ile ndoto yako kubwa kabisa ni vyema kupitia michakato sahihi ambayo itakuandaa vyema kwa ajili ya mafanikio yako ya kesho.....

Usimtamani aliye juu bali tamani kujifunza ni namna gani yeye ameweza kupenya, kwenye misitu, miinuko na changamoto nyingi njiani mpaka kufikia kilele cha mafanikio yake....

Kila mmoja ana ndoto kubwa, lakini kama huna ubavu wakufikia ndoto hiyo kwq sababu tu inahitaji either fedha nyingi na mtaji mkubwa basi ni vyema kutafuta njia mbadala na sahihi ambayo itaanza kuchora Romania yakufika kwenye kilele cha ndoto na maono yako.....

Unataka kumiliki petrol ⛽ na gharama yake ni zaidi ya mamilioni, basi uangushe mti wa mbuyu kwa shoka dogo ambalo utalitumia vyema kuukata ule mbuyu kwakuuzunguka taratibu hatimae utaungusha....

Lengo lako litabiki palepale maana unalijua ila changamoto ni.mtaji hivyo kama huna million Mia 600 lakini huwezi kukosa elfu kumi kama mtaji ambao utautumia kama msingi na daraja la kuelekea kileleni. Biashara ndogo inaweza kukupa uzoefu na kuwa daraja la kwako kesho....

Usitamani kuwa kileleni katika usiku mmoja tamani kuwa kileleni kwa kufuata njia sahihi ambazo zitakufikisha hapo kileleni, huku chini ukiwa umejenga msingi imara....

Yaogope maisha ya uyoga, ishi maisha ya Tembo, uzao mmoja, wanyama wote wanatambua kuna mkubwa anazaliwa leo, lakini miezi  yakutosha sana, ukilinganisha na uyoga au mbwa wabwekaji...

Mgemamoses@gmail.com 
Mgema Moses

Tuesday, January 11, 2022

JIHUSIANISHE NA WATU WENYE MUONO CHANYA

Kwa sisi wakristo  tukisoma katika Biblia takatifu, kuna maandiko yanasema (ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo) ni ujumbe ambao umesimamia kwenye msimamo wa kiimani zaidi ukiusoma kwa haraka haraka bila kuwa na takafakari ya ndani zaidi ili kujua nini mwandishi alikuwa Ana maanisha wakati anaavuviwa na Roho Mtakatifu.

Kujiona, kujiweka katika nafasi Fulani, iwe kifikra, mtazamo, watu unaojihusianisha nao wana asilimia kubwa sana yakuamua uishi vipi. Kuna wakati ni ngumu sana kumtambua kenge au nyoka katikati  ya samaki wenye umbo kama la nyoka au kenge, vilevile inaweza kuwa ni ngumu sana kumfahamu kamongo akiwa katikati  ya nyoka

Maana yangu ni kwamba aina ya watu unaotembea nao wanaasilimia kubwa ya kuathiri maisha yako katika, mwenendo, mtazamo na fikra zako, mfano ukitembea na watu wanaoishi uswahilini kuna asilimia kubwa sana ya wewe kuadapt yale mazingira  ya uswahilini, tabia na aina ya maisha wanayoishi watu wa uswahilini, hata kama ulitokea kwenye aina Fulani ya maisha.

Asilimia  kubwa ya watu wanaoishi uswahilini  wana aina yao ya maisha, staili  na mfumo wa maisha yao, umbea, kuwekeana miziki ya masimango, vichambo na kusutana, sio jambo la kushitusha mtoto kupata ujauzo na jamii isishangae, kuacha shule ni jambo la kawaida, hii inatokea kwa sababu  ya mazingira kuwashepu katika aina hiyo ya maisha.

Vilevile watu wanaoishi kwenye  mitaa Fulani  hivi ambayo haina uswahili  mwingi wana mtindo wao wa maisha ambao hata kama mtu hana kipato lakini mara nyingi anakuwa na mtazamo Fulani wa tofauti juu ya watoto wake na familia yake, hata utakuta hana elimu, hana kazi nzuri, mbangaizaji tu, na watoto wake wanasoma government  schools  bado atawasisitiza kusoma na kuwapa mtazamo ulio chanya zaidi.

Nilichojifunza association ya watu inaathili sana maisha ya mtu kuanzia, mtazamo wa ndani na mpaka tabia na matendo ya nje. Mtu anaweza kuwa alikuwa bora lakini akajiungamanisha na aina Fulani  ya watu na wale watu wakam-affect either chanya  au hasi

Hapa nataka kusema nini......?

Ni vyema kutambua kuwa hali ya maisha uliyo nayo isiwe sababu  ya kuamua kuishi kwenye kundi lenye aina moja ya maisha na wewe hasa kwa sisi ambao bado tunapambania kufikia level Fulani ya maisha, jenga tabia yakujichanganya na watu ambao tayari wanahatua zinazoonekana au tayari wanamwanga katika maisha yao....

Watu ambao wanahatua za maendeleo katika maisha yao na umeona wakipambana sana hadi kufika leo waliyopo. Ukiishi kwenye aina Fulani ya maisha, ukazungukwa na aina Fulani ya watu wenye mtazamo duni una hatari kubwa yakuishia kwenye matamanio  na kushindwa kuondoka kwenye eneo hilo kwa sababu  hakuna mtu anakupa kutamani kuondoka kwenye hiyo hali.

Watu wote wanafaida na umuhimu wake katika maisha ya kila siku, lakini tunapozungumzia hatua ya kusonga mbele katika maisha Fulani  ni vyema sana kuapply kanuni ya kujipendekeza kwa faida.

Mfano ukiwa na marafiki 20 wenye uwezo wa kati na wewe pekee yako ukawa na uwezo wa Chini zaidi yao, ni rahisi zaidi wewe kuinuka na kuwafikia wao kwa sababu kwanza kuanzia kuvaa, kuzungumza, fikra zako zitakuwa katika level ya hao rafiki zako hata kama bado katika umiliki wa Mali haujawa sawa nao, mfano unaweza ukawa huna uwezo wa kununua nguo za special  dukani lakini ukatumia nguo zako za mtumba kuziweka vizuri na kuwa katika mwonekano sawa na wenzako hata kama sio mlingano wa kila kitu.

Katika zama hizi za kukuwa kwa sayansi  na teknolijia  ni vyema sana, kuishi maisha yenye faida na focus  Fulani kuliko kuishi kishikaji zaidi, usiishi kwenye level ya watu ambao hawawezi kukuongezea chochote  kwenye  maisha yako, ni kweli ni ngumu kupewa pesa na mtu lakini walau wakupe machango wa mawazo na fikra chanya ambazo zitakutoa hatua moja kwenda hatua nyingine.

Maisha ni uamzi wa nini unakitaka katika kuhakikisha unatimiza malengo na ndoto zako, cha msingi ni kutengeneza channel sahihi na watu sahihi wenye mtazamo mpana katika maisha yao, kuliko kuwa na watu ambao mara zote wanafikri kidogo na baadhi yao kuishi kwenye misemo ya kiafrika etc maisha ni haya haya, hakuna ukiamua kuikataa hali yako mambo yanawezekana hakika.

Siku moja rafiki yangu aliniambia tukutane eneo Fulani maarufu sana hapa singida, chakula chake kidogo bei yake inahitaji moyo kutoa malipo ya chakula ambacho kiasi kile kile naweza kukipata tena katika ujazo mkubwa kuliko hicho wakati mwingine hata ubora unaweza kuwa sawa au wa mamantilie uwe bora zaidi, akaniambia mimi ntalipia wewe njoo, nikaenda pale, baada ya kukaa nikamwona mbunge wangu, mara akaja meneja wa kampuni Fulani, mara watu wa benki, mara wafanyabiashara Fulani wakubwa na maarufu sana hapa mkoani kwetu....

Baada ya kutoka akaniambia umejifunza nini, kabla sijajibu akasema, michongo yenye maana hupatikana maeneo kama haya, connection zenye kukuexpose wewe ziko maeneo haya, cheini za watu wenye uwezo wa kukushika mkono na kukupa hatua moja wako hapa, watu wenye kuweza walau kukuonyesha njia asilimia kubwa wanapatikana maeneo haya.

Ni kweli huna fedha, lakini huwezi kukosa elfu mbili ya kunywa soda eneo kama hili ambalo, linakutanisha watu wengi  wenye nafasi serikalini, wamiliki wa makampuni, mameneja wa makampuni na watu wenye mishe za kueleweka m hapa mjini...

Ni kweli  tupaswa kuwa watu wenye  bajeti yakupunguza matumizi yetu kwa asilimia kubwa, lakini katika kidogo unachopata basi kifanye kwa asilimia ndogo kiwe daraja la wewe kufanya hatua mpya kwenye maisha yako

Yawezekana upo mahali kwa sababu ya watu wanaokuzunguka, watu wenye fikra hafifu, watu ambao hawawezi hata kukushika mkono, watu ambao wanapambania kodi na chakula cha kila siku, kama una ndoto kubwa huwezi kuzifikia utaziota kama njozi za usiku tu...

Badilisha mtazamo, kumbuka ukikaa karibu na ua ridi utanukia walau manukato mazuri ya ua hilo. Ukikaa karibu na watu wakubwa katika mkoa au katika nchi ni rahisi zaidi kudodosa hata michongo ambayo kwa elimu yako, uzoefu wako unaweza ukajikuta unasikia hiyo nafasi na ukajipima na kujiona unafiti kwa nafasi hiyo

Ukiishi ndani ya box moja utapotea, jaribu kuwa na mambo mengi ambayo yatakupa uwanja mpana wakufikiri zaidi, ile kuona watu wanachoma nyama, wanateketeza laki kwa mara moja, kama una akili yenye mtazamo wakujifunza utahamasika kupambana na kumiliki fedha nyingi ambazo zitakupa kufanya chochote  unachotaka katika haya maisha......

Unajua wakati mwingine walevi wanafaida sana kwenye  baadhi ya maeneo, unaweza kujenga urafiki na mlevi na wewe sio mlevu lakini kwa sababu  upo karibu nao, akilewa anaweza  kukuambia jambo ambalo asingefanya hata kama ungemwekea bunduki kama hajalewa.

Jifunze  kutanua channel  zako kwa kuwa na watu wenye kada  tofauti na wewe, usiwaache marafiki zako lakini jaribu kutengeneza  watu wangine ambao unaweza kujifunza kwao, watu ambao unaweza kuwauliza jambo ikawa rahisi kukupa mawazo chanya......

Tembelea maeneo Fulani Fulani ambayo yatakupa changamoto mpya katika maisha yako, usiishi kwenye eneo moja la mzunguko wa watu wakawaida wenye mtazamo hasi.....

Prepared by 
Musa Zephaniah Mgema
0719110760
0755632375
mgemamoses@gmail.com 

Monday, January 10, 2022

ONDOA WATU WASIO SAHIHI KATIKA CYCLE YAKO

Niliwahi kusoma article ya Bill Gates, moja kati ya matajiri wakubwa duniani, alisema alipopata wazo la kuanzia biashara yake ya windo aliwashirikisha watu 1200, watu 900 walimwambia hicho kitu hakiwezekani, 200 waliunga mkono wazo la Bill Gates, watu 89 hawakuwa na mchango au wazo lolote, na watu 11 waliunga mkono wazo la Bill Gates.

Wakati nasoma article  hii, ilikuwa kama stori hivi kwangu, sikuchukulia kiundani sana kwa sababu  niliona kama ni stori za kawaida za watu ambao  tayari wamekwisha piga hatua kwenye maisha yao, niliona ni stori za kawaida kwa mtu ambae amefanikiwa, maana hata akisema uongo anaamini watu watakubali tu kwa sababu  yeye ametimiza malengo na ndoto zake.

Nimekuwa nikifanya kazi nyingi na mara nyingi kazi ikiwa imekwisha kuanza hasa ikiwa imeanza kuonyesha matokeo, watu hunipongeza na kunitia moyo, lakini karibuni nimetaka kuanzisha kitu pamoja na rafiki yangu, kwa sababu ya usomi na akili Fulani  ya kuamini katika kuanza, tulifanya utafiti kidogo  kwa watu wa eneo hilo, pamoja na watu wanaofanya biashara  kama hiyo

Asilimia  kubwa ya washindani katika ile biashara walisema hapana, hii biashara kwa sasa ni ngumu, biashara hii inahitaji uzoefu maana changamoto  zake zinahitaji mtu mzoefu sana na biashara. Nikajikumbusha baadhi ya michakato ya kuomba kazi kwenye mashirika binafsi (Private sectors) kwamba ukitaka kuomba kazi au tangazo la kazi likitoka lazima uwe na uzoefu Fulani....

Swali  langu likaja kusema, hivi huyu asie na uzoefu afanye nini sasa maana kila sehemu uzoefu  unahitajika, kazini  uzoefuzi, biashara  ni changamoto  inahitaji  mtu mzoefu, sasa tufanye nini.....

Ili kutoka hapa ni vyema kuwa na watu sahihi au ambao wanaweza  kukwambia fanya hili linawezekana, usipofanya umasikini itakuwa halali yako, katu hautaweza kuijua potential  yako, katu hutoweza kupiga hatua hata moja.

Watu wengi  wanakatisha tamaa sana, watu wengi wanacheka na wewe ila katika mioyo yao hawakutakiii mema hata kidogo, wengine wanaogopa kukwambia ukweli wa biashara  wanayofanya kwa sababu wanajua unaenda kuongeza options  kwa wateja wa bidhaa yako.

Wakatu mwingine wamekutazama wamegundua kuwa unayo potential  kubwa katika kazi, Ubuntu, pengine wanaogopa Elimu yako, pengine wanaogopa IQ yako,  maana unauwezo wa kwenda kufanya zaidi ya wao.

Wapo dream  killers Waepuke, usiwape Wazo lolote, usiwape nafasi katika maisha yako, usiwape chansi  kwenye maisha  yako, wanakupotezea muda, wanashikilia hatua zako, put them aside move forward, have right  people  kwenye njia yako.

Hakuna asie weza, pamoja na changamoto  zote hizi lakini, hakuna mtu aliye wahi kujaribu kwa moyo akashindwa kufanya jambo, akiwa na bidii, maarifa kidogo lazima aone hatua kwenye jambo lolote hata kama shetani atasimama mbele yako

Nimejifunza mambo mengi sana unaposhare jambo lako na watu hata wale wa karibu yako wanaweza kuwa mwiba kwako, achana na watu wasio  na msaada  kwako, share nao kwa mambo unahisi ndio yaliwakutanisha.

Chagua watu wa msingi ambao watakupa mawazo mazuri, watakupush, watakushauri kwa lengo la kujenga, watakuencourage kufanya hatua katika kila jambo lako

Play fair, Be positive 
2022 ni mwaka wa kupiga hatua 

Saturday, January 8, 2022

KATAA KUISHI MANENO YA VINYWA VYWA WATU, ISHI KUSUDI LA MUNGU.

Nimekuwa nikijifunza kwa muda mrefu kupitia watu mbalimbali waliofanikiwa na hata bado hawajafakiwa na walioshindwa kabisa. Lengo la kujifunza kwa watu wote hawa nikutamani kujua sababu ambazo zimewafanya waliofanikiwa  kufanikiwa na wale walioshindwa kushindwa.

Katika mfumo wa maisha yetu hasa Tanzania kwetu, tumekuwana maisha ambayo yameathiliwa sana na mitazamo  ya watu, jamii na hata familia zetu wenyewe, kila jambo ambalo linatokea kwenye maisha yetu nyuma yake kuna athari  ya watu, jamii, imani zetu, elimu na hata mitazamo  ya namna ambavyo mtu anaishi.


Friday, January 7, 2022

MAISHA NI MAHUSIANO BORA

Maisha ni fumbo amabalo ni ngumu sana kulifumbua inahitaji hekima, busara na mtazamo wenye ukomavu ndani  yake. Hakuna dunia ya pekee yako, hakuna mtu anae ishi katikati ya watu wengine akaishi kama yuko nyikani au jangwani.

Hii ni kwa sababu  tumeumbwa kwa kutegemeana, kushirikiana, kusaidiana na kuinuana, iwe moja kwa moja au kupitia mlango wa nyuma. Maisha ni picha isiyohitaji maelezo ya ziada, kwa aliye komaa kupitia picha tu anaweza kuelewa kinachomaanishwa na picha yenyewe.

Ni vyema kuishi maisha kwa utulivu, ushirika mwema, upendo, kuthamini wengine na kusameheana pale inapotokea mtofautiano. Kumbuka  katikati  ya watu kutofautiana, kupishana, kukwaruzana ni jambo la kawaida.

Kama kwenye nyumba za ibada watu wanaweza kutofautiana, kama Shetani pamoja na mazuri yote ambayo  alikuwa akipata huko mbinguni lakini bado, alitofautiana na Mungu  sembuse mtu kwa mtu, kutofautiana ni jambo  la kawaida kabisa.

Kutofautiana huletwa na kupishana kwa mitazamo na hoja, kukutetea maslahi ya kila mtu na Jamii yake, mambo  ya kazi, biashara na mambo mengine mengi kwenye  Jamii yetu, maofsini yawezekana ukatofautiana na sera ya mwajiri, mwajiri asiridhishwe na utendaji kazi wa mwajiriwa, hivyo lazima iwepo tofauti.

Lakini kutofautiana kwa hoja au mitazamo sio sababu ya kutengeneza uadui na chuki za kudumu kati yetu sisi kama binadamu, jitahidi  kufanya mambo ambayo yanalenga kuleta upendo kati yenu ili amani itawale, amani ikitawala lazima kuwe na matokeo yenye ufanisi katika kila jambo.

Unapoondoka mahali hata kama umeondoka kwa namna sio nzuri, ni vyema kusamehe na kusahau, kwa sababu  hata baada ya kazi kuna maisha. Ukifukuzwa kazi au mahali Fulani hata kama unahisi au unajua umekosewa ni vyema kuondoka mahali pale na kumshukuru Mungu kwa yote.

Pale unapofikri umeonewa, kunyanyaswa, kutokutendewa haki, udhika kwa muda kama binadamu lakini usishikilie jambo kwa miaka na miaka, huwezi jua kwa nini uliondoka mahali pale, Mungu huwa anajua kabla ya sisi kujua.

Tinachofikiri kwetu ni kibaya au kinatuumiza kumbuka kwa Mungu  inaweza kuwa ni sawa, na kile tunachohisi ni kizuri kwa upande wetu kwa Mungu inaweza kuwa sio sawa.

Mifano miwili halisi, Ayubu baada ya kupata majaribu makali, ilionekana kama Mungu amemwacha mpaka watu wake wa karibu wakaanza kusema amkufuru Mungu afe lakini alijua Mungu kwake ni nani.

Hawa aliona wema wa nyoka katika ile bustani, akaona huyu Mungu hafai kwa nini anatukatalia tenda hili, akaona kilichoko mbele yake ni chema kuliko yake kina faida kuliko maagizo ya awali kutoka kwa Mungu.

Matokeo ya watu hawa wawili yanaonyesha ni kwa kiasi gani maisha yetu ni fumbo na kesho yetu iko mikononi mwa Mungu, na Mungu ndie mwamzi wa kila kesho yetu. Usiishi kwa kufuata hisia na matakwa binafsi, tulia, jifunze, toa nafasi kabla ya kuchukua maamzi ambayo  unafikiri ni maamzi sahihi kwako.

Jenga mahusiano  bora na imara maana kesho yako huijui, ukifukuzwa kazi mahali, usitengeneze uadui pamoja na kufukuzwa kesho wanaweza kukurejesha maana yawezekana wanachukua maamzi kwa sababu ya maneno ya watu ambao wametengeneza fitina  na wanaona wewe ni bora kuliko wao.

Kuna wakati unafukuzwa kazi kwa sababu  watu wanataka kuprove yale mashitaka unayoshitakiwa nayo kama ni kweli, hivyo ukiondolewa jitahidi sana kuzuia hasira, kinywa kunena matusi, ugomvi na ukorofi, jitahidi kutulia na kuondoka.

Kama ulionewa haki yako haiwezi kupotea, pengo lake litaonekana kama walikuondoa kwa hila na fitina, yawezekana waliokuondoa walikuwa wanataka kuyadhibitisha yale mashitka kama ni ya kweli au uongo, 

Ukichoka mahali, usiondoke kama umefukuzwa, fuata utaratibu mzuri wa kuomba kuondoka mahali Fulani, kama walivyokupokea katika familia, kazini, kwenye nyumba za ibada, au mahali popote ni vyema ukiwa umepata mwanga wa kuweza kujitegemea, Mungu  amekuinua umepata kazi mpya, umepandishwa cheo ndani ya ofsi, umechoka kuwa sehemu ya familia, ofsi, biashara  nk, ondoka kwa amani, aga vyema, ili iwe kwa heri ya kuonana.

Kesho yangu siijui, kesho yako huijui ni vyema kulinda mahusiano  yako na watu, hao hata kesho watakutetea mahali, utakuwa na ujasiri wa kurudi mahali, maana uliondoka kwa amani, uliaga na kuondoka kwako, itakuwa kwa heri ya kuonana tena.
Hatuwezi kupendezana katika yote ila tunaweza kupunguza pengo la chuki, uadui na uhasama usiokuwa wa lazima.

Mwaka huu, utumiae kama mwaka wakujenga mahusiano bora kwa kadri  uwezavyo, hakika utakuwa mwaka bora wa kuzaa matunda. Zaidi jifunze kunyamaza, sio kila neno lazima uongee....

Moses_mgema Zephaniah 
0755632375
0719110760

Wednesday, January 5, 2022

TWEKA MPAKA KILINDINI

Luka 5:4

Ni maneno ya Bwana Yesu akimwambia Simoni pamoja na wenzake hii ilikuja baada ya Simoni na wenzake kufanya kazi ya kuvua samaki usiku kucha wasiambulie chochote kile.

Tukio hili lilitokea katika ziwa la Genesareti alipokuwa akisongwa na watu na kisha akaanza kufundisha, ndipo alipomwambia Simoni Petro habari ya kushusha nyavu katika ziwa like tena katika kina kirefu (kilindini).

Yawezekana umekuwa katika kufanya kazi na matokeo yamekuwa madogo ukilinganisha na kipato unachopata.

Hivyo kama wewe ni mmoja wapo somo hili litakufaa sana, vilevile kama mambo yako yanaenda vizuri linakuhusu pia kwa ajili ya kesho yako ambayo ni fumbo.

Ukitafakari habari ya Yesu na makutano pale kwenye ziwa la Genesareti utaona Bwana Yesu, alikuwa akihangaika sana katika kuwafundisha makutano, yale mazingira yalikuwa ni magumu sana kutokana na kwamba watu wengi walimsonga na yeye alitaka kuwafundisha zaidi katika utulivu, hivyo hakuona kama akiendelea katika hali ile ile atatimiza kusudi lake, ndipo akaamua atafute madhabahu ya kuwakutanisha wale watu pamoja, mahali atakapotulia ili awafundishe wale watu katika ustaarabu na utaratibu ambao Mungu ameukusudia..

Na alipogeuka akaona vyombo viwili vimeegeshwa pwani na wenye navyo wametoka, ndipo akikichagua cha mmojawapo na kukigeuza kuwa madhabahu yake ya muda.

Sasa Chombo kinawakilisha nini katika mazingira tuliyopo leo?. Chombo kinawakilisha kitu chochote cha kujipatia kipato, kumbuka chombo hicho Bwana alichokitumia kilikuwa ni cha akina Petro cha kuvulia samaki, kwasasa hivi chombo kinaweza kikawa, elimu ya mtu, ujuzi wa mtu, biashara ya mtu, fremu ya mtu, shamba la mtu, kiwanja cha mtu,n.k.

Lakini tunasoma katika habari hiyo, tunaona Bwana alipotazama hakuchagua vyombo vilivyokuwa kando kando vyenye wavuvi au samaki, kumbuka vilikuwepo tu vingi vizuri zaidi ya hivyo vilivyokuwa vinazungukazunguka maeneo yale, lakini yeye hakuchagua chochote kati ya hivyo bali alivichagua vile visivyokuwa na kitu ndani yake…(Na ndio maana somo hili linawahusu sana wale ambao shughuli zao haziendi sawa),

Sasa kilichotokea ni kwamba wakina Petro walifanya kazi ya kuchosha usiku kucha wakihangaika kutafuta samaki ukanda mzima wa ziwa la Genesareti kwa shida, na kujitoa kweli kweli lakini wasipate kitu, mpaka kulipokucha wakakata tamaa ya kuendelea kuvua tena, wakaona kilichobakia tu ni kukipumzisha chombo na kuzitengeneza nyavu zao tena, kisha kuzihifadhi mpaka wakati mwingine,

Lakini baadaye kidogo ndio tunamwona Bwana Yesu akisumbuka na wale makutano, ndipo wao wakamruhusu Bwana kutumia vile vyombo ili kutimiza kusudi lake la kuhubiri,. Na baada ya Bwana kumaliza kuhubiri, sasa wakati makutano yote wameshaondoka ndipo akawageukia wale wamiliki wa vile vyombo, na kuwaambia twekeni mpaka kilindini mkashushe nyavu zenu mkavue samaki.

Lakini wao walimwambia, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha pasipo mafanikio, na walipokubali tu kwenda kuvua walipata matokeo makubwa ya kushangaza, mpaka nyavu zao kuanza kukatika, mpaka kufikia hatua ya kuomba msaada kwa wingi wa Baraka hizo, maana zimekuwa nyingi mpaka kushindwa kuvuta zile nyavu kutokana na wingi wa samaki ikalazimisha kuomba msaada kutoka katika chombo cha pili, maana wingi wa samaki ulipelekea chombo chao kuanza kuzama ndani ya maji ya ziwa.

Yesu ni yeye Yule jana, leo na hata milele hajabadilika, leo pia anaweza kufanya kama alivyo fanya kwa Simon petro na wenzake.  Umejaribu kufanya mambo mengi kwa bidii na ufanisi mwingi lakini kwa bidii, lakini bado huoni matokeo yanayoendana na bidii yako

Leo hii hicho chombo chako kigeuze kuwa MADHABAHU YA KRISTO kwasababu anakitafuta hicho ili alifanye kusudi lake, kumbuka pale Yesu hakutafuta sinagogi la kuwakusanya wale makutano waliokuwa wanamsonga, hakutafuta hekalu, wala hakutafuta mahali patakatifu bali alitafuta MAHALI PA KUJIPATIA KIPATO KWA MTU, mahali ambapo mtu anapopategemea kujipatia mkate wake wa kila siku, na pia fahamu tu, siku zote Bwana anapaangalia mahali ambapo palipo patupu kama kwako wewe, Mahali ambapo pamefanyika kazi ya kuchosha miaka mingi, miezi mingi pasipo mafanikio yoyote, hapo ndipo anapopataka kwa ajili ya kazi yake, na akishamalizana napo hapo, ndipo atakwambia nenda katupe nyavu zako kilindini uvue samaki, kwa wingi wa atakachokupa Bwana utaita mpaka na marafiki na zako na maadui zako waje nao kushiriki Baraka zako Mungu alizokuandalia.

Leo Kazi yako wewe ni ya ufundi, una ujuzi wa kutosha kuhusu masuala ya ujenzi, na unaona mahali unapofanyia pengine ni kanisani kuna kasoro Fulani ya ujenzi, na shughuli zako za kijenzi haziendi sawa, umekuwa ukipata mapato kidogo kupitia hiyo,wakati mwingine unakosa kabisa kazi, huo ndio wakati wa kwenda kumruhusu Bwana atumie hicho chombo chako (ujuzi),

nenda mahali unapokusanyika (kanisa), kazi ya Mungu inapofanywa, angalia kasoro zinazohusiana na taaluma yako, na utumie ujuzi wako kurekebisha tatizo hilo bila kutazamia malipo yoyote, pengine umeona ukuta wa kanisa umebomoka au una ufa, uzibe, umeona mfumo wa maji haujakaa sawa na una ujuzi wa kufanya hivyo, urekebishe hata kama hauna chochote, umeona kanisa halina choo kinachostahili, na wewe una ujuzi wa namna ya kutengeneza vizuri, nenda kafanye hivyo, kajenge kwa ustadi wote, na maarifa yako yote, umeona kuna kasoro ya umeme na mfumo wa nyaya, na una ujuzi huo nenda karekebishe usisubiri hata mtu akamwambie, mruhusu Bwana atumie hicho chombo, na mwisho wa siku utaona matokeo na mtu asiyefanya hivyo wakati Fulani ukifika.

Au wewe ni polisi au mlinzi, anza kutoa mchango katika sekta hiyo ndani ya kazi ya Mungu..Usiseme Mungu kweli ataweza kutumia taaluma hii/ujuzi huu kwenye kazi yake??..kumbuka Yesu alitumia mtumbwi wa wavuvi kuwapelekea maelfu ya watu katika ufalme wa mbinguni…Na wewe vivyo hivyo mpe Bwana chombo chako.

Au wewe unafanya kazi ya upishi, na unaona kazi zako haziendi sawa, faida ndogo, na unaona kuna uhitaji mkubwa wa wapishi ndani ya nyumba ya Mungu, labda kwa ajili ya wazee wasiojiweza (wakristo), au wageni, au wenye mahitaji na mayatima (walio wakristo), ndani ya kanisa n.k usingoje uambiwe au uwe na kitu kwanza ndio ufanye, wewe mwenyewe anza kuchukua hatua ya kujitolea kwenda kuifanya, tena pasipo hata kuombwa.

Wewe ni mtengeneza bustani, na ndiyo kazi yako umekuwa ukifanya kwa ajili ya kujipatia kipato..Lakini mazingira ya kanisani ni machafu au hayavutii, panaonekana ni mahali pasipo tofauti na sehemu nyingine yoyote, Tumia chombo chako (ujuzi) kurekebisha mazingira ya Mungu, pakavutia kama vile unavyopendezesha bustani za watu wengine,..unaweza ukaona ni jambo dogo lakini linamaana kubwa na Bwana akisharidhika atakuambia shuka vilindini..utaona milango Mungu anayokufungulia katika hiyo hiyo kazi yako ilivyo ya ajabu.

Wewe ambaye ulikuwa unatafuta kazi,na bado hujapata, angali unao ujuzi Fulani, usiuache ulale utumie huo ujuzi katika kazi ya ufalme wa mbinguni, kwamfano labda wewe ni “ IT ” (mjuzi wa katika teknolijia ya Kompyuta), unaweza uka unda wavuti na tovuti kwaajili ya kutangaza ufalme wa mbinguni, unaweza ukabuni programu za kutangaza kazi ya Mungu kirahisi katika mitandao fanya kiuaminifu kabisa..Na Bwana akishamaliza kutenda kazi kwa kutumia chombo chako, atakuambia shuka vilindini…Utaona nafasi ambayo ulikuwa unaitafuta kwa kuhangaika kwa muda mrefu pasipo mafanikio kama wakina Petro walivyokuwa..unaipata ndani ya kipindi kifupi tena chenye faida mara 100 zaidi ya kile cha mwanzo ulichokuwa unakihangaikia..

Lakini hizo zote zinakuja kwanza kwa kumtolea Bwana chombo chako akitumie, kwa ajili ya kazi yake, lakini kuna wengine hawapendi kumpa Bwana nafasi lakini wanataka Baraka za Bwana, utakuta mtu analo eneo kubwa limekaa pasipo matumizi yoyote, hataki hata kukaribisha watu wafanyie kazi za mikutano ya injili hapo, na bado anataka Mungu ambariki, ndipo hapo zile roho za udanganyifu zilizoachiliwa katika siku za mwisho zinaanza kumdanganya na kumshawishi, akanunue mafuta ya upako, anunue chumvi na maji ya Baraka akanyunyuzie kwenye kiwanja chake na kwenye biashara yake, aanze kukemea roho za laana katika kiwanja chake, au biashara zake, ili mambo yake yaanze kwenda vizuri.

Utamkuta mwingine anazo fremu za vyumba na zimekosa mpangaji wa kufanyia biashara au tution,..na wakati huo huo kuna wakristo wenzake wamekuja kumwomba awape angalau fremu moja wawe wanafanyia bible study au maombi wakati wa jioni kwa muda huku wanatafuta eneo lingine..lakini kwasababu hajui uweza wa Mungu, anawazuilia na kuona bora tu ziendelee kuwa zimefungwa.na wakati huo huo anazunguka kutafuta kuombewa na kununua maji na mafuta ya upako huku na kule hata wakati mwingine nchi na nchi..Mtu wa namna hii hawezi kutazamia miujiza kama waliofanyiwa wakina Petro.

Bwana anasema nikaribieni, nami nitawakaribia… Wakati mwingine kutokuwa full committed  katika eneo lako la utumishi umekuwa chanzo cha kazi ya  Mungu kuwa katika hali dhaifu na wewe hutaki kuifanya chako..(Hagai 1:1-12). 

Anza leo kufanya kama Simoni Petro alivyofanya na wenzake na Mungu atakubariki. Mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.

Tutaendelea na somo hili baadae......

Moses Zephaniah Mgema

moses@gmail.com 

Tuesday, January 4, 2022

NGUVU YA KUAMUA NA KICHUKUA HATUA YA UTHUBUTU

Tangu kuzaliwa kwa mitume wa Mungu, kuanzia Yesu, Yohana pamoja na wanafunzi wa Yesu, tunajifunza ni jinsi gani ambavyo walithubutu na kuamua kuchukua hatua ya vitendo ambavyo vilileta matokeo makubwa katika maisha yao 

Nimekuwa nikijifunza kupitia maisha yangu binafsi, maisha ya wengine hasa walifanikiwa kwenye kutimiza malengo na makusudi ya kuishi kwao duniani hapa.

Maisha yetu yanahitaji uthubutu ili kuweza kuona mambo yanatokea waziwazi, pasipokufanya maamzi mazito na magumu ni ngumu sana pia kuona ukiishi kwenye malengo na matamanio ya ndoto zako.

Iko nguvu ya ajabu na maana sana imbayo humsukuma mtu toka ndani inayompa courage na kumwonyesha kuwa inaweza, laminitis mara inapofikia kwenye hatua yakufanya maamzi mazingira huonyesha impossibility kubwa na kutengeneza hofu na wasiwasi wa kupoteza kuliko kupata na kufanikiwa.

Kufeli kwangu sio ukosefu  wa mtaji bali namna gani naweza kuchukua hatua ya uthubutu katika kile nakiona katika ule uhalisia wa ndani.

Ni kweli maisha ni magumu sana laminitis maisha hayo hayawezi kuwa rahisi kwa kufanya vitu rahisi bali unapaswa kufanya maamzi magumu ya uthubutu ili kujenga misuri na stamina ya kukabili hali yoyote ile ya kimazingira.

Wakati Isaya anatabili kuzaliwa kwa Yohana ambae alienda nyikani, hakuna mtu a angeweza kumwelewa kabisa, ni namna gani mtu aweza kuwa na akili timamu kwenda kuanzisha jambo nyikani. Sio rahisi hata kimono.

Lakini Yohana aliona fursa nyikani akathubutu haikuwa rahisi lakini alifanikiwa kwa sababu ile nguvu ya ndani aliweza kuitii na kufanya hatua ya uthubutu, kwa sababu alijua nini anafanya aliyabadili yale mazingira yakawa uhitaji wa watu, nyika ikawa mahali pakukimbilia.

Yesu alikabiliana na mazingira magumu sana yakutimiza kusudi la uwepo wake duniani, lakini pamoja na ugumu alioupitia, ila ile nguvu ndani yake aliiaply vyema katika mate do, akathubutu  na kuonyesha matokeo makubwa duniani  mpaka akatimiza lengo lake  duniani.

Nguvu ya uthubutu huleta matokeo makubwa, uoga, na kuzingirwa na mazingira ya hofu ya kupoteza imetusababishia watu wengi kuishi maisha yasiofaa sana, kumbe ni kwamba maisha yetu hayajengwe kwenye missing bora na imara yakuchukua hatua ya uthubutu.

Nilichojifunza ni kwamba vitu bora having kwa wepesi bali kwa nguvu na jitihada za maana sana, hakuna njia rahisi inaweza kukupa mafanikio, bali jitihada na marina mengi huleta matokeo chanya na halls.

Dunia ya Leo inatekwa na watu Wallace waliokubali kuwa watubwa Leo, ili kesho ya iwe bora, uthubutu na uchukuaji wa hatua ni silva kubwa bora kwa ajili ya matokeo chanya katika maisha yetu.

Hakuna utajiri katika maisha ya relaxation, hakuna mafanikio kwenye vitu vipyesi, achievers are hustlers, hawakati tamaa hawaoni kushindwa as long wako na afya wanaamini mafanikio ni haki ya.

Hivyo tukiwa kwenye mwanzo wa mwaka ni vyema kuhakikisha malengo na mipango uliyoweka inakwenda kwenye mpangilio sawa, shindwa jambo kwa nje ya sababu zilizo nje ya uwezo wako make it.......

Usikubali uwe mtumwa wa wengine wakati you can be you and see a very  big result kwenye maisha yako

Ipe nafasi nguvu ya ndani na ile mipango kichwani inakuwa na matokeo chanya katika maisha halisi ya nje.
Don't be a slave in 2022
By Moses Mgema
Mgemamoses@gmail.com