Wednesday, February 3, 2021

NGUVU YA MSAMAHA

Msamaha ni dawa, msamaha ni uzima jifunze kusamehe pale unapokosewa na aliyekukosea anapogundua kuwa amekosea na kuomba msamaha, wakati mwingine hata kama mtu hajakuomba msamaha samehe, msamaha ni kwa ajili yako sio kwa ajili ya alïyekukosea.

Kutokusamehe ni kubeba mzigo ambao hauna faida, na katika dunia tunayoishi leo huwezi kuishi bila kuudhiwa, kukosewa na kutendewa mambo ambayo ni kinyume na matarajio yako kwa sababu sisi ni binadamu na makosa yalianzia hapo zamani za edeni kwa Eva na Adamu....ni watu ambao walithubutu kumkosea Mungu huku wakijua uwezo na ukuu wake ije iwe wewe.....pamoja na makosa ya wengine Mungu aliamua kusamehe.

Unapokosewa fahamu na wewe pia huwa unakosea wengine na wanakusamehe, hivyo ukiwa katika ulimwengu huu, kukosea na kukosewa ni wajibu wa mwanadam, halafu kusamehe na kusamehewa ni tendo la lazima sio la hiyari,.... Kusamehe ni wajibu......ïli mradi unaishi duniani..

Msamaha ni suluhisho la uponyaji wa akili, afya ya mwili, msamaha ni ufunguo wa mahusiano mapya ambayo yalitiwa doa na kosa, msamaha ni uponyaji wa hisia zenye maumivu makali ndani yake, msamaha hurejesha furaha nakuondoa huzuni na hasira yenye uchungu ndani yake.

Yapo makosa ambayo sio rahisi hata ukiambiwa samehe ni ngumu lakini, Mungu anatutaka kusamehe 7x70 bila kujali ukubwa wa tatizo ila unachopaswa kufanya ni kusamehe tu.

Kuna namna inatokea kwenye maisha ni ngumu sana kusahau ila ndo unapaswa kusamehe bila kujali ukubwa wa kosa mfano, mume amekusaliti, umepigwa, mtu ameua ndugu yako, umeibiwa au kufanyiwa kitendo chochote ambacho kimeacha kovu moyoni na kwenye maïsha yako kwa ujumla, ni kweĺi tunarejea tu kwenye msingi wetu, Je usiposamehe ndio itarudi au kufuta kumbukumbu ya kilichotokea hapana kinabaki vilevile.

Umewahi kujiuliza gharama ambazo Mungu aliingia ili kutoa msamaha au kwa wakristo unaposoma neno lolote kwenye Biblia linalohusu ukombozi na msamaha wa Mungu kwetu huwa unachukuliaje, unaposoma Yohana 3:16 huo mstari huwa na maana ipi kwenye ufahamu wako.

MSAMAHA NI DARAJA JIPYA LA WASHINDI.
Kuna msemo mkubwa sana umekuwa ukisemwa na watu ingawa sijui kama watu wote wanaofanya kotesheni ya msemo huo huwa wana maanisha au huwa wanasema tu kwa sababu upo....
1.Weak people revenge. 
2.Strong people forgive. 
3.Intelligent people ignore.
Uliandikwa na Albert Einstein...
Maneno hayo ni mazito sana ukitafakari vyema, so maneno mepesi kama ambavyo mtu anaweza kulala nakuamka nakutamka tu kawaida.....

Ukiniuliza mimï leo mambo yapi ni msingi bora wa maisha yangu duniani nje ya wokovu na Imani yangu kwa Yesu kristo ambae ndiye alitufundisha kwa vitendo maana ya haya mambo matatu
1. Upendo
2.Msamaha
3. Utu 
Washindi wote husamehe bali failures hubaki na kinyongo, mzigo moyoni kwa kifupi ni watu dhaifu sana, watu wa kundi la kwanza.

Binafsi haya ni kati ya maeneo ambayo huwa najipima nayo kuona kiwango cha ukomavu wangu juu ya kufanya maamzi yenye kukulazimu hata kama yanakuumiza ila lazima uyafanye ili kuweza kuwa balozi mwema wa Mungu hapa duniani.

Najua sio jambo jepesi kufanya kwa vitendo, ila ndio tunapaswa kusamehe, kupenda na kuĺïnda utu kwa faida yetu wenyewe.
FAIDA YA KUSAMEHE 
1. Hurejesha mahusiano na kujenga kuheshimiana.

2. Hulinda amani na kuondoa chuki, maana kama unaweza kusamehe maana yake una upendo wa agape, upendo wa Kimungu.

3. Humfungua mtu aliyekosewa na aliyekosewa hivyo kuondoa uchungu, hisia zenye maumivu ambazo zinaweza kupelekea kuibuka kwa ugonjwa.

4. Huonyesha ukomavu wa akili, nafsi na roho na kumweleza mtu mhusika kama mtu anaeweza kubeba vitu na kuvimudu.

5. Hupima kiwango cha ukomavu wa kiroho maana utakuwa ukitenda sawasawa na agizo la Mungu 
Zipo faida nyingi kwa mtu ambae hupenda kusamehe na kuachilia. Naandika ujumbe huu nikiwa najua kuwa kuna mazingira ya kibinadamu ni jambo gumu kuĺiko ambavyo mtu anaweza kusema au kuandika wakati hali ya kukosewa au kutendewa jambo baya kwa kiwango cha kutisha.

Msamaha ni agizo msamaha ni kutenda, msamaha inaonyesha pia kiwango cha ustarabu, utii, utu, upendo, ukomavu na utofauti wako na watu wa kundi la kwanza la watu....

Ni ngumu ila tenda kwa manufaa yako binafsi
Mgema Moses
0755632375/0719110760


1 comment: