Tuesday, January 8, 2019

KWA KILA JAMBO ANZA, TEMBEA NA MALIZA NA MUNGU.

Pamoja na maarifa, ujuzi, elimu, shauku, uwezo mkubwa wa kufanya kazi, bidii ya kufanya kazi bila kuchoka.

Haitoshi kwenda pekee yako na kujitegemea mwenyewe au watu wanaokuzunguka.

Fedha na kila aina ya rasimali ulizonazo haziwezi kukubeba katika kila jambo.

Ufanyaje sasa ?
Kwa kila jambo tembea na Mungu, mshirikishe Mungu, mwache Mungu awe kiongozi kwa kila kazi yako.

Ukitembea na Mungu hakika huwezi kuona unaanguka kibiashara au katika kazi zako kwa sababu yeye atasimama na kupigana  na maadui wa kazi zako.

Ukiwa Mwaminifu kwa Mungu kwa kutoa fungu la kumi, hakika Mungu ataibariki kazi ya mikono yako.

Ukiwa mwaminifu kwa Mungu, Mungu atakutetea wakati wa ukame wako.

Kumbuka Biblia inasema yeye alikujua kabla ya misingi ya dunia kuumbwa, kwa hiyo hatima ya maisha yako iko mikononi mwake.

Kwa hiyo hata alipokuumba aliweka kusudi na maono yake ndani yako ili uyatimize kwa utukufu wake.

Kwa hiyo unapaswa kufahamu kuwa mafanikio yote, maarifa yote, ujuzi wote na utajiri ulio nao ni kwa sababu Mungu alipanga maono yake kupitia wewe, na amekupa uwezo wa kujua na kutambua uwezo wako na wewe kufanyia kazi, fahamu huyo ni Mungu.

Usikubali kutembea pekee yako mwaka huu tembea na Mungu hakika utaona matunda mazuri kwa sababu Mungu atakuwa na wewe.
Wakati mwingine biashara, kazi zetu hazisimami kisawasawa kwa sababu tujiona kuwa tunaweza bila Mungu.

Tumejitegemea sana sisi pasipokujua kuwa wakutegemewa pekee ni Mungu

Jiepushe na watu ambao wanaushauri mbaya kuhusu Mungu, acha kutegemea mwadamu, mfano kwenda kwa waganga, maana Biblia inasema kwamba amtegemeae mwanadam amelaaniwa kabisa.
Kwa hiyo kila mmoja lazima amtegemee Mungu kwa akili yake yote.
Pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni zote zinazotakiwa kwenye kanuni za kazi bado kanuni kubwa na yenye nguvu basi ni kumtegemea Mungu
Yeye ndiye anajua hatima ya maisha yako.
Msingi wa mambo yote mema ni Mungu tu.

Barikiwa kwa kusoma ujumbe huu mwanzoni kabisa kwa mwaka huu
Mwaka huu tembea Na Mungu
Acha kutembea pekee yako.

Moses zephania Mgema
0755632375.
mgemamoses@gmail.com
Dar es salaam Tanzania

*-2019 Is the year of achievements-*

No comments:

Post a Comment