Sunday, April 14, 2019

INJINI YA MAFANIKIO NI INTERACTION/ KUCHANGAMANA

Kutokana na kuishi kwenye dunia huru kila mtu ana aina ya maisha ambayo amependelea kuyaishi kwa Uhuru na uchaguzi ambao yeye binafsi ameona kwa njia hiyo basi ni sahihi.
Hata mimi, wewe na yule kila mmoja ana aina yake ambayo anaitumia kuendesha maisha yake.
Pamoja na kuwa na Uhuru wa maisha na uchaguzi wa mfumo wa maisha ambao kila mtu amependelea lakini sio kila mfumo ni sahihi sana kuishi bali wakati mwingine ni mbaya sana
Kuna watu wanapenda sana kuishi maisha ya kuchangamana na watu, wako huru kushirikiana na kila mtu, watu wanaamini katika nguvu ya umma na ushirika na wenzao.
Lakini kuna watu ambao ni wakimya sana na ni watu ambao wao kuchangamana au kuwakuta wakipiga stori na kushare mawazo na wenzao ni ngumu sana
Na Mara nyingi husema wanaishi maisha yao hawataki mtu afuatilie maisha yao. Lakini kiuhalisia maisha ya kujitenga na watu kwa mtu mwenye malengo na nia ya dhati ya kufikia ndoto zake lazima achangamane na watu.
Hii inafaida nyingi sana kuliko kutengeneza mazingira ya kuwa mkimya na kuishi maisha yako binafsi.
Watu wengi wanatafsiri vibaya sana baadhi ya maneno kama ambavyo nitaelezea hapo chini
1. Hekima
Watu wengi sana wanaamini kukaa kimya ndiyo hekima na busara, lakini kumbe hiyo sio hekima wakati mwingine ni kwa sababu ya ujinga, kiburi, majivuno na kukosa uelewa wa mambo mengi yanayohusu jamii. Kwa hiyo si kila mtu mkimya ni mnyenyekevu na mwenye busara.
2. Imani
Kuna imani zimejengeka kwenye jamii nyingi kwamba, ukimya nao ni jibu ni kweli. Lakini je hilo ni jibu sahihi au ni tango pori kwa hiyo wakati mwingine ni vema kusema ili kujisaidia wewe binafsi ila pia kumsaidia mwingine.
3.Hakuna mtu anaweza kuishi pekee yake.
Tunategemeana sana kwa mambo mengi, sijui umewahi kujiuliza huwa unaenda kazini kumfanyia nani kazi, je ni boss, wanyama au kuna walengwa wa kazi unayoifanya wanatakiwa kupata huduma yako.

Hapo jiulize sasa kwamba ni namna gani unaweza kuishi maisha yako bila kuwashirikisha wengine ?. Jibu rahisi kwamba hakuna mtu anaweza kuishi maisha yake pekee yake Bali tunategemeana.

Tunaendelea.............
Kuna aina ya maisha baadhi yetu tuliamua kuyaishi tangu tukiwa watoto kwa kulazimishwa na wazazi ndugu jamaa wa karibu, walimu na walezi wetu au hata baada ya mtu kukua anaamua kuishi maisha Fulani anayo yapendekeza yeye hata kama sio sahihi.

> kutokucheza na watu wa familia kadhaa kutokana na levo za maisha.
> Kuaminishwa imani Fulani hasa kwenye masuala ya imani, kwamba siwezi kucheza au kula kwa kina Jose kisa wao ni wakristo na Mimi ni mwislamu na kinyume chake.
>Wazazi kuwatenga watoto wao na kuwasimamia na kuwaondolea fursa ya kucheza wakiamini wanawapa malezi bora kumbe wanaua uwezo wa watoto wao na mengine mengi.

Social Interaction/Mchangamano ndani ya jamii ni muhimu sana.

Kama tulivyoumbwa toka mchakato wa kupatikana kwetu ulihusisha ushirikiano kati ya watu sio mtu na wewe au Mimi nikapatikana

Simpo kabisa kwamba binadamu aliumbwa kwa ushirika na ushirika una nguvu kubwa iletayo ushindi kwa mtu binafsi lakini pia kwa jamii.

Kuna faida nyingi na kubwa mno kwenye kushirikiana na wenzako mfano, kucheza pamoja, kupiga stori, kujiweka karibu na wenzao hii inakujengea uwezo wa
1. Kujifahamu zaidi
2. Kuwafahamu wengine
3. Na kufahamu zaidi mfumo wa maisha uko vipi kuanzia ngazi ya chini mpaka huko duniani.

Kupitia social groups interactions kuna elimu kubwa ambayo wakati mwingine huwezi kuipata ukiwa nje ya makundi haya ya kijamii. Mfano niliwahi kusoma historia ya moja ya matajiri hapa nchini kwamba pamoja na kwamba alianzisha biashara yake yeye kama yeye lakini amekuwa akipata mawazo mazuri sana kupitia kwenye makundi ya kijamii kama kwenye vijiwe vya kawaha na maeneo mengine alisema kwamba.
Alichogundua yeye watu wa chini huku mitaani wana mawazo mazuri sana ukilinganisha wakati mwingine na mawazo mengi yaliyopangiliwa kwenye vitabu wakati mwingine huwa na uhalisia wa maisha ya mbele zaidi ukilinganisha na stori za vujiweni vinavyogusa maisha halisi ya watu ambao wakati mwingine ndiyo wateja au walengwa wa huduma za kibisahara.

Changamoto kubwa ambayo vijana wengi tunapitia ni ile hali ya kujifungia kwenye mitazamo na mifumo Fulani ambayo kwa namna moja ama nyingine inatuua tukidhani kwamba tupo sahihi.
Mfano mtu anafungua Instagram account anaweka private, kila jambo binafsi ukifuatilia undani wa hiyo private eti hataki mazoea inasikitisha sana.
Kila mmoja ana Uhuru wa kufanya anachoona ni sahihi kwake na maisha yake lakini kama hakuna sababu ya kujitenga na wenzako kwa nini ujitenge kisa tu ulimwona Fulani kaweka private na wewe ndiyo hivyo tena.

Watu kama hawa unakuta anafanya hivi akiwa chuo anapomaliza chuo basi ameanzisha biashara Fulani ndo anaanza kujipendekeza kwa watu na kuwalazimisha wakati mwingine wamfollow kisa tu ameanzisha online business.

Je watu wakivunga utasema unalongwa kumbe wewe ndo mchawi wa hiyo online business au hata huku kwenye jamii husalimii majirani kwa lugha rahisi unafunga vioo ukifungua duka basi unaanzisha ushositito wasiponunnua eti wana wivu yako huyakumbuki, unajitia msamalia mwema na kuwatangazia wakati ulikuwa unawaona  mawe tu hapo kabla.

Unakuta mtu yupo kwenye group la whatsup ambalo hata hakuungwa alijiunga mwenyewe kupitia Link lakini mtu huyo, ni kimya, hachangiaji chochote, hata kuitikia salaam, au kusalimia au mtu kapositi hata kupongeza au kukosoa hakuna kimya tu. Unajiuliza je huyu mtu yupo hapa kwa bahati mbaya au shida ni nini.
Ukimuuliza atakuambia niache na maisha yangu lakini wakati huo yuko ndani ya group huo ni ushamba na kutokujutambua.

Maisha yetu ni ushirika, kushare ideas, having funs na mambo mengine kitu ambacho kina leta faida na manufaa kwenye kazi hata afya kiujumla.

Kuna faida za kuchangamana na makundi ya kijamii japo si kila kundi au group ni sahihi.
1.Inatengeneza connection na watu wapya.
2. Kujua tabia za watu, hii inakupa fursa ya kujua ni watu gani sahihi wakuambatana nao.
3. Ni rahisi kugundua uwezo wako kwa maana ya kipaji ambacho kinaweza kukufanya kufikia ndoto na malengo yako.
4. Kupitia socializations una nafasi kubwa ya kugundua fursa mpya za kibiashara, maana kupitia mazungumzo utagundua mahitaji ya watu lakini pia changamoto ambazo unaweza kuzigeuza nakuwa fursa kwako.
5. Ni rahisi kupata social support unapokuwa na jambo lako au unapoanzisha kitu chako, maana wateja au watazamaji wa kipaji chako kama wewe ni mwimbaji au unakipaji chako.
6. Ni platform ya kujitangaza na kuimbia dunia kuwa wewe ndo unahitajika kwa jambo Fulani.
7.Nafasi ya kujifunza kila siku vitu vipya.
8. Nafasi ya wewe kujijua, maana wakati mwingine tunajijua kupitia watu. Hivyo inapelekea kujua nguvu na udhaifu wako.
Note.
Hizi ni baadhi ya faida ambazo mtu anaweza kuzipata pale anapokuwa ni mtu wakushirikiana na wenzake ndani ya jamii.
Lakini pia kuna faida za kiafya maana kupitia interaction unajifunza mengi, lakini vilevile unaweza kuwa unapitia changamoto Fulani kwenye maisha lakini unapokuwa mchangamanaji kwenye jamii unaweza kujikuta unakutana na watu ambao wamewahi kupitia changamoto kama yako na wakavuka.
Hivyo kupitia shuda hizo unaweza kupata nguvu na imani kwamba kumbe hata wewe unaweza kutoka hapo.
NB.
Pamoja na faida nyingi lakini fahamu kuwa si kila social groups lazima uitaract nao, tazama makundi yenye faida.
Sio kila page ya Instagram, group la whatsup ujiunge eti kisa umeambiwa na Moses uwe na social groups interactions, tafuta groups, na hudhuria semina zenye manufaa kwako.
Ipo nguvu kwenye ushirikiano, na hakuna mtu anaweza kuishi mwenyewe kama yupo jangwani.
Maisha yetu ni ecology kwa maana kwamba tunategemeana, ukianzisha biashara mlengwa ni binadamu, unapoamka kwenda kazini mlengwa ni binadamu nk.

Moses z. Mgema.
0715366003/0755632375
mgemamoses@gmail.com

No comments:

Post a Comment