Monday, October 25, 2021

ROHO YA KUCHELEWA ( THE SPIRIT OF DELAY) EP 1.

Bwana asifiwe mtu wa Mungu
Nipende kumshukuru Mungu kwa nafasi ya pekee ambayo ametupa tena kwa neema ambayo ni upendeleo wa Kimungu kwetu.
Leo tutajifunza neno la Mungu lenye kichwa cha somo ROHO YA KUCHELEWA ( SPIRIT OF DELAY).
Katika somo hili tutaona mambo kadhaa ambayo yamekuwa chanzo cha watu wengi kuchelewa kufikia hatima zao na bado wanachukulia kawaida bila kujali muda wa nyakati za kutimiza baadhi ya mambo katika wakati uliokusudiwa.
Note
Sio kila jambo linalochelewa ni mpango wa Mungu hapana ndivyo ilivyo hata kwa upande wa kuwahi kuwa sio kila jambo linalowahi ni mpango wa Mungu. 
➡️Mambo mengine yanachelewa kwa sababu za michezo anayoicheza shetani katika ulimwengu wa Roho bila watu wengi kujua na hivyo kuchukulia kawaida.
➡️ Mambo mengine pia yanawahi sio kwa mpango wa Mungu bali shetani anaweza kuwa amechungulia mbali na kuiona baraka yako iliyo kuu hivyo anapenyeza baraka feki kwa haraka ili kukupishanisha na Baraka ya Mungu.
Lakini hapa tutazungumzia somo lenye kichwa cha somo la Roho ya kuchelewa ( Spirit of delay).
Daniel 10:13-21
Habari ya Daniel aliyejulikana kama Belteshaza ambae majibu ya maombi yake yalishikiliwa na mkuu wa uajemi.
Hapa tunaona pamoja na Daniel kuomba na kufunga kwa majuma matatu lakini bado malaika aliyeagizwa na Mungu kuleta majibu ya Daniel alishikiliwa kwa kwa siku 21 sawa na majumaa matatu ya ambayo Daniel pia alitumia kumwomba Mungu wake.
Hapa nataka uone ni kwa kiasi gani shetani yupo kwa ajili ya kupambana kuhakikisha kwamba hupati kuwa sehemu unayopaswa kwa wakati sahihi uliokusudiwa na Mungu.
Tunayo mifano mingi ambayo imekuwa kama maisha ya kawaida kwa vijana wengi, mfano mtu anamaliza shule badala ya kutafuta kazi hata ndogo kutwa anatembea na vyeti kuomba kazi maofsini, anashindwa kutambua kwamba uzima, elimu na afya aliyo nayo ni mtaji namba moja kwenye maisha.
Mwaka 2016 wakati natoka chuo, nilikuwa na akili nyingi sana kwa sababu nilikubali kuanzia kwenye kiwango nilichokuwa nacho nikaanzisha biashara ndogo ndogo ya chakula mkoani kwangu singida na biashara ilikuwa inakwenda vyema sana na kipato changu ilifikia ikawa inaanzia laki tatu kwa mwezi na mtaji wa kwanza ilikuwa Tsh 30000 tu nilianza na miwa, miwa akaadimika nakaingia kwenye uji, chai na hatimae niliifikia hatua ya kuuza chakula cha mchana na ukuajia wake ulikuwa mkubwa sana.
Wakati naanza kufikiria kufungua mgahawa wakimataifa nikapata tangazo la kazi ambalo lilinifanya kuomba kazi kwa kweli kati ya makosa nimewahi kufanya nikuacha kazi zangu kwenda kwenye kazi ambayo nilifikiri ingenipa zaidi kumbe nilikuwa narudi hatua kadhaa nyuma.

Usiku wa juzi ndio Mungu alinipa mafunuo kwamba watu wengi wanachelewa kufikia malengo kwa sababu shetani amejiingiza katikati ya fikra za watu nakuanzisha mission ambayo imekuwa ni chanzo cha kuchelewesha baadhi ya mambo hasa kwa vijana.

Kijana unakuta anapambana kutafuta ajira na umri unakwenda mwisho wa siku alikuwa na maono makubwa anakuja kuishi kwenye robo ya maono yake kisa alishindwa kutambua kwamba mtaji wa kwanza sio fedha bali ile akili ambayo amepewa na Mungu inaweza kuwa mtaji mkubwa wa kumfanya kuishi kwenye maisha aliyokusudiwa kwenye wakati sahihi.

Wengine wameondolewa shauku ya kuoa, fedha anayo, maisha ambayo yanaweza kuendesha familia vyema anayo lakini, hataki kuoa anaona kama wakati bado kumbe ndani yake shetani ameishaingia maana anajua kwamba kijana huyu akipata mke atakuwa amejipatia kibali kwa Bwana, na maana ya kibali ni upendeleo mkuu kutoka kwa Mungu na kuwa kwenye ndoa mtu anaweza kufanya vizuri zaidi kuliko akiwa pekee yake.
Wengine wamepandikizwa roho yakujiona bado ni watoto hasa vijana wa kiume, na mabinti nao Roho ya kuchaguachagua katika ule wakati sahihi ambao mtu alipaswa kuolewa hapa shetani anacheza na ufahamu wa binti mwisho wa siku umri unakwenda anaamua kuolewa na yeyote atakae kuja ili mradi amepata mume kumbe mtu sahihi alishakuja lakini kwa sababu ya kufungwa ufahamu binti alijiona bado au yule kijana alimwona sio hadhi yake.
Shetani pia amekamata kwenye eneo la elimu, kila jambo huwa linapaswa kuwa ndani ya muda fulani ndio maana kuna umri wa kuanza shule ya msingi na kuna umri mtu anapswa kuwa amemaliza chuo kikuu lakini unaweza anafeli masomo bila sababu za msingi na anakosa ufahamu hata wakuendelea na hatua ya cheti anarudia tena kidato cha nne anafeli tena, anarudia umri unakwenda na mtu anachukulia kawaida kumbe shetani amejiweka kwenye nafasi ambayo ni ngumu kuelewa isipokuwa uwepo wa Roho mtakatifu ndani yake ambayo itamfunulia vizingiti vilivyowekwa na shetani.
Magonjwa na changamoto zingine, ni kweli mtu amepata kazi lakini shida na matatizo ni chungu nzma kila wakati wa mshahara ukifika unasikia shangazi anaumwa, mama anaumwa, au misiba hivyo kumalizia fedha yote kwenye kutatua changamoto za kifamilia badala ya kupiga hatua ya maendeleo yako, hivyo unakuwa unazunguzunguka tua hapo.
Ndugu zangu inatupasa kumkatibia sana Mungu ili kuweza kutambua vita vya kiroho ambazo shetani amekuwa akizipigana dhidi ya ndoto na maono ya vijana wengi.
Biblia inasema katika kitabu cha Yak 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. 
Ukiishi karibu na Mungu ni rahisi sana kujua makusudi na malengo mabaya ya shetani hivyo ni rahisi kupigana vita hivyo maana unajua njia anazotumia shetani kuharibu au kukuchelewesha 
usikubali kupiga makitaimu sehemu moja kwa muda mrefu yawezekana sio wewe bali yupo adui amejipenyeza katika safari yakuelekea maono yako.
Na ili uweze kutambua haya yote ni vyema kuishi maisha yakumpendeza Mungu na shetani hawezi kupata mwanya wa kupenyeza roho zisizokuwa na ubora ambazo ni chanzo cha kukufanya kuishi maisha yasikusudiwa na Mungu.
Usifurahie na kuridhika na maisha yako ya kawaida jaribu kuishi maisha yenye kujitathmini kila wakati na kuishi kwenye maisha ya kuomba na kusoma neno la Mungu hapo ndipo utangudua kama unatembea kwenye njia sahihi au umehamishwa na ibilisi unasafiri kwenye njia isiyo yako.
Usione kawaida kutokuwa kwenye ndoa au kwenye mchakato wa kufunga ndoa waakati umri umefika na Mungu ameshakubariki una kazi nzuri na uwezo mzuri tu wa kuendesha maisha pamoja na mwenza wako.
Ukiona changamoto ni uchumi.au kikwazo fulani, ikatar hiyo hali kwa vitendo chukua hatua na Mungu atakuonekania kwenye hatua yako lakini usipoanza hatua fulani kila mwaka utaisha uko pale pale mambo hayaendi kumbe njiani shetani amekaa na wewe unaona kawaida.
Kushinda yote haya mwombe sana Mungu, mkaribie Mungu, mruhusu Roho mtakatifu aweke makao ndani yako ili kuweza kukupa maarifa ya kujua kila mtego na kuutegua. 
Somo hili litapatikana Youtube kuanzia wiki ijayo kwa njia ya video
Kuanzia ijumaa subscribe channeli ya ngu Ms Tv kwa maarifa ya kimungu na maisha ya kila siku
Moses Mgema
0755632375
0715366003
mgemamoses@gmail.com
God bless you so much





No comments:

Post a Comment