Wednesday, January 2, 2019

ASANTE 2018, KARIBU SANA 2019

Mwaka 2018 umepita, tuna sababu ya kumshukuru Mungu sana kwa mengi mazuri aliyotutendea, mengi magumu aliyotuvusha, haikuwa rahisi hata kidogo maana ndugu jamaa, marafiki, majirani wameshindwa kuambatana nasi kwa kuunza mwaka huu.

Wengi wamefariki na wengine wameingia wakiwa wagonjwa na wengine wanapitia changamoto mbalimbali, lakini yote juu ya yote ni vyema kumshukuru Mungu tu.

Ni kwa neema wala sio kwa welevu, ujanja, ubora na utakatifu mwingi uliotufanya kuwa hai, is by Grace tu ndiyo maana tuko ndani ya mwaka huu tena, hakika ni kwa neema tu.

2019 tumeuanza kwa amani na furaha kubwa, wengi tukiwa na matumaini makubwa kwa kuset, mipango, malengo, shauku na hamasa ya kwamba mwaka huu basi ni mwaka ambao ni mwaka wa taofauti kabisa.

Kiuhalisia imekaaje, kiuhalisia kabisa kugeuza mwaka ni kama kulala na kuamka siku mpya, au kutoka mwezi mmoja kwenda mwezi mwingine in short ni mwendelezo wa maisha yaleyale tu.

Kwa kweli ndugu yangu tufanye kazi zaidi kuliko kuongea, mipango bila utekelezaji wa majukumu au wa mipango hiyo, kikawaida imekuwa ni mazoea ya kila unapoanza mwaka watu kupanga mipango na malengo, lakini kadri siku zikiwa zinasonga basi watu wanafunika diary zao na kusahau zile hamasa za mwanzo wa mwaka kabisa.

Kuanza mwaka sio kigezo cha wewe kubadilika kitabia na kimtazamo bali, maamzi ya dhati ya kuacha tabia za mazoea ndiyo kitu kinaweza kukufanya kufikia malengo ya kile ulichokifanya.

Pasipo Kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kuongea bila kutekeleza unachozungumza tutakuwa tunaanza na kumaliza miaka na miaka tukiwa kwenye tabia zilezile.

Lazima mabadiliko yaanzie kwenye fikra na maamzi ya dhati toka moyoni hapo ndipo unaweza kuona kweli mwaka umebadilika na uko tofauti na mwaka uliopita.

Katika kila jambo unalofanya mshirikishe Mungu, maana Mungu ndiyo  mwamzi na maratibu wa kila jambo tunalofanya, ni signatory wa kila jambo kwenye maisha yetu hakuna sababu ya kuishi bila kumtegemea Mungu.

Kufanya mambo ambayo yanamsikitisha mzazi wako basi jua Mungu anasikitika zaidi na hapo unajichumia laana utakuwa ukifanya mambo lakini hufanikiwi kumbe umeishi maisha yenye kumchukiza muumba wako.

God ni kila kitu fanya kila jambo kwa kumshirikisha Mungu, toa sadaka, fanya ibada, achana na waganga, na kuwategemea viumbe ambao pia kesho na kesho kutwa watakufa, na Biblia inasema amtegemeae mwanadam amelaaniwa achana na kuwategemea viumbe kama wewe.

Jifunze mara kwa mara ili kuujengea ubongo wako maarifa mengi kwa ajili ya matumizi yako binafsi na jamii.

Epuka mogogoro isiyo ya Lazima, hata kama ni ya lazima basi jitahidi kuepukana nayo kwa kila hali.

Samehe kwa kadili uwezavyo, ni afya ya akili nafsi na moyo, ukiombwa msamaha samehe, ukijua kuwa kila mtu anakosea, waweza kukosewa kama binadamu samehe maana hujui kesho yako wewe

Usiwe mtu wa kubeba mambo yasiyokuwa na faidia hata kidogo, kumbuka jambo likitokea limetokea huwezi kulifuta zaidi ya kusamehe tu.

Ushirika na wenzako liwe ni jambo la lazima kwa mwaka huu, baraka zingine za mafaniko zimefungwa kwenye ushirikiano na watu, kupitia ushirika mzuri na watu hapo ndipo unajenga connection na channels zingine ambazo huwezi zipata ukiwa pekee yako kama mkiwa jangwani.

Hekima, Busara  ni jambo jema kwa mwelekeo mzuri wa maisha yetu.

Nikutakie baraka za Bwana kwa mwaka huu, ukawe mwaka wa ushindi na utajiri kwa kila nyanja ya Maisha yako.

Kumbuka mkono mlegevu huleta umasikini bali mkono wenye bidii hutajilisha.
2019 Is the year of achievements
By
Moses zephania Mgema
0755632375

No comments:

Post a Comment