Thursday, April 18, 2019

KUJIFUNZA NI SAFARI YA MAISHA YOTE YA MTU DUNIANI.

Tembea uone, usipotembea unaweza ukifiri kwamba maisha ya eneo unaloishi ni sawa na maisha ya watu wengine ambao wako maeneo mbalimbali ya dunia hii au wakati mwingine unaweza kufikiri kwamba sehemu unayoishi labda mna maisha duni kuliko maisha ya maeneo mengine ambayo huwa unasimuliwa na kupewa stori za huko au pia ukahisi maisha yako na jamii inayokuzunguka ndo mahali sahihi zaidi kuliko mahali pengine.

Ukitembea utajikuta unajifunza mambo mengi sana ambayo kwa ufupi yanakufanya ujue namna nyingine ya maisha ya watu, utamaduni, namna wanavyoadress matatizo, ushirikiano, mitazamo pamoja misingi halisi ya maisha yao.

Zipo stori nyingi sana duniani ambazo kwa ufupi ndizo zinazoyafanya maisha kuwa hasa ni completed circles ya maisha yetu ya kila siku bila kujal unaishi kwenye kusudi la maisha yako au kwa namna yoyote ambayo umeamua kuchagua kuishi.

Mchanganyiko wa maisha haya yanatufanya tujitenge sisi kwa sisi kutokana na levels za kielimu, kiuchumi, kisiasa, kiimani, kimitazamo na fikra. Hivyo kila mmoja wetu kufanya analoona jema analitenda ili kuifanya nafsi yake itulie na kujisikia Amani.

Wakati watu waliofanikiwa wakiwaza namna gani wataendelea kupaa na kuondoka mahali walipo, wanawaza, kuongezeka kwa fedha benki, majumba ya kibiashara, nk, Msomi mwenye kujua maana ya shule nae ataendelea kuhakikisha elimu yake inapaa juu sana ili kukidhi hitaji lake la kuwa na elimu kubwa.

Maisha yanaendelea, watu wa dini na imani nao huwa wanahakikisha kuwa wanafanya vizuri kwenye suala la kiroho huku wakitimiza matakwa kanuni na taratibu za ibada ambazo ndo fungu lao, muda wote watasoma neno, kuomba na kuwaza juu ya ufalme wa Mungu namna gani ataujenga na kuwa mwenye kufanya kusudi lake kwa kadri ya wito na utayari ndani.

Wapo wanasiasa, wanafalsafa, wanaharakati, na watu ambao wanapambania haki, maendeleo lakini pia kutengeneza mazingira ya wao kuonekana bora zaidi ya mwingine na mambo mengine mengi yahusuyo, itikadi, mila, taratibu na kanuni za vyama vyao.

Watu wengi wasio nacho either wanatokea kwenye makundi ya kijamii anabyo nimeyataja hapo juu lakini nimekuja gundua ni watu wenye upendo sana kwa wao kwa wao na hutiana moyo nyakati zote za furaha na nyakati za huzuni wakiamini kuwa hilo ni fungu lao.

Lakini inapokuja kwenye suala la usawa wa kiuchumi na maendeleo watu hawa wamekuwa ni watu wenye wivu, chuki na wenye kutamani siku moja kuona waliofanikiwa wakianguka chini ili kuwa sawa. Ndiyo maana mtu tajiri au aliyefanikiwa kwa kitu chochote kwenye maisha anapokwama maneno mengi huibuka mitaani hasa kutoka kwenye kundi la watu wa chini.

Ipo mifano mingi ambayo inaweza kukufanya ukaelewa nini nataka ujifunze hapa, mfano tulipokuwa shule watoto wengi sana tulipenda kuona yule mwenye uwezo darasani anashuka na kwel walikuwa wakiteleza stori inakuwa kubwa huku akinenewa mabaya, anajifanyaga sana huyu, anajipendekeza kwa walimu, mbinafsi, na hata akiongoza tulikuwa tunaamini anapendelewa na kubebwa na walimu ajabu sana .

Mtu mwenye Mali, uwezo akipatwa jambo baya asilimia kubwa watatengeneza scenario mbalimbali mbaya lengo ikiwa ni kuhakikisha nafsi zao zinafurahi kwa anguko lake hilo, utasikia kwanza alikuwa mwizi mzurumaji, muuji mtoa kafara na maneno mengi ambayo ukiyafuatilia kiundani hakuna maana hasa ndani yake.

Juzi hapa mahali nakaa tulipata changamoto ya nyumba ile kuuzwa na bank na utaratibu uliotumika haukuwa mzuri kwa sababu idhinisho la mahakama lilikuwa bado halijafika kwa aliyekuwa mmiliki halali wa nyumba, kwa tukio hilo kulikuwa na maoni mengi hasa toka kwa majirani, ukitazama watu walioumizwa na tukio hilo ni wale wenye nafuu ya maisha na baadhi yao walitoa machozi lakini wenzangu na mie ndo walishadadia kweli kweli kiasi unahisi kuna uadui kati ya hawa watu.

Sio kwamba matajiri wote wanaroho ya huruma na nzuri hapana ila tunatazama kwa asilimia kubwa.

Wala sio kila mtu masikini anashida hiyo hapana wengine wapo wenye upendo mzuri lakini asilimia kubwa anguko la mtu aliyefaniwa kiuchumi, kwa aina yoyote anapoanguka watu wengi sana wa chini hufurahi na kuzusha maneno mengi kama alikuwa anajidai, analinga ana majivuno nk.

Kwa njia hii
>Mtu mwenye chuki na wivu wa ubaya sio rahisi kufanikiwa sana.
>Masikini wataendelea kuwa masikini kama hawatabadili mitazamo yao na kuwa na imani potofu ya kuwa kila aliyefanikiwa anatumia vitu Fulani.
So is better to learn to appreciate for those who have already achieved and reached their dreams.

This will help poor people to have desire of working hard, learning from successful people and sometimes to pass on where successful people passed.

It gives an open space to the mind which brings easy way of cultivating ideas and coming with a clear solution, ways on how to move forward heading to the destination of our dreams.

Moses Zephania Mgema
0755632375/0715366003
mgemamoses@gmail.com
mosesmgema12.blogspot. com
Dar es salaam - Tanzania

No comments:

Post a Comment