Mungu amenissaidia, nmeamka salama kabisa. Nitoe pole kwa ndugu jamaa na marafiki ambao wanapitia changamoto mbalimbali, kwamba Mungu yupo atarejesha neema ya uzima au kuiondoa changamoto yoyote unayopitia sasa.
Mungu ni yule yule aliyemtendea Ayubu, lazaro na wengine, hata sisi pia lakini jambo jema ni kuendelea kumtumaini Mungu siku zote.
Leo ningependa tujifunze tena kitu muhimu na cha msingi sana hasa tunapoendelea na mchaka mchaka wa maisha ya kila siku.
Leo tutajifunza kitu kinaitwa
*-THAMINI YA WAZO LAKO-*
Mungu wetu ni Mungu wa maarifa na maajabu mengi ambayo kiufupi tu hakuna mtu anaweza kuyaelewa zaidi ya kukiri tu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha yetu.
Mungu alituumba akatupa uwezo na akili yakuweza kutumia ili kuzitambua fursa na kuzitumia vyema kwa manufaa binafsi, familia, jamii lakini kwa ajili ya utukufu wake yeye Mungu.
Wazo (Idea) ni moja ya silaha kubwa ambayo Mungu alimpatia mtu, na akampa uwezo wa kulinyumbua wazo hilo na kuwa faida kwake. Hapa ndipo tunaona watu wanagundua fursa mbalimbali zinazoendesha maisha yao.
Wazo (idea) ilimwijia Biligate, Wallace Wattle, mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg, wamiliki wa Twitter, whatsup, na mitaondao mingine ya kijamii hatimae leo tunatumia vitu hiv, Microsoft, Fb nk. ni kati ya viungo vya mawasiliano ambavyo vimerahisisha sana njia za mawasiliano ukilinganisha na zama za kale.
Wazo la wagunduzi wa baiskel, pikipiki, gari, treni, meli na ndege, liligeuka kuwa fursa ambayo imeleta mageuzi makubwa sana kwenye nyanja za usafiri na usafirishaji.
Wazo ni kitu cha Thamani sana kama kikiheshimiwa na kupewa heshima yake, wazo hugeuza umasiki kuwa utajiri, wazo hugeuza woga kuwa ujasili, hapo ndipo tunapata watu waliojitoa muhanga bila kujal hadhi zao na leo ni watu wa mfano na matajiri duniani kote.
Kila jambo huanza kama wazo, liwe jambo baya au zuri lakini asili yake ni wazo moyoni na kwenye ufahamu wa mtu kabla halijaja katika ubayana wake.
Mpira wa miguu ulianzia nchini England kama wazo la wafanyakazi kujiburudisha baada ya kazi, lakini leo ni kati ya sekta inayozalisha ajira na utajiri mwingi kwa vijana na jamii kwa ujumla hapa (IDEA WAS IMPLEMENTED)
Mifano ni mingi mno ambayo tunaweza kuitumia, *-WALLACE WATTLE-* moja ya matajiri waliotokea kwenye familia masikini huko nchini marekani mwishoni mwa miaka ya 1880s hadi alipofariki dunia miaka ya 1900s aliwahi kusema, kila mtu ana wazo jema lakini namna ya kulitekeleza hilo wazo.
Watu duniani wana Mawazo mazuri sana na baadhi ya Mawazo ya watu masiki leo, yaliwahi kuwa ngazi ya watu matajiri duniani.
Kupitia vijiwe vya kawaha na vijiwe vya stori mawazo mengi huzalishwa na ni mawazo kuntu sana, shida iliyopo wale wanao zalisha mawazo hayo wengi wao hufanya ivo ili kunogesha vijiwe na kufanya siku iende wakalale.
Wachache sana wanaokuwa ndani ya vijiwe hivyo hung'amua mawazo hayo na kuyakusanya na kuyafanyia kazi na leo hawa matajiri tulio nao duniani na hapa Tanzania.
Hujawahi kupita mitaa ya jiji la Dar es salaam ukawasikia wazee wakisema huyu Bakhresa tulikuwaga tuko hapa anatuuzia kashata na kawa na wana feel proud kabisa kusema ivo, yawezekana ndani ya stori hizo kuna Mawazo bora kabisa Bakhresa aliyapata na kuyaboresha na leo yamemfanya kuwa moja ya matajiri Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Nimekutana na mawakala na watu wengi wanaosema tulimpokea Shigongo alipotoka kwao Mwanza, na baadhi yao wanamwelezea kama mtu aliyekuwa duni sana lakini mwenye focus na malengo kwenye Idea yake.
Wengine wanasema waliuza naye magazeti,hata alipokuwa anaanzisha gazeti la uwazi akiwa hana kitu wengi wao walikuwa wanamtazama wanasema, wakati mwingine aliwaomba pesa ili kuzalishia gazeti la siku inayofuata na mengine mengi, lakini leo Ndugu Shigongo ameajili zaidi ya watu mia kuanzia kwenye hotel zake, Global publishers, Global online Tv na vitega uchumi vyake vingine kama, Dar live mbagala ukumbi maarufu kabisa wa burudani.
Wazo ni kito cha Thamani sana, Je ni namna gani unaitumia, hakuna masikini duniani maana kila mtu ana wazo, wakati mwingine mawazo yetu ni bora kuliko waliofanikiwa, lakini hayaonekani bora kwa sababu hatujayaweka katika utekelezaji kwa kumaanisha toka ndani.
Wazo bila kuamua kulitekeleza ni sawa na midori ya wauza nguo sokoni kariakoo.
Amua leo bila kujali mazingira ya kiuchumi, kimaisha, nk. Amua kutoka moyoni.
Kufeli na kufaulu huwa ni maamzi ya mtu binafsi, ukiamua kufeli ni rahisi, ila ukiamua kufaulu au kufanikiwa ni maamzi magumu ya kutamani kutoka hapo ulipo kwenda eneo lingine.
Wazo ni jema pale tu unapolifanyia kazi kwa uaminifu, na kumaanisha, maisha yamekuwa na changamoto nyingi sana lakini hatuwez kuacha kupambana.
Kila mtu huwa na wazo, hivyo hakikisha unapopata wazo hilo lifanyie kazi immediately, bila kuchelewa, unapochelewa wengine wataliona na kulifanyia kazi.
Epuka kushirikisha ideas zako kama unaona kwamba bado huna uwezo wa kutekeleza kwa wakati huo, maana ukishare tu na watu, watu wenye nafasi zao watalitumia na wewe kubaki kwenye kushangaa.
Tumia wazo lako vyema, kuna wakati kama utakuwa na mawazo mazuri na huyatendei kazi basi kuna hatariya wewe kuumia kila siku kwa kuona watu wengine wakiyatumia mawazo yako
Heri ya mwaka mpya.
Moses zephania Mgema
0755632375
mgemamoses@gmail.com
No comments:
Post a Comment