Sunday, April 14, 2019

MAARIFA KWENYE KARNE YA 21 NI MSINGI WA MAFANIKIO YAKO

Nimekuwa na muda mzuri sana wa kujifunza kila siku, na hayo yamekuwa ni maisha yangu sasa, na kupitia aina hii ya maisha nimejikuta binafsi nikipata nguvu na imani kwamba kwa kila jambo lina sababu ya kuwa mahali popote lilipo.
Kujifunza kama ambavyo waandishi wamekuwa wakiandika nami naungana nao kwa kusema: Kujifunza ni mchakato endelevu kwa yeyote ambae anaendelea kuishi.
Na tunajifunza kupitia mazingira yanayotuzunguka na Yale mapya tunayokutana nayo kila muda tunaopata tukitoka nje ya maeneo yetu tuliyoyazoea.

Kupitia kujifunza huku, tunawezesha akili zetu kushiba na kuwa na afya ya maarifa ambayo kwa namna moja ama nyingine maarifa hayo yakitumika vyema ndiyo yanayoweza kubadilisha mfumo mzima wa maisha ya mtu kutoka vile alivyo, namna anavyotazama, fikiria, kiwango cha kuamini kuwa alipo yawezekana si mahali pake lakini pia kupitia maarifa anaweza gundua kuwa ndani yake kuna uwezo wa ajabu kiasi kwamba akiamua kuutumia vyema unaweza kumpeleka mbali zaidi maishani.

Niliwahi kusikia msemo maarufu nchini Tanzania kuwa: " UKITAKA KUMFICHA JAMBO MTANZANIA BASI WEKA KWENYE MAANDISHI UTAKUWA UMEMALIZA KILA KITU" maneno haya sio mazuri sana kwa sababu yanajaribu kuelezea udhaifu wa watanzania wengi kuwa hatupendi kujifunza kwa Uhuru labda kwa shuruti kama inavyofanyika kwenye mfumo rasmi wa Taaluma ambao ni haki ya kila mtanzania kupata elimu hiyo.

Lakini kwa mtu ambae amekubali kuyafanya maisha yake kuwa ni yakujifunza kila muda, mtu wa namna hii huwa anakuwa na nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya mambo yake kwa sababu

1. Maarifa hujenga uwezo wa kufanya mambo kwa ufasaha hasa kwenye eneo husika.
2. Maarifa hujenga imani na kujiamini.
3. Maarifa huvumbua fursa zilizojificha.
4. Hujenga uwezo wa kufikiri zaidi.
5 unaufanya ufahamu wa MTU kuwa updated muda wote na active
6. Kujua mahitaji ya wakati uliopo na kuweza kuitabili kesho.
Hizi ni baadhi ya faida ambazo mtu anaweza kuzipata kama tu amedhamiria toka ndani kuwa maisha ya kujifunza yawe ni maisha yake.

Niliwahi kusoma kitabu kimoja hivi kilichoandikwa na Brian Trace kinaitwa "NO EXCUSES" niligundua mambo mengi sana ambayo yamechangia watu wengi kuishi maisha ambayo hayawastahili Kati ya mambo makuu niliyojifunza kupitia kitabu hicho ambacho pia kilibadili kabisa mtazamo wangu ni
1. Kuishi kweye sababu.
2. Kuamini mtu alipo ni kwa sababu ya mtu Fulani.
3. Kutokuwa na nidhamu binafsi nk.

Pamoja na kusoma kwa undani niligundua kuwa maisha ya mtu yapo ndani ya mtu mwenyewe bila kujali umekulia mazingira yapi as long as umeshakuwa mtu mzima na unaafya njema basi wewe ndiye utabaki kuwa mwamzi sahihi wa maisha yako au mwamzi wa maisha yangu.

Kufeli, kutokwenda shule, wazazi kutokuona umuhimu wa jambo Fulani yaani elimu nk, bado haiondoi uhalisia kwamba maisha ya mtu yako ndani ya maamzi yake mwenyewe.

Watu wengi tumekuwa wavivu sana kwa mambo mengi, kuwaza, kujitoa kuanzisha shughuli ndogodongo kama kuuza matunda, kuuza bidhaa zilizo na uwezo wa kuwa na mtaji mdogo badala yake tunawalalamika au kuwalalamikia wengine

Wengine wamepata nafasi ya kufanya kazi, kujiajiri kwa kazi zao lakini wamekosa nidhamu ya kazi yao, wanachelewa kwenda kazini, wanafanya kazi kana kwamba wamelazimishwa kufanya hivyo, hawana upendo na kile wanachokifanya mwisho wa siku ubora au ufanisi wa kazi umekuwa mdogo kitu kilichopelekea kupoteza ajira zao au hata biashara zao kufa.
Nidhamu mbovu juu ya vipato vyao kitu kinachopelekea mtu kuonekana ana kazi au biashara lakini hatua ya maendeleo iko pale pale kila mwaka unapopinduka ajabu sana.

Lakini kumbe chanzo cha haya yote ni ukosefu wa elimu na maarifa ya namna gani yakufanya ili kwa kila jambo ambalo mtu anafanya liweze kuwa endelevu na lenye kumfanya apige hatua ya maendeleo yake binafsi lakini pia familia.

Pamoja na kwamba ukisoma vitabu vingi sana hasa hizi inspirational books unaweza jikuta unaona ni kama umechelewa, au uone kumbe kufanikiwa ni rahisi, lakini kuna umuhimu wa kujifunza maana mazuri ni mengi kuliko mabaya kupitia elimu.

Tuwe ni watu wakujifunza, kupitia kujifunza utapata shuhuda za watu waliofanikiwa, utaongeza ujuzi na maarifa mapya juu ya kazi au biashara unayofanya na unaweza kuiboresha zaidi.

Utapata mbinu mpya za namna ya kufanya kazi zako lakini pia kama ni biashara unaweza gundua vitu vipya ambavyo kwenye mazingira yako havipo na wewe kuwa mwanzilishi wake.

Kwa hiyo kujifunza jambo nyeti na muhimu sana kwenye maisha yetu hasa kama unataka kufikia ndoto na malengo yako, tunafanikiwa kwa kuangailia wengine walifanya nini.
Elimu ina transform namna yakuwaza, kufikiri na namna ya kutenda.
Note.
Kusoma sana vitabu au kupata muda mwingi wa kujifunza na kuhudhuria semina za wajasirimali haimanishi kwamba ndiyo tiketi ya mafanikio hapana.
Kujifunza na kupata maarifa ni jambo moja lakini utekelezaji wa maarifa hayo ni jambo LA muhimu zaidi na hilo ndilo linaweza kuwa ndo msingi na ngao ya ushindi wa maarifa hayo.

Maarifa na ujuzi bila utekelezaji wake ni sawa na kukubaliana na msemo wa wahenga usemao, "PENYE MITI HAPANA WAJENZI"
JIFUNZE+ WEKA KWENYE UTEKELEZAJI = MAFANIKIO
Mungu ayape nguvu maono yako kwa nguvu unayoitumia kuhakikisha unafikia malengo yako.

Elimu ni mtaji wa kila jambo

Moses z. Mgema
0715366003/0755632376
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment