Friday, February 5, 2021

AINA YA MAAMZI NA UTULIVU HUPIMA KIWANGO CHA HEKIMA NA UKOMAVU WAKO.

Ukomavu wa mtu haupimwi kwa wingi wa miaka, wingi wa nywele nyeupe kichwani, wingi wa vizazi kutoka kwenye viuno ama tumbo lako hapana.
Ukomavu wa mtu mara nyingi unapimwa kutokana na uwezo wa kukabiliana na nyakati ngumu, nyakati tata na milima mîgumu ambayo unakutana nayo na vile unakabiliana nayo katika hali ya utatuzi na kuweka sawa bila kulazimishwa na mazingira presha na mazingira ya uhitaji wa jamii inayokuzunguka.
Kuna nyakati tata na ngumu sana kwenye maisha yetu ambazo huwa tunapitia, wakati mwingine zinaumiza, zinatuchafua, zinakatisha tamaa, zinatukumbusha nyakati ngumu ambazo hazijawahi kuwa rafiki bali maumivu makali ambayo hata huwa hatupendi kuzikumbuka kabisa.
Wakati mwingine unapewa nafasi yakuwa mtoa maamzi ambayo haki inapaswa kutendeka bila kujali asie na haki ataumia kwa kiwango gani. Ukomavu wako pekee ndiyo inahitajika, hekima na busara yako ndio inahitajika sio kitu kingine.
Nayakumbuka mazingira ya Mfalme Sulemani ambae alipaswa kufanya maamzi ya haki dhidi ya wamama wawili ambao walikuwa wanagombea mtoto mmoja. Ni hekima, busara na ukomavu wa hali ya juu ulihitajika kufanya maamzi, maamzi sahihi yalihitajï kiwango kikubwa cha hekima ili kutambua nani alistahili nini kati ya wamama hao.
Pamoja na Daudi kuwa shujaa wa waesrael kwa kumpiga Goriath nakuahidiwa zawadi kemukemu na mfalme saul lakini mwisho wa siku Saul aligeuka kuwa adui mkubwa wa Daudi, hekima pekee toka kwa Daudi ndiyo iliyomfanya kuishi katika nchi yake kwa amani bila kupata madhara toka kwa sauli.
Nimefuatilia habari ya Elizabeth Michael na Mama Mzazi wa Stivie Kanumba ambae ameshindwa kumsamehe Elizabeth kutokana na tukio la mwaka 2012 nh kweli ni jambo gumu kusahau lakini bado haiondoi ukweli kwamba imekwishakutokea na haina budi kusamehe na kusahau na maisha kuendelea mbele bila shida
Pamoja na kusongwa songwa kwa maneno ya yule mama bado Elizabeth amekuwa ni mtulivu, mpole na mwenye heshim, hekima na busara akijitahidi kulinda hadhi na heshima ya mama kwa umri lakini pia utù. Nimemsikiliza akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari hakika ni mtu mkomavu pekee ndiyo anaweza kusimama na kujibu kwa hekima na utulivu wa kiwango cha juu.
Pamoja na kukiri kuwa maneno ya yule mama yamekuwa msalaba wake na yuko tayari kwenda nayo kalvari bado alimeendelea kuwa mkimya, akitambua kuwa yule ni mama yake kwa umri na akasema muungwana akivuliwa nguo huchutuma.
Sio rahisi kwa binti staa, binti mdogo kuwa na mtazamo chanya kwa kiwango kikubwa kiasi kile, alikuwa na nafasi kubwa yakuyatumia mazingira haya kama njia ya kujiongezea followers, kutengeneza attensheni kwa jamii kwa maslahi ya biashara zake za uigizaji lakini amekuwa tofauti.
Ukomavu ni vile ambavyo unauwezo wa kuipa hekima ikuongoze katika kufanya maamzi, busara ni ishara ya ukomavu wa mtu.
Halisia tumeumbwa tukapewa hisia, maumivu na kukerwa lakini kwa mtu mwenye ukomavu wa fikra, akili ni katika uwezo wa kukabiliana na mazingira ambayo ni magumu na yenye changamoto zilizo changanyika na maumivu makali yaliyoujeruhi moyo na nafsi.
Mungu ameumbia utashi, hekima na busara ni vyema kujifunza kuishi kwenye aina hizi tatu za maarifa maana ndiyo njia ya kwanza bora za kuishi kwenye mazingira yeyote na kuyamudu.
Maamzi ya mtu aliyekomaa huwa na matokeo makubwa sana ushindi katika chanya. Tumwombe Mungu kama ambavyo Sulemani alimwomba ampe hekima ambayo ilikuwa msingi wa mafanikio yake katika utawala wake.
Ukomavu ni kiwango cha juu cha hekima, mtu mwenye hekima ana maarifa sahihi, na ufahamu wake ameujenga katika mtazamo chanya, haendeshwi na gadhabu, uchungu, chuki na kisasi ndani yake bali hekima humfanya mtu kuyaweka pembeni matakwa yake binafsi kwa ajili ya wengi na haki kutendeka kama ambavyo sulemani alifanya bila kujali alitumia hekima bora kabisa.
Learn to be matured
Mgema Moses
0715366003/0755632375


No comments:

Post a Comment