Saturday, January 8, 2022

KATAA KUISHI MANENO YA VINYWA VYWA WATU, ISHI KUSUDI LA MUNGU.

Nimekuwa nikijifunza kwa muda mrefu kupitia watu mbalimbali waliofanikiwa na hata bado hawajafakiwa na walioshindwa kabisa. Lengo la kujifunza kwa watu wote hawa nikutamani kujua sababu ambazo zimewafanya waliofanikiwa  kufanikiwa na wale walioshindwa kushindwa.

Katika mfumo wa maisha yetu hasa Tanzania kwetu, tumekuwana maisha ambayo yameathiliwa sana na mitazamo  ya watu, jamii na hata familia zetu wenyewe, kila jambo ambalo linatokea kwenye maisha yetu nyuma yake kuna athari  ya watu, jamii, imani zetu, elimu na hata mitazamo  ya namna ambavyo mtu anaishi.


Friday, January 7, 2022

MAISHA NI MAHUSIANO BORA

Maisha ni fumbo amabalo ni ngumu sana kulifumbua inahitaji hekima, busara na mtazamo wenye ukomavu ndani  yake. Hakuna dunia ya pekee yako, hakuna mtu anae ishi katikati ya watu wengine akaishi kama yuko nyikani au jangwani.

Hii ni kwa sababu  tumeumbwa kwa kutegemeana, kushirikiana, kusaidiana na kuinuana, iwe moja kwa moja au kupitia mlango wa nyuma. Maisha ni picha isiyohitaji maelezo ya ziada, kwa aliye komaa kupitia picha tu anaweza kuelewa kinachomaanishwa na picha yenyewe.

Ni vyema kuishi maisha kwa utulivu, ushirika mwema, upendo, kuthamini wengine na kusameheana pale inapotokea mtofautiano. Kumbuka  katikati  ya watu kutofautiana, kupishana, kukwaruzana ni jambo la kawaida.

Kama kwenye nyumba za ibada watu wanaweza kutofautiana, kama Shetani pamoja na mazuri yote ambayo  alikuwa akipata huko mbinguni lakini bado, alitofautiana na Mungu  sembuse mtu kwa mtu, kutofautiana ni jambo  la kawaida kabisa.

Kutofautiana huletwa na kupishana kwa mitazamo na hoja, kukutetea maslahi ya kila mtu na Jamii yake, mambo  ya kazi, biashara na mambo mengine mengi kwenye  Jamii yetu, maofsini yawezekana ukatofautiana na sera ya mwajiri, mwajiri asiridhishwe na utendaji kazi wa mwajiriwa, hivyo lazima iwepo tofauti.

Lakini kutofautiana kwa hoja au mitazamo sio sababu ya kutengeneza uadui na chuki za kudumu kati yetu sisi kama binadamu, jitahidi  kufanya mambo ambayo yanalenga kuleta upendo kati yenu ili amani itawale, amani ikitawala lazima kuwe na matokeo yenye ufanisi katika kila jambo.

Unapoondoka mahali hata kama umeondoka kwa namna sio nzuri, ni vyema kusamehe na kusahau, kwa sababu  hata baada ya kazi kuna maisha. Ukifukuzwa kazi au mahali Fulani hata kama unahisi au unajua umekosewa ni vyema kuondoka mahali pale na kumshukuru Mungu kwa yote.

Pale unapofikri umeonewa, kunyanyaswa, kutokutendewa haki, udhika kwa muda kama binadamu lakini usishikilie jambo kwa miaka na miaka, huwezi jua kwa nini uliondoka mahali pale, Mungu huwa anajua kabla ya sisi kujua.

Tinachofikiri kwetu ni kibaya au kinatuumiza kumbuka kwa Mungu  inaweza kuwa ni sawa, na kile tunachohisi ni kizuri kwa upande wetu kwa Mungu inaweza kuwa sio sawa.

Mifano miwili halisi, Ayubu baada ya kupata majaribu makali, ilionekana kama Mungu amemwacha mpaka watu wake wa karibu wakaanza kusema amkufuru Mungu afe lakini alijua Mungu kwake ni nani.

Hawa aliona wema wa nyoka katika ile bustani, akaona huyu Mungu hafai kwa nini anatukatalia tenda hili, akaona kilichoko mbele yake ni chema kuliko yake kina faida kuliko maagizo ya awali kutoka kwa Mungu.

Matokeo ya watu hawa wawili yanaonyesha ni kwa kiasi gani maisha yetu ni fumbo na kesho yetu iko mikononi mwa Mungu, na Mungu ndie mwamzi wa kila kesho yetu. Usiishi kwa kufuata hisia na matakwa binafsi, tulia, jifunze, toa nafasi kabla ya kuchukua maamzi ambayo  unafikiri ni maamzi sahihi kwako.

Jenga mahusiano  bora na imara maana kesho yako huijui, ukifukuzwa kazi mahali, usitengeneze uadui pamoja na kufukuzwa kesho wanaweza kukurejesha maana yawezekana wanachukua maamzi kwa sababu ya maneno ya watu ambao wametengeneza fitina  na wanaona wewe ni bora kuliko wao.

Kuna wakati unafukuzwa kazi kwa sababu  watu wanataka kuprove yale mashitaka unayoshitakiwa nayo kama ni kweli, hivyo ukiondolewa jitahidi sana kuzuia hasira, kinywa kunena matusi, ugomvi na ukorofi, jitahidi kutulia na kuondoka.

Kama ulionewa haki yako haiwezi kupotea, pengo lake litaonekana kama walikuondoa kwa hila na fitina, yawezekana waliokuondoa walikuwa wanataka kuyadhibitisha yale mashitka kama ni ya kweli au uongo, 

Ukichoka mahali, usiondoke kama umefukuzwa, fuata utaratibu mzuri wa kuomba kuondoka mahali Fulani, kama walivyokupokea katika familia, kazini, kwenye nyumba za ibada, au mahali popote ni vyema ukiwa umepata mwanga wa kuweza kujitegemea, Mungu  amekuinua umepata kazi mpya, umepandishwa cheo ndani ya ofsi, umechoka kuwa sehemu ya familia, ofsi, biashara  nk, ondoka kwa amani, aga vyema, ili iwe kwa heri ya kuonana.

Kesho yangu siijui, kesho yako huijui ni vyema kulinda mahusiano  yako na watu, hao hata kesho watakutetea mahali, utakuwa na ujasiri wa kurudi mahali, maana uliondoka kwa amani, uliaga na kuondoka kwako, itakuwa kwa heri ya kuonana tena.
Hatuwezi kupendezana katika yote ila tunaweza kupunguza pengo la chuki, uadui na uhasama usiokuwa wa lazima.

Mwaka huu, utumiae kama mwaka wakujenga mahusiano bora kwa kadri  uwezavyo, hakika utakuwa mwaka bora wa kuzaa matunda. Zaidi jifunze kunyamaza, sio kila neno lazima uongee....

Moses_mgema Zephaniah 
0755632375
0719110760

Wednesday, January 5, 2022

TWEKA MPAKA KILINDINI

Luka 5:4

Ni maneno ya Bwana Yesu akimwambia Simoni pamoja na wenzake hii ilikuja baada ya Simoni na wenzake kufanya kazi ya kuvua samaki usiku kucha wasiambulie chochote kile.

Tukio hili lilitokea katika ziwa la Genesareti alipokuwa akisongwa na watu na kisha akaanza kufundisha, ndipo alipomwambia Simoni Petro habari ya kushusha nyavu katika ziwa like tena katika kina kirefu (kilindini).

Yawezekana umekuwa katika kufanya kazi na matokeo yamekuwa madogo ukilinganisha na kipato unachopata.

Hivyo kama wewe ni mmoja wapo somo hili litakufaa sana, vilevile kama mambo yako yanaenda vizuri linakuhusu pia kwa ajili ya kesho yako ambayo ni fumbo.

Ukitafakari habari ya Yesu na makutano pale kwenye ziwa la Genesareti utaona Bwana Yesu, alikuwa akihangaika sana katika kuwafundisha makutano, yale mazingira yalikuwa ni magumu sana kutokana na kwamba watu wengi walimsonga na yeye alitaka kuwafundisha zaidi katika utulivu, hivyo hakuona kama akiendelea katika hali ile ile atatimiza kusudi lake, ndipo akaamua atafute madhabahu ya kuwakutanisha wale watu pamoja, mahali atakapotulia ili awafundishe wale watu katika ustaarabu na utaratibu ambao Mungu ameukusudia..

Na alipogeuka akaona vyombo viwili vimeegeshwa pwani na wenye navyo wametoka, ndipo akikichagua cha mmojawapo na kukigeuza kuwa madhabahu yake ya muda.

Sasa Chombo kinawakilisha nini katika mazingira tuliyopo leo?. Chombo kinawakilisha kitu chochote cha kujipatia kipato, kumbuka chombo hicho Bwana alichokitumia kilikuwa ni cha akina Petro cha kuvulia samaki, kwasasa hivi chombo kinaweza kikawa, elimu ya mtu, ujuzi wa mtu, biashara ya mtu, fremu ya mtu, shamba la mtu, kiwanja cha mtu,n.k.

Lakini tunasoma katika habari hiyo, tunaona Bwana alipotazama hakuchagua vyombo vilivyokuwa kando kando vyenye wavuvi au samaki, kumbuka vilikuwepo tu vingi vizuri zaidi ya hivyo vilivyokuwa vinazungukazunguka maeneo yale, lakini yeye hakuchagua chochote kati ya hivyo bali alivichagua vile visivyokuwa na kitu ndani yake…(Na ndio maana somo hili linawahusu sana wale ambao shughuli zao haziendi sawa),

Sasa kilichotokea ni kwamba wakina Petro walifanya kazi ya kuchosha usiku kucha wakihangaika kutafuta samaki ukanda mzima wa ziwa la Genesareti kwa shida, na kujitoa kweli kweli lakini wasipate kitu, mpaka kulipokucha wakakata tamaa ya kuendelea kuvua tena, wakaona kilichobakia tu ni kukipumzisha chombo na kuzitengeneza nyavu zao tena, kisha kuzihifadhi mpaka wakati mwingine,

Lakini baadaye kidogo ndio tunamwona Bwana Yesu akisumbuka na wale makutano, ndipo wao wakamruhusu Bwana kutumia vile vyombo ili kutimiza kusudi lake la kuhubiri,. Na baada ya Bwana kumaliza kuhubiri, sasa wakati makutano yote wameshaondoka ndipo akawageukia wale wamiliki wa vile vyombo, na kuwaambia twekeni mpaka kilindini mkashushe nyavu zenu mkavue samaki.

Lakini wao walimwambia, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha pasipo mafanikio, na walipokubali tu kwenda kuvua walipata matokeo makubwa ya kushangaza, mpaka nyavu zao kuanza kukatika, mpaka kufikia hatua ya kuomba msaada kwa wingi wa Baraka hizo, maana zimekuwa nyingi mpaka kushindwa kuvuta zile nyavu kutokana na wingi wa samaki ikalazimisha kuomba msaada kutoka katika chombo cha pili, maana wingi wa samaki ulipelekea chombo chao kuanza kuzama ndani ya maji ya ziwa.

Yesu ni yeye Yule jana, leo na hata milele hajabadilika, leo pia anaweza kufanya kama alivyo fanya kwa Simon petro na wenzake.  Umejaribu kufanya mambo mengi kwa bidii na ufanisi mwingi lakini kwa bidii, lakini bado huoni matokeo yanayoendana na bidii yako

Leo hii hicho chombo chako kigeuze kuwa MADHABAHU YA KRISTO kwasababu anakitafuta hicho ili alifanye kusudi lake, kumbuka pale Yesu hakutafuta sinagogi la kuwakusanya wale makutano waliokuwa wanamsonga, hakutafuta hekalu, wala hakutafuta mahali patakatifu bali alitafuta MAHALI PA KUJIPATIA KIPATO KWA MTU, mahali ambapo mtu anapopategemea kujipatia mkate wake wa kila siku, na pia fahamu tu, siku zote Bwana anapaangalia mahali ambapo palipo patupu kama kwako wewe, Mahali ambapo pamefanyika kazi ya kuchosha miaka mingi, miezi mingi pasipo mafanikio yoyote, hapo ndipo anapopataka kwa ajili ya kazi yake, na akishamalizana napo hapo, ndipo atakwambia nenda katupe nyavu zako kilindini uvue samaki, kwa wingi wa atakachokupa Bwana utaita mpaka na marafiki na zako na maadui zako waje nao kushiriki Baraka zako Mungu alizokuandalia.

Leo Kazi yako wewe ni ya ufundi, una ujuzi wa kutosha kuhusu masuala ya ujenzi, na unaona mahali unapofanyia pengine ni kanisani kuna kasoro Fulani ya ujenzi, na shughuli zako za kijenzi haziendi sawa, umekuwa ukipata mapato kidogo kupitia hiyo,wakati mwingine unakosa kabisa kazi, huo ndio wakati wa kwenda kumruhusu Bwana atumie hicho chombo chako (ujuzi),

nenda mahali unapokusanyika (kanisa), kazi ya Mungu inapofanywa, angalia kasoro zinazohusiana na taaluma yako, na utumie ujuzi wako kurekebisha tatizo hilo bila kutazamia malipo yoyote, pengine umeona ukuta wa kanisa umebomoka au una ufa, uzibe, umeona mfumo wa maji haujakaa sawa na una ujuzi wa kufanya hivyo, urekebishe hata kama hauna chochote, umeona kanisa halina choo kinachostahili, na wewe una ujuzi wa namna ya kutengeneza vizuri, nenda kafanye hivyo, kajenge kwa ustadi wote, na maarifa yako yote, umeona kuna kasoro ya umeme na mfumo wa nyaya, na una ujuzi huo nenda karekebishe usisubiri hata mtu akamwambie, mruhusu Bwana atumie hicho chombo, na mwisho wa siku utaona matokeo na mtu asiyefanya hivyo wakati Fulani ukifika.

Au wewe ni polisi au mlinzi, anza kutoa mchango katika sekta hiyo ndani ya kazi ya Mungu..Usiseme Mungu kweli ataweza kutumia taaluma hii/ujuzi huu kwenye kazi yake??..kumbuka Yesu alitumia mtumbwi wa wavuvi kuwapelekea maelfu ya watu katika ufalme wa mbinguni…Na wewe vivyo hivyo mpe Bwana chombo chako.

Au wewe unafanya kazi ya upishi, na unaona kazi zako haziendi sawa, faida ndogo, na unaona kuna uhitaji mkubwa wa wapishi ndani ya nyumba ya Mungu, labda kwa ajili ya wazee wasiojiweza (wakristo), au wageni, au wenye mahitaji na mayatima (walio wakristo), ndani ya kanisa n.k usingoje uambiwe au uwe na kitu kwanza ndio ufanye, wewe mwenyewe anza kuchukua hatua ya kujitolea kwenda kuifanya, tena pasipo hata kuombwa.

Wewe ni mtengeneza bustani, na ndiyo kazi yako umekuwa ukifanya kwa ajili ya kujipatia kipato..Lakini mazingira ya kanisani ni machafu au hayavutii, panaonekana ni mahali pasipo tofauti na sehemu nyingine yoyote, Tumia chombo chako (ujuzi) kurekebisha mazingira ya Mungu, pakavutia kama vile unavyopendezesha bustani za watu wengine,..unaweza ukaona ni jambo dogo lakini linamaana kubwa na Bwana akisharidhika atakuambia shuka vilindini..utaona milango Mungu anayokufungulia katika hiyo hiyo kazi yako ilivyo ya ajabu.

Wewe ambaye ulikuwa unatafuta kazi,na bado hujapata, angali unao ujuzi Fulani, usiuache ulale utumie huo ujuzi katika kazi ya ufalme wa mbinguni, kwamfano labda wewe ni “ IT ” (mjuzi wa katika teknolijia ya Kompyuta), unaweza uka unda wavuti na tovuti kwaajili ya kutangaza ufalme wa mbinguni, unaweza ukabuni programu za kutangaza kazi ya Mungu kirahisi katika mitandao fanya kiuaminifu kabisa..Na Bwana akishamaliza kutenda kazi kwa kutumia chombo chako, atakuambia shuka vilindini…Utaona nafasi ambayo ulikuwa unaitafuta kwa kuhangaika kwa muda mrefu pasipo mafanikio kama wakina Petro walivyokuwa..unaipata ndani ya kipindi kifupi tena chenye faida mara 100 zaidi ya kile cha mwanzo ulichokuwa unakihangaikia..

Lakini hizo zote zinakuja kwanza kwa kumtolea Bwana chombo chako akitumie, kwa ajili ya kazi yake, lakini kuna wengine hawapendi kumpa Bwana nafasi lakini wanataka Baraka za Bwana, utakuta mtu analo eneo kubwa limekaa pasipo matumizi yoyote, hataki hata kukaribisha watu wafanyie kazi za mikutano ya injili hapo, na bado anataka Mungu ambariki, ndipo hapo zile roho za udanganyifu zilizoachiliwa katika siku za mwisho zinaanza kumdanganya na kumshawishi, akanunue mafuta ya upako, anunue chumvi na maji ya Baraka akanyunyuzie kwenye kiwanja chake na kwenye biashara yake, aanze kukemea roho za laana katika kiwanja chake, au biashara zake, ili mambo yake yaanze kwenda vizuri.

Utamkuta mwingine anazo fremu za vyumba na zimekosa mpangaji wa kufanyia biashara au tution,..na wakati huo huo kuna wakristo wenzake wamekuja kumwomba awape angalau fremu moja wawe wanafanyia bible study au maombi wakati wa jioni kwa muda huku wanatafuta eneo lingine..lakini kwasababu hajui uweza wa Mungu, anawazuilia na kuona bora tu ziendelee kuwa zimefungwa.na wakati huo huo anazunguka kutafuta kuombewa na kununua maji na mafuta ya upako huku na kule hata wakati mwingine nchi na nchi..Mtu wa namna hii hawezi kutazamia miujiza kama waliofanyiwa wakina Petro.

Bwana anasema nikaribieni, nami nitawakaribia… Wakati mwingine kutokuwa full committed  katika eneo lako la utumishi umekuwa chanzo cha kazi ya  Mungu kuwa katika hali dhaifu na wewe hutaki kuifanya chako..(Hagai 1:1-12). 

Anza leo kufanya kama Simoni Petro alivyofanya na wenzake na Mungu atakubariki. Mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.

Tutaendelea na somo hili baadae......

Moses Zephaniah Mgema

moses@gmail.com 

Tuesday, January 4, 2022

NGUVU YA KUAMUA NA KICHUKUA HATUA YA UTHUBUTU

Tangu kuzaliwa kwa mitume wa Mungu, kuanzia Yesu, Yohana pamoja na wanafunzi wa Yesu, tunajifunza ni jinsi gani ambavyo walithubutu na kuamua kuchukua hatua ya vitendo ambavyo vilileta matokeo makubwa katika maisha yao 

Nimekuwa nikijifunza kupitia maisha yangu binafsi, maisha ya wengine hasa walifanikiwa kwenye kutimiza malengo na makusudi ya kuishi kwao duniani hapa.

Maisha yetu yanahitaji uthubutu ili kuweza kuona mambo yanatokea waziwazi, pasipokufanya maamzi mazito na magumu ni ngumu sana pia kuona ukiishi kwenye malengo na matamanio ya ndoto zako.

Iko nguvu ya ajabu na maana sana imbayo humsukuma mtu toka ndani inayompa courage na kumwonyesha kuwa inaweza, laminitis mara inapofikia kwenye hatua yakufanya maamzi mazingira huonyesha impossibility kubwa na kutengeneza hofu na wasiwasi wa kupoteza kuliko kupata na kufanikiwa.

Kufeli kwangu sio ukosefu  wa mtaji bali namna gani naweza kuchukua hatua ya uthubutu katika kile nakiona katika ule uhalisia wa ndani.

Ni kweli maisha ni magumu sana laminitis maisha hayo hayawezi kuwa rahisi kwa kufanya vitu rahisi bali unapaswa kufanya maamzi magumu ya uthubutu ili kujenga misuri na stamina ya kukabili hali yoyote ile ya kimazingira.

Wakati Isaya anatabili kuzaliwa kwa Yohana ambae alienda nyikani, hakuna mtu a angeweza kumwelewa kabisa, ni namna gani mtu aweza kuwa na akili timamu kwenda kuanzisha jambo nyikani. Sio rahisi hata kimono.

Lakini Yohana aliona fursa nyikani akathubutu haikuwa rahisi lakini alifanikiwa kwa sababu ile nguvu ya ndani aliweza kuitii na kufanya hatua ya uthubutu, kwa sababu alijua nini anafanya aliyabadili yale mazingira yakawa uhitaji wa watu, nyika ikawa mahali pakukimbilia.

Yesu alikabiliana na mazingira magumu sana yakutimiza kusudi la uwepo wake duniani, lakini pamoja na ugumu alioupitia, ila ile nguvu ndani yake aliiaply vyema katika mate do, akathubutu  na kuonyesha matokeo makubwa duniani  mpaka akatimiza lengo lake  duniani.

Nguvu ya uthubutu huleta matokeo makubwa, uoga, na kuzingirwa na mazingira ya hofu ya kupoteza imetusababishia watu wengi kuishi maisha yasiofaa sana, kumbe ni kwamba maisha yetu hayajengwe kwenye missing bora na imara yakuchukua hatua ya uthubutu.

Nilichojifunza ni kwamba vitu bora having kwa wepesi bali kwa nguvu na jitihada za maana sana, hakuna njia rahisi inaweza kukupa mafanikio, bali jitihada na marina mengi huleta matokeo chanya na halls.

Dunia ya Leo inatekwa na watu Wallace waliokubali kuwa watubwa Leo, ili kesho ya iwe bora, uthubutu na uchukuaji wa hatua ni silva kubwa bora kwa ajili ya matokeo chanya katika maisha yetu.

Hakuna utajiri katika maisha ya relaxation, hakuna mafanikio kwenye vitu vipyesi, achievers are hustlers, hawakati tamaa hawaoni kushindwa as long wako na afya wanaamini mafanikio ni haki ya.

Hivyo tukiwa kwenye mwanzo wa mwaka ni vyema kuhakikisha malengo na mipango uliyoweka inakwenda kwenye mpangilio sawa, shindwa jambo kwa nje ya sababu zilizo nje ya uwezo wako make it.......

Usikubali uwe mtumwa wa wengine wakati you can be you and see a very  big result kwenye maisha yako

Ipe nafasi nguvu ya ndani na ile mipango kichwani inakuwa na matokeo chanya katika maisha halisi ya nje.
Don't be a slave in 2022
By Moses Mgema
Mgemamoses@gmail.com 

Monday, October 25, 2021

ROHO YA KUCHELEWA ( THE SPIRIT OF DELAY) EP 1.

Bwana asifiwe mtu wa Mungu
Nipende kumshukuru Mungu kwa nafasi ya pekee ambayo ametupa tena kwa neema ambayo ni upendeleo wa Kimungu kwetu.
Leo tutajifunza neno la Mungu lenye kichwa cha somo ROHO YA KUCHELEWA ( SPIRIT OF DELAY).
Katika somo hili tutaona mambo kadhaa ambayo yamekuwa chanzo cha watu wengi kuchelewa kufikia hatima zao na bado wanachukulia kawaida bila kujali muda wa nyakati za kutimiza baadhi ya mambo katika wakati uliokusudiwa.
Note
Sio kila jambo linalochelewa ni mpango wa Mungu hapana ndivyo ilivyo hata kwa upande wa kuwahi kuwa sio kila jambo linalowahi ni mpango wa Mungu. 
➡️Mambo mengine yanachelewa kwa sababu za michezo anayoicheza shetani katika ulimwengu wa Roho bila watu wengi kujua na hivyo kuchukulia kawaida.
➡️ Mambo mengine pia yanawahi sio kwa mpango wa Mungu bali shetani anaweza kuwa amechungulia mbali na kuiona baraka yako iliyo kuu hivyo anapenyeza baraka feki kwa haraka ili kukupishanisha na Baraka ya Mungu.
Lakini hapa tutazungumzia somo lenye kichwa cha somo la Roho ya kuchelewa ( Spirit of delay).
Daniel 10:13-21
Habari ya Daniel aliyejulikana kama Belteshaza ambae majibu ya maombi yake yalishikiliwa na mkuu wa uajemi.
Hapa tunaona pamoja na Daniel kuomba na kufunga kwa majuma matatu lakini bado malaika aliyeagizwa na Mungu kuleta majibu ya Daniel alishikiliwa kwa kwa siku 21 sawa na majumaa matatu ya ambayo Daniel pia alitumia kumwomba Mungu wake.
Hapa nataka uone ni kwa kiasi gani shetani yupo kwa ajili ya kupambana kuhakikisha kwamba hupati kuwa sehemu unayopaswa kwa wakati sahihi uliokusudiwa na Mungu.
Tunayo mifano mingi ambayo imekuwa kama maisha ya kawaida kwa vijana wengi, mfano mtu anamaliza shule badala ya kutafuta kazi hata ndogo kutwa anatembea na vyeti kuomba kazi maofsini, anashindwa kutambua kwamba uzima, elimu na afya aliyo nayo ni mtaji namba moja kwenye maisha.
Mwaka 2016 wakati natoka chuo, nilikuwa na akili nyingi sana kwa sababu nilikubali kuanzia kwenye kiwango nilichokuwa nacho nikaanzisha biashara ndogo ndogo ya chakula mkoani kwangu singida na biashara ilikuwa inakwenda vyema sana na kipato changu ilifikia ikawa inaanzia laki tatu kwa mwezi na mtaji wa kwanza ilikuwa Tsh 30000 tu nilianza na miwa, miwa akaadimika nakaingia kwenye uji, chai na hatimae niliifikia hatua ya kuuza chakula cha mchana na ukuajia wake ulikuwa mkubwa sana.
Wakati naanza kufikiria kufungua mgahawa wakimataifa nikapata tangazo la kazi ambalo lilinifanya kuomba kazi kwa kweli kati ya makosa nimewahi kufanya nikuacha kazi zangu kwenda kwenye kazi ambayo nilifikiri ingenipa zaidi kumbe nilikuwa narudi hatua kadhaa nyuma.

Usiku wa juzi ndio Mungu alinipa mafunuo kwamba watu wengi wanachelewa kufikia malengo kwa sababu shetani amejiingiza katikati ya fikra za watu nakuanzisha mission ambayo imekuwa ni chanzo cha kuchelewesha baadhi ya mambo hasa kwa vijana.

Kijana unakuta anapambana kutafuta ajira na umri unakwenda mwisho wa siku alikuwa na maono makubwa anakuja kuishi kwenye robo ya maono yake kisa alishindwa kutambua kwamba mtaji wa kwanza sio fedha bali ile akili ambayo amepewa na Mungu inaweza kuwa mtaji mkubwa wa kumfanya kuishi kwenye maisha aliyokusudiwa kwenye wakati sahihi.

Wengine wameondolewa shauku ya kuoa, fedha anayo, maisha ambayo yanaweza kuendesha familia vyema anayo lakini, hataki kuoa anaona kama wakati bado kumbe ndani yake shetani ameishaingia maana anajua kwamba kijana huyu akipata mke atakuwa amejipatia kibali kwa Bwana, na maana ya kibali ni upendeleo mkuu kutoka kwa Mungu na kuwa kwenye ndoa mtu anaweza kufanya vizuri zaidi kuliko akiwa pekee yake.
Wengine wamepandikizwa roho yakujiona bado ni watoto hasa vijana wa kiume, na mabinti nao Roho ya kuchaguachagua katika ule wakati sahihi ambao mtu alipaswa kuolewa hapa shetani anacheza na ufahamu wa binti mwisho wa siku umri unakwenda anaamua kuolewa na yeyote atakae kuja ili mradi amepata mume kumbe mtu sahihi alishakuja lakini kwa sababu ya kufungwa ufahamu binti alijiona bado au yule kijana alimwona sio hadhi yake.
Shetani pia amekamata kwenye eneo la elimu, kila jambo huwa linapaswa kuwa ndani ya muda fulani ndio maana kuna umri wa kuanza shule ya msingi na kuna umri mtu anapswa kuwa amemaliza chuo kikuu lakini unaweza anafeli masomo bila sababu za msingi na anakosa ufahamu hata wakuendelea na hatua ya cheti anarudia tena kidato cha nne anafeli tena, anarudia umri unakwenda na mtu anachukulia kawaida kumbe shetani amejiweka kwenye nafasi ambayo ni ngumu kuelewa isipokuwa uwepo wa Roho mtakatifu ndani yake ambayo itamfunulia vizingiti vilivyowekwa na shetani.
Magonjwa na changamoto zingine, ni kweli mtu amepata kazi lakini shida na matatizo ni chungu nzma kila wakati wa mshahara ukifika unasikia shangazi anaumwa, mama anaumwa, au misiba hivyo kumalizia fedha yote kwenye kutatua changamoto za kifamilia badala ya kupiga hatua ya maendeleo yako, hivyo unakuwa unazunguzunguka tua hapo.
Ndugu zangu inatupasa kumkatibia sana Mungu ili kuweza kutambua vita vya kiroho ambazo shetani amekuwa akizipigana dhidi ya ndoto na maono ya vijana wengi.
Biblia inasema katika kitabu cha Yak 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. 
Ukiishi karibu na Mungu ni rahisi sana kujua makusudi na malengo mabaya ya shetani hivyo ni rahisi kupigana vita hivyo maana unajua njia anazotumia shetani kuharibu au kukuchelewesha 
usikubali kupiga makitaimu sehemu moja kwa muda mrefu yawezekana sio wewe bali yupo adui amejipenyeza katika safari yakuelekea maono yako.
Na ili uweze kutambua haya yote ni vyema kuishi maisha yakumpendeza Mungu na shetani hawezi kupata mwanya wa kupenyeza roho zisizokuwa na ubora ambazo ni chanzo cha kukufanya kuishi maisha yasikusudiwa na Mungu.
Usifurahie na kuridhika na maisha yako ya kawaida jaribu kuishi maisha yenye kujitathmini kila wakati na kuishi kwenye maisha ya kuomba na kusoma neno la Mungu hapo ndipo utangudua kama unatembea kwenye njia sahihi au umehamishwa na ibilisi unasafiri kwenye njia isiyo yako.
Usione kawaida kutokuwa kwenye ndoa au kwenye mchakato wa kufunga ndoa waakati umri umefika na Mungu ameshakubariki una kazi nzuri na uwezo mzuri tu wa kuendesha maisha pamoja na mwenza wako.
Ukiona changamoto ni uchumi.au kikwazo fulani, ikatar hiyo hali kwa vitendo chukua hatua na Mungu atakuonekania kwenye hatua yako lakini usipoanza hatua fulani kila mwaka utaisha uko pale pale mambo hayaendi kumbe njiani shetani amekaa na wewe unaona kawaida.
Kushinda yote haya mwombe sana Mungu, mkaribie Mungu, mruhusu Roho mtakatifu aweke makao ndani yako ili kuweza kukupa maarifa ya kujua kila mtego na kuutegua. 
Somo hili litapatikana Youtube kuanzia wiki ijayo kwa njia ya video
Kuanzia ijumaa subscribe channeli ya ngu Ms Tv kwa maarifa ya kimungu na maisha ya kila siku
Moses Mgema
0755632375
0715366003
mgemamoses@gmail.com
God bless you so much





Friday, October 22, 2021

HUDUMA YA UIMBAJI NDANI YA KANISA

Mwalimu: Musa (Moses) Zephania Mgema
Ijumaa tarehe 22/10/2021
FPCT -Singida town centre church.
Uimbaji ni nini ?
Ni sanaa ambayo inatumika kuwasilisha ujumbe kwa njia ya lahani (chord) na mpangilio wa sauti wenye kutengeneza ladha yenye mvuto kusikiliza.
➡️Uimbaji asili yake ni mbinguni. Huduma hii ilianzia mbinguni na kiongozi wa huduma hii huko mbinguni alikuwa anaitwa lusifa kabla ya kuasi.
Ezekieli 28:13-15
➡️Huduma ya uimbaji ni moja kati ya huduma muhimu ndani ya kanisa kwa sababu imefanyika chumvi nzuri kwa ustawi wa kanisa na hata huduma nje ya kanisa.
Uimbaji katika mfumo wa injili kwa maana ya nyimbo za kiroho sio burudani bali ni huduma nyeti na ya msingi wala sio burudani au huduma ya ziada ndani ya kanisa.
➡️Huduma ya uimbaji ni huduma ambayo haina mwisho maana hata baada ya unyakuo kazi pekee tutakayoifanya huko mbinguni ni kuimba tu.
Ufunuo 5:9-10
Ufunuo 15:2-4
➡️Hapa duniani kazi ya uimbaji ilianza muda mrefu tangu enzi za agano la kale ni hii ni mara tu baada ya kuumbwa kwa Adamu na Hawa.
Mwanzo 4:21

KWA NINI HUDUMA YA UIMBAJI NDANI YA KANISA.
1petro 4:10-11
1Nyakati 6:31-32
1. Huduma ya uimbaji ikitumika vyema kwa kuongozwa na Roho mtakatifu, maombi na Neno la Mungu huleta mavuno mapya ndani ya kanisa.
2. Hufanya moyo wenye huzuni kupata furaha na Amani.
3. Hubadili moyo mgumu kuwa laini 
      1samweli 16:23
4. Mtu dhaifu hutiwa nguvu na uzima 
     1samweli 18:6-9
5. Hudhihilisha uwepo wa Mungu.
      2Nyakati 20:21-22
     2Falme 3:15-16
     Matendo 16:25-26
HUDUMA INAYOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU, MAOMBI PAMOJA NA NENO LA MUNGU-
1.  Huonya na kufundisha kolosai 3:16
2.  Ni mahubiri kamili  Isaya 48:20
3.  Huleta faraja kwa waliokosa tumaini.
4. Humsifu na kumshukuru Mungu kwa matendo makuu 
Nb:
Zipo pia nyimbo za upuuzi kama ambavyo 
 Amosi 6:5 anaonyesha.
➡️Kama mtumishi wa Mungu unaetumika kwa njia ya uimbaji ni muhimu haya yafuatayo kuwa sehemu ya wimbo unaohudumia watu
1. Roho mtakatifu kuhusika
2. Neno la Mungu kujaa kwa wingi ndani ya mwimbaji.
3. Kufanya maandalizi kabla ya huduma kwa maana ya kuomba, kusoma neno na kuruhusu Roho mtakatifu kukuongoza ili kufanya huduma yenye connection ya mbingu na wewe kama mhdumu.
➡️Huduma ikiwa na uongozi wa Mungu lazima iwe ni ibada kamili ambayo itadhihilisha matendo makuu ya Mungu, mfano uponyaji, Faraja, nk.

➡️Tunaweza kujifunza kupitia wimbo alio imba Musa mtumishi wa Mungu na Israel baada ya kuwashinda wamisri.
 Ufunuo 15:3
➡️Ulikuwa wimbo wa matendo makuu ya Mungu
Aina nyingine ya nyimbo ni nyimbo ya mwanakondoo (Wimbo mpya) ambao unaelezea namna Yesu anavyostahili kuabudiwa, kupewa sifa kwa matendo makuu ambayo ametenda kupitia msalaba.
Zaburi 40:1-3
Ufunuo 14:1-3
Ufunuo 15:5-9
Wimbo ukitungwa kwa uongozi wa Mungu mwenyewe huwa ni wimbo wenye nguvu na huleta matokeo kusudiwa.
Ukiona waimbaji/mwimbaji anaimba na wala hakuna connection ya Kimungu, hiyo ni ibada ya sanamu ambayo imebeba kujiburudisha nafsi na ni makelele mbele za Mungu.
➡️Mwimbaji lazima ajawe na Roho mtakatifu kwa wingi ndani yake, Neno la Mungu na awe mtu ambae anaiombea huduma yake kwa kujitoa ili kuwa na huduma bora na yenye nguvu za Mungu.
➡️Ipo mifano ya huduma za uimbaji katika agano jipya na agano la kale ambavyo Mungu alohudumia watu kupitia waimbaji 
Luka 1:41&67
Efeso 5:18-20.
Kwa ufupi uimbaji ni kazi ya Roho mt. nje ya Roho mt.  uimbaji unabaki kuwa burudani tu, maana ni ngumu sana kuyaona matendo ya Mungu yakidhihilika.
➡️Uimbaji ukiwa na uongozi wa Mungu hiki tegemea kukiona kwa ukubwa katika huduma yalo ya uimbaji  2Nyakati 5:13-15
Neno la Mungu ni huduma kamili ya uimbaji hivyo kwa sababu neno ni chanzo cha ujumbe na mafunuo mengine ya kimungu lazima mwimbaji awe amejaa neno ndani yake, hii husaidia kuwa na huduma yenye matokeo.
Zaburi 45:1
Wakolosai 3:16
Mwisho.
Msingi wa huduma yeyote ya kimungu lazima iongozwe na 1. Neno la Mungu
                       2. Roho mtakatifu
                       3. Maombi na utii wa Mungu.
Ukiwa na hivi vyote lazima uwe na huduma ya nguvu za Mungu ndani yake
Mungu akubariki sana kwa kunisikiliza
0715366003 whatsup
0755632375 call and sms
mgemamoses@gmail.com




Thursday, September 23, 2021

UJASIRI NDANI YA YESU

Bwana Yesu asifiwe!

Waebrania 10:35 anasema,,"Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu"

Ukisoma mstari huu ndani yake kuna kitu cha thamani na cha ajabu sana kinaitwa "UJASIRI" na huo ujasiri unaweza ukautunza au ukautupa ,"MSIUTUPE" maana yake unaweza kuwa nao na ukautupa.
Ndani ya "UJASIRI" kumebebwa kitu kinaitwa "THAWABU " 
Ukisoma katika kiingereza anasema hivi,,,,"Therefore do not throw away your confidence, which has a great reward."
Kiswahili anasema hivi,," Kwa hiyo, msipoteze ujasiri wenu, maana utawapatia thawabu kubwa" Sasa ukiunganisha na neno la 
Efeso 6:10 anasema "Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake" Utaona neno hili "HODARI" limetumika katika Waebrania 10:35 kama "UJASIRI" ambao ndani yake tunapewa "Thawabu KUBWA".

NINI MAANA YA UJASIRI/UHODARI.
UJASIRI-Maana yake ni uwezo alionao mtu wa kujiamini mbele za Mungu juu ya maisha yake yasiyo hukumiwa na dhambi moyoni mwake.

 1 Yohana 3:21 anasema hivi,,"Wapenzi, miiyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu"
Sasa jiulize swali hili pamoja na mimi, Ni nini kina hukumu moyoni? 
KUHUKUMIWA MOYONI"...kuna letwa na "DHAMBI" iliyo moyoni ambayo inapoteza UHODARI/UJASIRI wa mtu mbele za Mungu.

 Kama umepoteza "UJASIRI" ndani yako maana yake "UMETUPA UJASIRI" wako kwa kuruhusu dhambi iingie kwako, na madhara yake thawabu  unaipoteza ukiwa hapa hapa duniani.

Kama umepata "UJASIRI" wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, maana yake umefutiwa dhambi, na moyoni mwako umepewa

 "UZIMA WA MILELE" Sasa unaporuhusu dhambi unapoteza "UZIMA WA MILELE" uliyo ndani, na maandiko yanasema MNA UZIMA WA MILELE NINYI MNAOLIAMINI JINA LA MWANA WA MUNGU" (1 Yohana 5:13)

SABABU ZA KUTUNZA UJASIRI.
Ni kutufikisha katika Tumaini ambalo Bwana ametuandalia watoto wake .
Waesfeso 3:12 "Katika yeye tuna ujasiri na uwezo wa kukaribia tumaini kwa njia ya kumwamini"
Huwezi kulikaribia "TUMAINI" uliloliweka ndani ya Kristo kama huna "UJASIRI NA UWEZO" unaokupa wewe kutarajia unachokitarajia katika Kristo.

Hakikisha haupotezi "UJASIRI" wako usije ukashindwa kukaribia tumaini lako uliloliweka kwa Yesu. Maana ujasiri na uwezo ndivyo vinakutengezea mazingira ya kukutana jibu lako/yetu. Ujasiri na uwezo unavipata ukiwa ndani ya Yesu.
UJASIRI UNARUHUSU KUPEWA NEEMA NA KIBALI MBELE ZA MUNGU 
.
Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji"
Katika maneno hayo kuna..."KITI CHA NEEMA" na kuna....KUPEWA REHEMA..na pia kuna...KUPATA NEEMA. Kazi moja wapo ya kiti cha Neema ni sisi "TUPEWE REHEMA" kiingireza anasema,,, "GIVEN MERCY" Mercy inamaana ya "HURUMA"
Kwa maana hiyo kiti cha NEEMA kinatoa "HURUMA NA NEEMA" vinavyomsaidia mtu mwenye ujasiri ndani yake kutumia "NEEMA INAYOTOA MSAADA Msabato Neema hutoka kwa Mungu na Kwan njia y'all Neema tunapata kibali mbele Zach Mungu "
Kwa hiyo wakati wowote mahali popote anapohitaji msaada kutoka Kwa Mungu  night Neema yake Pelee ndio sababu yakupokea majawabu na mahitaji yako/yangu, maana kwa njia ya kristo tumepewa neema ya kupokea chochote tuombacho.

Maandiko yanasema hivi,,"Wapenzi, miiyo yetu isipotuhukumu tunaujasiri kwa Mungu, na lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa tumezishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake" (1 Yohana 3:21-22)

Ukiomba na hauna ujasiri ndani yako huwezi kupokea unachokiomba, kwa sababu "NEEMA" ya kukusaidia haipo
 kwa nini haipo?
Kwa sababu huna uwezo wa kusimama mbele za Bwana, maana dhambi hukosesha ujasiri na kibali cha kwenda mbele za Mungu, maana hukumu husimama mbele ya mwenye dhambi na kumwondolea ujasiri.

"TWAJUA YA KUWA MUNGU HAWASIKII WENYE DHAMBI; BALI MTU AKIWA MCHA MUNGU, NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE HUMSIKIA HUYO" (Yohana 9:31)
Hili neno tumejifunza leo Kama msingi wa maombi yetu kwa sababu sisi tumepata Neema ya kristo ambayo imetuokoa na hatuko na dhambi inayohukumu mioyo yetu maana Bwana amekwisha kutusamehe na huo ndio ujasiri tulio nao unatufanya kwenda mbele zake kupeleka mahitaji yetu.
Kwa uhakika huo tunaamini kila tukipelekacho kwa Mungu naamini tutapokea sawasawa na mapenzi take. 
Amen
Prepared by Moses 
Moses z Mgema 
0715366003
24/09/2021