Thursday, April 18, 2019

AIBARIKI KAZI YA MWENYE BIDII.

Aibariki kazi ya mikono yako wewe mwenye bidii, hii ni ahadi ya Mungu kwa kila atendae kazi kwa nafasi yake.

Pamoja hayo yote kwa maana ya ahadi za Mungu ambae ndiyo muumba wetu bado iko haja ya kila mtu kujitathimini kama kweli nafasi aliyo nayo anaitendea haki sawa sawa na kusudi la kuumbwa na kuwekwa duniani.

Kwa kazi ya mikono yako yenye ufanisi wa hali ya juu kwa maana ya innovation, creativities, passion and love of it, daily learning kwa lengo la sustainability ndiyo misingi ya kufikia malengo na maono yako bila kujali muda ambao utafikia kwenye kilele cha matokeo yako.

Changamoto ni nyingi njiani kuliko wepesi kwa sababu inaamini kuwa kitu chochote kizuri kinahitaji maarifa mengi, ujuzi, uvumilivu, kwa maana ya njia tupitazo ni ngumu na zenye kusongwa na changamoto na vikwazo vingi.

Wengi waliofanikiwa kwenye mambo yao, kwa maana ya wafanyabiashara, wasomi, wachezaji wa michezo yote, waimbaji, na kwa kila kazi ambayo mtu amefikia kilele cha mafanikio basi hapo mwanzo alipambana sana huku akiweka uvumilivu na imani kubwa ya kwamba ipo siku atafikia malengo yake.

Huku njiani kuna mambo mengi sana mfano kuna watu wanakutia moyo sana na wanatoa semina bomba zenye kuinspire na kumotivate kwamba yeye kama ametoboa basi hata wewe unaweza, lakini ya wezekana mtu yule yule baada ya kumfuata na kuhitaji japo wazo jema alikujibu au kukutendea tofauti na ukivyotarajia, kuna ndugu yako ulimtegemea na alikuahidi jambo Fulani ukitimiza mambo Fulani yawezekana umetimiza yote lakini tena kwa kutumia gharama na akiba yako yote ukijua kuwa kuna support ndogo itafanyika mahali utakapopelea lakini mwisho wa siku yule MTU amekuangusha.

Kuanguka ukiwa unakimbia sio jambo la kushangaza kwa sababu unakuwa kwenye mwendo wa speed na mzunguko wa damu unakuwa juu sana ukilinganisha na ukiwa unatembea au umetulia mahali. Hivyo inuka jikung'ute endelea na mwendo.

Hata safari ya kuikimbilia ndoto na kusudi la Mungu kwako, kuna kuanguka, kuumia na kupoteza kabisa lakini usikate tamaa, no turning back utakuwa mke wa Luthu ambae aligeuka na kuwa nguzo ya chumvi.

Iko misemo na maneno matamu sana kwenye dunia ya Leo yenye kutia moyo, lakini yenye kuumiza ambayo ni machungu neno moja tu ulishike SITOKATA TAMAA.

Usikatishwe tamaa na maneno ya watu kwa sababu kusudi la kuumbwa kwako lazima litimie pambana iamini ndoto na uwezo mkuu ndani yako.

Fanya kwa nafasi yako kwa viwango vya ubora na uwekezaji wa nguvu, maarifa, ujuzi na kila kitu kinachohitajika kufanywa na wewe Fanya halafu Mungu anajua namna ya kufanya juu yako.

Jua kila kazi ufanyayo iwe kwa kutumia kipaji, kazini, unafanya biashara mlengwa mkuu ni mtu, hivyo Fanya huku ukiposition wewe kwenye nafasi ya mteja, msikilizaji wa nyimbo yako mtazamaji wa mpira unaocheza nk. then ujiulize je ingekuwa ndo Mimi natazama au nasikiliza ningeenjoy kazi hii ?

Usifanye kazi kama by the way Fanya hiyo kazi kama hutofanya tena hata kama una malengo ya kybadilisha hapo mbeleni.

Usiwaze matokeo ya kazi wakati hujaweka mikakati ya kuona hayo matokeo unataka uyapate, cha msingi waza matokeo hayo huku ukitimiza michakato ya kufikia huko kwa kufuata michakato sahihi na kwa uaminifu.

Kuwa na Imani na kazi yako lakini kumbuka imani bila matendo matokeo yake yanabaki kuwa ni zero.

Love, be patient, care, corporate with others, Think about the consumers before you serve or release your work hapo utajijuta una fly like Eagle kwa sababu utakuwa umetimiza majukumu yako.
Kila mtu Leo anapambana sana kuhakikisha afanikiwa na kuwa boss au mweshimiwa, hakuna mtu anataka kuwa mtumwa, wa mtu mwingine hivyo pambana kwa kadri ya nguvu zako.
Kazi rahisi itakupa matokeo rahisi, kazi iliyobebwa na umaanisha mkubwa ndani yake itakupa positive results.
Hakuna uchawi wala uganga kwenye mafanikio mchawi ni mimi au wewe hasa pale unaposhindwa kutimiza majukumu yako sawa sawa.

Moses Zephania Mgema
mgemamoses@gmail.com
mosesmgema12.blogspot. com
0755632375/0715366003

No comments:

Post a Comment