Tuesday, February 2, 2021

IMEKUWA TABIA YA WATU WENGI

Ni rahisi zaidi kumsema mtu aliyeshindwa kwenye jambo fulani, alifeli mtihani, biashara ilianguka, alipoteza kazi au amekuwa akifanya chini ya kiwango kwenye majukumu yake.
Ni rahisi zaidi kumtukana mcheza mpira anapokuwa uwanjani nakumsemea maneno mabaya huyu hajui, anakosaje goli jepesi vile, anapitwaje kirahisi, huyu kipa shati anafungwaje kizembe vile huo ni mdomo wa mtu mmoja akiwa amekaa jukwaani na wakati mwingine anaporomosha maneno yasio na staha kwa mchezaji, ni rahisi sana.
Utakuta mtu/watu wako busy huyu mwimbaji hajitambui kabisa ona mwenzake ameubadilisha muziki kuwa biashara anapiga pesa kila kukicha yeye yupo yupo tu hana mpango.
Watu wanasahau hata kukumbuka kuwa mpaka unamfahamu kuwa huyu ni mchezaji tena akiwa kwenye timu kubwa ni juhudi zake ndiyo maana umepata wasaha wa kutoa pesa yako kwenda kutazama mpira, ndiyo maana kutwa headphone masikioni na kukera watu kwa muziki mkubwa katika subwoofer hapo nyumbani kwako.
Kidole karibu na kidole gumba ni rahisi zaidi kumnyoshea yule mtoto aliyeanguka mtihani huku ukiwa umesahau kuwa vidole vitatu vinakuelekea wewe na kukumbusha kuwa mbona na wewe hukuwa ukifaulu masomo ?, mbona wewe hata kazi zako huzifanyi vizuri ndiyo maana kuĺa kuku hapa nyumbani ni mpaka bibi atuma kutoka kwetu singida, hata hawa wakizungu huwezi kununua walau kwa mwezi mara moja ?
Ni rahisi zaidi kumkosoa kiongozi kwamba hafanyi vizuri wakati wewe hata kuwa balozi wa nyumba kumi ulishindwa,
Yapo mengi yanatokea kwenye mzunguko wa maisha yetu, hisia na mawazo ya watu wengi yamejengwa kwenye hasi zaidi kuliko chanya. Mtu akianguka kwenye jambo fulani ni mzembe mjinga, hajielewi, mvivu, hajisomei, mbinafsi nk.
Ndiyo maana leo utakuta vijana wako kwenye mahusiano mmoja akikosea hata kidogo suluhisho tuvunje mahusiano, tuvunje uchumba kama ndio bado tuko kwenye uchumba mambo yenyewe ndïo haya mimi basi....sababu yenyewe ya kitoto wee, nani kakwambia utaolewa na malaika ambae ukiwa nae hatakosea, umewahi kujiuliza kwa nïni wazazi waliishi au wanaishi mpaka sasa na unawasifia sana kuwa ni wazazi bora na wamejenga familia imara.
Asilimia kubwa ya mambo hata kama yamekuja au kutokea kwa namna ya mtu kukosa kutimiza wajibu wake sawasawa ni vyema kujenga hisia na mtazamo chanya kwenye ufahamu wako kabla kinywa hakijasema, sio kila aliyeshindwa kufunga goli, kuzuia goli amependa iwe ivo, sio kila mtu aliyefeli mtihani, biashara, nk ni kwa sababu ya uzembe au kutokutimiza wajibu wake hapana.
Nimejifunza sana kwa baadhi ya watu ambao walifanya isivyosawa katika mtazamo wa watu wengi wakasemwa vibaya, ooh wazembe, wavivu hawajielewi nk walipotatuliwa vyanzo vya kufanya vibaya wamekuwa watu bora sana.
Vilevile kuna baadhi ya watu wanafanya vitu kwa viwango vyao waliojiwekea mfano kwenye kiwanda cha muziki na mpira, biashara na elimu, kuna baadhi wanaimba kama burudani, kipato anachoingiza amelizika nacho na ameamua kuseti kuishi kwa kiwango hicho, sïo kila mwanamziki, mcheza mpïra anataka kuwa Dïamodo, Mbwana Samatta, hashmu Thabiti mwingine ndoto yake iĺikuwa kufikia levo aliyepo ndio maana baada yakufika hapo ametulia na kuĺinda kiwango hicho na amedumu hapo.
Kuna watu wanatamani kufikia levo ya umilionea, ubiĺionea lakini kuna mwingine ameridhika na uwezo wa kusomesha watoto, kumïliki nyumba, kupata gari yake au kutokumiliki hata gari lakini ndio uchaguzi wake aliochagua.
Kuna mifano mingi hata shuleni kuna wanafunzi huwezi kuwakuta wamekuwa wa kwanza hata kumi bora lakini yupo kwenye viwango vya ufaulu, kama wastani ni 50 basi piga ua galagaza yupo, watafeli sana au kufaulu sana lakini yeye yupo kwenye wastani wakumvusha daraja jingine ndiyo viwango alivyoamua kuishi navyo.
Mwisho sio kila mtu anataka kuwa kama wewe unavyotaka, sio kila mtu ambae hafanyi au hakufanya vizuri imesababishwa na uzembe au kupenda hapana kuna mengine hutokea kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa kujizuia.
Asilimia kubwa ya watu hutamani kuwa bora katika kila jambo lakini yapo mazingira yanalazimisha kuwa hapo alipo au kufeli kwake.
Badala yakuja na majumuïsho ya majibu yatokanayo na matokeo yaonekanayo kwa macho ni vyema pia kuwa na muda wakumtazama mtu huyo kwa jicho chanya, hii itarahisisha sana kukupa relief ya kujua chanzo cha tatizo hata unapokuja kutoa majibu yako yawe na uhakika kuwa ni kweli..
Ni rahisi zaidi kujidanganya kwa kusoma kichwa cha habari juu ya kitabu nakujipa majibu ya kusudi la mwamdishi juu ya kile kimefunikwa ndani ya kava la kitabu....
Ukiwa mkosoaji jaribu kuwa mtafiti zaidi utakuwa bora na mwelevu
Smartness.
Mgema Moses
0715366003/0755632375

1 comment:

  1. Bado tunagombana kitu kidogo tu me na wewe nadhan ukielewa kuna mahali unaenda but naona bado hujawa serious na unachokifanya

    ReplyDelete